Ushauri kwa Serikali kuhusu Shambulizi na utekaji wa Bandari ya Msumbiji na IS

Majuzi jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzani JWTZ lilitoa onyo kwa kwa wananchi wa maeneo ya misitu iliyoko mipakani na nchi ya Msumbiji.

Agizo hilo ni kwa ajili ya operesheni maalum inayotarajiwa kuanza kufanywa na JWTZ ili kukabiliana na kikundi cha kigaidi ambapo inaaminika kuwa kimeanzisha makazi ndani ya misitu hiyo.

Msitu wa Ruvuma ni moja na misitu mingine iliyopo katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo inakaa ndai ya mipaka kati ya Tanzania na Msumbuji.

Tangu mwaka 2017 kundi la kigaidi lilingia katika jimbo la Cabo Delgado lililoko kaskazini mwa nchi hiyo na kuteka bandari muhimu na ya kimkakati yaani "strategic port" ya Macimboa da Praia.

Jimbo la Cabo Delgado lina hifadhi ya gesi nyingi asilia na eneo hilo zipo kampuni mbili maarufu duniani za Exxon mobil ambayo ni ya kimarekani na hushughulika na uchimbaji wa mafuta na gesi na Total ya Ufaransa ambayo pia imekuwa ikishughulika na uchimbaji wa mafuta na gesi tangu mwaka 1924.

Hapa kuna matatizo mawili makubwa kwanza ni tatizo la kiuchumi kwa jimbo la Cabo Delgado ambapo utekaji wa bandari hii muhimu kutazuia usafirishaji wa nishati za mafuta na gesi kwenda nchi za mbali kupitia hizi kampuni za Exxon na Total.

Pia hali hiyo itapelekea kuvuruga mradi mkubwa unaofanywa na makampuni haya makubwa khasa katika miundombinu walokwishaijenga.

Jambo jingine kubwa ni usalama kwa nchi za Msumbji ambayo ni jirani zetu na Tanzania ambayo ndo jirani kabisa.

Kikundi hiki cha kigaidi hakitakuwa na uwezo wa kukaa sana eneo hilo la bandari ya Mocimboa da Praia bali kitatafuta makazi ya kudumu ambayo mpaka sasa ni misitu ya Ruvuma na mingine iliyomo karibu na mipaka na nchi jirani.

Kama ilivyo kwa vikundi vingi vya kigaidi kiliwemo cha Boko Haram ambacho kina makazi katika msitu mnene wa Sambisa ambao ni eneo sawa na nchi ya Ufaransa, kikundi hiki kitakuwa kinafanya mashambulizi mjini Cabo Delgado na kisha kukimbilia misituni kupanga mashambulizi mengine.

Kikundi hiki ni sehemu ya kinachoitwa ISCAP yaani Islamic State Central African Province na kimeazimia kuweka makazi ya kudumu nchini Msumbiji.

Sasa hadi sasa raia wapatao 1300 wameuawa na kikundi hiki na wengine wapatao 250,000 wamepoteza makazi.

Lakini hatuna haja ya kuhangaika kufahamu ni sababu zipi zimekifanya kikundi hiki kiingie kwa urahisi nchini Msumbiji bali ni kuwepo kwa serikali dhaifu, legelege na yenye kuendekeza Ufisadi ya raisi Nyusi.

Hapa fikiria, unakuwa na kikundi cha kimataifa cha kigaidi ambacho kinatishia usalama na amani katika nchi jirani zinazoizunguka Msumbiji ikiwemo Tanzania na hapo ndipo tatizo linapoanzia.

Kitakachotokea hapo twaita ni "regional implications" yaani matatizo kwa nchi jirani ambayo yamesababishwa na mmoja wa nchi wajumbe wa SADC ambae amefumbia macho masuala ya usalama wa taifa.

Hii ni fursa na wajibu wa Tanzania ambayo imeisaidia Msumbji katika harakati za kujigania Uhuru wa nchi hiyo, kuketi vikao na kujadili suala hili ambalo halihitaji ushauri kutoka Marekani wala Ulaya.

Raisi John Magufuli akiwa mwenyekiti wa SADC atakuwa na nafasi ya kuitisha kikao cha dharura na wakuu wa nchi majirani hususan raisi Nyusi na kumpatia msaada anaohitaji.

