Ushauri kwa Serikali na Huduma za Jamii Tanzania

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,883
109,213
Binafsi ni mwana CCM kindakindaki tokea ilipobuniwa 1977, kabla ya hapo nilikuwa TANU Youth League.

Ingawa ni mwana CCM lakini si kila jambo la serikali linaniridhisha, kuna ambayo tukipata nafasi tunayafikisha vikaoni lakini hivi sasa imekuwa ngumu sana kufikisha ujumbe kwenye ngazi za maamuzi, sifahamu kwanini wakati sasa hivi tunaishi kwenye dunia inayopitia kwenye miongo ya mawasiliano habari (IT).

Kwanza naishauri CCM iboreshe namna ya kuwasiliana na ngazi za uongozi; pili naishauri serikali kuu, mawaziri wote mpaka Rais wa Tanzania waige mfumo wa Zanzibar wa "sema na Rais".

Kwa kukosa njia za kufikisha ujumbe kwa haraka nimeona bora ushauri wangu niutoe hapa JF, nafahamu utawafikia walengwa wote.

1) Nashauri huduma zinazotelewa bure na serikali ziwe za kulipia rasmi, kwa zote namaanisha zote. Kuanzia huduma zinazotolewa Polisi, iwe mtu ukitaka huduma yoyote ya kipolisi ulipie, kama siyo siku hiyo hiyo basi uandikiwe una deni kwa kupewa huduma hiyo na utailipa kupitia control numbers.

Rushwa imezidi serikalini, kama haujaombwa waziwazi basi utazungushwa kupatiwa huduma mpaka utie akili utowe rushwa au atokee "kishoka" wa hapo akusomeshe utowe rushwa, ndipo huduma yako ishughulikiwe.

Kwa mambo kama hayo, iwekwe wazi tu, kuwa ukienda kushitaki Polisi unapewa control number unalipia unapewa huduma, na afisa ataekuhudumia atalipwa mgao wake hukohuko official kabisa.

Ili kupigana na rushwa, kama tumeshindwa kuweka sheria kali ni vyema tukaihalalisha tu malipo kwa kila huduma.

Au kama ilivyofanywa kwenye matibabu, iwekwe bima ya lazima kwa kila raia awe analipia hizo huduma, na pesa zitazotokana na hiyo bima waongezewe mishahara na posho watoa huduma badala ya kuzungusha watu ili wale rushwa serikalini. Hii ni kwa wizara na idara zote zinazotoa huduma za bure kwa jamii, ambako ndiko kunakonuka uozo wa rushwa.

Kauli za viongozi kama zile za "za polish ya viatu", "kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake" zimekuwa zikihalalisha rushwa kiaina, sasa iwe ni wazi kabisa ihalalishwe kwa kuzilipia hizo huduma.

Polisi, mahakama, uhamiaji, ardhi, huduma zote za bure za manispaa. Ongezea na wewe kwengine.

Tunataka tuwe ni wateja rasmi wenye kuweza kudai haki zetu tunaponyimwa huduma kwa wakati.
 
KWANINI KIPINDI HIKI CHA MAMA RUSHWA IMEZIDI NA UZEMBE KAZINI KULIKO KIPINDI CHA MAGUFULI? huduma zilipiwe hasa ya kipolisi.polisi ofisi za serikal za vijiji na mtaa ndyo maeneo yanayoongoza kwa rushwa.hata na hvyo bila uongoz imara hata km unalipia huduma mambo bdo n yaleyale
 
Usaliti.
 
Nilileta wazo huduma za Kipolisi ziwe "private", Sasa nimeboresha wazo "privatization" ianzie serikalini wapate ujuzi.

Hizo idara zote zinazotowa huduma za bure ziwe ni vyanzo vya pesa na watu walipwe vizuri rasmi, badala ya kuteswa raia.
 
Suala la rushwa ni kwa serikali karibu zote za Afrika. Lazima tutibu kwanza mzizi wa tatizo.

Mishahara mingi ya wafanyakazi wa serikali ipo chini haikidhi uhalisia wa maisha.Hivyo wanajiongeza kwa kuomba rushwa.
Ndiyo maana nimeshauri badala ya rushwa huduma zilipiwe kwa bima ili mishahara iongezeke.
 
CCM wanajivunia kuongoza banana republic!

A bunch of dumb fools.
hiyo kawaida ya uongozi wote duniani, lazima muwepo mnaolalamika bila kuleta njia kifanyike nini.

Mapapai yaliyovunda hayajifichi.
 
Mfano mzuri ni jana kariakoo, moto uliotokea, hakuna huduma ya zima moto.

Sasa kwanini kujna vituo vya zimamoto kama hawana hata ubunifu wa kuwa na na malori kumi au kumi na tano ya maji wakati wote?

Au kuwa na ubunifu wa kuweka matank ya reserve -, mfano kariako ulipotokea moto karibia majumba yote yana visima vya maji.

Ubunifu unatushinda Watanzania, akili zetu zimelala sana, tunachowaza ni kulewa, ngoma, uasherati, kujionesha kwa watu na mambo ya kijingajinga tu.
 
Binafsi ni mwana CCM kindakindaki tokea ilipobuniwa 1977, kabla ya hapo nilikuwa TANU Youth League.

Ingawa ni mwana CCM lakini si kila jambo la serikali linaniridhisha, kuna ambayo tukipata nafasi tunayafikisha vikaoni lakini hivi sasa imekuwa ngumu sana kufikisha ujumbe kwenye ngazi za maamuzi, sifahamu kwanini wakati sasa hivi tunaishi kwenye dunia inayopitia kwenye miongo ya mawasiliano habari (IT).

Kwanza naishauri CCM iboreshe namna ya kuwasiliana na ngazi za uongozi pili naishauri serikali kuu, mawaziri wote mpaka Rais wa Tanzania waige mfumo wa Zanzibar wa "sema na Rais".

Kwa kukosa njia za kufikisha ujumbe kwa haraka nimeona bora ushauri wangu niutowe hapa JF, nafahamu utawafikia walengwa wote.

1) Nashauri huduma zinazotelewa bure na serikali ziwe za kulipia rasmi, kwa zote namaanisha zote. Kuanzia huduma zinazotolewa Polisi, iwe mtu ukitaka huduma yoyote ya kipolisi ulipie, kama siyo siku hiyo hiyo basi uandikiwe una deni kwa kupewa huduma hiyo na utailipa kupitia control numbers.

Rushwa imezidi serikalini, kama haujaombwa waziwazi basi utazungushwa kupatiwa huduma mpaka utie akili utowe rushwa au atokee "kishoka" wa hapo akusomeshe utowe rushwa, ndipo huduma yako ishughulikiwe.

Kwa mambo kama hayo, iwekwe wazi tu, kuwa ukienda kushitaki polisi unapewa control number unalipia unapewa huduma, na afisa ataekuhudumia atalipwa mgao wake hukohuko official kabisa.

Ili kupigana na rushwa, kama tumeshindwa kuweka sheria kali ni vyema tukaihalalisha tu malipo kwa kila huduma.

Au kama ilivyofanywa kwenye matibabu, iwekwe bima ya lazima kwa kila raia awe analipia hizo huduma, na pesa zitazotokana na hiyo bima waongezewe mishara na posho watowa huduma badala ya kuzungusha watu ili wale rushwa serikalini. Hii ni kwa wizara na idara zote zinazotowa huduma za bure kwa jamii, ambako ndiko kunakonuka uozo wa rushwa.

Kauli za viongozi kama zile za "za polish ya viatu", "kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake" zimekuwa zikihalalisha rushwa kiaina, sasa iwe ni wazi kabisa ihalalishwe kwa kuzilipia hizo huduma.

Polisi, mahakama, uhamiaji, ardhi, huduma zote za bure za manispaa. Ongezea na wewe kwengine.

Tunataka tuwe ni wateja rasmi wenye kuweza kudai haki zetu tunaponyimwa huduma kwa wakati.
Umerumia akili gani hapo?

Kwa hiyo, kwa sababu rushwa imeshindikana kudhibitiwa na serikali yetu ya CCM, basi ihalalishwe kwa kulipia huduma ambazo kimsingi ni WAJIBU wa serikali.

Kwa nini usiishauri CCM isiibe kura na badala yake iwe ina concede kushindwa ikiwa kwa haki?

Umewaza ujinga
 
Nalitupia hili hapa.

Hivi hao wawekezaji tunaoambiwa wanawekeza na kuongezeka bwelele, wananchangia nini kwenye huu Uchumi wetu?

Ninavyofikiri kuwa, uchumi unavyo kua na Huduma za Jamii ndivyo zinavyo kua, au?
Nisaidieni.
Hizo idara zote zinazotowa huduma za bure ziwe ni vyanzo vya pesa na watu walipwe vizuri rasmi, badala ya kuteswa raia.

ubunifu wa kuweka matank ya reserve

Nini kimewashinda kuifanya nchi iwe na trillion dollar economy?
 
Kwani Tanzania kuna huduma ya Bure? Kodi mnalipa za Nini kumbe?

Hata hivyo, sidhani hicho ulichoshauri ni suluhisho. Hata TANESCO kuna mashtaka ya rushwa, mteja analipia gharama za kuunganishwa umeme na Bado anatozwa rushwa.

Rushwa ni malipo yasiyo Halali Ili kufanya Mtu kutoa favor isiyo Halali, au kupewa favor isiyo Halali. Ndio maana katika Sheria ya rushwa mtoaji na mpokeaji wanachkuliwa ni wakosaji.
 
Back
Top Bottom