Ushauri kwa waislamu Tanzania, hasa walio mtandaoni

Ushauri kwa waislamu Tanzania, hasa walio mtandaoni

marais wa kwanza waliokomboa nchi za afrika.julias nyerere tanzania,mkristo.jomo kenyata kenya,mkristo.milton obote uganda mkristo. keneth kaunda zambia mkristo.samora michael msumbiji mkristo.kwame nkuruma ghana mkristo.nelson mandela SA mkristo.Azikiwe Nigeria mkristo. robert mgabe zimbabwe mkristo.melkiolondadae burundi mkristo.patric lumumba DRC mkristo.liberia,rwanda,afrika ya kati,senegal,buknabe kote uko marais wa kwanza ni wakristo?uko nako vp?uislam unaonewa?mbona mnanongwa na nyerere alisoma akaja akatake over waislam walikua wanavua samaki fell muachen mzee wa watu apumzike
 
Tatizo la waislamu TZ ni waislamu wenyewe yaani BAKWATA inawageuka watu iliopaswa kusimamia maslahi yao...
Maslahi yepi imeshindwa kuyasimamia? na imewageuka vipi waislamu?
 
Rais wa tanzania ni muislamu, makamu wa rais muislamu, rais wa zanzibar muislamu, makamu wa kwanza na wa pili ni muislamu, wazir wa ulinzi muislamu, waziri wa fedha muislamu, waziri wa elimu muislamu. Bado mnalalamika tu? Kweli magaidi ni magaidi tu.

Hau uliowataja hapo wote ni viongozi wa kisiasa ambao hawaitaji usomi kuongoza kwa mujibu wa katibu, nenda sasa kwenye nyadhifa za kitaalamu kama wakurugenzi, makatibu wakuu etc, ndo utaelewa naongea nini we KAFIR
 
Wanatibiwa bure?

Kwani ulitaka kwa kuwa serikali inaweka pesa zake, basi watibiwe bure? Hiyo hospitali gani ya serikali watu wanatibiwa bure. I now can see your nonsense arguments you are trying to make.

Kuna mtu mbaya lakini ukikosa tusi kwake nyamaza tu. Hakuna point hapo unajaribu kuonyesha hasira zako na umekosa la kufanya. Matatizo ya usilamu yanatokana na uislamu na solution itatokana na uislamu. usitafute solution serikalini. That will be another rubbish.
 
Maslahi yepi imeshindwa kuyasimamia? na imewageuka vipi waislamu?

Mfano ktk suala la mahakama ya kadhi wakati wenzao wakipigia chapuo ipatikane wao wanapiga kumbo ikosekane...

Wanapinga mahakama hizi kusimamiwa au kuendeshwa na serikali.

Yapo mengi hilo ni miongoni mwao.
 
WanaJF,
Nimefikiria muda mrefu kuhusu sakata hili la kufa na kupona la mahakama ya kadhi. Ni wazi kuwa mahakama ni muhimu katika jamii. Lakini pamoja na umuhimu wake, nadhani tukikaa chini na kutafakari, kuna mengi ya umuhimu zaidi. Jambo la kwanza kwa Nchi kama Tanzania ambayo kwaajili ya uongozi mbovu wa waliokuwa madarakani kwa nyakati tofauti lingepaswa kupewa kipaumbele ni Elimu. Ona jinsi Elimu inavyochezeshwa gwaride, hadi tumefikia hatua ya kuweka div. 5, ili kuficha waliofeli.

Nirudi kwenye mada,
Nasema ushauri kwa waislamu kuwa waongeze nguvu kwenye elimu dunia. Waongeze shule zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu, zenye ubora. Waongeze vyuo vikuu vinavyoendeshwa na taasisi za kiislamu, wakitaka wawapokee waislamu tu haidhuru, lakini ni bora wakawapokea wote kama zifanyazo taasisi za kikristu. Elimu bora Tanzania inahitajika. Na Elimu bora Tanzania haiwezi kutolewa na Serikali tu. Ona madhehebu ya kikristo walivyoweka kipaumbele katika elimu. Hesabu tu vyuo vikuu vinavyoendeshwa na madhehebu ya kikristo. Hesabu shule za sekondari zenye ubora wa hali ya juu zinazoendeshwa na taasisi za kikristo. Sijui taasisi za kiislam zinaendesha vyuo vikuu vingapi, lakini nafahamu walau moja ile ya Morogoro, iliyokuwa chuo cha Tanesco, ambayo walipewa na serikali ili kuwatuliza.

Tazama kwenye afya, ona ni vituo vingapi vya afya, hospitali, hadi hospitali za rufaa zinazoendeshwa na taasisi za dini? Nafahamu walau hospitali ya rufaa ya KCMC na Bugando zinaendeshwa na taasisi za kikristo. Hospitali za kawaida ni nyingi. Zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu sizifahamu, zinaweza kuwa nyingi kuliko hizo, au la. Kwenye suala la afya ndipo pa kutumia nguvu nyingi. Huko ndipo pa kuwa na hitaji la kuweka kambi Bungeni kama kutakuwa na haja.

Nadhani sio vizuri kusubiri siku zote kubebwa na serikali. Kila madhehebu wana sheria zao, sheria zao ambazo hazipaswi kwenda kinyume na sheria za Nchi. Sioni sababu ya kutumia nguvu kubwa kudai mahakama badala ya kuwekeza kwenye mambo ya maandeleo kama elimu, afya, nk. Kwanini tunadhani maisha yetu lazima kupelekana mahakamani?

Ndiyo maana nasema natoa ushauri kwa waislamu hasa waJF maana ndo watakaosoma ushauri huu, Waislamu wawekeze nguvu nyingi kwenye mambo ya maendeleo zaidi kuliko mahakama. Wawekeze kwenye elimu na afya. Achaneni mambo ya mahakama. Mahakama ya nchi inaweza kumaliza yote, ikiwa kutakuwa na haja. Lakini kwa mtu optimistic hawezi kutumia nguvu nyingi kwenye hilo.

Sio haki kwa wabunge: wawakilishi wa wananchi kupoteza muda kujadili kuwa waislamu wawe na mahakama ya kadhi au la. Ni wazi watajadili, hasa wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Ili kila mchangiaji aonekane anawajali waislamu, ataunga mkono mahakama ya kadhi, watafanya funika kombe mwanaharamu apite. Ili tu waislamu wa jimbo lake wasimtose, ili tu waislamu wasikikatae chama chake. Lakini nasema tena sio haki wabunge wapoteze muda katika jambo hili ambalo sio kipaumbele cha taifa. Sio haki lakini litajadiliwa kwaajili wa woga wa kupoteza kura.

Mniwie radhi, kama kuna moja hatapendezwa na ushauri wangu. Ukweli utabaki kuwa kuwekeza kwenye elimu, hasa elimu dunia na afya ni bora kuliko kuwekeza kwenye mahakama.

Ushauri mzuri sana sana. Ingawa watakutupia mawe kwa sababu siku zote ukweli ni mchungu kama shubiri. Mimi ni muislamu lakini nakushukuru kwa andiko hilo lililokwenda shule.
 
Mfano ktk suala la mahakama ya kadhi wakati wenzao wakipigia chapuo ipatikane wao wanapiga kumbo ikosekane...

Wanapinga mahakama hizi kusimamiwa au kuendeshwa na serikali.

Yapo mengi hilo ni miongoni mwao.

Acheni kuwaonea Bakwata ata ambapo hawastaili kubeba lawama, ishu ya mahakama ya kadhi haijakataliwa na Bakwata imekwamia kwenye kamati ya Bunge na sote ni mashahidi namna Bakwata walivyopaza sauti zao,na pia hii ishu haikusimamiwa na Bakwata peke yake bali tahasisi zipatazo 12 za kiislamu mkiwamo nyie Ansar sunni na Wahabi.

Mbona kwenye bunge maalum la katiba hao wanaojifanya wakombozi wa kiislamu kina Sheikh Kundecha na Prof Njozi waliikubali katiba mpya isiyo na mahakama ya kadhi? kwa nini baada ya kutoka kwenye posho wanakuja kuidai tena wakati wanajua wazi katiba mpya walioipitisha wao kwa niaba ya waislamu ndio imekataa kwa nguvu zote ata kuitambua tu hii mahakama ya kadhi? kwa nini awa hamuwazungumzi mnawaona Bakwata tuu?

Hivi mnafikiri awa Bakwata wakiwa chombo cha harakati bila ya hekima kuna amani tena kwa nature ya dini yenu ya kiislamu??
 
Acheni kuwaonea Bakwata ata ambapo hawastaili kubeba lawama, ishu ya mahakama ya kadhi haijakataliwa na Bakwata imekwamia kwenye kamati ya Bunge na sote ni mashahidi namna Bakwata walivyopaza sauti zao,na pia hii ishu haikusimamiwa na Bakwata peke yake bali tahasisi zipatazo 12 za kiislamu mkiwamo nyie Ansar sunni na Wahabi

Mbona kwenye bunge maalum la katiba hao wanaojifanya wakombozi wa kiislamu kina Sheikh Kundecha na Prof Njozi waliikubali katiba mpya isiyo na mahakama ya kadhi? kwa nini baada ya kutoka kwenye posho wanakuja kuidai tena wakati wanajua wazi katiba mpya walioipitisha wao kwa niaba ya waislamu ndio imekataa kwa nguvu zote ata kuitambua tu hii mahakama ya kadhi? kwa nini awa hamuwazungumzi mnawaona Bakwata tuu?

Hivi mnafikiri awa Bakwata wakiwa chombo cha harakati bila ya hekima kuna amani tena kwa nature ya dini yenu ya kiislamu??

Dini yenu akina nani? Mi mnyakyusa Wa mpuguso dini yangu mkristo Wa madhebu ya kilutheri acha kuwa mbashiri kwa vitu usivyovijua...

Awali uliuliza swali nami nilikujibu nikidhani hujui na unataka kujua kumbe Una lengo tofauti tafadhali huwa sifanyagi utoto Wa marumbano ya kidini nilichofanya ni kutoa views tu maana nipo serikalini na ninashuhudia mengi Sana kuhusu hawa ndugu zetu that's why nikachangia....

Naomba nikuache uendelee na wengine.
 
Kwani ulitaka kwa kuwa serikali inaweka pesa zake, basi watibiwe bure? Hiyo hospitali gani ya serikali watu wanatibiwa bure. I now can see your nonsense arguments you are trying to make.

Kuna mtu mbaya lakini ukikosa tusi kwake nyamaza tu. Hakuna point hapo unajaribu kuonyesha hasira zako na umekosa la kufanya. Matatizo ya usilamu yanatokana na uislamu na solution itatokana na uislamu. usitafute solution serikalini. That will be another rubbish.

Point sent mkuu. Akina Ritz, FaizaFoxy and the likes wanapiga ushabiki tu hamna kitu ........................... kama wangekuwa urgument ni lazima wangeona walau few weakness kwenye hii Kadhi. Tatizo wameifanya hii issue kama ushabiki wa Simba na Yanga ndiyo maa Ritz yuko busy kukubali au kusifia kila point ya mzee Mohamed.

Ila wanachonishangaza waislam pale wanapodai kuwa Kadhi ni sehemu ya ibada kwao halafu hapo hapo wanadai hiyo Kadhi ijihusishe na mambo ya mirathi na ndoa tu. Sasa kama ni sehemu ya ibada kwa nini wanaomba nusunusu ............... waombe kila kitu mpaka kupigwa mawe kwa wale wanaozaa nje ya ndoa. Na wale tunaogongana nao kwenye mabaa kule Sinza na kwenye kiti moto nao wahukumiwe vilevile. Wale wauza baa wenye majina ya Asha na akina Halima sijui wao wawanaadhibiwa vipi....!!

Point yangu ni kwamba ........................ kuna watu wako so opportunistic such that hawajali madhara yake kwa Taifa. Ni kama vile mafisadi wanavyochota pesa zetu bila huruma na kujifanya bado wanamapenzi na nchi yetu. Haiwezekani mtu apiganie kadhi kiasi hicho eti kwa kuwa Kanisa linapewa 60 billion au eti wakristo wanapendelewa kwenye ajira. Hapa wanataka kumaanisha kuwa wanapigania pesa na maslahi maana kadhi haitabadili MoU. Kama ni kweli baada ya miaka 50 ya Uhuru bado wanaonewa kwenye elimu, afya na ajira kwa nini wasilipiganie hilo badala ya kupigania Kadhi na kujinja vitoweo!!?
 
Sisi waislamu wala hatuiitaji hiyo mahakama sijui wakina nani wanataka kutuharibia uislamu wetu, mpaka kuna muda huwa nashangaa hizi mada zinatoka wapi coz hata Msikitini kwenu huwa hatuizungumzii hiyo mahakama, asante kwa ushauri mtoa mada
 
Dina,

Hapa hutoweza kuelewa chochote.

Kitafute kitabu changu, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924
- 1968)The Untold Story of the Muslim Struggle Against British
Colonialism in Tanganyika,"
Minerva Press, London 1998.

Sehemu ya Tatu ya kitabu inaitwa: "Conspiracy Against Islam."
Hapa ndipo kuna mengi na ukimaliza yote yanayotokea leo utayajua.

Utajua vipi Kanisa na Serikali zinavyofanya kazi kwa ushirikiano wa karibu.
Utajua kwa nini mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika hawatajwi.

Utajua kwa nini BAKWATA imesuswa na Waislam lakini Serikali haikubali
ukweli kuwa BAKWATA haimuwakilishi yeyote ila wenyewe.

Utajua, utajua, utajua...
Utajua kwa nini Wizara ya Elimu, NECTA haiwezi kuachiwa Waislam wakaingia.

Utajua kwa nini Prof. Malima hakudumu Wizara ya Elimu.
Unajua kila aliyejaribu kuleta suala la Waislam katika Bunge hakurudi bungeni?

Kitwana Kondo, Manju Msambya...
Sheikh Abubakar Mwilima
alileta suala hili Kamati Kuu ya CCM na huo ndiyo
ukawa mwisho wake...

Sheikh Hassan bin Amir na Tewa Said Tewa walitaka kujenga Chuo Kikuu mwaka
1968 kupitia East African Muslim Welfare Society (EAMWS)...

Unaujua mwisho wao?

Mengi, mengi, mengi yatakufunukia.
Utajua ni vipi Kanisa linaweza kupewa Bilioni 91 kila mwaka na isiwe chochote.

Utajua kwa nini Sheikh Ponda alipojaribu kurejesha Wakfu (Mali ya Allah) kwa
Waislam kwa kutaka kujenga msikiti alioupa jina Masjid Hassan bin Amir
yamemkuta yaliyomfika...

Nikuulize.

Unaujua mchango wa Sheikh Hassan bin Amir katika uhuru wa Tangayika?
Unajua Sheikh Hassan bin Amir alikuwa nani katika kupigania uhuru wa
Tanganyika?

Unajua kwa nini Sheikh Ponda alipenda kuupa jina la ule msikiti jina la
Sheikh Hassan bin Amir?

Hata viongozi wa BAKWATA hawathubutu kulitaja jina hili na ndimi zao.
Wanaogopa kama wanavyoogopa wanasiasa wa sasa.

Unajua kuna ''Award ya Sheikh Hassan bin Amir," inatolewa kila mwaka
kwa vijana wa Kiislam masikini lakini wana uwezo mkubwa wa masomo?

Jiulize huyu Sheikh Hassan bin Amir alikuwa nani...?
Tumalizie hapa.

Chapatikana bookshop yoyote Tanzania...ama kuna sehemu maalum...nami nkiperuzi.
 
Na mimi kama Muislam nakushauri huu ushauri wako upeleke Kanisani.

Kawaambie hivi toka toka uhuru mpaka sasa wasomi wa Kikirsto wamejazana serikali kila idara wamelisaidiaje taifa letu kutoka kwenye nchi masikini duniani, unajua kuwa Tanzani ipo kwenye nchi 20 masikini wa kutupwa duniani huko serikalini kazi yenu kufanya ufisadi tu.

Halafu nyie Wakirsto ndiyo mnabebwa unajua kama kila mwaka Kanisa linapewa bilioni 61.9.

Ahsante.
We muislamu mwenzangu kipi ambacho hujaelewa kwenye huo ushauri tuliopewa? Acha ufia dini jibu fact, weka point hizo hela wanapewa na nani ? Factor ni elimu, afya na mahakama ulitakiwa uelezee kipi sisi kama waislamu tunatakiwa tupiganie sio unalalamika tu,
 
Nimecheka sana post ya Mtu hapo juu aliyefananisha Na mnyama flani wa kufuga.. Lakini Kwa post kama hizi naanza kuamini kuna kila dalili Za kufanana Na mnyama huyo..!

Ati "..wasomi wa kikristu wamejazana kila idara serikalini .. " nadhani kuna tatizo Kama sio akili basi mawazo yaliyotoboka..! Watu mmawaza negative tu all time kuhukumiwa sio Kusoma, matibabu, Afya ,Maji , Umeme noo hiyo si inshu Bali kuhukumiana , kukomeshana, kurithiana Na kutalikiana Na kulogana basi.. Mengine sio Hoja kwenu..
Na kama ingekuwa ukiwa kiongozi muislamu nchi ndiyo inakuwa na maendeleo au watu wanakuwa matajiri basi Zanzibar ingekuwa na maendeleo makubwa sana na watu wake wangekuwa ni matajiri sana maana tangu ipate uhuru au Mapinduzi 51 years go Rais, Makamu wa rais, Waziri Kiongozi (Enzi zile) na nafasi zote za juu Zanzibar zinashikwa na waislamu

cc Ritz
 
Dini yenu akina nani? Mi mnyakyusa Wa mpuguso dini yangu mkristo Wa madhebu ya kilutheri acha kuwa mbashiri kwa vitu usivyovijua...

Awali uliuliza swali nami nilikujibu nikidhani hujui na unataka kujua kumbe Una lengo tofauti tafadhali huwa sifanyagi utoto Wa marumbano ya kidini nilichofanya ni kutoa views tu maana nipo serikalini na ninashuhudia mengi Sana kuhusu hawa ndugu zetu that's why nikachangia....

Naomba nikuache uendelee na wengine.

Hakuna swali ulilojibu we mnyia, acha kutafuta pa kutokea eti hupendi malumbano kwani hapa umekuja kufata nini kama unajua hauna point za msingi.

Nimekuuliza nyinyi waislamu mnanyimwa haki gani za kiraia au za kikatiba na serikali mpaka mseme mnaonewa? hakuna ulipo jibu. Nimeuliza hapa awa Bakwata wameukwamisha vipi huu mchakato wakati mswada ulishakamilika na ukafikishwa mpaka kwenye kamati bungeni? akuna ulipojibu,unachotaka ni kutafuta angle ya kuchomokea. Na maswali yote nimeyatoa kwenye malalamishi/maelezo yako.

Anyway, naendelea kukupa hongera kwa kuwa serikalini,wewe ni mwanajf wa kwanza na utakuwa wa mwisho kwa hayo mafanikio ya aina yake. nakushauri uchapishe na tshirts kabisa za kukutambulisha kuwa uko serikalini maana kujitambulisha kila thread hapa jf pekee haitoshi :behindsofa:
 
Wewe Una muda Sana Mimi sina...

Akili yangu na yako hazilingani hata upeo wetu Wa kuelewa mambo na kuteua vipaumbele vya msingi ni tofauti Sana.

Siwezi fanana nawe unayejiita team flani na kushabikia vitu vya kipuuzi na kushinda JF kupigania na kujinasibisha na wapuuzi...

Hatuwezi kuwa ktk kundi moja Mimi nawe na hata ninachoongea uwezo wako Wa Ku grasp meaning ni mdogo Sana.

Umeshindwa Ku link sentensi "nipo serikalini" na ujumbe mzima au mtiririko Wa mawazo na kuishia na maneno ya shombo...

Uwezo wako ktk kujadili issues ni mdogo Sana zaidi ya kujadili mambo binafsi ya watu na walio ktk kundi duni mno la fikara(wapuuzi)

Anyway thanks kwa mda wako.
 
Wewe mwenye uwezo mkubwa wa akili umeshaaga alafu unaendelea kujibu mtu asiyekuwa na uwezo wa kufikiri??? We ulishaaga basi chukua time, otherwise na wewe uwezo wako ni funyu kuliko wangu kichwani. Potea!!
 
Mkuu achana na huyo mkinga sana sana atakupakaza mavi
 
Wewe mwenye uwezo mkubwa wa akili umeshaaga alafu unaendelea kujibu mtu asiyekuwa na uwezo wa kufikiri??? We ulishaaga basi chukua time, otherwise na wewe uwezo wako ni funyu kuliko wangu kichwani. Potea!!

Nimeaga kwa nani? Kuaga kuna wakilishwa na msamiati gani?

Nikuage hapa JF nimekuja kwako? nipotee umenielekeza wewe kuja JF?

Huwa sina kawaida wala mazoea ya kusalimu amri kwa wapuuzi....

Muda hauchukiliwi bali unatumiwa....

Kima Kama wewe unaewaza kula na kunya tu na ambae fikra zako hazivuki nyayo za miguu yako kamwe siwezi salimu amri mbele yako.
 
Back
Top Bottom