Tamaduni za kipekee na za ajabu Afrika

Mr What

JF-Expert Member
Oct 22, 2016
1,177
2,086

Getty


Utamaduni ni jinsi binadamu anavyokabili maisha katika mazingira yake. Hii pamoja na ujuzi, Imani, Sanaa, sheria , mila, desturi, ambavyo mtu anajipatia kama mwanajamii. Inapokuja kwamba mambo fulani yanakubaliwa na jamii fulani kutekelezwa basi huitwa utamaduni wa jamii hiyo. Tutakubaliana kwamba walau kila mmoja wetu ni sehemu ya utamaduni fulani, na tunajivunia tamaduni zetu kwa vile ni sehemu ya maisha yetu. Waswahili husema msahau mila ni mtumwa!

Katika baadhi ya jamii za Kiafrika na dunia kwa ujumla baadhi ya tamaduni hujitokeza na kuonekana kuwa za kipekee, kwa jamii nyingine.

Katika Makala hii tunaangazia baadhi ya tamaduni zinazoonekana kuwa za kipekee kutoka baadhi ya mataifa ya Kiafrika.

Shangazi kufanya ngono na mume wa mpwa wake

Utamaduni wa shangazi wa bibi harusi kufanya tendo la ndoa na mume wa mpwa wake huenda likawa jambo la ajabu katika jamii nyingi, lakini sio jambo geni kwa Jamii ya Banyankole (au Manakole).

Wanyankole ni wenyeji wilaya za Mbarara, Bushenyi, Ntungamo, Kiruhura, Ibanda, Isingiro na Ntungamo magharibi mwa Uganda.

Ndoa katika jamii hii, sawa na jamii nyingi za Kiafrika ni jambo muhimu sana kwani wazazi hufurahishwa na ndoa za watoto wao ambao huwapatia wajukuu na kuendeleza kizazi.

Heshima ya familia ya bibi harusi ni jambo muhimu sana, na hii itatokana na binti yao kuolewa akiwa bikra.

Lakini bibi harusi anapoolewa na kubaini kuwa mumewe ana tatizo la kufanya tendo la ndoa, humfahamisha shangazi yake, ambaye huhakikisha iwapo kweli mume wa mpwa wake hawezi kufanya tendo hilo, kwa kufanya tendo la ndoa mume wake ili kujiridhisha kwamba kweli ana tatizo hilo au la.

Anapobaini kuwa kweli mkwe hajiwezi kimapenzi huwapatia wanandoa ushauri kuhusu hatua inayofuata... unaweza kuwa ushauri wa ufundi wa tendo hilo kama atabaini kuwa ndilo tatizo , au ushauri wa matibabu, pale anapoona mkwe anauhitaji.

Utamaduni mwingine ambao huenda ukawa ni wa nkipekee katika jamii hii ya magharibi mwa Uganda ni ule wa baba mkwe kushiriki tendo la ngono na mke wa mwanaye wa kiume.

‘’Katika mila ya Kinyankole ni jambo lililokubalika tangu jadi kwa baba wa mwanaume kufanya tendo la ndoa na mke wa mwanaye yaani mkwe. Hii inafahamika kama ’kwenda kuona ni wapi ng’ombe za mahali zilikoenda,‘’alinieleza mkazi wa Kampala ambaye hakutaka jina lake litajwe, ambaye pia ni Myankole.

’Licha ya kwamba mila hii ilikatazwa na serikali kutokana na kwamba ilionekana kuchangia kueneza maambukizi ya HIV/UKIMWI, bado katika maeneo ya vijiji vya wafugaji hasa wanaohamahama bado inatekelezwa japo kwa usiri sana.... ni vigumu kwa mtu wa nje kujua ila wanafamilia wenyewe'', alisema na kuongeza kuwa : ''Mfano babu yangu amekuwa akilala na wake za watoto wake, ingawa hawapendi lakini wanalazimika kufanya hivyo kwa kuwa ni mila ’’, aliiambia BBC.

Serikali ya Uganda ilipiga marufuku mila za kushiriki mapenzi kiholela baina ya watu wa familia ambazo zilisemekana kuchangia maambukizi ya HIV/UKIMWI.

Mwanamke mwingine wa Kinyankole ameiambia makala hii: ''Kutokana na elimu na dini na kuchangamana kwa Wanyankole na jamii nyingine, baadhi yao wamekuwa wakiachana na tamaduni hizi, japo ni wengine bado wanauendeleza''.

Kuogeshwa ndani ya maziwa
Kabila la Wanyankole lina tabaka mbili Bahima na Biru, huku Wahima wakiwa ni wafugaji na Biru wakiwa ni wakulima.

Katika utamaduni wa Wahima wiki moja kabla ya kuolewa, bibiharusi huogeshwa ndani ya maziwa ya ng'ombe na kuyanywa kila siku na kisha hapakwa mafuta ya ngombe ili ngozi yao iwe laini.

Ni kasoro kwa mwanamke wa Kihima kuwa mwembamba. Hivyo basi Bibi harusi mtarajiwa hulishwa nyama, maziwa na mafuta ya ngombe ili aweze kunenepa na kuwa na mwili nyororo.

Unene wa mwili wa mwanamke ndio urembo wake Kulingana na utamaduni wa kihima mwanamke mwembamba huonesha kuwa familia anapotoka ni maskini sana.

Utamaduni wa mjane kulala na maiti

Utamaduni huu unapatikana katika kabila la Wajaluo ambao ni jamii za Wanailotiki wanaopatikana katika Magharibi mwa Kenya na Mara upande wa Tanzania -Afrika mashariki. Jamii hii inafahamika kwa kutunza utamaduni wao kwa miaka mingi.

Kinyume na tamaduni nyingine, katika jamii ya Wajaluo wa Kenya, mjane anatarajiwa kulala chumba kimoja na marehemu mume wake kabla ya kuzikwa.

Kulingana na Wajaluo, hii ni sehemu ya mila inayolenga kuwatakasa wanawake wajane- ili wawe tayari kwa ajili ya kuolewa tena.

Wakati mwanamke mjane anapolala chumba kimoja na marehemu mumewe, anatarajiwa kuota ‘’ndoto za lazima’’ akiwa na marehemu kimapenzi, mara ya mwisho, ndipo awe ‘huru’ na tayari kuolewa tena. Iwapo hataota ndoto ya aina hiyo, hufanyiwa matambiko ya kimila zaidi ili kumtakasa na kumuweka huru ili aweze kuolewa tena. Licha ya kwamba mila hii inaendelea kutekelezwa Wajaluo hasa wanaoishi katika maeneo ya vijijini, baadhi yao wameonekana kuiacha kutokana na Ukristo na maisha ya kisasa.

Mila ya kusindikiza roho ya mfu
Mila nyingine ya kipekee katika jamii ya Wajaluo ni mila ya kufukuza roho ya mfu. Mila hii hufanywa kwa tambiko ambalo hufanywa na wanaume pekee. Shughuli hii hufanyika kwenye mto, ili kuhakikisha maji yanaisomba roho ya kifo. Aina ya mnyama anayeuliwa katika tambiko hili hutegemea hadhi ya marehemu.

Mtoto au kijana mdogo anapofariki , jogoo huchinjwa, na iwapo marehemu ni mzee basi mnyama huuawa na tambiko hutekelezwa tena kwa jogoo.

Kumchapa viboko maiti aliyejinyonga/kujitoa uhai

Huenda sio mara ya kwanza kusikia kuhusu imani zinazoambatana na kifo cha mtu aliyejinyonga.
Wakati mtu anapojinyonga mtini katika eneo la Nyanza na baadhi ya maeneo mbali mbali ya Magharibi mwa Kenya, mwili wake hutandikwa viboko vingi kabla ya kushushwa kutoka kwenye mti au sehemu aliojinyongea, na maiti huzikwa mbali na nyumbani kwao katika eneo linaloelezewa kama ‘gunda’ lililotengwa kwa ajili ya mazishi ya watu waliojinyonga na kutengwa.

Utamaduni huu pia hutekelezwa na jamii ya Abaluhya wa Magharibi mwa Kenya na jamii nyingine za nchi mbali mbali za Kiafrika.

Wanawake kuoana (Nyumba ntobu)

Katika mila, desturi na tamaduni za makabila mengi muundo wa familia hasa ndoa hutofautiana. Ndoa kawaida huhusisha mwanaume na mwanamke, lakini katika mkoa wa Mara, wilaya ya Tarime, Tanzania, utamaduni wa wanawake kuwaoa wanawake wenzao bado ni jambo la kawaida.

Alipozungumza awali na BBC mkazi wa mkoa wa Mara nchini Tanzania Wegesa mwanamke wa miaka 60 amemuoa mwanamke mwenzake -Nyanshwi mwenye umri wa miaka 35 alisema ‘’Kwa mila na desturi msichana harithi kwahiyo nimemchukua mka mwana wangu na sasa tumeishi miaka 15…tunaishi vizuri ananisaidia shamba tunaenda naye , maji ananiendea. ’’

Awali utamaduni huu uliwawezesha wanawake wagumba kuwaoa wanawake watakaowazalia watoto na wanaume wengine na kuitwa wao.

Ukeketaji/Upasuaji wa sehemu za siri za wanawake

Kenya, Ruel: Tukio la ukeketaji wa wanawake wa kabila la Kuria mwaka 1958.

Ukeketaji wa wanawake umekuwa mojawapo ya mila ambazo zimepingwa sana katika sehemu mbali mbali duniani ikiwemo Afrika. Mataifa kadhaa yamefaulu kuharamisha utamaduni huo lakini bado kunazo jamii zinazotekeleza utamaduni huo kisiri.

Ukeketaji unafanyika kwa njia mbali mbali kulingana na aina ya upasuaji ama oparesheni inayofanyiwa sehemu ya siri ya mwanamke; Kwa mfano Katika jamii ya Wakurya , upande wa Kenya na Tanzania, jamii ya Wamaasai kutoka nchi hizo, pamoja na Wasomali, kila mwanamke anatarajiwa kuwa amekeketwa.

Unyanyapaa unaozingira wanawake ambao hawakupitia mila hii (FGM) ni jambo linalojitokeza katika utamaduni huu ambapo mwanamke ambaye hajakeketwa huonekana mwenye kasoro kubwa, kiasi kwamba hukejeliwa na kunyanyapaliwa na jamii. Baadhi ya watu wa jamii hizi hata hivyo wameanza kuepuka utamaduni huu.

Tohara au Sunna (jadi): Hii inahusisha kuondolewa kwa ncha ya kisimi. Hii ndio operesheni pekee ambayo, kiafya, inaweza kufananishwa na tohara ya kiume.

Kutoboa sehemu za siri: Hii inahusisha kuondolewa kwa sehemu za siri, na mara nyingi pia labia minora. Ni operesheni ya kawaida na inafanywa kote Afrika, Asia, Mashariki ya Kati na Peninsula ya Arabia.

Tohara ya Mafarao: Hii ni operesheni kali zaidi, inayojumuisha uondoaji pamoja na kuondolewa kwa sehemu za siri na kushona.

Mtindo wa kipekee wa nywele (Amasunzu)

Wanaume wa Kinyarwanda waliochana mtindo wa nywele wa Amasunzu, unaoaminiwa kuanza kuchanwa karne kadhaa zilizopita.
Amasunzu ni mtindo unaojitokeza kuwa wa kipekee miongoni mwa tamaduni za Kiafrika. Mtindo huu wa nywele unaaminiwa kuwa ulianza miongoni mwa Wanyarwanda zaidi ya miaka 500 iliyopita. Ni mtindo uliopendwa na watu wa tabaka mbali mbali za kijamii nchini Rwanda na rika tofauti ulikuwa na maana tofauti.

Kwa wapiganaji uliashiria nguvu na ushujaa. Kwa wasichana wadogo ilikuwa ni alama ya ubikra. Ulikuwa ni mtindo wa hadhi kwani ni watu waliokuwa na hadhi katika jamii waliouchana. Amasunzu ni njia ya kuupendezesha mwili.

Kwa kuwa Amasunzu ni mtindo ambao unatengenezwa bila vibanio, unahitaji kutembea na kuchanuo ili kuendelea kuzichana nywele ili ziwe nadhifu wakati wote pale zinapolegea. Mti ndo huu umekua ukiendelea kutoweka kwa miongo kadhaa iliyopita, lakini umeanza kujitokeza tena hasa miongoni mwa vijana wa Kinyarwanda.

Nyota wa filamu ya Black Panther Lupita Nyong'o, katika Tuzo za Oscars 2014. alichanwa mtindo wa nywele ambao mbunifu wake wa mitindo ya nywele Vernon François alisema aliubuni kutokana na mtindo kitamaduni wa Rwanda wa karne zilizopita -Amasunzu.

Kwa kuwa Amasunzu ni mtindo ambao unatengenezwa bila vibanio, unahitaji kutembea na kuchanuo ili kuendelea kuzichana nywele ili ziwe nadhifu wakati wote pale zinapolegea. Mti ndo huu umekua ukiendelea kutoweka kwa miongo kadhaa iliyopita, lakini umeanza kujitokeza tena hasa miongoni mwa vijana wa Kinyarwanda.

Ndoa za kupangwa

Katika ndoa ya Kisomali bibi harusi huishi kwa wazazi wa mume wake baada ya kuolewa
Hadi hivi karibuni ndoa katika jamii ya Wasomali iliangaliwa kama kitu kinachounganisha sio mwanamke na mwanaume pekee bali pia familia na koo.

Hadi hivi karibuni kabisa, ndo nyingi za Kisomali zilikuwa ni za kupangwa, na kwa kawaida zilikuwa zinapangwa baina ya wazee wenye utajiri na baba wa msichana aliyetaka kumuoa. Utamaduni huu bado inaendelea kutekelezwa katika maeneo mengi ya vijijini katika karne hii ya 21.

Kwa kawaida mwanaume hulipa mahali kwa familia ya bibi harusi mtarajiwa – Wanyama hasa ngamia au pesa.

Bibi harusi Msomali huishi na familia ya mume wake baada ya kuolewa, huku wazazi wake wakimpatia nymba na vifaa vya nyumbani. Hata hivyo kuendelea kutumia ubini wa familia yake.

Mwili kuzikwa ukiketi

Katika eneo la magharibi mwa Kenya kwa kuhofia laana, kulingana na desturi za jamii ya Wabukusu wakazi wa magharibi mwa Kenya kichwa cha mfu kinafaa kuzikwa kikiangalia mbali na boma, na vitu kama viatu, shati, au tai vinafaa kulegezwa katika mwili wa marehemu.

Ili kutekeleza utamaduni huo wazee wa kabila hilo waliwafukua na kuwazika watu wao walioaga dunia kwa sababu ya Corona walipokuwa wakizikwa na maafisa wa afya.

Hatua hiyo ilichukuliwa ili kuzuia jamaa za walioaga dunia kuikaribia miili ya wapendwa wao wakati wa mazishi na hivyo maafisa wa afya ndio waliopewa jukumu la kuizika miili yao.

Wazee wa jamii hiyo walisema iwapo hilo halingefanyika inaaminika mtu aliyefariki anaweza kuitesa familia yake katika ndoto zao.

Kupiga matiti pasi

Utamaduni au mtindo wa 'kupiga matiti pasi' ili kuyazuia yasiwe makubwa umekithiri Afrika Magharibi na hasa nchini Cameroon.

Wanaotekeleza hilo hudai kwamba hatua ya kuzuia kukua kwa matiti ya wasichana wanaoanza kubaleghe huwazuia wasichana wadogo kuwavutia wanaume na hivyo basi kuepuka dhuluma za kimapenzi lakini jambo hilo limetajwa na wanaharakati kama ukiukaji wa haki za wasichana na dhuluma za kijinsia.

Jiwe hutiwa katika moto kama kaaa kisha kupitishwa juu ya matiti kwa lengo la kuyapunguza. Nchini Cameroun ambako utamaduni huo umekithiri, serikali na mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yanapambana na wovu huo ili kuzuia mateso kwa maelfu ya wasichana.

Kupiga matiti pasi ni zimwi kama utamaduni wa kuwakeketa wasichana katika baadhi ya jamii Kiafrika.
Athari za kitendo hicho kwa Jane hazitaisha hivi karibuni na zinamuathiri hadi wakati huu katika maisha yake ya utu uzima.
 
Wazungu Ni washenzi Sana,

Wamatubrain-wash waafrica tuone mwanaume kuoà wake wengi Ni dhambi na unyanyasaji wa kijinsia.

ila mwanaume kuolewa na mwanaume mwenzake Ni Haki za binadamu
 
Kwahiyo suala la Usagaji kwa Wakurya lipo kabisa kimila na katika utamaduni wao
 
Kwahiyo suala la Usagaji kwa Wakurya lipo kabisa kimila na katika utamaduni wao
Hapana..
Mara nyingi maelezo yanayotolewa ni misleading
‘’Kwa mila na desturi msichana harithi kwahiyo nimemchukua mka mwana wangu na sasa tumeishi miaka 15…tunaishi vizuri ananisaidia shamba tunaenda naye , maji ananiendea. ’’
Mka-Mwana maana yake ni mkwe, siyo mke!

Hapo inakuwa huyo mama hana mtoto wa kiume wa kuzaa ila ana mali hasa mifugo ambayo haitakuwa na mrithi, maana Ke (mabinti zake) hawarithi kwao (ila wanarithi kwa waume zao, huko walikoolewa)..

So, mama anaomba kijana wa kiume wa ndugu (especially wa shemeji yake) anachumbia na kuoa kwa niaba ya kijana wa mama (asiyekuwepo). Huyo anayeolewa anamuita mama, mama mkwe. Watoto atakaozaa wanamuita mama, bibi yao.

Sababu kubwa za kufanya hivyo ni:-
1). Kuendeleza ukoo au uzao.
2). Kupata warithi wa mali za hiyo familia.
NB: Mabinti waliozaliwa na huyo mama hawawezi kurithi mali zake, ila huyu aliyeolewa anarithi, pia watoto atakaozaa wanarithi.

Hapa nimejaribu kutoa ufafanuzi tu, siyo kwamba naunga mkono hiyo Mila.
 
Kwahiyo suala la Usagaji kwa Wakurya lipo kabisa kimila na katika utamaduni wao
Hawasagani, bsli mke alioa humtafuta mwanamme, anaweza kuwa ndugu wa mwanamke muoaji, au asiwe ndugu, huyo mwanamme kazi yake ni kumuingilia huyu aliye olewa akipata mimba, akazaa watoto huwa mama muoaji.
 
Back
Top Bottom