Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
Mkuu mimi kama wa buku 7, sipendi CDM ife.
Inatusaidia sana kuona mabaya yetu, lakini hili la F4F wenu kutaka kufanya mapinduzi ndani ys CDM ili wawatoe real time thinkers linachekesha.
Of all the places bifu lenu mnalileta JF!
Kweli F4F noma.

bado humfahamu vizuri zzk wewe
 
Mheshimiwa sana Lema, kamanda ambaye nina imani nawe........katika hili siafikiani na wewe moja kwa moja. Nina mawazo sawa na yako kuwa yuko msaliti ndani ambaye baadhi ya wafuasi wake hawako nasi tena. Lakini wewe kama kiongozi wa ngazi ya juu chamani, tena mjumbe wa kamati kuu, hukupaswa kuyazungumzia haya humu JF. Nadhani itajengeka picha ya Mwigamba kuonewa hivi punde. Inaonekana wewe binafsi na Zitto Kabwe hampatani, na sasa mnarushiana vita vya maneno. Hata kama wewe hutaitika wito wa kulipeleka hili ngazi za Chama, Chama lazima kikuite ili uyathibitishe hayo na hatua stahiki zichukuliwe kwa ama wewe (ikithibitika unadanganya) ama Zitto ikithibitika ni msaliti. Vinginevyo hatutatofautiana na CCM, na hivyo kuyachelewesha mabadiliko.


Jambo alilo lifanya lema ni la kukemewe na kamwe si la kuunga mkono kabisa.

Lema amepotoka kabisa ni wa kukemewa kwenye hili

Lema acha kutuvuruga unayo nafasi ya kuongea kwenye chama.

Huu ni ujinga.
 
Mkuu leo sisi wa Lumumba tuekaa viti vya VIP tukitazama mpambano na myukano ndani ya zizi la CHADEMA.
Mie naenda agiza popcorn na kuangalia episode hii inaendeleaje.
Tumeaonya kutofua nguo za ndani hadharani kwa afya hawasikii.
Sasa ndio inadhihirika hawa F4F wakikamata nchi, patakuwepo na idara maalum ya Majungu.

Kwi kwi kwi. Umeongea sana mkuu nadhani kazi yetu imeshatimia.
 
Malcolm K alikuwa mwanaharakati
CHADEMA ni chama kilichopo kwa mujibu wa sheria za nchi

inashangaza mtu anagombea posho anakuja kumtumia Malcolm X kudanganya watu humu

Huyu mtoto ni aibu. Wew fikiria mtu ana masters degree anaishi bila kazi ya kueleweka. Anakesha mitandaoni, lakini anasomesha wadogo zake, amepanga nyumba kubwa nzuri. Halafu bado wajinga wachache wanamwamini eti mpiganaji kisa anapambana na Zitto. Watakapokuja kumjua sura yake halisi itakuwa too late. Hili ndilo lishushu lenyewe lilisomea kusababisha mitafaruku katika taasisi na vyama vya upinzani. Watu wenye upeo mdogo kama Lema hawawezi kumuelewa. Lakini sie tumeshamjua tutapambana naye hadi achanganyikiwe na atarudishwa makao makuu Kijitonyama akakae bechi. Hatoki huyu.
 
Huo ndio mchezo wa hapa mjini CDM. Wewe ukitaka ukubalike kirahisi kwenye viongozi wa Juu wa chama (mwenyekiti na katibu mkuu) onyesha tu upo against Zitto na tena ujifanye una siri nyingi kumhusu yeye, utakumbatiwa mara moja. Kuna kijana sasa hivi yupo hapa makao makuu na aliijariwa kwa kuleta taarifa maalumu kuhusu Zitto na ndio ticket iliyompa kazi. Taarifa zilizopo ni kwamba huyu kijana ni shushu, lakini atakumbatiwa kwa sababu tu anamwaga sumu kuhusu Zitto.

Hata huyu kibaraka Ben alikuwa hatakiwi hata kuonekana hapa makao makuu, lakini siku moja akaja akaomba sana aonane na Katibu Mkuu, akakubaliwa kwa shakashaka. Alipopata mwanya akammwagia katibu mkuu -----, lundo la uwongo kuhusu Zitto akimweleza jinsi walivyokuwa wanapanga mipango naye pamoja, lakini sasa yeye amegundua kosa na anaomba msamaha na akaahidi kusaidia kummaliza Zitto. Kuanzia siku hiyo akakumbatiwa akakabidhiwa na ofisi. Kumbe maskini wa Mungu Ben hata hajawahi kuonana na Zitto!!

Mkakati uliopo ni kuhakikisha Zitto anaondoka CHADEMA kabla 2014 haijagota. Wamegundua haondoki na hababaiki na chochote. Kibaya zaidi hawajaona akifanya kosa la kikanuni litakalohalalisha kufukuzwa. Alichofanya Lema hapa ni kum-provoke ili alipuke wapate pa kuanzia kwenye Kamati Kuu ijayo ambaye itaitishwa any time ndani ya mwezi huu wa 11. Washauri wa Zitto wamshauri awe mbali kabisa na ujinga huu, watalia.

Mimi binafsi nimepania nitajibu kila post ya hawa wajinga, ninawajua vizuri kuliko wanavyojijua wao. Makao Makuu kumebadilika sana, huyu Ben Sanane mnayemsifia hapa JF anaonekana choo kabisa na amejikunyata saa zote kama kuku. Ukweli utajulikana na tutajua nani mkweli.

Nonesense,

Huwezi kutafuta public sympathy kwa kuandika uongo.Ungeleta shahidi hata kidogo tu hapa kuhalalisha uongo wako huu.

Kwa kuwa usaliti wako umekua exposed unatafuta kila mbinu ya kujisafisha.Njoo na ID yako
 
unamawazo sahihi, mtizamo sahihi na nakuelewa vyema ILA Sidhani wewe kama kiongozi wa chama chako na mwenyekupenda maendeleo yake upo sehemu sahihi.

ni kwamba chadema hakuna mfumo wa vikao au inakuwaje mbona mnazungumza humu...kila siku tunasema cdm siyo chama ni mkusanyiko tu c mmeonaa eeh:shocked:
 
Jambo alilo lifanya lema ni la kukemewe na kamwe si la kuunga mkono kabisa.

Lema amepotoka kabisa ni wa kukemewa kwenye hili

Lema acha kutuvuruga unayo nafasi ya kuongea kwenye chama.

Huu ni ujinga.

Hata kemewe kamwe madamu amemgusa Zitto. Kumshambulia Zitto ndiyo impunity yenyewe kwenye CDM. Fanya kosa lolote lakini wewe mshambulie Zitto kosa lako litakuwa limesamehewa. Mark my words Lema hatakemewa, atapongezwa na sasa watakuwa wanashangilia huko waliko Dodoma. Na vijana wao akina Ben wanaripoti jinsi alivyowasha moto!
 
Wacha wasaliti wajulikane jamii ijue. huyu mnafiki amesababisha madiwani wetu wakafukuzwa. Ana unafiki mkubwa sana. nikikumbuka jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kuwaambia madiwani wagome kuomba radhi.
Huyu mnafiki chama kinaendelea kumlea japo amesababisha madhara makubwa kwa chama. Chama kuwafukuzwa vijana akina Juliana Shonza, Mtela Mwampamba, Habib Mchange (Masalia) ni kwa sababu yake. Huyu kiongozi anatakiwa kushughulikiwa.

His days are numbered!

Kwi kwi kwi haya maneno kutoka kwa Mungi aka king of king yawafikie wote wasio na majina kama Masawe,MREMA, N.K pia wale majina kama Zitto zuber, Mohamedi Mtoi, Mabere Marando, Profeser Abdala safar et al na amani kwenu kina john, Benidict, john shibuda, Gobless Lema, yericko et al. Ngoja niendelea kunywa kahawa yangu na kashata pembeni nikishuhudia mtanange.
gombesugu si vibaya ukachungulia hapa.
 
Last edited by a moderator:
Mnaitana katika ushirika wenu wa wanga kwa kukiombea CHADEMA mabaya.Haitokei ,traitors wanashughulikiwa squarely.So just go home.Usivute kiti kusubiri
K...................A..................m...................A.....?..tanzania yetu sote.
 
Yes...na wanamuogopa mno
mpaka Lema nae sasa ni attack dog ya Mbowe...
wanatamani kumfukuza but hawajui wanachama watasemaje so
kinachofanyika ni kushawishi watu kama hivi...

huwa najiuliza kwanini mashabiki wa zitto ni wanachama wa ccm...".kuna kitu kinawaunganisha"
 
Nonesense,

Huwezi kutafuta public sympathy kwa kuandika uongo.Ungeleta shahidi hata kidogo tu hapa kuhalalisha uongo wako huu.

Kwa kuwa usaliti wako umekua exposed unatafuta kila mbinu ya kujisafisha.Njoo na ID yako

mkuu achana naye, simpend kweli anajifanyaga kila jambo anajua.
 
Utamfanya nini wewe? wacha kujidai kutisha watu. Ungekuwa una uwezo wa kufanya kweli ungekuwa unatembea na vichupa vya sumu?

Safari hii mmeshikwa pabaya sana na hasira zimezidi, posho zimechelewa nini huko makao makuu?
Naona umeamua kumpa makavu live hajitambui yabidi apepewe.
 
Huyu mtoto ni aibu. Wew fikiria mtu ana masters degree anaishi bila kazi ya kueleweka. Anakesha mitandaoni, lakini anasomesha wadogo zake, amepanga nyumba kubwa nzuri. Halafu bado wajinga wachache wanamwamini eti mpiganaji kisa anapambana na Zitto. Watakapokuja kumjua sura yake halisi itakuwa too late. Hili ndilo lishushu lenyewe lilisomea kusababisha mitafaruku katika taasisi na vyama vya upinzani. Watu wenye upeo mdogo kama Lema hawawezi kumuelewa. Lakini sie tumeshamjua tutapambana naye hadi achanganyikiwe na atarudishwa makao makuu Kijitonyama akakae bechi. Hatoki huyu.

