kwasiku anapokea 10,000 ambayo kwa mwezi ni sawa na 300,000 ukizidisha x 12 = 3,600,000 na bei ya pikipiki mpk unaikalia juu BOXER ni 2,500,000 ukitoa unapata faida kwa mwaka mzima kapata 1,100,000.
Kumbuka hapo sijaweka bei ya service kubwa ambayo n jukumu la boss mwenye pikipiki,tufanye kwa mwaka mzima service ya pikipiki katumia 100,000 ukitoa kutoka kwenye ile faida yake ya 1,100,000 unapata baki ya
kwa mwaka mzima amenunua pikipiki ya 2.5M inayompa faida ya 1,000,000. ukigawa kwa siku 365 = 3,013 kwa siku,hii maana yake wanaofanya biashara ya pikipiki wakawapa madereva mikataba Faida yao kwa siku ni BUKU 3.
Buku 3 tukimaanisha ELFU 3 biashara yenye mtaji wa 2.5M 🙌 🙌,kuna biashara zinahitaji moyo sana mtu kuzifanya,biashara yakutoa faida 3,000 kwa siku hivi nikiwa na mtaji wa 100,000 siwezi pata kweli? tuongelee hii faida kwa siku 3,000Tsh.
Maana yake boss ukipewa 10k kwa siku na dreva,yako ktk hiyo ten ni 3000 tu sasa ndugu zangu wamiliki pikipiki hizi hesabu mnazifahamu au hamna haja nazo?