Ushauri kwa Serikali kuhusu Shambulizi na utekaji wa Bandari ya Msumbiji na IS

Kizzy Wizzy

JF-Expert Member
Aug 2, 2013
3,136
2,000
Natumaini mu wazima wa Afya.

Naomba nitumie nafasi hii kuikumbusha jamii na serikali madhara yaliyowahi kutokea kwa nchi jirani Kenya miaka ya juzi tu walipojaribu kuingiza jeshi Lao Somalia.

Najua tuna intelijensia nzuri ya kuwakabili hawa IS lakini kama tutajitosa basi tujitahidi iwe ni kulinda mipaka na maeneo yetu tu.

Tusifungamane na kama itatulazimu basi tuzidishe umakini sana na ikibidi intelijensia tuliyonayo izidi maradufu haswa kwenye miji mikubwa.

Nafkiri nyote mnajua hawa jamaa wakiamuaga, maisha yao huwa sio kipaumbele.

Mahoteli makubwa, majumba makubwa, masoko na vituo vya usafiri sehemu ambazo kuna mikusanyiko mikubwa intelijensia iongezwe.

Tuandae pia namna ambavyo wananchi watapata utaalam wa kuwatambua wajitoa muhanga ili iwe rahisi kuwatolea taarifa kabla hawajaleta madhara.

Ushauri huu ni iwapo tutaamua ku "engage"

Tofauti na hapo kama hatutakuwa tayari basi tujiweke pembeni kwanza.

Ugaidi huwa unavuruga uchumi wa nchi.
 

Joselela

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,464
2,000
Unajua kuna mambo ambayo yalikuwa yamepangwa tangu 2016 huko lakini serikali inavyosema jambo mnaidharau na kuona ni wauwaji.

Fuatilia maeneo ambako makundi ya magaidi yalianza na vyanzo vyake hasa ni nini.

Kuna mijitu inashinda mitandaoni kazi kusema go fulani wakati hao ndio wameingia mikataba.

Tutawanyoosha intelijencia yetu ipo makini hakuna haja ya kufundishana.
 

Kizzy Wizzy

JF-Expert Member
Aug 2, 2013
3,136
2,000
Unajua kuna mambo ambayo yalikuwa yamepangwa tangu 2016 huko lakini serikali inavyosema jambo mnaidharau na kuona ni wauwaji....

Fuatilia maeneo ambako makundi ya magaidi yalianza na vyanzo vyake hasa ni nini..

Kuna mijitu inashinda mitandaoni kazi kusema go fulani wakati hao ndio wameingia mikataba..

Tutawanyoosha intelijencia yetu ipo makini hakuna haja ya kufundishana.
Okay kama intelligence ipo vizuri basi ni vyema
 

kitonsa

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
641
1,000
umeongea vizuri ugaidi kupambana nao ni ngumu, hata mabeberu mwenye interejestia ya juu wanashambuliwa
 

Iselamagazi

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
4,260
2,000
Natumaini mu wazima wa Afya.

Naomba nitumie nafasi hii kuikumbusha jamii na serikali madhara yaliyowahi kutokea kwa nchi jirani Kenya miaka ya juzi tu walipojaribu kuingiza jeshi Lao Somalia...
Siamini sana kwamba una ufahamu mkubwa sana wa masuala haya zaidi ya wenye mamlaka! Ebu tuwaachie wafanye kazi yako.
 

MTOCHORO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
3,531
2,000
Kuna dini nyingine ni za taabu sana, ona sasa wanataka TPDF wakafanye tena Operation Safisha kama ile ya Renamo
 

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
11,641
2,000
Majuzi jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzani JWTZ lilitoa onyo kwa kwa wananchi wa maeneo ya misitu iliyoko mipakani na nchi ya Msumbiji.

Agizo hilo ni kwa ajili ya operesheni maalum inayotarajiwa kuanza kufanywa na JWTZ ili kukabiliana na kikundi cha kigaidi ambapo inaaminika kuwa kimeanzisha makazi ndani ya misitu hiyo.

Msitu wa Ruvuma ni moja na misitu mingine iliyopo katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo inakaa ndai ya mipaka kati ya Tanzania na Msumbuji.

Tangu mwaka 2017 kundi la kigaidi lilingia katika jimbo la Cabo Delgado lililoko kaskazini mwa nchi hiyo na kuteka bandari muhimu na ya kimkakati yaani "strategic port" ya Macimboa da Praia.

Jimbo la Cabo Delgado lina hifadhi ya gesi nyingi asilia na eneo hilo zipo kampuni mbili maarufu duniani za Exxon mobil ambayo ni ya kimarekani na hushughulika na uchimbaji wa mafuta na gesi na Total ya Ufaransa ambayo pia imekuwa ikishughulika na uchimbaji wa mafuta na gesi tangu mwaka 1924.

Hapa kuna matatizo mawili makubwa kwanza ni tatizo la kiuchumi kwa jimbo la Cabo Delgado ambapo utekaji wa bandari hii muhimu kutazuia usafirishaji wa nishati za mafuta na gesi kwenda nchi za mbali kupitia hizi kampuni za Exxon na Total.

Pia hali hiyo itapelekea kuvuruga mradi mkubwa unaofanywa na makampuni haya makubwa khasa katika miundombinu walokwishaijenga.

Jambo jingine kubwa ni usalama kwa nchi za Msumbji ambayo ni jirani zetu na Tanzania ambayo ndo jirani kabisa.

Kikundi hiki cha kigaidi hakitakuwa na uwezo wa kukaa sana eneo hilo la bandari ya Mocimboa da Praia bali kitatafuta makazi ya kudumu ambayo mpaka sasa ni misitu ya Ruvuma na mingine iliyomo karibu na mipaka na nchi jirani.

Kama ilivyo kwa vikundi vingi vya kigaidi kiliwemo cha Boko Haram ambacho kina makazi katika msitu mnene wa Sambisa ambao ni eneo sawa na nchi ya Ufaransa, kikundi hiki kitakuwa kinafanya mashambulizi mjini Cabo Delgado na kisha kukimbilia misituni kupanga mashambulizi mengine.

Kikundi hiki ni sehemu ya kinachoitwa ISCAP yaani Islamic State Central African Province na kimeazimia kuweka makazi ya kudumu nchini Msumbiji.

Sasa hadi sasa raia wapatao 1300 wameuawa na kikundi hiki na wengine wapatao 250,000 wamepoteza makazi.

Lakini hatuna haja ya kuhangaika kufahamu ni sababu zipi zimekifanya kikundi hiki kiingie kwa urahisi nchini Msumbiji bali ni kuwepo kwa serikali dhaifu, legelege na yenye kuendekeza Ufisadi ya raisi Nyusi.

Hapa fikiria, unakuwa na kikundi cha kimataifa cha kigaidi ambacho kinatishia usalama na amani katika nchi jirani zinazoizunguka Msumbiji ikiwemo Tanzania na hapo ndipo tatizo linapoanzia.

Kitakachotokea hapo twaita ni "regional implications" yaani matatizo kwa nchi jirani ambayo yamesababishwa na mmoja wa nchi wajumbe wa SADC ambae amefumbia macho masuala ya usalama wa taifa.

Hii ni fursa na wajibu wa Tanzania ambayo imeisaidia Msumbji katika harakati za kujigania Uhuru wa nchi hiyo, kuketi vikao na kujadili suala hili ambalo halihitaji ushauri kutoka Marekani wala Ulaya.

Raisi John Magufuli akiwa mwenyekiti wa SADC atakuwa na nafasi ya kuitisha kikao cha dharura na wakuu wa nchi majirani hususan raisi Nyusi na kumpatia msaada anaohitaji.

Pamoja na kwamba Tanzania kwa sasa ipo kwenye mchakato wa shughuli za kujiandaa na uchaguzi mkuu, lakini hili la Msumbji nalo linahitaji kipaumbele au hatua za haraka kwa sasa yaani "immediate action.".

Tanzania ilimweka mzee merehemu brigedia Hashim Mbita hadi Alfonso Dhlakama na RENAMO walipoweka silaha chini na hali kadhalika tukawa na mzee Luteni jenerali Mwakalindile (ambae alikaa Maputo tangu 1988 hadi 2003) akifanya doria eneo lile huku akiwa balozi.

Mzee Mwakalindile alikwenda Msumbiji kwa kazi maalum ya kuhakikisha Frelimo inakuwa na jeshi imara na baadae yeye na mzee Katikaza waliendelea kuilinda Msumbji kwa kuhakikisha jeshi na usalama wa nchi hiyo vinakuwa sawa.

Ili kuwaenzi wazee hawa serikali ya Tanzania chini ya raisi John Magufuli wana wajibu wa kuhakikisha Msumbiji inakombolewa kutoka kwa kikundi hiki cha kigaidi na kihuni na Msumbiji inarudi kuwa salama kama ilivyokuwa huko nyuma.

Hili ni jaribio jingine kwa JWTZ na vikosi vyote vya kijasusi na usalama vya Tanzania kuhakikisha vinampatia msaada raisi Nyusi.

Katika hili tutabaini lengo au madhumuni khasa ya kikundi hiki, nani alie nyuma yake, wapi wanapata silaha na ni nani anawafadhili.

Isije kuwa hii ni janja ingine ya nchi za kibeberu ambazo zimekuwa zikitamani eneo zima la ghuba ya Mtwana hadi Maputo na Capo Delgado na wamepata pa kuanzia.

Nchi za kibeberu zipo katika vita ya kijigraphia yaani "geopolitical war" ya kutafuta maeneo yenye rasilimali za kudumu na pia kupunguza nguvu ya ushawishi wa China kwa bara la Afrika.

Hivyo mabeberu wapo tayari kutumia vikundi mbalimbali katika sehemu ambazo ni dhaifu kiusalama kama Msumbiji ili kudhoofisha kasi ya juhudi za kujitegemea kwa nchi hizo.

Baada ya hapo raisi Nyusi aketishwe chini na apewe mwongozo wa kuwa rasi ngangari na asie legelege tena.

Ikiwezekana Tanzania sasa hivi iziangalie kwa jicho la tatu hizi nchi ambazo hayati Mwalimu Nyerere alitumia muda wake kuhakikisha zinakuwa huru.

Tukumbuke Msumbji ikiwa salama basi Tanzania na nchi zote jirani zitakuwa salama salmini.

Mungu Ibariki Afrika Mungu Ibariki Tanzania.
 

Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
9,699
2,000
Umeandika kwamba Rais Nyusi ni legelege ndio maana kashindwa kukabiliana na kuzorota usalama, huku ni kukosa adabu na nidhamu mbaya.

Ina maana hata Buhari wa Nigeria, Idriss Derby wa Chad wao pia ni legelege sababu uasi wa bokoharam umezorotesha usalama huko kwao?

Pia Rais Alsis wa Misri naye utamuita legelege kisa wanamgambo wa ISIS wanafanya ghasia na kuzorotesha usalama huko Sinai?

Isitoshe serikali ya Msumbiji haijakiri imeshindwa kuwadhibiti hao wahuni ila ni suala linalohitaji muda (rejea nchi za Nigeria, Cameroon,Chad mpaka Sasa zinapambana na Bokoharam).
 

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
11,641
2,000
Umeandika kwamba Rais Nyusi ni legelege ndio maana kashindwa kukabiliana na kuzorota usalama, huku ni kukosa adabu na nidhamu mbaya.

Ina maana hata Buhari wa Nigeria, Idriss Derby wa Chad wao pia no legelege sababu uasi wa bokoharam umezorotesha usalama huko kwao?

Pia Rais Alsis wa Misri naye utamuita legelege kisa wanamgambo wa ISIS wamefanya ghasia huko Sinai?

Isitoshe serikali ya Msumbiji haijakiri imeshindwa kuwadhibiti hao wahuni ila ni suala linalohitaji muda (rejea nchi za Nigeria, Cameroon,Chad mpaka Sasa zinapambana na Bokoharam).
Hapana, ni huyu mmakonde ni mwenzetu kabisa na ni zao la Nachingwea.

Kwa maana hiyo ni kwamba huyu ni mwanajeshi alieiva.

Hivyo kama magaidi wameingia Msumbiji na yeye yupo, wewe waona nisimpe changamoto?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom