Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
Mkuu kuna ushahidi usio na
chembe ya doa. Wacha tujitibu magonjwa sugu wenyewe kabla hatujaanza
kuwatibu wengine.
hili gonjwa la usaliti na unafiki wacha tulifanyie kazi kwa njia hii.
chama kimeulea ugonjwa muda sana

Mkuu wangu, kama kuna ushahidi usiotiliwa shaka, si kuna njia ambazo chama kimejiwekea! Sidhani kama JF ni mojawapo.

Huku si sahihi
 
mkuu kuna ushahidi usio na chembe ya doa.
mnataka huruma toka kwa wanachama. Ukweli mchungu ni kuwa hakuna wa kumgusa zitto hapo makao makuu mnamuogopa kuliko rama igondu. Mnalilialia tu,jaribuni kumfukuza muone!
 
We all knows that ZZK is betrayal and hypocrate but i dont think this a good way of judging/ criticise him.

Pamoja na kwamba Lema hajamtaja zitto kwenye post yake, hii conclusion yako ina hit point
 
hivi vitu ambavyo vinazungumzika na kupatiwa ufumbuzi jamani kuliko kupublicise kwa watu ehe Mola ibariki cdm hasa katika kipindi cha mpito.

Tunajua lema ana backup ya slaa kumchafua zitto. We dr heshma yako itashuka sana jama ukiendlea kufuata ushauri wa huyo mwehu lema.
Zitto ana backup kubwa chamani,mfukuzeni muone mbna mnalialia tu pemben kama watoto? Chama tumekjenga kwa shda hiki.
 
Mkuu wangu, kama kuna ushahidi usiotiliwa shaka, si kuna njia ambazo chama kimejiwekea! Sidhani kama JF ni mojawapo.

Huku si sahihi

Mkuu vuteni subira tuone kamanda atakavyotupia humu ishu ya unafiki wa posho, ambayo kwa imani yangu itabeba mambo mengi yenye taswira halisi ya huyu msaliti
 
Mungi usilete porojo hapa, weka ushahidi wa UKWASI wa ZITTO. alisha-declare mali zake kwenye tume ya maadili. zitto ahongeki kirahisi kama Godbless J Lema aliyehongwa milioni 30 akaachia ubunge mwaka 2005.

Nadhani humjui Lema wewe ndio unaona milioni thelasini ni pesa , tumeambiwa leo tutaambiwa unafiki wa Zitto kuhusu Posho
 
Zitto
anaungwa mkono na
chadema pamoja na Lema kukataa posho. tatizo ni pale Zitto anapokataa posho kinafiki. Hivi inawezekanaje Zitto akatae posho ya sh 80 elfu, huku anafanya matanuzi makubwa ya kifisadi? Zitto hana biashara nyingine zaidi ya ubunge lakini cha ajabu ana ukwasi wa kutisha. Anatakiwa
kuchunguzwa.

Zitto mtu wa ajabu... amekataa posho za elfu 80 za wazi, halafu anapokea
mabilioni ya kifisadi kificho tena ya hovyo yenye lengo la kuiangamiza
chama ambacho watanzania maskini wamekiamini.

Mkuu wangu, kuna kitu kimeanza kupotoshwa hapa.

Kumbukumbu zilizopo hazionyeshi kama Zitto anapinga (hachukui) hii posho
ya kujikimu (shilingi elfu 80). Posho asiyoichukua (anayopinga) ni ya vikao yaan Sitting Allowance (laki 2). Posho ambayo hata chama kilipendekeza ifutwe kabisa
 
Hapo ndipo utakapoona TOFAUTI kati ya Lema na Zitto katika hiki Chama.Wakati Zitto anaamini,anaishi na kuisimamia misingi ya Chadema Lema yeye anapingana na misingi ya Chama,Inashangaza kuona baadhi yenu mkiunga mkono hoja muflisi ya wakuja kama Lema dhidi ya Kiongozi Mkubwa kabisa ndani ya Chama,Kweli mmepotoka sana,You need to be exorcized from Lema satanism,Really.Kweli wakuja ni wakuja tu.
 
Hapo ndipo utakapoona TOFAUTI kati ya Lema na Zitto katika hiki Chama.Wakati Zitto anaamini,anaishi na kuisimamia misingi ya Chadema Lema yeye anapingana na misingi ya Chama,Inashangaza kuona baadhi yenu mkiunga mkono hoja muflisi ya wakuja kama Lema dhidi ya Kiongozi Mkubwa kabisa ndani ya Chama,Kweli mmepotoka sana,You need to be exorcized from Lema satanism,Really.Kweli wakuja ni wakuja tu.
Tuambie misingi ambyo Lema kavunja sio kupayuka tu bila fact.
 
Mkuu vuteni subira tuone
kamanda atakavyotupia humu ishu ya unafiki wa posho, ambayo kwa imani
yangu itabeba mambo mengi yenye taswira halisi ya huyu msaliti

Subira tunavuta, lakini tumehoji HII NDIO NJIA SAHIHI? Vikao halali vya chama havipo siku hizi?
 
Wakati Lema unajiandaa kumchafua Zitto na article yako namba two ya kufikirika ebu kumbuka msemo maarufu 'what goes around comes around',Think twice!
 
Godbless J Lema,
Mimi nakukubali katika harakati za ukombozi wa taifa hili. Lakini naomba kukushauri kitu kimoja: Katika siasa kubali kutofautiana na watu fikra. Na sio kila mara unaotofautiana nao fikra basi ni maadui zako. Ni wazi kabisa kwamba Mwenyekiti wetu Mbowe angesema nawachukulia kama maadui wale wote anaotofautiana nao kifikra, CHADEMA isingekuwa hapo ilipo.

Kila shilingi ina pande mbili. Sio sahihi kumjudge mtu kwa kuangalia weakness zake peke yake. Naamini CHADEMA imefika hapo ilipo kwa juhudi kubwa za viongozi wake WOTE na wanachama wake. Na ninaposema wote nina maana ya WOTE. Sio vyema mtu mmoja au kikundi cha watu kujiona kuwa wao ni bora zaidi ya wengine. Kila mtu anayo madhaifu yake kama alivyo na mazuri yake. Hakuna mtu aliyekamilika, sio CDM, sio CCM na sio popote.

Wanasema mbwa ukishamjua jina hakusumbui Lema.... Tafakari braza...

Huu ni ujumbe MUHIMU SANA kwa CDM. Na mmeshauriwa mambo yenu myamalize ndani ya vikao vya ndani, siyo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
 
Tuambie misingi ambyo Lema kavunja sio kupayuka tu bila fact.

1. Ilani ya CDM (2010-2015) katika suala la posho za vikao iko wazi kabisa. Msimamo ni kuzifuta kabisa, na si kwa wabunge pekee, bali kwenye mfumo mzima wa Utumishi wa UMMA.

Hoja kwamba CDM haiongozi Serikali hivyo kushindwa kuzifuta haina
mashiko, kwan wabunge wake walipaswa walau kuzikataa ili kuonyesha mfano

(kama afanyavyo Zitto)

2. Sheria ya Utawala wa Bunge ya Mwaka 2008 haiitambui posho hii
(Sitting Allowance). Kifungu cha 19 kinazitambua posho za kujikimu, usafiri na wasaidizi.

Lakini kifungu hiki cha 19 ndio kinatoa mwanya kwa Rais kutoa posho zingine kwa wabunge kwa namna anavyoona inafaa, na ndipo inapoingia hii
"Sitting Allowance"

Kimsingi posho hii ya vikao inatolewa kwa kudra za Mh. Rais ambaye pia ni M/Kiti wa CCM, anayetekeleza sera za CCM (kulipana posho za vikao). Sasa kwa mbunge wa Upinzani kumshawishi Rais awaongezee posho hii ni kwenda kinyume na Sera za CDM, ilani ya CDM na Misingi ya CDM ambayo tuliamini wabunge wetu wataisimamia
 
Mwenyekiti analalamika, katibu analalamika, naibu analalamika, wajumbe wanalalamika, wabunge wamalalamika, bavicha wanalalamika..hivi chadema hamna jinsi ya kukaa na kumaliza hizi tofauti zenu kwenye vikao vya chama? wafukuzeni hao mnaowaita wasaliti mbona shonza na mwenzie mliwafukuza? Fukuza na hao
 
The earlier a Cancer is detected, the easier it is to treat and more likely the treatment s going to be successfully. Nyie VIGOGO WA CHAMA endeleeni kufuga hilo GONJWA (CANCER). Hakika mwisho wake hautakuwa mzuri.:frusty:
 
Tuambie misingi ambyo Lema kavunja sio kupayuka tu bila fact.

Mbona unajichetua ufahamu?Si anapigania posho au hata hulijui mkuu,Suala la kupunguzwa au kufutwa kabisa kwa posho ilikuwepo katika ilani ya Uchaguzi wa mwaka 2010 na ni moja ya mambo ambayo Dr Slaa alikuwa anayanadi sana katika campaign zake za Urais.Wakati unamtetea mtu flani jaribu basi hata kumuelewa huyo unayemtetea misimamo yake ni ipi la sivyo utaishia kudhalilika na kuonekana mjinga!!
 
Mkuu wangu, kuna kitu kimeanza kupotoshwa hapa.

Kumbukumbu zilizopo hazionyeshi kama Zitto anapinga (hachukui) hii posho
ya kujikimu (shilingi elfu 80). Posho asiyoichukua (anayopinga) ni ya vikao yaan Sitting Allowance (laki 2). Posho ambayo hata chama kilipendekeza ifutwe kabisa

ahaaaa...... hapo sawa. nadhani kwenye thread ya baadaye tutaona picha halisi ya nini tutajadili.

bado tunasisitiza kuwa nia na dhamira ya chadema ni kufuta posho zote za hovyo. Siyo kukataa posho za wazi halafu gizani unapokea fedha chafu???
 
Wakati Lema unajiandaa kumchafua Zitto na article yako namba two ya kufikirika ebu kumbuka msemo maarufu 'what goes around comes around',Think twice!

Ondoa neno kuchafua. maana linaondoa dhana ya uwazi.

Hakuna mtu anayemchafua mtu, bali ukweli unawekwa wazi watu wajue
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom