Ushauri: Kazi ya aibu malengo hayatimii

Ushauri: Kazi ya aibu malengo hayatimii

Umeandika vyema vile nilikuwa nawaza.
Kwa hesabu hizi huwa sioni lengo la mkataba kwenye pikipiki.
Bila Shaka wenye uzoefu watakuja kutuelimisha vizuri,maana bado hainiingii kichwani kuita hii ni biashara labda tutafitie jina lingine
kwa upande wangu siiti biashara ila naiita ni kibubu,mtu ananunua pikipiki ili atunze hela yake kwamaana nyingine kaepuka kuweka hela kwenye kibubu kaamua nunua pikipiki,kibubu si biashara kibubu ni kibubu tu.
 
Vipi bajaji mkuu?

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
kama unaendesha mwenyewe naweza sema ni biashara ila kama huendeshi bado siiti ni biashara kwasababu ni kumnufaisha tu huyo uliempa akuletee hesabu.

kwangu mimi mpaka kitu nikiite biashara ni lazima sifa ya kwanza kininufaishe mimi,kinifaidishe mimi kisha wewe mfanyakazi au msaidizi au msimamizi wangu ndio ufuate.

Bajaji/PikiPiki ni viingiza hela ila kwangu siviiti biashara kwasababu havianzi nitajirisha au nifaidisha mimi anaanza faidika dereva wa chombo sasa hiyo biashara ushubwada? yani dereva ndio anakua boss wakati mimi ndio nimetoa mihela yangu kununua chombo,ujinga huo hii kwangu si biashara otherwise dereva wa pikipiki/bajaji hiyo uwe wewe mmiliki.

kama dereva ni wewe mmiliki bajaji/pikipiki hizo ni biashara tena biashara ambazo kila mwenye uwezo wa kuifanya namshauri aifanye maana sio tu inalipa ila inalipa kweli kweli na kwa haraka ni biashara inayoweza kukutoa toka 0 to 100 kwa muda mfupi sana ukiwa na malengo.
 
Back
Top Bottom