Acha kujitoa ufahamu! Pitia posts zote kuanzia post
#1 hadi 18, suala la MoU limeelezewa vizuri mno na
MchunguZI pamoja na wengine wengi. Anzisheni Hospitali zetu muone kama mtanyimwa kuingia mkataba na Mou.
Patience96,
Inawezekama kabisa kuwa haya usemayo yanatoka moyoni na
unaamini kuwa huo ndiyo ukweli kuwa Waislam wanaweza kwa
juhudi zao au kwa msaada wa nchi za Kiislam wakafanya kama
mnavyofanya nyie.
Kuwa Waislam wanaweza wakaleta fedha kutoka nje wakajenga
shule, vyuo na hizo hospitali.
Hali halisi tofauti kabisa.
Kuna mfumo ndani ya serikali ya Tanzania uko pale kuhakikisha
kuwa Uislam haupati nguvu Tanzania.
Mifano tunayo mingi na mimi nimeieleza hapa mara nyingi.
Nimeeleza jinsi EAMWS ilivyohujumiwa, kupigwa marufuku kwa
kuwa ilikuwa na mipango ya kujenga chuo kikuu.
Hii ilikuwa mwaka wa 1968.
Katika miaka ya 1970s Organisation of Islamic Countries (OIC)
ilitaka kujenga chuo kikuu Tanzazania.
Mradi huu ukahujumiwa.
Darul Imaan ilitaka kujenga chuo cha ufundi Kibaha.
Mradi huu pia ukahujumiwa na kwa juhudi za Aboud Jumbe mradi
ukapelekwa Zanzibar.
Wizara ya Elimu...
NECTA...
Sheria ya Ugaidi...
Ndiyo unaona hata historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika hadi
leo imekuwa ni kitendawili.
Hakuna anaeitaka ielezwe wala iandikwe.
Wajerumani wakati wa Vita Kuu ya Pili waliwakusanya Wayahudi
katika Ghetto nchini Poland ambako hapakuwa na maji.
Wajerumani hao hao wakawa wanawashutumu Wayahudi kwa uchafu.
Leo sisi mnatushutumu kuwa hatuna vyuo kama nyinyi, hatuna
hospitali kama nyinyi, hatuna shule kama nyinyi.
Mnatuambia kuwa tungelikuwa na hospitali na sisi serikali ingetupa
bilioni 91 za MoU kama manazopewa nyinyi.
Linalonisikitisha sana ni kuwa na mnaposema maneno haya mnasema
kwa kejeli bila kujali hisia zetu kuwa tunajisikiaje.
Nadhani
Patience96 umepata kusikia kuwa Waislam wanataka
kufanya maandamano kuhusu Ndalichako wa NECTA kwa kuwahujumu
wanafunzi wa Kiislam na polisi ikisema kuwa watakaoandamana
watashughulikiwa na nguvu za dola...
Tuishie hapa lakini nakusihi jitulize na fikiri.
Nilitaka kusahau.
Naamini unajua kuwa kuna fedha zinatoka CRDB zinakwenda Kanisani
kila mwaka.