Sina ujasiri wa kuacha kazi

Sina ujasiri wa kuacha kazi

Simara

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2014
Posts
7,613
Reaction score
24,249
Habari wana JF.

Mtanisamehe kama nitaandika bila mpangilio, wengine hatuna utaalamu sana wa Lugha.

Wale watu wa dhihaka na kuona mtu akileta mada humu mnaona anajisifia plz, naomba mkae pembeni.

Nilijiekea dhamira na malengo nikifikisha 40 yrs nitaacha kazi sababu malengo yangu yatakua yametimia, ila Mungu ni Mkuu nimetimiza malengo yangu mwaka jana December nikiwa na 38 yrs.

Ila naogopa sana kuacha kazi, nimejikuta sina ujasiri kabisa.

Kwanini naacha kazi??
1. Sina passion na kazi hata kidogo, sipendi kuajiriwa.

2. Mshahara ninaopata kazini, naupata kwenye biashara tena zaidi pia niliweka FDR ambako nako kunanipa hela nzuri tu kila baada ya miezi 3. Hivyo, hata nikiyumba kibiashara nina uhakika wa kupata hela nzuri tu. Pia nina vitega uchumi vingine nisingependa kuviweka wazi ila vipo vinajiendesha vyenyewe mimi ni kupita tu kuangalia mara chache.

3. Kulea watoto wangu kwa ukaribu zaidi roho inaniuma kwa week napata siku mbili za kukaa full na watoto wangu.

4. Mume wangu anasafiri sana, hivyo nakosa muda wa kukaa nae pia anakua ananihitaji nimsindikize kwenye safari zake nashindwa. Natamani nipate muda zaidi nimlee pia Mume wangu

pamoja na yote hayo najikuta nakosa ujasiri kabisa, mlioacha kazi mliwezaje? Mlipata changamoto gani? Mlijutia? naomba ushauri.

Nimeona heri niombe ushauri huku sehemu ambayo sifahamiki.
 
Kama umejiweza vilivyo m ushauri wangu ni bora uache kazi usimamie biashara zako angali saivi una nguvu zako ukifika 60 ubavu huo huna tena kama sasa

Ongeza familia watoto wawili ni kidogo sanaaa fikiria kesho yako usijekosa ata wa kumtuma dukani
 
Kama umejiweza vilivyo m ushauri wangu ni bora uache kazi usimamie biashara zako angali saivi una nguvu zako ukifika 60 ubavu huo huna tena kama sasa

Ongeza familia watoto wawili ni kidogo sanaaa fikiria kesho yako usijekosa ata wa kumtuma dukani
Asante kwa ushauri Mkuu.
Nina watoto wanne.
 
Upo public au private?
Public

Hiki pia kinachangia, nilijaribu kumshirikisha mzazi wangu mmoja naacha kazi alifunga kuniombea sababu Taasisi ninayofanyia ni moja ya Taasisi ambayo inanibeba sn na inafanya mtu akijua upo sehemu hiyo unapata msaada kwa haraka, so kwetu wanaona kama nimechanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom