Ushauri kwa waislamu Tanzania, hasa walio mtandaoni

Hapo jibu la moya kwa moya kama litajaniwia gumu au!?

Lakini yule Mzanaki angelitufaa /kufaa mno kwa kukugeiya majawaba...! Ila ndo keshatukwepa na ati FIKARA zake ndo hawa ma-ghost waziendeleza, daah!

Kazi nakuwatia weye sasa, popote tapomuona yeyote awaye, mwenye kumkubali yule Mzanaki Nyerere papo kwa hapo ulizo hilo lisukugeiye tabu, mgeiye hapo huenda ukafahamu uzuri.

Shukraan nami naendelea watafuta wamfahamuyo hoyo bwana Nyerere ili wanisaidie sababu za kwa nini kuwaondoshea Waislaamu wapenzi /wakarimu walompokea bila ya ajizi wala uwizi, kuwabadalishia ile EAMWS na kuwatwika Umalouni hunu tuuonao hapa na kutuekea kitahanani hiki cha "BAKWATA" ....!?

Menifahamu uzuri au mekuwata pahala ...!?

Mekufahamu vizuri mkuu...

Amani iwe nawe.
 
WanaJF,
Nimefikiria muda mrefu kuhusu sakata hili la kufa na kupona la mahakama ya kadhi. Ni wazi kuwa mahakama ni muhimu katika jamii. Lakini pamoja na umuhimu wake, nadhani tukikaa chini na kutafakari, kuna mengi ya umuhimu zaidi. Jambo la kwanza kwa Nchi kama Tanzania ambayo kwaajili ya uongozi mbovu wa waliokuwa madarakani kwa nyakati tofauti lingepaswa kupewa kipaumbele ni Elimu. Ona jinsi Elimu inavyochezeshwa gwaride, hadi tumefikia hatua ya kuweka div. 5, ili kuficha waliofeli.

Nirudi kwenye mada,
Nasema ushauri kwa waislamu kuwa waongeze nguvu kwenye elimu dunia. Waongeze shule zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu, zenye ubora. Waongeze vyuo vikuu vinavyoendeshwa na taasisi za kiislamu, wakitaka wawapokee waislamu tu haidhuru, lakini ni bora wakawapokea wote kama zifanyazo taasisi za kikristu. Elimu bora Tanzania inahitajika. Na Elimu bora Tanzania haiwezi kutolewa na Serikali tu. Ona madhehebu ya kikristo walivyoweka kipaumbele katika elimu. Hesabu tu vyuo vikuu vinavyoendeshwa na madhehebu ya kikristo. Hesabu shule za sekondari zenye ubora wa hali ya juu zinazoendeshwa na taasisi za kikristo. Sijui taasisi za kiislam zinaendesha vyuo vikuu vingapi, lakini nafahamu walau moja ile ya Morogoro, iliyokuwa chuo cha Tanesco, ambayo walipewa na serikali ili kuwatuliza.

Tazama kwenye afya, ona ni vituo vingapi vya afya, hospitali, hadi hospitali za rufaa zinazoendeshwa na taasisi za dini? Nafahamu walau hospitali ya rufaa ya KCMC na Bugando zinaendeshwa na taasisi za kikristo. Hospitali za kawaida ni nyingi. Zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu sizifahamu, zinaweza kuwa nyingi kuliko hizo, au la. Kwenye suala la afya ndipo pa kutumia nguvu nyingi. Huko ndipo pa kuwa na hitaji la kuweka kambi Bungeni kama kutakuwa na haja.

Nadhani sio vizuri kusubiri siku zote kubebwa na serikali. Kila madhehebu wana sheria zao, sheria zao ambazo hazipaswi kwenda kinyume na sheria za Nchi. Sioni sababu ya kutumia nguvu kubwa kudai mahakama badala ya kuwekeza kwenye mambo ya maandeleo kama elimu, afya, nk. Kwanini tunadhani maisha yetu lazima kupelekana mahakamani?

