Ushauri kwa waislamu Tanzania, hasa walio mtandaoni

Dopas

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2010
Posts
1,151
Reaction score
392
WanaJF,
Nimefikiria muda mrefu kuhusu sakata hili la kufa na kupona la mahakama ya kadhi. Ni wazi kuwa mahakama ni muhimu katika jamii. Lakini pamoja na umuhimu wake, nadhani tukikaa chini na kutafakari, kuna mengi ya umuhimu zaidi. Jambo la kwanza kwa Nchi kama Tanzania ambayo kwaajili ya uongozi mbovu wa waliokuwa madarakani kwa nyakati tofauti lingepaswa kupewa kipaumbele ni Elimu. Ona jinsi Elimu inavyochezeshwa gwaride, hadi tumefikia hatua ya kuweka div. 5, ili kuficha waliofeli.

Nirudi kwenye mada,
Nasema ushauri kwa waislamu kuwa waongeze nguvu kwenye elimu dunia. Waongeze shule zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu, zenye ubora. Waongeze vyuo vikuu vinavyoendeshwa na taasisi za kiislamu, wakitaka wawapokee waislamu tu haidhuru, lakini ni bora wakawapokea wote kama zifanyazo taasisi za kikristu. Elimu bora Tanzania inahitajika. Na Elimu bora Tanzania haiwezi kutolewa na Serikali tu. Ona madhehebu ya kikristo walivyoweka kipaumbele katika elimu. Hesabu tu vyuo vikuu vinavyoendeshwa na madhehebu ya kikristo. Hesabu shule za sekondari zenye ubora wa hali ya juu zinazoendeshwa na taasisi za kikristo. Sijui taasisi za kiislam zinaendesha vyuo vikuu vingapi, lakini nafahamu walau moja ile ya Morogoro, iliyokuwa chuo cha Tanesco, ambayo walipewa na serikali ili kuwatuliza.

Tazama kwenye afya, ona ni vituo vingapi vya afya, hospitali, hadi hospitali za rufaa zinazoendeshwa na taasisi za dini? Nafahamu walau hospitali ya rufaa ya KCMC na Bugando zinaendeshwa na taasisi za kikristo. Hospitali za kawaida ni nyingi. Zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu sizifahamu, zinaweza kuwa nyingi kuliko hizo, au la. Kwenye suala la afya ndipo pa kutumia nguvu nyingi. Huko ndipo pa kuwa na hitaji la kuweka kambi Bungeni kama kutakuwa na haja.

Nadhani sio vizuri kusubiri siku zote kubebwa na serikali. Kila madhehebu wana sheria zao, sheria zao ambazo hazipaswi kwenda kinyume na sheria za Nchi. Sioni sababu ya kutumia nguvu kubwa kudai mahakama badala ya kuwekeza kwenye mambo ya maandeleo kama elimu, afya, nk. Kwanini tunadhani maisha yetu lazima kupelekana mahakamani?

Ndiyo maana nasema natoa ushauri kwa waislamu hasa waJF maana ndo watakaosoma ushauri huu, Waislamu wawekeze nguvu nyingi kwenye mambo ya maendeleo zaidi kuliko mahakama. Wawekeze kwenye elimu na afya. Achaneni mambo ya mahakama. Mahakama ya nchi inaweza kumaliza yote, ikiwa kutakuwa na haja. Lakini kwa mtu optimistic hawezi kutumia nguvu nyingi kwenye hilo.

Sio haki kwa wabunge: wawakilishi wa wananchi kupoteza muda kujadili kuwa waislamu wawe na mahakama ya kadhi au la. Ni wazi watajadili, hasa wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Ili kila mchangiaji aonekane anawajali waislamu, ataunga mkono mahakama ya kadhi, watafanya funika kombe mwanaharamu apite. Ili tu waislamu wa jimbo lake wasimtose, ili tu waislamu wasikikatae chama chake. Lakini nasema tena sio haki wabunge wapoteze muda katika jambo hili ambalo sio kipaumbele cha taifa. Sio haki lakini litajadiliwa kwaajili wa woga wa kupoteza kura.

Mniwie radhi, kama kuna moja hatapendezwa na ushauri wangu. Ukweli utabaki kuwa kuwekeza kwenye elimu, hasa elimu dunia na afya ni bora kuliko kuwekeza kwenye mahakama.
 
Wakitumia neno la kuudhi dhidi yangu, wala sio tatizo, hata wakinitukana. Ila ukweli utabaki huu, na ukweli huu utawasuta siku za usoni.
 
Ni kweli kabisa ndugu dopas mana suala la elimu na afya ni muhimu saa katika maisha ya mwanadamu ila sijaelewa kitu kimoja pale unaposema waislamu waongeze nguvu kwenye elimu dunia unakua na mana gani?
 
Nina maana ya kuwa elimu itakayomfaa mtu yeyote bila kujali dini, au hata kama hana dini. Elimu dunia ni elimu inayotolewa na shule zote. Kinyume chake labda ingekuwa elimu ahera, ile inayokazia madrasa tu- Qura'an, biblia tu n.k.,
 
kwahiyo wewe hapo ndo una elimu dunia sana au?
 
WanaJF,
Nimefikiria muda mrefu kuhusu sakata hili la kufa na kupona la mahakama ya kadhi. Ni wazi kuwa mahakama ni muhimu katika jamii. Lakini pamoja na umuhimu wake, nadhani tukikaa chini na kutafakari, kuna mengi ya umuhimu zaidi. Jambo la kwanza kwa Nchi kama Tanzania ambayo kwaajili ya uongozi mbovu wa waliokuwa madarakani kwa nyakati tofauti lingepaswa kupewa kipaumbele ni Elimu. Ona jinsi Elimu inavyochezeshwa gwaride, hadi tumefikia hatua ya kuweka div. 5, ili kuficha waliofeli.

Nirudi kwenye mada,
Nasema ushauri kwa waislamu kuwa waongeze nguvu kwenye elimu dunia. Waongeze shule zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu, zenye ubora. Waongeze vyuo vikuu vinavyoendeshwa na taasisi za kiislamu, wakitaka wawapokee waislamu tu haidhuru, lakini ni bora wakawapokea wote kama zifanyazo taasisi za kikristu. Elimu bora Tanzania inahitajika. Na Elimu bora Tanzania haiwezi kutolewa na Serikali tu. Ona madhehebu ya kikristo walivyoweka kipaumbele katika elimu. Hesabu tu vyuo vikuu vinavyoendeshwa na madhehebu ya kikristo. Hesabu shule za sekondari zenye ubora wa hali ya juu zinazoendeshwa na taasisi za kikristo. Sijui taasisi za kiislam zinaendesha vyuo vikuu vingapi, lakini nafahamu walau moja ile ya Morogoro, iliyokuwa chuo cha Tanesco, ambayo walipewa na serikali ili kuwatuliza.

Tazama kwenye afya, ona ni vituo vingapi vya afya, hospitali, hadi hospitali za rufaa zinazoendeshwa na taasisi za dini? Nafahamu walau hospitali ya rufaa ya KCMC na Bugando zinaendeshwa na taasisi za kikristo. Hospitali za kawaida ni nyingi. Zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu sizifahamu, zinaweza kuwa nyingi kuliko hizo, au la. Kwenye suala la afya ndipo pa kutumia nguvu nyingi. Huko ndipo pa kuwa na hitaji la kuweka kambi Bungeni kama kutakuwa na haja.

Nadhani sio vizuri kusubiri siku zote kubebwa na serikali. Kila madhehebu wana sheria zao, sheria zao ambazo hazipaswi kwenda kinyume na sheria za Nchi. Sioni sababu ya kutumia nguvu kubwa kudai mahakama badala ya kuwekeza kwenye mambo ya maandeleo kama elimu, afya, nk. Kwanini tunadhani maisha yetu lazima kupelekana mahakamani?

Ndiyo maana nasema natoa ushauri kwa waislamu hasa waJF maana ndo watakaosoma ushauri huu, Waislamu wawekeze nguvu nyingi kwenye mambo ya maendeleo zaidi kuliko mahakama. Wawekeze kwenye elimu na afya. Achaneni mambo ya mahakama. Mahakama ya nchi inaweza kumaliza yote, ikiwa kutakuwa na haja. Lakini kwa mtu optimistic hawezi kutumia nguvu nyingi kwenye hilo.

Sio haki kwa wabunge: wawakilishi wa wananchi kupoteza muda kujadili kuwa waislamu wawe na mahakama ya kadhi au la. Ni wazi watajadili, hasa wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Ili kila mchangiaji aonekane anawajali waislamu, ataunga mkono mahakama ya kadhi, watafanya funika kombe mwanaharamu apite. Ili tu waislamu wa jimbo lake wasimtose, ili tu waislamu wasikikatae chama chake. Lakini nasema tena sio haki wabunge wapoteze muda katika jambo hili ambalo sio kipaumbele cha taifa. Sio haki lakini litajadiliwa kwaajili wa woga wa kupoteza kura.

Mniwie radhi, kama kuna moja hatapendezwa na ushauri wangu. Ukweli utabaki kuwa kuwekeza kwenye elimu, hasa elimu dunia na afya ni bora kuliko kuwekeza kwenye mahakama.
Na mimi kama Muislam nakushauri huu ushauri wako upeleke Kanisani.

Kawaambie hivi toka toka uhuru mpaka sasa wasomi wa Kikirsto wamejazana serikali kila idara wamelisaidiaje taifa letu kutoka kwenye nchi masikini duniani, unajua kuwa Tanzani ipo kwenye nchi 20 masikini wa kutupwa duniani huko serikalini kazi yenu kufanya ufisadi tu.

Halafu nyie Wakirsto ndiyo mnabebwa unajua kama kila mwaka Kanisa linapewa bilioni 61.9.

Ahsante.
 
Nasema tu usiridhike na elimu ya madrasa, ambayo haitakusaidia sana kama mwanadamu anayeishi dunia hii. Elimu ahera ina umuhimu wake, kwani sisi sote ni waja wa mwenyezi Mungu. Lakini kama inakufanya ugeuke kuwa alkaida, boko haram, al shabab, nk, wakati hata hujui unachodai, haina maana. Ni kuulize swali. Nini madai ya makundi haya ya kiislam yenye siasa kali? yanayochinja wakristo kila kukicha? Labda huwezi kujibu swali hilo. Lakini nasema tena haitoshi kuanzisha na kuridhika na shule au hata chuo kikuu kwa ajili ya kufundisha elimu ahera tu. Elimu dunia ni yote kwa mwanadamu.
Tazama mfano wa wakristo kuna shule ngapi Tanzania zinazofundisha elimu yote: Elimu dunia na elimu ahera.
 
kimtu kinajifanya eti chenyewe kina elimu dunia kubwa sanaa kiasi cha kudhani eti nacho ki consultant,
haya hebu tuone hiyo elimu dunia yako,usikute una diploma ya housekeeping
 
WanaJF,
Nimefikiria muda mrefu kuhusu sakata hili la kufa na kupona la mahakama ya kadhi. Ni wazi kuwa mahakama ni muhimu katika jamii. Lakini pamoja na umuhimu wake, nadhani tukikaa chini na kutafakari, kuna mengi ya umuhimu zaidi. Jambo la kwanza kwa Nchi kama Tanzania ambayo kwaajili ya uongozi mbovu wa waliokuwa madarakani kwa nyakati tofauti lingepaswa kupewa kipaumbele ni Elimu. Ona jinsi Elimu inavyochezeshwa gwaride, hadi tumefikia hatua ya kuweka div. 5, ili kuficha waliofeli.

Nirudi kwenye mada,
Nasema ushauri kwa waislamu kuwa waongeze nguvu kwenye elimu dunia. Waongeze shule zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu, zenye ubora. Waongeze vyuo vikuu vinavyoendeshwa na taasisi za kiislamu, wakitaka wawapokee waislamu tu haidhuru, lakini ni bora wakawapokea wote kama zifanyazo taasisi za kikristu. Elimu bora Tanzania inahitajika. Na Elimu bora Tanzania haiwezi kutolewa na Serikali tu. Ona madhehebu ya kikristo walivyoweka kipaumbele katika elimu. Hesabu tu vyuo vikuu vinavyoendeshwa na madhehebu ya kikristo. Hesabu shule za sekondari zenye ubora wa hali ya juu zinazoendeshwa na taasisi za kikristo. Sijui taasisi za kiislam zinaendesha vyuo vikuu vingapi, lakini nafahamu walau moja ile ya Morogoro, iliyokuwa chuo cha Tanesco, ambayo walipewa na serikali ili kuwatuliza.

Tazama kwenye afya, ona ni vituo vingapi vya afya, hospitali, hadi hospitali za rufaa zinazoendeshwa na taasisi za dini? Nafahamu walau hospitali ya rufaa ya KCMC na Bugando zinaendeshwa na taasisi za kikristo. Hospitali za kawaida ni nyingi. Zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu sizifahamu, zinaweza kuwa nyingi kuliko hizo, au la. Kwenye suala la afya ndipo pa kutumia nguvu nyingi. Huko ndipo pa kuwa na hitaji la kuweka kambi Bungeni kama kutakuwa na haja.

Nadhani sio vizuri kusubiri siku zote kubebwa na serikali. Kila madhehebu wana sheria zao, sheria zao ambazo hazipaswi kwenda kinyume na sheria za Nchi. Sioni sababu ya kutumia nguvu kubwa kudai mahakama badala ya kuwekeza kwenye mambo ya maandeleo kama elimu, afya, nk. Kwanini tunadhani maisha yetu lazima kupelekana mahakamani?

Ndiyo maana nasema natoa ushauri kwa waislamu hasa waJF maana ndo watakaosoma ushauri huu, Waislamu wawekeze nguvu nyingi kwenye mambo ya maendeleo zaidi kuliko mahakama. Wawekeze kwenye elimu na afya. Achaneni mambo ya mahakama. Mahakama ya nchi inaweza kumaliza yote, ikiwa kutakuwa na haja. Lakini kwa mtu optimistic hawezi kutumia nguvu nyingi kwenye hilo.

Sio haki kwa wabunge: wawakilishi wa wananchi kupoteza muda kujadili kuwa waislamu wawe na mahakama ya kadhi au la. Ni wazi watajadili, hasa wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Ili kila mchangiaji aonekane anawajali waislamu, ataunga mkono mahakama ya kadhi, watafanya funika kombe mwanaharamu apite. Ili tu waislamu wa jimbo lake wasimtose, ili tu waislamu wasikikatae chama chake. Lakini nasema tena sio haki wabunge wapoteze muda katika jambo hili ambalo sio kipaumbele cha taifa. Sio haki lakini litajadiliwa kwaajili wa woga wa kupoteza kura.

Mniwie radhi, kama kuna moja hatapendezwa na ushauri wangu. Ukweli utabaki kuwa kuwekeza kwenye elimu, hasa elimu dunia na afya ni bora kuliko kuwekeza kwenye mahakama.

Hongera sana mkuu endelea kuwashauri waelimike hawa jamaa!wakati taifa likihitaji shule nyingi na vyuo vikuu nyie mnadai kadhi???
 
Na mimi kama Muislam nakushauri huu ushauri wako upeleke Kanisani.

Kawaambie hivi toka toka uhuru mpaka sasa wasomi wa Kikirsto wamejazana serikali kila idara wamelisaidiaje taifa letu kutoka kwenye nchi masikini duniani, unajua kuwa Tanzani ipo kwenye nchi 20 masikini wa kutupwa duniani huko serikalini kazi yenu kufanya ufisadi tu.

Halafu nyie Wakirsto ndiyo mnabebwa unajua kama kila mwaka Kanisa linapewa bilioni 61.9.

Ahsante.
Kama sio wakristo hata hao waislamu wachache wasingesoma. Ni waislamu wangapi wamesoma shule za kikristo ambao sasa wapo madarakani. Nakushangaa hii karne ya 21 unadai mahakama ya kwenda kumshitaki mke wako, au kudai mali alizoacha marehemu, badala ya kufikiria namna ya kuboresha mahusiano katika familia (ndoa) na pia namna ya kujitegemea kiuchumi, kujitafutia kwa jasho lako kuliko kutegemea mirathi.

Hapa ndipo ninaposema kuna ya haja kuwekeza kwenye elimu itakayomwezesha mtu utambuzi huu. Elimu itakayomfanya mtu awe optimistic, sio kufikiria tu kesi za kupelekana mahakamani, ambazo pengine zinaweza zisitokee hadi kufa. Ona sasa wakereketwa wote mmejazana Dodoma kushinikizwa tu hiyo hoja ijadiliwe.

Wewe Ritz kwa akili yako unaona hiyo ni kipaumbele kuliko kuwekeza kwenye vipaumbele vya kitaifa kama elimu na afya?
 
Na mimi kama Muislam nakushauri huu ushauri wako upeleke Kanisani.

Kawaambie hivi toka toka uhuru mpaka sasa wasomi wa Kikirsto wamejazana serikali kila idara wamelisaidiaje taifa letu kutoka kwenye nchi masikini duniani, unajua kuwa Tanzani ipo kwenye nchi 20 masikini wa kutupwa duniani huko serikalini kazi yenu kufanya ufisadi tu.

Halafu nyie Wakirsto ndiyo mnabebwa unajua kama kila mwaka Kanisa linapewa bilioni 61.9.

Ahsante.

Nimecheka sana post ya Mtu hapo juu aliyefananisha Na mnyama flani wa kufuga.. Lakini Kwa post kama hizi naanza kuamini kuna kila dalili Za kufanana Na mnyama huyo..!

Ati "..wasomi wa kikristu wamejazana kila idara serikalini .. " nadhani kuna tatizo Kama sio akili basi mawazo yaliyotoboka..! Watu mmawaza negative tu all time kuhukumiwa sio Kusoma, matibabu, Afya ,Maji , Umeme noo hiyo si inshu Bali kuhukumiana , kukomeshana, kurithiana Na kutalikiana Na kulogana basi.. Mengine sio Hoja kwenu..
 
kimtu kinajifanya eti chenyewe kina elimu dunia kubwa sanaa kiasi cha kudhani eti nacho ki consultant,
haya hebu tuone hiyo elimu dunia yako,usikute una diploma ya housekeeping
Huwezi kuacha kutafuta elimu kwa sababu tu mwenzio hana. Haya mi kama sina wewe ndiyo usiitafute.

Kumbuka nimezungumzia taasisi za kidini na sio mimi na wewe. Uwezo wako wa kujadili hoja inaonesha tu elimu uliyopata. Badala ya kujibu hoja au kukaa kimya kama huna jibu, unahama hoja kwa kutaka kujustify ujinga
 
Back
Top Bottom