Mkuu kwanza ili upate vitu bei rahisi inabidi utafute mtu anaemaliza unaongea nae bei ya kitanda na godoro kama anavitu vingine vizuri vya ndani basi chukua kwa bei ya maelewano yenu......5/6 kitanda ni 90 hadi 100 hiki ni kizuri kweli used godoro ni 100 hadi laki 120 kwa bei hii linakuwa zuri sana na ambalo halibonyei katikati.....
vyombo na vitu vingine kama pasi,gesi,feni,mziki hivi vyote unaweza washusha wanaomaliza....mfano gesi wanauzaga 20 hadi 30,na pasi 20 pia....
ishi kwa kujibana nakumbuka nilikuwa nakula 1000 siku nyngne 500 kwasiku nikasave hadi mil 3 lak 4 bila mkopo......hata ukiwa na hela usiifuje bila sababu...
Mishe ya kufanya inategemea na unasoma chuo gani na course ganj, ila kuna mdada dodoma chuo alikuwa anauza juice vidumu 3 hadi 4 hii alikuwa anaweka kwenye migahawa kama 2 hivi....pia kuna kuuza viatu vya kike na makava ya simu (kabla lecture haijaanza unatangaza pale mbele ya wengine), vilevile unaweza kuwa unaagiza mpunga shinyanga au mbeya (inategemea na umbali wa chuo chako) alafu unakoboa then unawatangazia wenzio na vioffer vizuri hauwezi kosa pesa.....
Pia unaweza kununua nguo za mtumba magauni,sketi,brouse,suluari hizo kuna connection ya ilalaboma unaoata kea 2000 na elfu 1500 hadi za 500 zipo...ila suluari ni kuanzia 3000 hadi 5000 mara nyingi nzuri ni elfu4 na elfu 5...hizo nguo wanachuo wakike wanapenda pendeza kama ni quality nzuri utapata pesa tu....
Mishe zako zinaweza kuwa viziri endapo ukioata mwanamke anaejitambua, kuna wamaobahatika na wanatoboa mfano kuna mshkaji wangu alikuwa na girl wake wao walikuwa wanauza juice, dagaa, mchele alafu kuna wengine walifungua genge (zamzam kusimamia)