Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
ulijuaje kuwa msaliti na mnafiki anayetajwa ni zitto?

si mwenyewe ulimtaja jana! Ukaandka na no za uwongo eti zilituma hela kwa kina ben sa8.! Mwenye akili anajua kua boss wako anamaansha zitto
 
Siasa za ukabila.You're stooping too low.Kama kuna kiongozi au mwanachama wa CHADEMA ambae CCM mnamhusudu sana basi mchukueni akagombee huko kwenu.

Interesting indeed.....!

sijaona kilaza kama huyu jamaa, wama jf hamna haja ya kujibizana na mpuu* zi kama huyu mchumia tumbo akishirikiana na mc lema kukiharibu chama. Watu wa arusha nawaonea huruma kwa kuwa na mbunge ambaye hajui kujenga hoja ila ni mtu wa vurungu. Lenma katetee wananchi wako kama ukitaka kumchafua ZZK, utapotea ktk siasa za nchi hii. Hakuna mtu ambaye hamfaham ZZK uaminifu na uzalendo wake kwa nchi hii na ndani ya cdm hamna anaeutilia mashaka hata kidogo. Kumbuka adui yako ni CCM na sio ZZK.
 
si mwenyewe ulimtaja jana! Ukaandka na no za uwongo eti zilituma hela kwa kina ben sa8.! Mwenye akili anajua kua boss wako anamaansha zitto

unamaanisha mnafiki na msaliti tunayemjadili ni Zitto?
 
Wakati Lema unajiandaa kumchafua Zitto na article yako namba two ya kufikirika ebu kumbuka msemo maarufu 'what goes around comes around',Think twice!

mbona hamkumwambia zitto wakati anawashauri wale madiwani wa arusha wagome,katkati ya kampeni arumeru anatangaza uraisi ....ndio comes around yake
 
we are not interested in these cheap F4F , internal wranglings za CHADEMA.
Leteni mambo ya kitaifa hapa,
QUOTE=Mshombsy;7723170]

Maelezo ya Lema juu ya CHADEMA kuwafukuza wanafiki kwa kufanya maamuzi magumu ni ya kutafuta kuungwa mkono na wanachama wa CHADEMA, sioni ubaya kabisa kwa kusema ndani kuna wanafiki. Wale wanaosema angeongelea kwenye vikao nadhani ameonyesha kutekeleza ilo kwa kusema chama kifanye maamuzi magumu hata kama 2015 hawatashika dola lakini watakuwa wamebadilisha watu fikra.

Maelezo yake hayatofautiani na Zitto aliposema Kuna mbunge wa upinzani anadai kuwekewa kauzibe kwenye posho. Na hii mngesema basi Zitto angeitolea kwenye vikao vya chama na si kwenye majukwaa ya kijamii.

Zitto aliitoa ili apate huruma ya jamii kwasababu inagusa jamii. Lema hapa ni kwa wanaCHADEMA suala la wanafiki litakapofika kwenye chama.

Niseme tu kwamba namuhusudu Zitto kwa ujasiri wake wa kupambana lakini anashindwa kuelewa lengo la yeye kuwa mpinzani ni nini na kwanini yuko CHADEMA.

Ninaachokiona kwa watu hawa wawili hasa upande wa Zitto ni kuwinda pointi za kisiasa zaidi kuliko kupeperusha itikadi ya chama. Itikadi ina umuhimu kwenye chama kwani ndo inatoa mwelekeo na inaunganisha wanachama.

Hivyo lazima itikadi itetewe, ifagiliwe na itafutiwe pointi za kisiasa ili kuvuta watu zaidi kwenye chama na hii ndo lengo la Lema. Zitto anaenda kinyume ni yeye tu yani anamwangalia Zitto atoke vipi. Kwa mambo yanayogusa maslahi ya umma ni vizuri kuwa na msimamo wa ki-chama.

Ukianzia suala la posho, kukaguliwa na CAG ni wazi Zitto mbali ya kuwa naibu katibu hakuwahi kuhuliza chama chake msimamo juu ya posho na kama kimekamilisha hesabu kwa mujibu wa taratibu kabla ya kulifikisha mbele ya kamati za bunge.

NI KWANINI ALILIPELEKA SUALA LA HESABU KAMATI YA BUNGE? Anajua kabisa kwamba maono ya wengi ni kwamba CHADEMA ni cha wenyewe, yeye anatengwa kitu ambacho si kweli, alijua kabisa watu watasema jamaa wa Kanda ya kaskazini hawajakamilisha hesabu na kuna kitu hapo. Lengo lake lilifanikiwa.

Utategemea Naibu katibu mkuu ahakikishe Chama chake kinakamilisha hesabu ili kisimwaribie uhadilifu wake mbele ya wanakamati, hiyo miaka yote alisema hawawakilishi hesabu alikuwa haudhulii vikao na kuuliza kama walishawakilisha kwa Msajili? Ni kucheza na fikra za watu "chama cha kikanda, chama cha wenyewe". Na anaelewa kabisa mwisho wake ungekuwa hivyo. Mahojiano na clouds fm alisema ikifika zamu ya CHADEMA yeye hatakuwa mwenyekiti wa kikao cha kamati kuondoa mgongano wa kimaslahi. Hii inaonyesha anajua yeye ni CHADEMA, kwanini hakuwapelekesha wahasibu wa chama na viongozi wenzake kulinda heshima ya chama ambacho ye ni kiongozi.

Tukirudi kwenye suala la posho hivi hawakuitana wabunge wa CHADEMA kabla ya kikao cha bunge na kuwa na uhamuzi wa pamoja?. Lakini akasimama mwenyewe na kusema hataki posho. Ikalazimu Chama kutoa taarifa badae kumuunga mkono juu ya posho.

NANI AMESIKIA WABUNGE CCM NA WINGI WAO WANAKATAA POSHO HATA MABILIONEA KAMA MO DEWJI? Hakuna. Wali-caucus na kuja na uhamuzi wa pamoja kwa manufaa ya chama wa kuunga mkono posho. Kama ingewazamisha ni wote si mmoja mmoja.

Hii ndo ilikuwa hoja ya Lema kwa kila nafasi mtu aliyonayo awe mbunge, mwanachama au kiongozi ni kukipigania chama, kukipa pointi za kisiasa, kujua lengo ni chama kuchukua dola, kuvutia wanachama

Inawezekana lugha ya Lema haikustahili lakini ujumbe wake ni kwa watu kujitambua kwanini ni wapinzani na kwanini wako chama fulani.

Natambua Zitto analitumikia taifa kama mbunge lakini haiondoi wajibu wa kukikuza chama kwa hoja za pamoja.

Hatutaki kumpa mtu urais alafu aanze kutafuta pointi za kisiasa za jumuiya ya Afrika Mashariki.[/QUOTE]
 
Ondoa neno kuchafua. maana linaondoa dhana ya uwazi.

Hakuna mtu anayemchafua mtu, bali ukweli unawekwa wazi watu wajue

Hivi unaijua dhana 'UWAZI' kweli au umeikariri tu poor thing,to play a some's lap-dog is really an exhausting job..By the way mnaogopa nini kuitisha kikao kuutafuta ukweli kuhusiana na tuhuma zenu dhidi ya Zitto?Kuja huku mtandaoni na kujaribu kumchafua Zitto hamtafanikiwa kabisa kwasababu pia Zitto ana watu wake huku wanaomkubali na wameapa kufa naye.
 
ndani ya chadema mwanasiasa mwenye mizania ya Zitto ni Dr.W.Slaa peke yake wengine wanafuatia hawa kina Godbless J Lema ni makinda sana kisiasa walipata kura kwa sababu wananchi walichoshwa na CCM zile zilikuwa ni kura za hasira tu
 
Last edited by a moderator:
Mheshimiwa Lema,

Naamini wewe ni mtu mwenye busara na ndio maana wananchi katika jimbo lako wamekupa dhamana ya kuwawakilisha Bungeni. Hivi kwa busara zako, hayo malumbano mnayoendeleza hapa JF ilhali mna vikao mwafaka ndani ya chama ni kwa manufaa ya nani?

Kwa sie ambao angalau tunaafikiana na harakati zenu za kuikomboa Tanzania kutoka katika lindi la umasikini unaorutubishwa na ufisadi, tabia hii ya kugeuza social media kuwa kumbi za kujadili masuala mnayoweza kuyajadili ndani ya chama inatuvunja moyo sana.

Pamoja na kutofautiana kwangu na Zitto katika masuala mbalimbali, napingana nawe kwa nguvu zote katika uamuzi huu ambao naomba uniruhusu kuuita usio wa busara hata chembe wa kujadili tofauti zenu za kimtazamo mtandaoni.

Majuzi niliandika makala hii Makala yangu Ktk RAIA MWEMA Toleo la Okt 30, 2013: "CCM Itang'oka, Chadema Itaweza Kuongoza?" ~ Kulikoni Ughaibuni ambayo awali ilichapishwa kwenye jarida la RAIA MWEMA na moja ya maswali niliyouliza ni utayari wenu kuongoza Tanzania pindi CCM iking'oka madarakani.

Haihitaji darasa maalum la uongozi kutambua kuwa malumbano ya hadharani baina ya viongozi wa ngazi za juu wa chama chochote kile hayajengi, regardless ya mantiki ya mada husika.

Mmekuwa mkilalamika kuhusu hujuma mnazofanyiwa na CCM na taasisi za dola, na wengi tuliwaunga mkono kwani ili demokrasia ya kweli ifanye kazi thabiti shurti kuweke level field. Lakini yayumkinika kuhitimisha kuwa kwa mwenendo huu wa kujibishana kwenye mitandao ya jamii, adui yenu mkubwa kwa sasa ni ninyi wenyewe. Tofauti zenu za kimitazamo zinaweza kujadiliwa na hata kumalizwa ndani ya vikao husika, if not katika maongezi binafsi as viongozi wa chama kimoja.

Hebu jiulize, pamoja na uselessness yao na hata kukinzana kwao, when did you see Nape na Lowassa wakija JF 'kuonyeshana ubabe'? Si kwamba hakujawa matukio yanayoashiria bayana uwa wanasiasa hao 'picha haziivi' lakini angalau wana akili na busara za kutambua kuwa tofauti au hata uhasama wa kisiasa shurti viandane na kuthamini maslahi ya Chama chao.

Huu ni ushauri wa bure tu lakini una haki ya kuupuuza. Nimalizie kwa kukuuliza, hiyo kesho ukishatundika kuhusu 'Unafiki wa Zitto kuhus posho' itakisaidia vipi chama chenu katika harakati za kuing'oa CCM hapo 2015?

Swadakta kaka CHhli huyu lema anaonesha moja kwa moja kuwa chuki ndizo zamuongoza kufanya maamuzi yake....kwa mara ya kwanza Nimeona hata magazeti makini ya uchunguzi yakimmulika kuwa jamaa hana busara. Mambo kama haya yaliitokea NCCR Mageuzi....tafakari.
 
Hivi unaijua dhana 'UWAZI' kweli au umeikariri tu poor thing,to play a some's lap-dog is really an exhausting job..By the way mnaogopa nini kuitisha kikao kuutafuta ukweli kuhusiana na tuhuma zenu dhidi ya Zitto?Kuja huku mtandaoni na kujaribu kumchafua Zitto hamtafanikiwa kabisa kwasababu pia Zitto ana watu wake huku wanaomkubali na wameapa kufa naye.

hicho kiingereza chako dah!

anyway, kinachoshangaza ni jinsi mnavyomtaja zitto, ambaye hakutajwa na mtoa mada. hii inaonyesha dhahiri mnafahamu hakuna mnafiki na msaliti ndani ya chadema zaidi yake. Suala la kuwa na watu wa kufa naye siyo ajabu kulisikia kwako. huyo msaliti alishakuwa na mtandao ndani ya chama na nje ya chama hivyo siyo ajabu vile vile akifa na mtandao wake.
 
ahaaaa......
hapo sawa.
nadhani kwenye thread ya baadaye tutaona picha halisi ya nini
tutajadili.

bado tunasisitiza kuwa nia na dhamira ya chadema ni kufuta posho zote za
hovyo. Siyo kukataa posho za wazi halafu gizani unapokea fedha
chafu???

Hii ndio hulka ya wanasiasa wengi, mambo wanayoyafanya na wanayoyasema
mbele ya wapiga kura wao ni tofauti na yale wanayoyafanya sirini. Ndio
maana binafsi simwamini na si mfuasi wa mwanasiasa yeyote lakini ninaiamini misingi wanayoisimia.

Katika hili la kupinga Sitting Allowance, nasimama na misingi
anayoisimamia Mh. Zitto, nikiamini nimesimama na misingi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo.

Haya ya sirini/gizani yakijulikana yawekwe wazi katika njia ambazo chama kimejiwekea. Na kama kuna jinai basi sheria za Jamhuri nazo zichukue mkondo
wake. Tujiepushe kuwa wapelelezi wenyewe na watoa hukumu kwa wakati huo
 
Chadema mnazidi kujidhihiri namna tulivyo wadhahifu kihoja na tuliokosa utaratibu wa kueleweka wa namna ya kukabiliana na matatizo ya ndani kama haya.Jamani ndani ya Chama kuna utaratibu wa kuitisha vikao?Kwanini msiitishe hivyo vikao na kuyajadili haya mambo badala ya kukimbilia mtandaoni na kuvuana nguo?Mnakuwa kama watoto bana!Badilikeni bana acheni hizo immatured politics zenu mtakiua Chama.Na hawa Viongozi wakuu wa Chama wananipa wasi wasi na ukimya huu,Mpaka sasa sijasikia tamko lolote kutoka Makao makuu hii inamaanisha kuwa haya yote yanayojiri hapa mtandaoni yana baraka kutoka Makao makuu kwasababu haiwezekani wakati Mwigamba alipofanya hivi walikuwa wepesi kujibu hata kama waliishia kujivua nguo zaidi kuliko kujisafisha lakini mradi walijibu kwa wakati.
 
Lema kama mapambano umeyaanza na wanachama wenzako na kuwaweka CCM pembeni jua kuchukua dola itakuwa ngumu kwenu,unajinasibu kutetea wananchi wakati si kweli wewe pia ni mchumia tumbo,mtu maslahi.

Kweli naamini hakuna mwanasiasa mwenye nia ya dhati katika kuwasaidia wananchi ikiwemo wewe Lema.
 
hili bandiko la Lema sio msimamo wa chama ni chuki zake binafsi kwa Zitto

ameongelea usaliti na unafiki kama kusimamia sheria ndio usaliti na unafiki mwacheni Zitto awee

Joto hasira ya Posho kaja kuimalizia JF

dhambi ya uoga hata biblia imesema waoga hawataingia mbinguni

Lema kuthibitisha wewe sio mwoga mtaje huyo msaliti

ni bora kutompa mtu tumaini kuliko kumpa mtu tumaini la uongo

chadema mna laghai wananchi kwa kichaka cha UKOMBOZi

ukombozi uliojaa magumashi, baada ya Zitto kushtukia mnamwita msaliti

natoa special tribute kwa Neiwa kwa comment za maridhawa
 
Last edited by a moderator:
Lema kama mapambano umeyaanza na wanachama wenzako na kuwaweka CCM pembeni jua kuchukua dola itakuwa ngumu kwenu,unajinasibu kutetea wananchi wakati si kweli wewe pia ni mchumia tumbo,mtu maslahi.

Kweli naamini hakuna mwanasiasa mwenye nia ya dhati katika kuwasaidia wananchi ikiwemo wewe Lema.

Kwa upeo wako mwanasiasa mwenye nia ya kuwasaidia wananchi ni wale wanaowapigia magoti wasaliti???!!

Poor you!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Nimefuatilia mjadala sana leo ukizingatia ilikuwa ni Jumamosi kwamba hatukuwa na kazi nyingi sana za Kibunge hasa baada ya kuanzisha mjadala unaosema " Usaliti na Unafiki unavyoliangamiza Taifa " na nimeona mjadala na nimejifunza mambo mengi sana sikumtaja Mtu ila Watu wengi wametaja majina ya Watu , sijui kwanini ? ila naendelea kutafakari , kesho nitaandika kuhusu mada inasema " UNAFIKI WA ZITTO KUHUSU POSHO " na mpaka saa nane mchana nitakuwa nimewasilisha na jambo hili halina mgogoro na kanuni za Chama kwani ni jambo liko wazi kwenye vyombo vya habari .

Asanteni

Vikao vya chama vipo na wewe ni mjumbe wa kamati kuu kwa nini usisubiri hukohuko kuliko kuja kuropoka jf.

yaani wewe jamaa sijui hata kama unawashauri wenye akili.

mkuu wewe hauna tofauti na Juliana Shonza na mtela mwampambe. ujinga uleule waliokua wanaufanya wao wewe unaurudia leo.

Lema unaua chama mchana kweupe.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la CHADEMA huyo wanayemwita msaliti ana nguvu na wakifuata njia za sheria na demokrasia anaweza kuwashinda kirahisi sana akawa yeye ndo mwenyekiti.

Sasa ndo maana wanazunguuka zunguuka kujaribu kutafuta loop hole ya kumuondoa.

Qanamuogopa huyo 'msaliti' kuliko wanavyoigopa CCM...
kumbe wewe ni zittofobia?
 
hicho kiingereza chako dah!

anyway, kinachoshangaza ni jinsi mnavyomtaja zitto, ambaye hakutajwa na mtoa mada. hii inaonyesha dhahiri mnafahamu hakuna mnafiki na msaliti ndani ya chadema zaidi yake. Suala la kuwa na watu wa kufa naye siyo ajabu kulisikia kwako. huyo msaliti alishakuwa na mtandao ndani ya chama na nje ya chama hivyo siyo ajabu vile vile akifa na mtandao wake.

How does it sound,mind-blogging or what?Don't mind anyway.Tatizo lenu mnaoshabikia Zitto kufukuzwa mna very narrow scope of modern world political understanding!Tafuta novel ya Mtunzi Sidney Sheldon inayoitwa 'The Sky is falling' ili uwafahamu wanasiasa na sura zao halisi.That's my only advice to you!!
 
ahaaaa...... hapo sawa. nadhani kwenye thread ya baadaye tutaona picha halisi ya nini tutajadili.

bado tunasisitiza kuwa nia na dhamira ya chadema ni kufuta posho zote za hovyo. Siyo kukataa posho za wazi halafu gizani unapokea fedha chafu???

GREAT THINKERS LETS tujaribuni kufikiria kidogo hizi issue hata watu tunao waamini ni safi CCM kama magufuli, mwakyembe, hawapingi posho!! ni kwa nini? ni kwa sababu hawana dili hata ya laki mbili out of hizo posho!! sasa wataishije? je ww povu linaekutoka ukiondolewa hiyo income yako utaishije?

kataa posho uwe na means yako nyingine ya kuishi either unafanya biashara au unaurithi kutoka kwa wazazi wako, hizi falsafa za eti principles ndicho nakiona kama unafiki!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom