Nimesikia na Kamanda Kileo nae anaandaa bandiko lake kuhusu usaliti wa Zitto, na kuwepo kwake gerezani.
Nadhani yeye hakujifunza kitu kutoka kwa Prison Graduate baada ya kutoka Segerea. Yeye Lwakatare, hakutaka kumnyooshea yeyote kidole, zaidi ya kuhimiza mshikamano kwa viongozi wote, na kushauri juu ya dhana ya kufukuzana kwa faida ya chama kikielekea kwenye uchaguzi 2014/2015.
Sasa kwa kuwa, viongozi wetu hawa wameona njia hii ya mitandao ya kijamii ndio njia sahihi kuelezea malalamiko yeo na CHAMA kinawaangalia basi ni vizuri tu.
Lakini ni vizuri zaidi sisi wapenzi wa mabadilo tukajiandaa kwa matokeo makubwa zaidi pale wanaoshutumiwa nao wakiamua kutumia njia hii hii kujibu mapigo. Kwan hata uvumilivu wa kibinadamu na kiuongozi una kikomo chake.
Kwa kuwa sisi nafasi zetu ni ndogo, kauli zetu si za kiongozi na sauti zetu hazisikiki, basi ngoja tukae pembeni ili tuwaone hawa wajuzi wa siasa wakivuana nguo hadharani. Ghafla swali linanijia, NI KWA FAIDA YA NANI?