Pamoja na kwamba Tanzania kwa sasa ipo kwenye mchakato wa shughuli za kujiandaa na uchaguzi mkuu, lakini hili la Msumbji nalo linahitaji kipaumbele au hatua za haraka kwa sasa yaani "immediate action.".

Tanzania ilimweka mzee merehemu brigedia Hashim Mbita hadi Alfonso Dhlakama na RENAMO walipoweka silaha chini na hali kadhalika tukawa na mzee Luteni jenerali Mwakalindile (ambae alikaa Maputo tangu 1988 hadi 2003) akifanya doria eneo lile huku akiwa balozi.

Mzee Mwakalindile alikwenda Msumbiji kwa kazi maalum ya kuhakikisha Frelimo inakuwa na jeshi imara na baadae yeye na mzee Katikaza waliendelea kuilinda Msumbji kwa kuhakikisha jeshi na usalama wa nchi hiyo vinakuwa sawa.

Ili kuwaenzi wazee hawa serikali ya Tanzania chini ya raisi John Magufuli wana wajibu wa kuhakikisha Msumbiji inakombolewa kutoka kwa kikundi hiki cha kigaidi na kihuni na Msumbiji inarudi kuwa salama kama ilivyokuwa huko nyuma.

Hili ni jaribio jingine kwa JWTZ na vikosi vyote vya kijasusi na usalama vya Tanzania kuhakikisha vinampatia msaada raisi Nyusi.

Katika hili tutabaini lengo au madhumuni khasa ya kikundi hiki, nani alie nyuma yake, wapi wanapata silaha na ni nani anawafadhili.

Isije kuwa hii ni janja ingine ya nchi za kibeberu ambazo zimekuwa zikitamani eneo zima la ghuba ya Mtwana hadi Maputo na Capo Delgado na wamepata pa kuanzia.

Nchi za kibeberu zipo katika vita ya kijigraphia yaani "geopolitical war" ya kutafuta maeneo yenye rasilimali za kudumu na pia kupunguza nguvu ya ushawishi wa China kwa bara la Afrika.

Hivyo mabeberu wapo tayari kutumia vikundi mbalimbali katika sehemu ambazo ni dhaifu kiusalama kama Msumbiji ili kudhoofisha kasi ya juhudi za kujitegemea kwa nchi hizo.

Baada ya hapo raisi Nyusi aketishwe chini na apewe mwongozo wa kuwa rasi ngangari na asie legelege tena.

Ikiwezekana Tanzania sasa hivi iziangalie kwa jicho la tatu hizi nchi ambazo hayati Mwalimu Nyerere alitumia muda wake kuhakikisha zinakuwa huru.

Tukumbuke Msumbji ikiwa salama basi Tanzania na nchi zote jirani zitakuwa salama salmini.

Mungu Ibariki Afrika Mungu Ibariki Tanzania.
Mkuu umeandika kwa uzuri sana, hongera sana
 
Ni lazima pia tujiandae na gharama zitakazoambatana na kuipa msaada wowote Mozambique dhidi ya hili kundi. Huenda hatuna tofauti kubwa sana nao kiusalama ni mapema sana kuwaita wazembe. Kinachoendelea kule tumekiona kikianza, kustawi na kukomaa kule Nigeria. Tumeona harakati za Kenya na Uganda kule Somalia na gharama zake. Tunawazidi nini?
Unataka ujue ss tunawazd nn??? Ss ni nchi ya ahadi toka zaman. Ukiwa RAIA wa kawaida huwez elewa namna nchi yko inavyolindwa ndo maana mnaishia kuvituhum vyombo vya usalama tu mda wote, lkn nyuma ya pazia kuna kazi kubwa sana nyuma ya pazia inafanyika usiku na mchana kuhakikisha nchi yetu iko salama. Ndo maana tumekuwa hatuna masihara na mtu yoyote anaecheza na nchi yetu kwa maslah yke binafsi au kikundi cha watu, ila cha ajabu nyie mkisikia mtu haonekan au kapotea bs mnakimbilia mitandaoni na kuanza kulalama bila kujua sababu ya huyo mtu kupotezwa. Ni bora apotee mmoja ili elfu moja wabaki salama.
 
Hili kundi lilianzia tanzania ndo lile lilikuwa linaua watu ovyo. Rais wetu amewashugulikia wakasambaratika wakaenda kujikusanya nchi jirani. Wengine tunaona wapo gerezani hadi leo. Na kuna wagimbea tunaona wanasemasema watawatoa.
Ila wengi wao tuliwapoteza wakiwemo wale mawriter wa news
 
Umeandika kwamba Rais Nyusi ni legelege ndio maana kashindwa kukabiliana na kuzorota usalama, huku ni kukosa adabu na nidhamu mbaya.

Ina maana hata Buhari wa Nigeria, Idriss Derby wa Chad wao pia ni legelege sababu uasi wa bokoharam umezorotesha usalama huko kwao?

Pia Rais Alsis wa Misri naye utamuita legelege kisa wanamgambo wa ISIS wanafanya ghasia na kuzorotesha usalama huko Sinai?

Isitoshe serikali ya Msumbiji haijakiri imeshindwa kuwadhibiti hao wahuni ila ni suala linalohitaji muda (rejea nchi za Nigeria, Cameroon,Chad mpaka Sasa zinapambana na Bokoharam).
Nchi ya Nigeria ni ndogo sana kwa kikundi kikubwa kama Boko Haram kuweka himaya huko.

Kwanini nchi kubwa kama Russia, Brazil, China, USA ni salama lakini nchi ndogo kama Nigeria ishindwe kuondokana na magaidi wa boko haram?

Huo ni uzembe mkubwa sana. Na udhaifu mkubwa kuliko kawaida.
 
Nchi ya Nigeria ni ndogo sana kwa kikundi kikubwa kama Boko Haram kuweka himaya huko.

Kwanini nchi kubwa kama Russia, Brazil, China, USA ni salama lakini nchi ndogo kama Nigeria ishindwe kuondokana na magaidi wa boko haram?

Huo ni uzembe mkubwa sana. Na udhaifu mkubwa kuliko kawaida.
Dah!..yaani unafananisha hizo nchi za USA,Russia, China ,Brazil na Nigeria?

Au kwakuwa ni kubwa kieneo kuliko Nigeria ndio uone Nigeria ni wazembe? Mbona DRC ni kubwa kuliko Nigeria ila huko mashariki hakukaliki? Au ukubwa wake ni tatizo?

Hizo nchi ulizotaja uwezo wao kiteknolojia, kiuchumi, kijasusi na kijeshi zimeipita Nigeria kwa miaka kadhaa.

Ukubwa au udogo wa nchi sio kigezo pekee cha nchi kumudu kudumisha usalama.
 
Unataka ujue ss tunawazd nn??? Ss ni nchi ya ahadi toka zaman. Ukiwa RAIA wa kawaida huwez elewa namna nchi yko inavyolindwa ndo maana mnaishia kuvituhum vyombo vya usalama tu mda wote, lkn nyuma ya pazia kuna kazi kubwa sana nyuma ya pazia inafanyika usiku na mchana kuhakikisha nchi yetu iko salama. Ndo maana tumekuwa hatuna masihara na mtu yoyote anaecheza na nchi yetu kwa maslah yke binafsi au kikundi cha watu, ila cha ajabu nyie mkisikia mtu haonekan au kapotea bs mnakimbilia mitandaoni na kuanza kulalama bila kujua sababu ya huyo mtu kupotezwa. Ni bora apotee mmoja ili elfu moja wabaki salama.
Huwa nawashangaa wanaomlilia Kanguye, Gwanda mitandaoni
 
Ndugu yangu Kataskopos!!

Hii mada inatakiwa kutulia ili kuijadili, na sio kwa staili yangu hii ambayo ni kama nimepita tu kuchungulia JF!!!

Hata hivyo, kwanza niseme jambo moja ambalo naamini hata wewe unaweza kunitetea kwamba mimi sio mtu wa kupenda kudondoshea jumba bovu watu wengine kwa our own failures!

Hata yale mavitabu yenu mnayotuambia kwamba "Chanzo cha Umaskini Afrika ni Ukoloni", binafsi nimekuwa nikibisha; na hoja yangu ipo pale pale kwamba "how come Ulaya ambayo Industrial Revolution iliwatokea in 1700's" isababishe umaskini wa bara ambalo hadi wakati huo walikuwa hawana uwezo hata kutengeneza shati?!

Yote hiyo ni kwavile tu sipendi kudondoshea jumba bovu wengine kama excuse ya our own failure!!!

Kwa hili la mtoa mada, with reference to Mozambique, nadhani nimeanza kuwa stupid!!!

Of course, Msumbiji kuna Waislamu... but the question is: Kuna Uislamu gani pale wa ku-influence the so-called Islamic Terrorism?

Swali lingine: Is it a coincidence kwamba similar terrorism ilianza Mkoa wa Pwani, with possible extension to Lindi na Mtwara at the peak of gas discoveries?!

Is it a coincidence kwamba hayo pia yalianza kutokea Mozambique at the peak of gas discovery?!

Hivi pale MKIRU ni kutokana na ubora wetu wa kupambana na magaidi ndo maana tuliweza kuwafyekelea mbali au Mastermind wa tuliowafyekelea mbali walishaona "no more gas activities in Tanzania"?!

Kujibu hayo, inahitaji muda wa kutafiti!!

Lakini kwavile nimeshaanza kuwa na shaka basi jibu langu kwa mtoa mada wacha lizingatie shaka yangu!!!

Mosi, I don't trust Military Contractors!!!

Pale Mozambique kwa mfano, tayari kuna Russian Military Contractors (private) wanaosaidia majeshi ya serikali kupambana na magaidi!! Hawa watu make money by killing people!!

Labda niseme jambo moja: Leo hii ningekuwa na private military company, ningekuwa na proxies za ku-initiate vurugu in the name of terrorism a moment Tanzania watakapoanza kuchimba gas! Baada ya hali kuwa tense, ama oil companies au hata serikali yenyewe, wangefanya kama walivyofanya Msumbiji kutafuta private military companies ili kuweka kusaidia kulinda investments that worths billions of dollars!!!

Lakini ningefanya hayo endapo ningekuwa na military company au nina uwezo wa kuanzisha military company! Kinyume chake, lau kama ningekuwa serikalini huku nikiwa mzalendo kweli kweli, basi kinachotokea Mozambique hivi sasa kingenifanya "nianze kutia maji nywele zangu" kabla kinyozi hajanifikia!!!

Kwanza, ningeanzisha special force ya kupambana na ugaidi! Kule Lindi na Mtwara ningeimarisha kambi za jeshi za huko ili kuwa tayari kwa lolote!!

Ningefanya hayo kwa sababu moja tu: Isije mambo yanaanza kunielemea ndipo naanza kuhangaika kutafuta military contractors kutoka nje kama walivyofanya Mozambique!! Military Contractors ambao biashara yao ni migogoro ya kivita duniani!!!

Nasisitiza: Lau kama ningekuwa na mkono wangu kwenye any of the Private Military Contractors pale Mozambique, ningekuwa na proxies wa ku-fund wale magaidi hata kama waliingia magaidi hayo yaliingia Mozambique kwa utashi wao wenyewe!

Ninge-fund magaidi ili wasiishiwe pumzi; kwa sababu wakishaishiwa pumzi, na hatimae kukata roho, kitakachofuata ni ama mkataba wangu wa kazi kwisha kwa sababu no more violence or kupunguziwa areas of military coverage!!

Lolote kati ya hayo linamaanisha LOSING MONEY MAKING OPPORTUNITY!! As a military contractor firm, faraja yangu ni kuona ikibidi, magaidi waenee kote nchini, na kwavile mnayo raslimali ya kutosha, nina guarantee ya kulipwa!!!!!

Narudia... hayo nimeropoka tu kwa sababu sijafanya utafiti wowote ingawaje suala la kuchukua tahadhali kabla ya hatari, lenyewe halihitaji utafiti, hususani kwa kuangalia muktadha huu!!

Hoja ya msingi ni uwepo wa vikundi vya kigaidi na namna ya kuwakabili bila kujali kinachowasukuma kuwepo kwao!!!
..
IMG-20200820-WA0038.jpg
 
Back
Top Bottom