Ndiyo maana nasema natoa ushauri kwa waislamu hasa waJF maana ndo watakaosoma ushauri huu, Waislamu wawekeze nguvu nyingi kwenye mambo ya maendeleo zaidi kuliko mahakama. Wawekeze kwenye elimu na afya. Achaneni mambo ya mahakama. Mahakama ya nchi inaweza kumaliza yote, ikiwa kutakuwa na haja. Lakini kwa mtu optimistic hawezi kutumia nguvu nyingi kwenye hilo.

Sio haki kwa wabunge: wawakilishi wa wananchi kupoteza muda kujadili kuwa waislamu wawe na mahakama ya kadhi au la. Ni wazi watajadili, hasa wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Ili kila mchangiaji aonekane anawajali waislamu, ataunga mkono mahakama ya kadhi, watafanya funika kombe mwanaharamu apite. Ili tu waislamu wa jimbo lake wasimtose, ili tu waislamu wasikikatae chama chake. Lakini nasema tena sio haki wabunge wapoteze muda katika jambo hili ambalo sio kipaumbele cha taifa. Sio haki lakini litajadiliwa kwaajili wa woga wa kupoteza kura.

Mniwie radhi, kama kuna moja hatapendezwa na ushauri wangu. Ukweli utabaki kuwa kuwekeza kwenye elimu, hasa elimu dunia na afya ni bora kuliko kuwekeza kwenye mahakama.

Umeongea kwa utulivu mkubwa,ila umewadhihaki sana waislamu bila kujua kuwa
1.Waislamu waliahidiwa na CCM hiyo mahakama ya kadhi,na kwahiyo sio kosa waislamu wakiifatilia ahadi waliyopewa.
2.Hukutoa sababu za waislamu kutokua na hizo hospitali za rufaa na mashule mazuri.
3.Hukutaka kufikiri kwanini waislamu walibebwa kwa kupewa eneo la Tanesco ili wajenge chuo cha kiislamu.
4.Hukutaka kutafakari ni kwanini nchi moja ila watu wake wana matabaka,wengine wana Elimu sana,lakini wengine hawana elimu sana.
NB:Sisi wananchi tulipaswa kuungana na kuilaumu CCM,tena nashauri CCM ingeshitakiwa na kutozwa faini juu ya hii ahadi ambayo inavunja katiba ya nchi.Haya mambo ni ya ku-neutralize,tusijenge matabaka na kujengeana chuki.Tuliokoe Taifa letu kwanza badala ya kuleta majigambo na mbwembwe za nani zaidi.
 
WanaJF,
Nimefikiria muda mrefu kuhusu sakata hili la kufa na kupona la mahakama ya kadhi. Ni wazi kuwa mahakama ni muhimu katika jamii. Lakini pamoja na umuhimu wake, nadhani tukikaa chini na kutafakari, kuna mengi ya umuhimu zaidi. Jambo la kwanza kwa Nchi kama Tanzania ambayo kwaajili ya uongozi mbovu wa waliokuwa madarakani kwa nyakati tofauti lingepaswa kupewa kipaumbele ni Elimu. Ona jinsi Elimu inavyochezeshwa gwaride, hadi tumefikia hatua ya kuweka div. 5, ili kuficha waliofeli.

Nirudi kwenye mada,
Nasema ushauri kwa waislamu kuwa waongeze nguvu kwenye elimu dunia. Waongeze shule zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu, zenye ubora. Waongeze vyuo vikuu vinavyoendeshwa na taasisi za kiislamu, wakitaka wawapokee waislamu tu haidhuru, lakini ni bora wakawapokea wote kama zifanyazo taasisi za kikristu. Elimu bora Tanzania inahitajika. Na Elimu bora Tanzania haiwezi kutolewa na Serikali tu. Ona madhehebu ya kikristo walivyoweka kipaumbele katika elimu. Hesabu tu vyuo vikuu vinavyoendeshwa na madhehebu ya kikristo. Hesabu shule za sekondari zenye ubora wa hali ya juu zinazoendeshwa na taasisi za kikristo. Sijui taasisi za kiislam zinaendesha vyuo vikuu vingapi, lakini nafahamu walau moja ile ya Morogoro, iliyokuwa chuo cha Tanesco, ambayo walipewa na serikali ili kuwatuliza.

Tazama kwenye afya, ona ni vituo vingapi vya afya, hospitali, hadi hospitali za rufaa zinazoendeshwa na taasisi za dini? Nafahamu walau hospitali ya rufaa ya KCMC na Bugando zinaendeshwa na taasisi za kikristo. Hospitali za kawaida ni nyingi. Zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu sizifahamu, zinaweza kuwa nyingi kuliko hizo, au la. Kwenye suala la afya ndipo pa kutumia nguvu nyingi. Huko ndipo pa kuwa na hitaji la kuweka kambi Bungeni kama kutakuwa na haja.

Nadhani sio vizuri kusubiri siku zote kubebwa na serikali. Kila madhehebu wana sheria zao, sheria zao ambazo hazipaswi kwenda kinyume na sheria za Nchi. Sioni sababu ya kutumia nguvu kubwa kudai mahakama badala ya kuwekeza kwenye mambo ya maandeleo kama elimu, afya, nk. Kwanini tunadhani maisha yetu lazima kupelekana mahakamani?

Ndiyo maana nasema natoa ushauri kwa waislamu hasa waJF maana ndo watakaosoma ushauri huu, Waislamu wawekeze nguvu nyingi kwenye mambo ya maendeleo zaidi kuliko mahakama. Wawekeze kwenye elimu na afya. Achaneni mambo ya mahakama. Mahakama ya nchi inaweza kumaliza yote, ikiwa kutakuwa na haja. Lakini kwa mtu optimistic hawezi kutumia nguvu nyingi kwenye hilo.

Sio haki kwa wabunge: wawakilishi wa wananchi kupoteza muda kujadili kuwa waislamu wawe na mahakama ya kadhi au la. Ni wazi watajadili, hasa wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Ili kila mchangiaji aonekane anawajali waislamu, ataunga mkono mahakama ya kadhi, watafanya funika kombe mwanaharamu apite. Ili tu waislamu wa jimbo lake wasimtose, ili tu waislamu wasikikatae chama chake. Lakini nasema tena sio haki wabunge wapoteze muda katika jambo hili ambalo sio kipaumbele cha taifa. Sio haki lakini litajadiliwa kwaajili wa woga wa kupoteza kura.

Mniwie radhi, kama kuna moja hatapendezwa na ushauri wangu. Ukweli utabaki kuwa kuwekeza kwenye elimu, hasa elimu dunia na afya ni bora kuliko kuwekeza kwenye mahakama.

Canon law imesimama, mfano, inasema wazi pale ambapo itapingina na secular/ civil law ya nchi husika basi ile ya ile nchi ita-prevail; lakini ni ngumu sana kwani inasimamia haki haswa na mara nyingi mambo yanaishia kwa Paroko, Askofu, issue nzito kwa Papa!!!
 
mtoa mada umekosa kazi, yaan kumuelimisha muislamu ni kazi sn hii mijamaa ni mibishi utadhani inajua kitu kumbe hamna lolote!

Plz msije mkanichoma nikiwa hai. R.I.P RUBANI.
 
Kuna fisadi kama Nyerere alishirikiana na Kanisa kufanya ufisadi.
Nyerere aliiba hela ngapi BOT na kuanzisha benki yake mwenyewe kama alivyofanya Idrissa? Unatetea mafisadi kwa sababu mnakula wote? Siku zenu zaja.
 
Patience96,
Ninaposoma maswali kama haya ndipo ninapozidi kuamini kuwa watu wetu
wengi sana hawana ujuzi wa mambo haya na kuna umuhimu mkubwa sana
wa kuelimishana.

Tatizo hili si la kuondolewa kama unavyoondoa kitu juu ya meza.
Wala si tatizo la Rais aliye madarakani kulishughulikia.

Hili ni tatizo sawa na lile la Rwanda ambako kuna jamii ya Watusi mabwana
na Wahutu watwana.

Limeshahabiana sana.
Tatizo hili litaondoka kwa sisi wenyewe kwanza kukubali kuwa lipo tatizo.

Hapa kwetu bado hatujafika hatua hiyo.

Waislam wametembea nchi nzima wakifanya mikutano kutahadharisha
kuhusu Mfumokristo.

Serikali imekuwa kimya.

Waislam wameandamana kuhusu Ndalichako na NECTA wakilalamika kuwa
Baraza la Mitihani Tanzania linahujumu wanafunzi wa Kiislam na upo ushahidi.

Serikali imekuwa kimya.
BAKWATA ipo lakini matatizo yote haya ya Waislam...

BAKWATA iko kimya kama ilivyokuwa kimya serikali.
Mfumokristo hauwezi kufanya kazi kama BAKWATA itakuwa haipo.
Mohamed,
Unaweza kutuambia ni kwa nini kiwango cha elimu nchini Tanzania chini ya rais muislamu na ndugu yake muislamu pale wizara ya elimu kimekuwa kinashuka mwaka hadi mwaka? Labda tuanzie hapo.
 
Mkuu huyu msomi aliyevaa msalaba shingoni huku anakunywa bia ni nani.

3.JPG
Dini yetu haikatazi kunywa pombe. Hata Yesu alikunywa wine na kula mkate wa kuoka.
 
Unapong`ang`ania kupewa mahakama unataka tujifunze nini kutoka kwako. Je, unataka tufikir kuwa wewe ni mtenda makosa sana kiasi kwamba unataka ujiwekee mahali pa kuhukumiwa? Je, unataka tufikir kuwa wewe ni mtu usiye na msamaha kiasi kwamba unataka kuwaandalia wenzako mahali pa kuwashtaki? Nini maana ya kutaka mahakama ya kumshtaki mkeo? Je, ni kutaka kutuonesha kuwa humpendi au ulimwoa kwa bahati mbaya? Think twice guys
 
Ukana Shilungo,
Mimi nilidhani umesema Ponda ni Mrundi kwa kutojua ndiyo maana nikakusahihisha.

Una haki ya kuamini unachopenda.
 
Halafu nyie Wakirsto ndiyo mnabebwa unajua kama kila mwaka Kanisa linapewa bilioni 61.9.

Ahsante.

Hebu nami nijuze mkuu. Hawa wakristu wanapewa pesa hizo ktk sekta gani? Isije ukawa unasema juu ya hospitali kama Bugando, KCMC, na zingine zinazoitwa DDH. Huko wote hata waislamu tunakwenda kutibiwa. Hakuna ubaguzi. Lakini hili la kadhi, NO! Ni kutafuta maneno.
 
Nyerere aliiba hela ngapi BOT na kuanzisha benki yake mwenyewe kama alivyofanya Idrissa? Unatetea mafisadi kwa sababu mnakula wote? Siku zenu zaja.
Ndiyo maana nakuambia unapenda kuikota maneno mitaani tufahimishe Idrissa anamiliki benki gani na hana hisa ngapi.

Unajua wakati wa Nyerere kwa nini BOT ilichomwa moto, Nyerere aliwauzia wazungu mgodi wa Mwadui.
 
Hebu nami nijuze mkuu. Hawa wakristu wanapewa pesa hizo ktk sekta gani? Isije ukawa unasema juu ya hospitali kama Bugando, KCMC, na zingine zinazoitwa DDH. Huko wote hata waislamu tunakwenda kutibiwa. Hakuna ubaguzi. Lakini hili la kadhi, NO! Ni kutafuta maneno.
Wanatibiwa bure?
 
Back
Top Bottom