Ushauri: Kazi ya aibu malengo hayatimii

Ushauri: Kazi ya aibu malengo hayatimii

Wasalaam wapendwa

Mimi ni kijana ninamiaka 26 nafanya kazi ya kufagia kwenye hotel moja nimejichanga. Sasa nina milioni 3 lakini nikiangalia mbele sioni mwanga wa kazi hii

Naombeni ushauri niachana na hii kazi ya kufagia kwa sababu mimi ni mtoto wa kiume je nikiacha mnanishauri nifanye biashara gani kwa mtaji huo wa milioni 3?

Karibuni kwa maoni yenu wakuu
Unapatikana wapi kwa sasa mkuu?
 
Usiionee aibu kazi yako. Hilo moja. Hata Ulaya, Japan na nchi nyingine zilizoendela kuna wafagiaji. Na ni hao hao wazungu, Wajapan... Hiyo haina maana kuwa ufe ukiwa mfagiaji. Kwanza ipende kazi yako. Halafu jikaze usevu pesa. Weka akiba mpaka pale akiba itakapo kuruhusu kuondoka na kufanya biashara, kama unapenda biashara.
Wewe muache tu alete ubishoo hiyo ilikuwa miaka ya 90 siku hizi watu hawachagui kazi kinachoangaliwa ni mpunga tu.

Yaani namhakikishia mtoa mada akiacha tu hiyo kazi haichukui wiki anaingizwa mtu mwingine.

Usije kuidharau hata siky moja kazi inayokuingizia kipato yaani utapata laana utashangaa kila biashara unayoiweka haiuziki halafu utaanza kuikumbuka hiyo kazi na hutoipata.

Afadhali labda kama una mke unaanzisha biashara mke anasimamia wewe unaenda kazini kuchakarika
 
Duuuh laana tena mkuu! Sina mke
 
Fungua kampuni ya kufanya usafi majumbani kwa watu, Kuvua nguo, Kufanya usafi wa nje ya nyumba nk kwa sababu umebobea katika mambo hayo, Unahitaji tu nguvu kazi ya vijana na matangazo ili kuwafikia kastama, Watu wengi sana wanahitaji wasaidizi wa kazi za usafi lakini hakuna anaesubutu kufanya hivyo.
 
Asante mkuu ushauri mzuri aisee
 
Ushauri mzuri sana, ila si kwa hilo salio mkuu
Tafuta sehemu ambayo haijaendelea Sana tafuta uwanja wa barabarani kwa 2M hafu 1M Anza biashara yoyote ili mradi sehemu ni ya kwako hakuna pango lazima utaenda tu.

Mm huwa ninamini ardhi ni utajiri wa kwanza ukishakua nayo mambo mengine yanakuja tu sijui kwa wengine wanaonaje.
 
Ondoa hilo neno, kazi ya aibu

Ushauri wa kufungua saluni na boda umekaa sawa,

Boda itakuwa ni nzuri zaidi na upige wewe mwenyewe
 
Labda unajua kipato chake kwa siku mkuu
jamaa ananiambia kuna siku huwa analaza hadi 50 au 60 na siku zingine chini ya hapo au pungufu ya 30, sasa sijui kama ni kweli ila pikipiki ni yake.

ninachofahamu ni kuwa sasa anajenga kibanda chake
 
Back
Top Bottom