Ushauri: Naacha chuo nijikite biashara ya sarafu mtandaoni FOREX

Escotter20

JF-Expert Member
Jul 20, 2020
465
842
Habar wakuu

Mimi ni mwanafunzi wa kozi ya technical education in electric and electronics eng, umri wangu 23yrs

Nimekuja hapa kuomba ushauri, nimefanya uchunguzi wangu wa kina kwa miaka5 pamoja na kutafuta maarifa baada ya kujaribu forex nimeona Ina manufaa kwangu... Hivyo nimekuja kuomba ushauri naacha chuo ili nijikite zaidi huko.. Hoja zangu Ni kama ifuatavyo

1. Shule naona inapoteza muda na lengo la shule ni kutafuta hela as long as nimepata shortcut ya pesa why niendelee na shule?

2. Kujiepusha kuwa miongon mwa wahanga wa ajira mbeleni, ni heri nijiondoe mapema nikajitafute!!

3. Kitu ninachokisoma sijawahi kufikiria kama ningesoma, naona nilifata mkumbo, kuepusha majuto zaidi Ni heri nijichomoe mapema?

4. All in all what determines a man is his/her success, u choose to be part of success through FOrex

Hizo ndio points zangu.. Naomba ushauri na mawazo, ningeweza kuomba watu wanaonizunguka but najua sio rahisi wao kumkubalia na na mimi, but naamin humu JF kuna watu wenye upeo mkubwa, nakaribisha michango.
 
Kama fellow dropout, hakikisha hiyo biashara tayari inakuingizia kipato cha kutosha matumizi yako ya kila mwezi (angalau mara 1 na nusu ili uwe na savings). Iwe hivi kwa angalau miezi 3 iliyopita kuonesha ni kitu stable. Pia uwe na pesa pembeni ya kutosha at least mwaka wa matumizi usipopata kazi yoyote nyingine.

Na pia usiondoke chuo kiholela. Andika barua ya kupostpone. Vyuo vingi unaweza kupostpone mpaka miaka miwili na ukarejea ulipoishia. Ukiondoka kiholela ukirudi unaanza upya. Usisahau pia kutoa taarifa kwa walipa ada. Likely hawatafurahi ila wao kujua mapema ni vizuri zaidi kuliko kujua uliwadanganya.

Kama hauna vigezo hivi asilimia zako za kushindwa hustle zitakuwa kubwa sana na ni vema ubaki chuo tu.
 
Back
Top Bottom