Usalama wa Taifa: Mpo likizo?

Status
Not open for further replies.
Kazi za kuzuia wapiga picha ni kazi za usalama wa taifa wa kizamani. UT hawapo livu wala hawaja lala wala hizo ulizoainisha si kazi zao kwa sasa.

kazi zao wanazojitungia au walizokabidhiwa kwa mujibu wa sheria? Maana kama zile za kujitungia hizo tunazijua..!
 
Kazi za kuzuia wapiga picha ni kazi za usalama wa taifa wa kizamani. UT hawapo livu wala hawaja lala wala hizo ulizoainisha si kazi zao kwa sasa.

Si kwamba TISS wapo livu/usingizini; hawapo virtually. Kinachoitwa TISS ni usalama wa watawala.

Watanzania sie maskini tunaishi kwa neema ya Mungu tu, na si vinginevyo.

Sasa utawala bora na usalama wa taifa wapi na wapi?

Taasisi nyeti kama benki kuu ndio limekuwa chaka la wezi. Bado tunasema kuna usalama wa taifa....pambaaf.
 
Zitto: Usalama wa Taifa butu

na Mwandishi Maalum, Detroit Marekani
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema ipo haja na ulazima wa haraka wa kuzipitia na kuzifanyia marekebisho sheria zinazohusu masuala ya Usalama wa Taifa, ili ziende na wakati.

Zitto, alisema hayo jana katika chakula cha jioni alichoandaliwa na Watanzania wanaoishi katika Jimbo la Michigan, nchini Marekani na kuongeza kuwa, sheria kubwa zilizopo, hasa ile ya uundwaji wa Idara ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996 zimeifanya idara hiyo kuwa butu.

“Tunahitaji kuwa na idara inayofikiria kimkakati... hatuwezi kuivunja bali inahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo. Nchi haiwezi kutokuwa na Usalama wa Taifa, inahitaji ‘overhaul,” alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Alisema changamoto nyingi za kiuchumi nchini zinahitaji kuangaliwa kwa namna ya pekee na watu wa Usalama wa Taifa na kuhakikisha kuwa idara hiyo kweli inakuwa ni ya Usalama wa Taifa na si ya ‘viongozi pekee’.

Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Jiji la Detroit, pia Zitto alitoa wito kwa vyombo mbalimbali vya serikali kuhakikisha vinakuwa na rekodi sahihi ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi, ili kuweza kufahamu mchango wao katika maendeleo ya taifa. Alitolea mfano wa nchi kama India ambayo wananchi wake walioko nje wanachangia mabilioni ya dola kila mwaka.

“Lazima na sisi tuhakikishe wananchi wetu wanapata nafasi ya kutambuliwa mchango wao, hasa wa mapato wanayoyachangia katika uchumi wa nchi.

“Mchango wa Watanzania kwenye uchumi ni mkubwa na fedha wanazotuma nyumbani zinazidi mapato ya sekta nzima ya madini,” alisema Zitto huku akinukuu takwimu za Kampuni ya Western Union.

Pia alitoa changamoto kwa Watanzania hao kufuatilia na kujihusisha na mambo ya nyumbani na wasikae kama watu wanaoangalia kutoka mbali. Alisema ni jukumu la kila Mtanzania kushiriki kwa nafasi yake katika ujenzi wa Tanzania.

“Huko nyuma kulikuwa na tabia ya kuwaona wale wanaoishi nje ya nchi kama wakimbizi, lakini lazima tubadilike na kuwaona kuwa ni Watanzania wenzetu ambao wao pia wanahitaji ulinzi wa taifa lao,” alisema.

Pia alitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa vijana wawili; Walter Mazulla na Vonetha Nkya waliouawa kinyama kwenye mji huo karibu miaka miwili iliyopita. Hadi hivi sasa waliofanya vitendo hivyo hawajatiwa mbaroni.

Zitto anatoa kauli hiyo wakati ahadi ya Serikali ya Tanzania kufuatilia suala hilo, haijafanyiwa kazi.

Zitto alikiri kufurahishwa kwake kwa ukarimu alioonyeshwa na Watanzania wa Detroit na alitoa wito wazidi kushirikiana, hasa kwa vile wako mbali na nyumbani. Alitoa pendekezo kuwa wakati umefika kwa balozi zetu hasa zile kubwa kama za London, New York, Washington DC, Brussels, Paris na Berlin zianze kuwa na maofisa wa jumuiya ambao watakuwa ni kiungo kati ya Watanzania na balozi zao.

“Wakati mwingine tunasikia mabalozi wanalalamika kuwa Watanzania hawajiandikishi kwenye balozi zao; sasa wajiandikishe ili kiwe nini wakati hata wale waliojiandikisha hawaonekani kupata faida yoyote ile?” alihoji Zitto na kusema ipo haja ya kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania kama walivyo wale wa nchi nyingine wanapata ulinzi wa serikali yao.

“Mmarekani hata akiwa na matatizo mahali popote pale, nchi yake iko tayari kufuatilia na sisi lazima tuwalinde wananchi wetu,” alisema Zitto huku akishangiliwa na Watanzania hao.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania hao, Ayub Mfinanga, alimshukuru Zitto kwa kukubali wito wa jumuiya hiyo kuwatembelea na kwa kuonyesha ukaribu wake na wananchi.

Mfinanga alisema kuwa kufanikiwa kwa ziara hiyo fupi kumewapa funzo la kuweza kuandaa ziara za viongozi wengine kama hiyo na ambazo zinaweza kuhusisha hata majimbo mengine ya karibu, na hivyo kuendeleza umoja wa Watanzania.

Zitto yuko nchini Marekani katika ziara ya wiki tatu akiwakilisha Tanzania katika programu ya mafunzo kwa viongozi vijana kutoka nchi 22 duniani iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Kukutana kwake na Watanzania huko kulitokana na mwaliko wa jumuiya hiyo, ili kumuonyesha shukrani na kutambua mchango wake katika mabadiliko makubwa ya kifikra yanayoendelea nchini.

Mwishoni mwa wiki hii, Zitto anatarajiwa kuzungumza na mojawapo ya jumuiya kubwa zaidi ya Watanzania katika Jiji la Houston, Jimbo la Texas nchini Marekani. Ziara yake fupi kwa Watanzania Michigan iliandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Michigan kwa ushirikiano na tovuti za Watanzania.

Mazungumzo ya Zitto na jumuiya hiyo ya Watanzania yalirushwa moja kwa moja kwa njia ya mtandao wa http://www.bongoradio.com na kufuatiliwa na Watanzania katika nchi za Marekani, Canada, China, Poland, Uingereza, Ujerumani na Tanzania kwenyewe.

Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 10 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
usalama wa taifa kwa ujumla iko hoi, kama ingekuwa makini, huu ufisadi unaoisumbua nchi wala usingekuwepo,au ungekuwa wa kiasi kidogo. wao watendaji wakuu wa chombo hiki ni mafisadi wakuu wa kupindukia, kwanza ajira pamoja na kuwa siri lakini wanagwana wao na watoto na ndugu zao, kiasi kuwa ufanisi unakuwa hakuna, si hizi hakuna siri, kila kitu kinachofanywa na wao kinajulikana kwa raia.
kashfa ya EPA mmoja wa watuhumiwa ni afisa mwandamizi wa idara hii, alichukua pesa baada ya kuona viongozi wanachota nae akaamua kudang'anya eti shughuli maalumu akapewa mihela kazi iliyofanyika haijulikani.

yule mbunge aliyeteuliwa na rais (anatoka mbeya) alikuwa staff wa celtel, babake alikuwa ndo bosi wa idara hii, so utaona jinsi uwajibikaji unavyokinzana fadhila, what special does he have! ila kwa kuwa babake aliwezesha mambo fulani akalipwa fadhila kwa kijana kupewa ubunge, asnte

na geofrey, tz, - 8.05.08 @ 09:54 | #10069

tujielimishe juu ya sheria hiyo ya usalama wa taifaa ya mwaka 1996 kwanza kabla ya kuanza kuilaumu taasisi hii.Lazima kuna jambo limefanyika ili kuifanya kuwa butu.
Huenda mafisadi walipokuwa wakipora waliihasi -castrate kwa manufaa yao.
kama kuna anaeifahamu vema sheria hiyo atuelimishe.
Ni kweli hii siyo taasisi iliyosimamia ukombozi wa bara la Afrika.Siyo ile iliyokinga kifua wakati karibu nchi zote za bara hili zilipokumbwa na mapinduzi ya kijeshi.
Kuna nini, nani anafuta rekodi hii.
Nayo ilitumiwa kuiba fedha za EPA,ikanyamaza.Lakini ktk uchaguzi wachache walipewa tenda yaCCM.Tuwe macho.

na yuli, usa, - 8.05.08 @ 10:27 | #10076

Ndugu Zitto, jitahidi hivyo hivyo kuelezea yake yote amabyo viongozi wa Tanzania wanafanya ambayo yanaoonyesha jinsi wasivyo na mapenzi na nchi yetu.
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa ni fisadi wa kutosha na Rais anaelewa kwa nini amemuweka hapo. Tuanshangaa katika ripoti ya Richmond ametajwa kama mtu aliyesaidia sana kampuni hiyo hewa kupata mkataba. Ina maana na yeye alikuwa anachotewa sehemu ya yale mamillion 152 ya kila siku.
Hivi Rais unakumbuka taarifa iuliyosomwa bungeni kuhusu usalama wa taifa na sakata la Richmond? Mheshimiwa Zitto, kikao cha Bunge cha 12 kiwe cha kuikumbusha serikali kuwa nchi hii ni ya Watanzania na si ya Kikwete na rafiki zake pamojana watoto wao. Aachie ngazi kama hawezi kuwawajibisha wale wote wanaoshutumiwa kwa ufisadi akiwemo Hosea, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Hosea mwenyewe ana pesa nje ya nchi na wala hili halina mjadala. Mwulizeni Chenge.

