Baba mkwe wangu alifariki mwaka 1993 mwanangu akiwa na miaka 9. Alimpa mwanangu shamba kwa sababu alikuwa ni wajina wake. Eneo hilo halikuguswa na yoyote kwa sababu siku zote linajulikana ni la mwanangu.. Pia alimpa mjukuu mwingine mtoto wa mke mwenzangu eneo ambalo pia halikuguswa. Mwaka juzi Bibi yake mwanangu alimwomba alime sehem kidogo ya shamba nae akakubali ili eneo lisikae tu. Sasa mama mkwe wangu amefariki wifi zangu na shemeji yangu wanataka lile eneo ligawanywe kwa wajukuu wengine ambao hata walikuwa hawajazaliwa wenye jina la baba mkwe wangu. Ukoo uliingilia wifi zangu na shemeji yangu wakasema wana karatas ambazo walisaini wao na bibi yangu hayo mabadiliko yafanyike, lakini wameambiwa walete na hawajaleta. Sasa shemeji anamzuia mwanangu kuendeleza eneo lake na karatas ameshimdwa kuzileta..je afanyeje?