Haha hahaaaaa Gosh!

Kumbe wivu ni kupanga nyumba kubwa na kusomesha wadogo zake?

Kete ya ushushu na usaliti ni yako maana ushahidi upo.Huna jeuri ya kupambana nami kwa sababu ujasiri wa kuni-face na kuni-challenge physically huna na hata kwenye mtandao kwa kiwewe na woga umejificha nyuma ya ID Fake .Mimi nipo kwenye Mwanga lakini wewe hata huko gizani ulikojificha unaniogopa.You are such a coward!

Kama una uwezo wa kujenga hoja njoo jenga hoja na sio kunijadili.Utaumia bure!
 
Nonesense,

Huwezi kutafuta public sympathy kwa kuandika uongo.Ungeleta shahidi hata kidogo tu hapa kuhalalisha uongo wako huu.

Kwa kuwa usaliti wako umekua exposed unatafuta kila mbinu ya kujisafisha.Njoo na ID yako

Silikiliza wewe malaya wa kisiasa, huna uwezo wa kujua ID yangu. Narudia tena huna. Unataka ushahidi gani hapa? Huyu mjinga mwenzako Lema kaleta ushahidi gani? Ngoja uje makao nikupige ngumi ndio utanitambua mimi ni nani. Eti "usaliti wako umekuwa exposed", kuna lisaliti zaidi yako wewe ndani ya CDM? By the way hiyo kadi yenyewe ya CDM umeshachukua kwa sababu ulikuwa huna!!
 
Safari yetu ya kubadilisha utawala inaonekana kufika ukingoni na nifuraha ya kila Mtu mwenye hisia ya ukweli katika maisha na ninapotazama mbali sana ninaona jinsi ambavyo Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa ni bahati mbaya sana uwezi kuwaepuka katika harakati hizi lakini tukiwa makini tunaweza kuwathibiti .

Kama Chadema leo itashindwa kuwachukulia hatua wasaliti wa wazi wa kazi hii njema ni vipi Chadema itaweza kuitaka Serikali na Rais iwajibishe Viongozi wake katika ufisadi na wizi wa mamilioni ? Na Wananchi lazima wajue lengo kubwa na muhimu la Chadema kwanza liwe kubadilisha fikra na mitazamo na kuupa UMMA elimu na mamlaka na nguvu ya kusimamia Taifa lao katika kuhoji ,kudadisi na kukemea , kwani UMMA usipojua wajibu wake katika kusimamia rasilimali na Taifa lao , ukweli utabaki kuwa Nchi itabadilishwa na kufanikishwa na Jamii iliyoamua kuishi matendo dhahiri ya ukweli na haki na sio unafiki na usaliti .

Viongozi wote wa Siasa wanatokana na Jamii kwa hiyo jamii Thabiti inayo furahia UTU ni Nchi bora tutakayoijenga lakini Jamii yenye woga na hofu na Sifa itazaa Taifa lenye usaliti na Wanafiki . Usaliti na Unafiki unaliangamiza Taifa sana . Maombi na Dua za Watu wengi kuelekea 2015ni kutaka kuona Chadema inachukua Nchi , lakini Dua na Sala hizi zina Imani kubwa na Viongozi wa Chadema na sio rangi ya Chadema , hivyo ni muhimu Chadema kuchukua hatua sasa ya kusafisha Chama na kama hatua hiyo muhimu ya kuondoa Watu wenye rangi mbili italeta madhara katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwamba tunaweza tusishinde dola basi madhara hayo ni muhimu kwani lengo letu lisiwe tu kwenda Ikulu bali kubadilisha fikra ya utawala katika kutenda na kuamua .

“ Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja aliye ndani “ Chadema lazima ifanye maamuzi sasa ya kusafisha Nyumba yake la sivyo itakuja kujuta katika siku za mwisho , wasaliti wote waondolewe hasa yule Kiongozi wao kwani hakuna genge la usaliti lisilokuwa na Kiongozi , kuna Watu wengi Vijana wamekuwa wahanga na ndoto zao kupotea katika Siasa kwa sababu waliongozwa vibaya na Kiongozi mkubwa anayeratibu usaliti ndani ya Chama .

Mtu huyu wote tunamjua ni matumaini yangu Usaliti wake sasa utafika kikomo kama Chama kitaamua kuwa na busara za kutosha katika kujenga siku njema zinazokuja . Mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya katika Chama yanayohusu usaliti na amewaponza Vijana wengi na kuangamiza ndoto zao kwa sababu ya mambo yake binafsi .

“ To me, the thing that is worse than death is betrayal. You see, I could conceive death, but I could not conceive betrayal.” Malcolm X



Lema Godbless - Mp

LEMA, I think this is NOT RIGHT
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom