Ushauri: Nakusudia kufungua kesi ya madai dhidi ya Airtel Money Tanzania Ltd

Rukie

Member
Sep 27, 2022
78
123
Habari za leo,

Mimi ni mfanyabiashara na ni mtumiaji wa huduma za Airtel Money.

Juzi tarehe 3 Machi 2023 nilifanya muamala wa kuhamisha pesa kutoka Airtel money kwenda Benki, akaunti yangu binafsi pesa ilitoka ila kwenye akaunti haikuingia.

Nilipiga simu huduma kwa mteja wakasema kuwa wao wana limited access hawawezi kuona kama pesa imeingia kwenye akaunti au la na waka ahidi kuwasiliana na kitengo husika kwa ajili ya kufuatilia.

Nilifanya mawasiliano na benki wakasema pesa haijaingia kwenye akaunti yangu.

Sasa changamoto kila ukiwasiliana na Airtel ni siasa, wanajibu kuwa suala lako tunalifanyia kazi ndio majibu yao halafu hawaeleki, wana double standard sana.

Sasa uamuzi nimeuchukua ninakusudia kuwasiliana na wanasheria waniandalia notice ya madai ili nidai pesa yangu ni zaidi ya 1 million.

Naomba ushauri kama kuna hatua za ziada naweza kuzichukua ili nipate haki yangu kwa wakati.

MREJESHO
Niliwasiliana na mwanasheria akaandika Notise ya madai Leo asubuhi nikaipeleka Morocco na saa 10 jioni pesa yangu imewekwa kwenye akaunti.

Asante sana kwa ushauri wenu.
 
Nenda ofisini kwao na notisi ya madai utasaidiwa swala lako fasta. Hakikisha pia una ushahidi pesa imetoka kwenye account yako benk. Hivyo anzia benk kuchukua statement
 
Nenda ofisini kwao na notisi ya madai utasaidiwa swala lako fasta. Hakikisha pia una ushahidi pesa imetoka kwenye account yako benk. Hivyo anzia benk kuchukua statement
Poapoa Asante sana ntafanya hiyo
 
njoo kesho HQ pale Morocco utasaidiwa, beba na kitambulisho chako cha taifa .
 
Wewe siyo wa kwanza kupitia hyo changamoto na hakuna aliye wahi kuwashtaki...subiri hela yako
Itaingia
 
Back
Top Bottom