Ushauri: Chadema achaneni na ndoto za urais!

Ushauri: Chadema achaneni na ndoto za urais!

Mzee hakuna chama kitafanikiwa kushika dola bila kupata sapoti ya wasio wanachama kama independent voter ambao ndi wengi,kudhani nyie cdm mtafanikiwa kwa kutumia wanachama wenu ni kujidanganya,hao ccm wenyewe wanashinda kwa kuwa wanapigiwa kura hata na wasio wanachama,mkijifungia kwenye kachumba kadogo ka chama cha wanachama mtachukua muda mrefu sana bila mafanikio.Mnahitaji kuvutia watu kama mimi pia ambao sio wanachama ili tushawishike kuwapigia kura.CHADEMA ina wanachama wangapi tanzania nzima?je kura zao pekee zinatosha kuwapa dola?amka usingizini hata kama usingizi ni mtamu kiasi gani mzee
lini m.a.g.a.m.ba walipigiwa kura zaidi ya kuchakachua,nenda hukohuko kadanganyane na akina nepi ooo sorry nape
 
It is amazing kujiona umeamka...na wengine bado wako usingizini.... Kama kweli umeamka basi bado unatembea huku unausingizi...usingeweza shauri Slaa arudi tena kwenye ubunge hana faida tena kule kazi yake imeshachukuliwa na wabunge wengi tu wa cdm. Hata kama Slaa hagombei urais ni bora akabaki katibu mkuu kuliko kugombea ubunge akafanye nini ameshavuka level hiyo....
 
lini m.a.g.a.m.ba walipigiwa kura zaidi ya kuchakachua,nenda hukohuko kadanganyane na akina nepi ooo sorry nape
Endelea kuuchapa usingizi..kama umekaa chini na bado unaamini umesimama matokeo yake huwezi kusimama kamwe,kwanza inabidi ukubali kwamba umekaa chini ndio uweze kusimama.Ukweli ni kwamba kuna mahali mnakosea nyie wapinzani wa bongo,ndio mana hamfanikiwi kutokana na ubishi na kujua kwingi,hebu tazameni wenzenu wote majirani wamefanikiwa ni nyinyi tu ndio mpaka leo mnasota kukiondoa chama kilichotawala toka tanzania ipate uhuru...hakuna chama kilichosalia madarakani kwa kipindi chote cha uhuru zaidi ya ccm,yote hiyo ni kutokana na wapizani wa bongo kutojua kujipanga;mngefuata ushauri wa nyerere kupitia kwa mrema 1995 wa kuweka nguvu kwenye ubunge mgekua mmeshafanikiwa sasa,lakini ndio mana tunasema hamjachelewa wekeni nguvu kwenye ubunge achaneni na urais,mtafanikiwa kirahisi.
 
Endelea kuuchapa usingizi..kama umekaa chini na bado unaamini umesimama matokeo yake huwezi kusimama kamwe,kwanza inabidi ukubali kwamba umekaa chini ndio uweze kusimama.

Jibu swali langu why cdm wafanye hivo na siyo CUF, TLP, NCCR, nk?
 
It is amazing kujiona umeamka...na wengine bado wako usingizini.... Kama kweli umeamka basi bado unatembea huku unausingizi...usingeweza shauri Slaa arudi tena kwenye ubunge hana faida tena kule kazi yake imeshachukuliwa na wabunge wengi tu wa cdm. Hata kama Slaa hagombei urais ni bora akabaki katibu mkuu kuliko kugombea ubunge akafanye nini ameshavuka level hiyo....
Hata mbowe alishavuka kama kigezo cha kuvuka ni kugombea urais,hoja yako hapa inakua dhaifu sana labda ulete nyingine,otherwise endelea kuuchapa usingizi.
 
Jibu swali langu why cdm wafanye hivo na siyo CUF, TLP, NCCR, nk?

Nimelidharau kwa kuwa unaonekana una tatizo la kukurupuka kuchangia bila kusoma vizuri thread...ungesoma vizuri hili swali lako lisingekuwepo kwani jibu lake liko kwenye thread,kweli ukitaka kumficha mtz jambo liweke kwenye maandishi,hivi kwanini hampendi kujisomea nyie watu?
 
ungesema
chadema waache kusimamsha wagombea
kwa sababu ya uchakachuaji wa kura kama mlivo chakachua matokeo ya uraisi hapo sawa,kodogo ningekuelewa.
maana kwenye ubunge nako
mtachakachua kama kawa,halafu utakuja tena na mawazo yako hafifu.chadema muachane na ubunge mukeze nguvu kwenye udiwani?
 
Speed ya Chadema inawaogofya magamba kwa hiyo mnaamua kutoa ushauri ili magamba yenu yasiwavuke. Ushauri wako kawape CCM wenzio waambie 2015 wasigombee maana wataambulia patupu. Finito
 
Tatizo Kim mwenyewe amekimbia, lakini namsifu kwa kujibu hoja za watu bila kutetereka!!
 
kwa hiyo unaamini kabisa chadema watakusikiliza!? Na kufuata ushauri wako!? Unajua wewe una mawazo ya kimasikini kabisa!? Yaani ni sawa sawa na kumwambia mtu bora uwe masikini tu naona utajiri umekushinda!? Unajua mtu au mwanaume kama mwanaume inabidi uhustle au ustraggle, so chadema ni mwanaume inabidi ahustle, unajua katika kuarchive something masnitch huwa wana exist, snitch mmoja ni kama wewe, Never forgive up chadema, walianza na wabunge 5 je unajua sasa hivi wapo wangapi!? Kama wangekuwa wanafuata ushauri kama wako unadhani ingekuwaje!? Sasa hivi wameteka kanda ya ziwa,kaskazini kule kusini Mbeya na Iringa pamoja na mpanda kati je unadhani zamani ilikuwaje!? no retreat, no surrender, freedom is coming tomorrow!

ningekugongea like mkuu sema basi tu natumia aka kasimu akana opt ya like.
 
Inaonekana unajua unachosema, kwasababu hatuna tume huru ya uchaguzi ccm itatumia dola kuhakikisha urais hautoki mikononi mwao, lakini umesahau watakapoona hakuna chalenge kwenye nafasi hiyo watajiimarisha zaid kuchakachua kwenye majimbo. Tukiwa na tume huru ya uchaguzi na fair play ikazingatiwa utakuwa muda muafaka kutoa huo ushauri kwa wapinza. Kwasasa nivema wapinzani washambulie pande zote ili angalau huyu mdudu ccm (mwizi wa mali za wanyonge na muasisi wa ufisadi) alemewe achoke na hatimaye afe.
 
Speed ya Chadema inawaogofya magamba kwa hiyo mnaamua kutoa ushauri ili magamba yenu yasiwavuke. Ushauri wako kawape CCM wenzio waambie 2015 wasigombee maana wataambulia patupu. Finito

kumbukeni lakini hata Igunga kabla ya uchaguzi maneno yalikua ni haya haya hapa,lakini baada ya uchaguzi mkawa mnalaumiana wenyewe kwa wenyewe na mabegi kibao ya visingizio ikiwemo ile sababu ya kudumu ya kuibiwa kura kila tunapokuwa tumeshindwa,lakini tukishinda huwa hatusemi na sisi labda tumeiba kura,hii ndio ajabu yake.Mi naomba mdau kama tunaona ana hoja tumjibu kwa hoja tuache jazba mawazo yake pengine yanaweza kuboreshwa yakasaidia kwa namna moja ama nyingine
 
halafu jamaa anakataa tusilikune khaa!! tutalikuna mpaka litoke damu.

Tatizo wengi hamna hoja naona mnanichosha tu labda tusubiri kesho asubuhi yatakuja majembe ya chadema yenye hoja...
 
Tatizo Kim mwenyewe amekimbia, lakini namsifu kwa kujibu hoja za watu bila kutetereka!!

Tatizo hawa jamaa kuna kitu wanacho wanataka kuniambia lakini jinsi ya kukiwasilisha ndio tatizo ngoja tusubiri majembe yao asubuhi labda yatakua na jipya,hawa nimewashika pabaya ndio mana wengi wao wanaleta vioja tu kasoro mmoja tu ndio ameongea kidogo kitu kinachoeleweka!
 
..Slaa aachwe nje ya bunge akifanya kazi ya kukijenga chama btn now and 2015.

..2015 CDM watakuwa na wakati mgumu sana kwasababu majority ya wagombea wao itabidi wasimame wenyewe wakati wa kampeni.

..bila kuimarisha chama ktk ngazi ya wilaya na kata basi CDM wasahau kuchukua Uraisi, pamoja na kuunda serikali.
 
Nambie nchi au uchaguzi wowote ambao chama kilishinda na kuongeza hesabu ya WABUNGE bila kuwa na Mgombea Urais mzuri..Pengine hufahamu misingi na malengo ya ya uchaguzi mkuu..Uchaguzi siku zote unaanza na kujipanga na mgombea Urais kwanza, na hata Marekani unaona nguvu kubwa inawekwa ktk mtu wa kupambana na Obama, huyu akiwa na nafasi ya uhsindi ndiye atawarahisishia Wabunge Ushindi wao pia na akiwa sio chaguo la Wananchi basi hata nafasi ya wabunge kushinda hushuka.

Malengo ya kugombea Uchaguzi mkuu ni kuongoza nchi na sio kuwakilisha majimbo. Kwa taarifa yako tu hakuna chombo kinachoweza kwenda pasipo kiongozi, Hata mtumbwi unaotegemea nguvu ya wapiga kasia ni lazima uongozwe na nahodha mzuri..
 
Back
Top Bottom