Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,577
- 113,771
Huu ni Ushauri wa Bure kwa Rais Samia kwenye mabadiliko tarajiwa ya cabinet kufuatia Ripoti ya CAG, namshauri Rais Samia, asibabaike sana na kuangalia ma vyeti ya usomi kwenye uteuzi wa cabinet yake, atumie watu wenye uzoefu, mfano Waziri wa Fedha wa sasa Dr. Mwigulu Mnchemba ni msomi mzuri wa uchumi, ana 1st Class ya degree ya uchumi kutoka UDSM, lakini sio mtu wa ki fedha fedha!. Hajawahi kushika na B na ma B na ma B mikononi mwake kama Dr. Charles Kimei alipokuwa CRDB, hivyo Wizara ya Fedha akimpa Dr. Kimei, fedha zitakuwa zimefika kwenyewe.
Kwenye biashara na uwekezaji, kuna wasomi wawili, madaktari wa PH.D, je, wanewahi kufanya chochote hata kuuza nyanya tu? Kwenye Biashara Uwekezaji ampe Deo Mwanyika, kina Sumri, kina Shabiby, Abood etc, watu wenye uzoefu wa kufanya biashara.
Aunde Baraza dogo lenye mawaziri wenye uzoefu, ukiwa na mtu mwenye uzoefu, hawezi kupigwa kirahisi kama msomi mwenye vyeti lakini hajawahi kuuza hata toothpicks!
Ni ushauri tu.
Paskali