na Jennifer Henrick, Finland (kwa sasa), - 8.05.08 @ 10:34 | #10080

yote sawa mh. Zito, mimi nakuunga mkono katika maeneo mengi kwnai mchango wako kw ahakika hauna budi kuungwa mkono.

lakini kwa mujibu wa taarifa ya gazeti hili iliyotolewa jana wanafunzi 900 shule ya msingi ya Airport wilayani Kigoma wanakaa chini, je hapa pia tunahitaji kubadili sheria ya usalama wa taifa au kwa mbunge wa kigoma kuacha kuhudhuria hafla ya chakula cha jioni nchini marekani ili awapatie madawati watoto walioko mkoani mwake.

huu usanii wa kuchagua wabunge wanaoishi Dar na safari zisizokwisha nje ya nchi utatumaliza watanzania, tuamke!

na mashilatu, ngara, - 8.05.08 @ 08:18 | #10087

kwa kweli hii idara ni muhimu sana na kama uwajibikaji wake ni wa mashaka mashaka basi tumekwisha.mimi naungana na geofrey hapo kuwa tatizo linaanza watu tunaowapa kazi hizo, nijuavyo idara hii inatakiwa iwe na watumishi wenye sifa ya uzalendo na wenye akili zisizo za kawaida lakini leo baba akibahatika kupata kazi kwenywe idara hii basi ukoo nzima watapata kazi kwenye idara hii na hii ni hatari kwa kuwa tunakuwa na watu wasio na uwezo wa kufanya kazi hizo na wakati mwingine wanadhana kuwa wao ndio wenye nchi na huwatisha watu bila sababu kwa hiyo ili tusonge mbele ni lazima tufanye mabadiliko makubwa kama wanavyopendekeza wadau.

na faisal, tz, - 8.05.08 @ 08:38 | #10098

idara hii ni nyeti na tupo ambao hatukubali kutumika na mafisadi ndio maana tumeamua kuanika baadhi ya taarifa za ufisadi kwani tunaona bila kufanya hivyo serikali haishughulikii mafisadi bali huwalinda.
nakubaliana na Komredi Zitto na namwomba asirudi nyuma na tutaendelea kumpa ushirikiano hata pale tutakapopata taarifa za kumdhuru kama zile za wakati ule tutampa kwani wapo watu katika idara hii na serikalini waliosahau wajibu wao kwa taifa na kuamua kushirikiana na mafisadi kulihujumu taifa.
Ni vema idara hii ikaendelea kuwepo kwani BADO TUPO AMBAO HATUKUBALI KUPOKEA HATA SENTI TANO ZA KUTURUBUNI ingawa wapo wengi wetu pia wanaorubunika kirahisi na hao ndio tatizo kubwa kwa taifa.
Hivyo,watanzania wasife moyo kwani tuliokubali kuitumikia nchi masaa 24 kwa kila siku ya maisha yetu katika hali zote bado tupo japo wengi wetu ni wa nafasi cha kati na chini na wachache sana ni wale wa ngazi za juu.Tuendelee kupeana taarifa za kiusalama na ndani ya muda fulani(siutaji)tutaangamiza mafisadi na genge lao japo linalindwa na wakubwa hasa Ikulu.Kama Ikulu isingeweka vikwazo idara yetu ingeshawamaliza mafisadi wote na tungekuwa kwenye ukurasa mwingine kitaifa.

na muhamed a.nzoloka, pretoria,afrika kusini, - 8.05.08 @ 08:59 | #10104

Mashilatu. Zitto si mbunge wa kigoma mjini kwenye hiyo shule ya Air port.N a Zitto hakenda Marekani kuhudhuria hafla ya chakula. kama huna hoja kaa kimya.Kwanini unakuwa mbumbu?

na Nkamba Mayunga, Shinyanga Tanzania, - 8.05.08 @ 09:00 | #10105

i dont undrstand why all this ,suala kubwa watanzania wamekatatamaa sana kwa sasa"siku moja nilitazama kuni klubwa la watu wakionekana kukosa matumaini nikajiuliza swali ,nani atwakoa watu hawa ,najuliza maswali mengi hivi kweli viongozi wa nchi hii wanaliona hilo .utawaoana wanacheka kwenye Luninga kama vile hakuna kibaya kinachoendelea ,,why JK is quite,tanzanians have been robed every thing,but not the brain .idont think ZITO IS right to make such statement while in Us angekuja huku kwetu Loliondo which is now called a state of blood .....aone madhila wanayofanyiwa wahadzabe na wamasai

na JUMA , loliondo, - 8.05.08 @ 09:10 | #10108

mashilatu kabula ya kuandika msg zako ujifunze kutafakali kwanza, unaandika nini.kama jambo hulijui bora ukae kimya,pia uelewe msg zinazoandikwa sehemu hii ya maoni zinasomwa na watu mbalimbali wenye elimu zao pia wengine uzalendo na nchi yao.sasa wewe bwana mashilatu kutoka usukumani kwenu unakurupuka na utumboutumbo wako, jifunze kutafakali kabula ya kutenda la sivyo watu watakucheka.

na j, tz, - 8.05.08 @ 10:18 | #10131

Zitto anaonekana kuwa mtanzania wa kweli na anyependa nchi! Usalama wa Taifa katika nchi yetu ni kitengo cha ajabu sana na mara moja tu nimesikia kikitoa ripoti sahihi! Ni pale zombe alipowaua wafanyabiashara wa madini kutoka Morogoro!
Vyombo vingine vya ulinzi angalao vinasikika hata kama ni habari za porojo! Mara nyingi tunaisikia Polisi na ujambazi wake! Jeshi na Komoro yake! Tunasikia ubabaishaji wa Hosea na rushwa yake! Hata mgambo tu wa Ilala nao tunawasikia wakiiwaibia Mama Lishe lakini hakuna kinachofanywa na Usalama wa taifa! Habari za EPA, TTCL, IPTL, Minara ya Benki, Majengo ya NSSF, Richmond, Buzwagi n.k. hakuna hata moja lililoanzishwa na usalama wa taifa! Hata kumshauri Rais habari ambazo ni rahisi kuzipata kutoka uswahilini kama kutowachagua akina Vijisenti kwenye nafasi za uwaziri hawafanyi na ndo maana mambo yanatuharibikia!

na LCD, Vientiane, Laos, - 8.05.08 @ 10:23 | #10133
 
Nimeona habari hii katika gazeti la Tanzania Daima, nikaona si vyema ikapita hivi hivi bali tupate tafakuri za wachambuzi mbalimbali.

Zitto: Usalama wa Taifa butu

na Mwandishi Maalum, Detroit Marekani

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema ipo haja na ulazima wa haraka wa kuzipitia na kuzifanyia marekebisho sheria zinazohusu masuala ya Usalama wa Taifa, ili ziende na wakati.

Zitto, alisema hayo jana katika chakula cha jioni alichoandaliwa na Watanzania wanaoishi katika Jimbo la Michigan, nchini Marekani na kuongeza kuwa, sheria kubwa zilizopo, hasa ile ya uundwaji wa Idara ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996 zimeifanya idara hiyo kuwa butu.

“Tunahitaji kuwa na idara inayofikiria kimkakati... hatuwezi kuivunja bali inahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo. Nchi haiwezi kutokuwa na Usalama wa Taifa, inahitaji ‘overhaul,” alisema Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Alisema changamoto nyingi za kiuchumi nchini zinahitaji kuangaliwa kwa namna ya pekee na watu wa Usalama wa Taifa na kuhakikisha kuwa idara hiyo kweli inakuwa ni ya Usalama wa Taifa na si ya ‘viongozi pekee’.
 
Hatukuwa na haja ya kuunda vyombo vingi ku-deal na issues ambazo chombo kilichopo kinaweza kushughulikia masuala hayo. Kuundwa kwa PCCB kulikuwa na maana gani kama hawa TISS wapo na wanafanya kazi vizuri. Naunguna na Mhe. Zitto kuwa hao jamaa wamebaki kama kuku anayeshuhudia vifaranga vyake vikizolewa na mwewe.

Nimebahatika kuongea na baadhi yao. Ukiwauliza kwa nini yale makeke ya TISS ambayo wengi wetu tumekuwa tukiyaona yameenda wapi? wana jibu moja kuwa hata ufanye kazi namna gani, uandike ripoti kwa wakubwa namna gani utabatizwa mzushi na mnafiki. Nani anawaambia hiyo siri wanayo wao.

Hapa mimi napata shida kidogo. Nathubutu kusema, kuna uwezekano mkubwa sana kwamba 'the UFISADI' kaingia na kuota mizizi ndani ya chombo hiki nyeti. Wazee mnajua, walikuwa wapi wakati nyumba za serikali zinauzwa kimizwengwe? Kwani wakubwa wa hiki chombo wao hawakuchukua? Kama wamechukua tuwatenge vipi na ufisadi? Kama wamekuwa sehemu ya ufisadi, hamuoni kama macho yao yamefumbwa kuona 'Mnyantusu na Mzee wa vijisenti na wenzake wengi wakijinafasi kwa kuzoa kwa nguvu zao zote kile kinachojipitisha mbele zao? Ebu acheni hawa wadogo wadogo wanaofanya kazi TISS, je wakumbwa maisha yao yako je? mbona tunayajua?

Nimalizie kwa kusema, Mlundikano wa vyombo vinavyoshughulikia masuala yanayofanana ni matokeo ya chombo fulani kilichopo kushindwa kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake. Sasa kwa vile watalaam wetu ni wababaishaji au labda wanafanya kwa makusudi, badala ya kuboresha (overhaul hasa) chombo kilichopo ili kilete ufanisi wanaunda kingine kibovu zaidi na chenye watu wasio na maadili kufanya kazi hiyo na matokeo yake ni Watanzania kutundikwa msalabani wakifia dhambi za wengine.
 
Hivi karibuni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. ZITTO KABWE wakati akiwa katika chakuka cha jioni alichoandaliwa na Watanzania waishio katika Jimbo la Michigan (Marekani) aliwaeleza Watanzania hao kuwa Sheria ya uundwaji wa Idara ya Usalama wa Taifa Na. 15 ya mwaka 1996 imeifanya Idara hiyo kuwa butu na kwa hiyo ipo haja na ulazima wa kuipitia na kuifanyia marekebisho. Kauli ya Mbunge huyo ililenga kuonyesha kwamba ubutu wa Idara ya Usalama wa Taifa ni ule wa kushindwa kukabiliana na vitendo vya kifisadi.

Kauli hiyo ya ZITTO ilinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari likiwemo gazeti la Tanzania Daima la tarehe 8 Mei, 2008. Kimsingi, shutuma za namna hiyo kwa Idara ya Usalama wa Taifa zimekuwa zikitolewa mara nyingi hasa tangu vitendo vya kifisadi kuanza kuitikisa nchi.

Kauli hiyo ya Mhe. ZITTO KABWE pamoja na lawama zinazotolewa kwa Idara ya Usalama wa Taifa zinapaswa kuangaliwa kwa mapana hasa kwa kuzingatia kuwa nchi yetu ya Tanzania inafuata mfumo wa utawala unaoitwa “Parliamentary system of government” ambao chimbuko lake ni Uingereza. Ndani ya mfumo huo kuna mihimili mitatu ya dola yaani Serikali (executive), Bunge na Mahakama. Katika mfumo huo Serikali inakuwa moja kwa moja ni sehemu ya Bunge, lengo likiwa ni kulifanya Bunge na Serikali kuwa ni vyombo vinavyotegemeana na kwa hiyo vinapaswa kufanya kazi zao kwa ushirikiano mzuri ili kuweza kufikia lengo la kuwaletea wananchi maendeleo na ustawi wa jamii.

Ni vyema pia tutambue kuwa wajibu wa Bunge ni kuisimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kama Ibara ya 63(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inavyoeleza. Kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 63(3) ya Katiba hiyo, Bunge linasimamia utekelezaji unaofanywa na Serikali kwa kutumia njia ya kuwauliza Mawaziri maswali Bungeni kuhusu utekelezaji unaofanywa na Wizara, halikadhalika kujadili utekelezaji wa kila wizara uliofanywa katika mwaka uliotangulia pamoja na kutoa ushauri unaofaa kuzingatiwa katika mwaka wa fedha unaofuata.

Aidha, ni wajibu wa Bunge kuiwezesha Serikali kutekeleza wajibu wake kwa wananchi kwa kutunga Sheria na kupitisha bajeti. Hatua hiyo ndiyo inayoiwezesha au kuirahisishia Serikali kutekeleza majukumu yake.

Vivyo hivyo, kwa upande wa Mahakama kama muhimili wa tatu, majukumu yake yemeelezwa bayana katika Ibara ya 107 A na 107 B ya Katiba. Kwa mujibu wa Ibara hiyo, mamlaka ya utoaji wa haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki Mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya Katiba na Sheria za nchi. Kwa maneno mengine Bunge ni chombo cha uwezeshaji kwa Mahakama. Kwamba, Bunge linao wajibu kutunga Sheria zitakazowezesha Mahakama kutekeleza ipasavyo shughuli zake za utoaji haki, kwani bila Bunge kutunga Sheria mbali mbali Mahakama haitaweza kutimiza wajibu wake wa utoaji haki.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa hapo juu ni kwamba, Bunge ni chombo cha uwezeshaji kwa Serikali na kwa Mahakama. Dhana ya utengano wa madaraka baina ya mihimili hiyo mitatu ya Dola, haipo kikamilifu katika mfumo wa utawala unaitwa “Parliamentary System of Government:, badala yake kuna maingiliano na ushirikiano mkubwa wa kimadaraka miongoni mwa mihimili hiyo.

Kwa kuzingatia ukweli huo, je, ni sahihi kuilaumu serikali (executive) peke yake au Idara ya Usalama wa Taifa kwa kushindwa kukabiliana na vitendo vya kifisadi? Kwa nini watu wamekuwa wepesi kuilaumu Serikali (executive) na wamekuwa bubu kwa mihimili mingine ya dola? Je, Bunge pamoja na wabunge wake akiwemo ZITTO KABWE ambao wanailaumu serikali hasa Idara ya Usalama wa Taifa walikuwa wakifanya nini katika kuisimamia serikali vizuri ili kuweza kuondokana na vitendo vya kifisadi? Mbunge ZITTO KABWE anaposema Idara ya Usalama wa Taifa ni butu kutokana na sheria iliyoiunda, anategemea nani atarekebisha sheria hiyo? Sambamba na hilo, sheria hiyo ni ya mwaka 1996, kwa kipindi hicho chote ZITTO KABWE hakutambua kasoro ya sheria hiyo hadi leo mwaka 2008? Je ni kweli anatimiza ipasavyo wajibu wake kama Mbunge?

Kwa maoni yangu, mihimili yote mitatu inapaswa kushutumiwa na kunyoshewa vidole vya lawama kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kifisadi na siyo serikali (executive) au Idara ya Usalama wa Taifa peke yake. Ni ukweli usiopingika kwamba kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa mihimili hiyo mitatu ndiko kulikotufikisha hapa tulipo.

Wanasiasa (Wabunge) akiwemo ZITTO KABWE wasikwepe lawama wanazopaswa kuzibeba kwa uzembe walioufanya. Kama kweli wanathamini dhamana waliyoibeba wanapaswa kwenda kwa wananchi na kuomba radhi (msamaha) kwa uzembe waliofanya ambao umesababisha kukithiri kwa vitendo vya kifisadi ambavyo vimesababisha maisha magumu kwa wananchi waliowachagua. Wabunge hawana haki ya kuilaumu serikali au Idara ya Usalama wa Taifa peke yake, bali wao pia pamoja na Idara ya Mahakama wanapaswa kulaumiwa. Kuilaumu Idara ya Usalama wa Taifa au sheria inayoiunda ni kuitoa kafara kwa makosa ambayo si yake.
 
Ninakubaliana kwa mantiki na mwanabodi mmoja hapo juu aliyesema kuwa usalama wa taifa upo kwa ajili ya viongozi, nakubaliana naye sana tu.

Na kibaya zaidi wamelishwa yamini za kiitikadi kiasi kwamba napata shaka sana kwa hawa jamaa pale ambapo chama kipya kikipata ridhaa yetu kuongoza sijui watafanya kazi kwa mazingira gani.

Kingine ni kuwa, zile operesheni za maadui wa vita baridi zimeisha na ninapata shida kutoamini kuwa hawa wazee wa shughuli wanafanya kazi kwa mtindo uleeee?? Hebu fikiria mtu anasema kuwa balali yuko huru na hatafutwi, ina maana rais alikosea kutengua uteuzi wake?? au niwaulize wanabodi kuwa ni jeshi gani lipo ktk mizania ya kwanza hapa nchini?? maana kama usalama wa taifa umekuwa ni kwa niaba ya CHAMA basi tuwatume wabunge wetu waifute waje na kitu kipya au la hakutakuwa na jipya zaidi ya kulindana na kuchafuana kwa malengo ya kupashana joto
 
Hawa bado wanafanya kazi kwa mazingira ya vita baridi na chama kimoja, hawajajua kuwa sasa tupo kwenye mfumo wa vyama vingi unaotawaliwa na ubepari, zamani walikuwa wananweza kuuliza mtu gari amenunua kwa pesa gani lakini naona sasa hizi role zote wamezitupa na wenyewe wameamua kuwa mabepari.

Siwezi kuamini kuwa hawajui kuwa viongozi wetu wanajilimbikizia mali kwa kuwaibia wananchi, hili wanalijua ila kwa kuwa wapo kwa ajiri ya kulinda masirahi ya viongozi wanakaa kimya au inawezekana viongozi wanawapa na wenyewe madili ili wasiseme madhambi yao.

ikitokea ukaamua kumsema fisadi hadharani wewe ndo unafuatiliwa kama kwamba wewe ndo fisadi, utanyanyaswa kila sehemu yako kuanzia kazini au biashara mpaka unapokaa kujua unakulaje na hatima yake utapewa kakesi kaqdogo uangaike nako wakati wanaendelea kuibia taifa.
 
Naomba kuungana na maoni ya Mzee Busara.

Kimsingi, kauli ya zitto ni ya kuungwa mkono lakini mapungufu katika sheria ya Usalama wa Taifa Na 15 ya mwaka 1996 hayawezi kuwa kigezo pekee cha madai kwamba Idara ya Usalama wa Taifa kuwa butu. Ninaamini kwamba zipo sababu zingine kama alivyosema Mzee Busara ambazo zimechangia Idara hiyo kuwa butu kama inavyodaiwa. Sheria ya TISS sio ya kwanza na ya mwisho kuwa na mapungufu.

Kitaaluma, Zitto ni mwanasheria na anafahamu daima kwamba sheria siyo Dogma au imani ya dini inayofundishwa bila kubadilika, sheria hubadilika kulingana na mahitaji na wakati. Mbali na sheria iliyounda TISS mapungufu katika sheria mbalimbali yanapojitokeza hufanyiwa marekebisho pindi inapoonekana kuna haja ya kufanya hivyo.

Kisiasa, Zitto ni mbunge hivyo alikuwa na nafasi nyingine nzuri ya kuzungumza kuhusu sheria ya TISS ndani ya Bunge badala ya kuzungumza suala hilo akiwa Marekani. Hatua kama hiyo inaweza kuonekana ni ya kisiasa zaidi kuliko maslahi ya Taifa. Baadhi ya Watanzania tunajiuliza inakuwaje Mwanasheria ambaye pia ni mbunge kutoka chombo cha kutunga sheria za nchi anazungumzia ubovu wa sheria nje ya Bunge (chombo chenye mamlaka ya kutunga sheria).

Zitto hana budi kuzingatia busara za Mzee Busara kwamba, Bunge ni moja ya mihimili mitatu ya dola ‘three arms of the government’. Mihimili yote mitatu inafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa, hivyo suala la Ufisadi haliwezi kumalizwa kwa kutoa shutuma dhidi ya mhimili mmoja (Serikali) bali pia Mahakama na Bunge zinapaswa kulaumiwa kwa hilo.

Jambo alilofanya ZITTO ni kujitoa katika kipimo cha mizania (checks and balances) ya uwajibikaji wa mihimili mitatu katika dola moja ya Tanzania au utatu timilifu wa dola ya Tanzania. Hivyo, kauli ya Zitto pekee haitoshi kuthibitisha Ubutu wa sheria ya TISS pasipo kuangalia wajibu wa mihimili mingine ya Dola katika nchi yetu.

Hivi karibuni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. ZITTO KABWE wakati akiwa katika chakuka cha jioni alichoandaliwa na Watanzania waishio katika Jimbo la Michigan (Marekani) aliwaeleza Watanzania hao kuwa Sheria ya uundwaji wa Idara ya Usalama wa Taifa Na. 15 ya mwaka 1996 imeifanya Idara hiyo kuwa butu na kwa hiyo ipo haja na ulazima wa kuipitia na kuifanyia marekebisho. Kauli ya Mbunge huyo ililenga kuonyesha kwamba ubutu wa Idara ya Usalama wa Taifa ni ule wa kushindwa kukabiliana na vitendo vya kifisadi.

Kauli hiyo ya ZITTO ilinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari likiwemo gazeti la Tanzania Daima la tarehe 8 Mei, 2008. Kimsingi, shutuma za namna hiyo kwa Idara ya Usalama wa Taifa zimekuwa zikitolewa mara nyingi hasa tangu vitendo vya kifisadi kuanza kuitikisa nchi.

Kauli hiyo ya Mhe. ZITTO KABWE pamoja na lawama zinazotolewa kwa Idara ya Usalama wa Taifa zinapaswa kuangaliwa kwa mapana hasa kwa kuzingatia kuwa nchi yetu ya Tanzania inafuata mfumo wa utawala unaoitwa “Parliamentary system of government” ambao chimbuko lake ni Uingereza. Ndani ya mfumo huo kuna mihimili mitatu ya dola yaani Serikali (executive), Bunge na Mahakama. Katika mfumo huo Serikali inakuwa moja kwa moja ni sehemu ya Bunge, lengo likiwa ni kulifanya Bunge na Serikali kuwa ni vyombo vinavyotegemeana na kwa hiyo vinapaswa kufanya kazi zao kwa ushirikiano mzuri ili kuweza kufikia lengo la kuwaletea wananchi maendeleo na ustawi wa jamii.

Ni vyema pia tutambue kuwa wajibu wa Bunge ni kuisimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kama Ibara ya 63(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inavyoeleza. Kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 63(3) ya Katiba hiyo, Bunge linasimamia utekelezaji unaofanywa na Serikali kwa kutumia njia ya kuwauliza Mawaziri maswali Bungeni kuhusu utekelezaji unaofanywa na Wizara, halikadhalika kujadili utekelezaji wa kila wizara uliofanywa katika mwaka uliotangulia pamoja na kutoa ushauri unaofaa kuzingatiwa katika mwaka wa fedha unaofuata.

Aidha, ni wajibu wa Bunge kuiwezesha Serikali kutekeleza wajibu wake kwa wananchi kwa kutunga Sheria na kupitisha bajeti. Hatua hiyo ndiyo inayoiwezesha au kuirahisishia Serikali kutekeleza majukumu yake.

Vivyo hivyo, kwa upande wa Mahakama kama muhimili wa tatu, majukumu yake yemeelezwa bayana katika Ibara ya 107 A na 107 B ya Katiba. Kwa mujibu wa Ibara hiyo, mamlaka ya utoaji wa haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki Mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya Katiba na Sheria za nchi. Kwa maneno mengine Bunge ni chombo cha uwezeshaji kwa Mahakama. Kwamba, Bunge linao wajibu kutunga Sheria zitakazowezesha Mahakama kutekeleza ipasavyo shughuli zake za utoaji haki, kwani bila Bunge kutunga Sheria mbali mbali Mahakama haitaweza kutimiza wajibu wake wa utoaji haki.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa hapo juu ni kwamba, Bunge ni chombo cha uwezeshaji kwa Serikali na kwa Mahakama. Dhana ya utengano wa madaraka baina ya mihimili hiyo mitatu ya Dola, haipo kikamilifu katika mfumo wa utawala unaitwa “Parliamentary System of Government:, badala yake kuna maingiliano na ushirikiano mkubwa wa kimadaraka miongoni mwa mihimili hiyo.

Kwa kuzingatia ukweli huo, je, ni sahihi kuilaumu serikali (executive) peke yake au Idara ya Usalama wa Taifa kwa kushindwa kukabiliana na vitendo vya kifisadi? Kwa nini watu wamekuwa wepesi kuilaumu Serikali (executive) na wamekuwa bubu kwa mihimili mingine ya dola? Je, Bunge pamoja na wabunge wake akiwemo ZITTO KABWE ambao wanailaumu serikali hasa Idara ya Usalama wa Taifa walikuwa wakifanya nini katika kuisimamia serikali vizuri ili kuweza kuondokana na vitendo vya kifisadi? Mbunge ZITTO KABWE anaposema Idara ya Usalama wa Taifa ni butu kutokana na sheria iliyoiunda, anategemea nani atarekebisha sheria hiyo? Sambamba na hilo, sheria hiyo ni ya mwaka 1996, kwa kipindi hicho chote ZITTO KABWE hakutambua kasoro ya sheria hiyo hadi leo mwaka 2008? Je ni kweli anatimiza ipasavyo wajibu wake kama Mbunge?

Kwa maoni yangu, mihimili yote mitatu inapaswa kushutumiwa na kunyoshewa vidole vya lawama kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kifisadi na siyo serikali (executive) au Idara ya Usalama wa Taifa peke yake. Ni ukweli usiopingika kwamba kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa mihimili hiyo mitatu ndiko kulikotufikisha hapa tulipo.

Wanasiasa (Wabunge) akiwemo ZITTO KABWE wasikwepe lawama wanazopaswa kuzibeba kwa uzembe walioufanya. Kama kweli wanathamini dhamana waliyoibeba wanapaswa kwenda kwa wananchi na kuomba radhi (msamaha) kwa uzembe waliofanya ambao umesababisha kukithiri kwa vitendo vya kifisadi ambavyo vimesababisha maisha magumu kwa wananchi waliowachagua. Wabunge hawana haki ya kuilaumu serikali au Idara ya Usalama wa Taifa peke yake, bali wao pia pamoja na Idara ya Mahakama wanapaswa kulaumiwa. Kuilaumu Idara ya Usalama wa Taifa au sheria inayoiunda ni kuitoa kafara kwa makosa ambayo si yake.
 
USALAMA WA TAIFA BUTU

Wana – JF hoja alizotoa MZEE BUSARA ni nzito na hazina budi kujadiliwa kwa kina. Hoja hizo zimekata kiu yangu na kufungua milango zaidi ya fahamu kuhusu mjadala juu ya hoja ya ZITTO KABWE aliposema “USALAMA WA TAIFA BUTU”.

Nimesoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo pia inapatikana katika bodi yetu ndani ya jamiiforums.com na kuona MZEE BUSARA ndiye mchangiaji aliyezama zaidi ya wana JF wengine katika kuijadili mada hiyo ya ZITTO KABWE.

Kama kuna dhamira ya dhati ni vyema ZITTO KABWE na wana- JF wengine wajitokeze kujibu hoja za MZEE BUSARA ambaye katika mada hii ameleta changamoto mpya kwa kufukua yale ambayo hapo awali hayakuweza kujadiliwa na wana - JF.

MZEE BUSARA ametuonyesha mahusiano yaliyopo baina ya Mihimili mitatu ya Dola yaani Bunge, Serikali na Mahakama na kwamba ile dhana ya utengano wa madaraka baina ya mihimili mitatu ya Dola, haipo kikamilifu katika mfumo wa utawala unaoitwa ‘ Parliamentary system of government’ badala yake kuna ushirikiano mkubwa wa kimadaraka miongoni mwa mihimili hiyo.

Halikadhalika, Bunge ni chombo cha Usimamizi na uwezeshaji kwa serikali na Mahakama. Kama hali ni hiyo kwa nini lawama zote ni kwa serikali (executive) tu, hasa Idara ya Usalama wa Taifa.

Mimi binafsi naunga mkono hoja ya MZEE BUSARA kwamba hatuna sababu ya msingi kuelekeza lawama zetu kwa serikali (executive) tu na kuacha Mihimili mingine hasa Bunge kwa sababu utenganisho wa madaraka ambao ni kamilifu unapatikana katika mfumo wa utawala unaojulikana kama ‘ Presidential system of government’ ambao chimbuko lake ni Marekani na siyo katika mfumo wa ‘ Parliamentary system of government’ ambao ndio msingi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wana – JF tujadili kwa kina hoja ya MZEE BUSARA ya uhusiano uliopo kati ya Mihimili mitatu ya Dola ili kudhibiti vitendo vya kifisadi nchini.

Hivi karibuni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. ZITTO KABWE wakati akiwa katika chakuka cha jioni alichoandaliwa na Watanzania waishio katika Jimbo la Michigan (Marekani) aliwaeleza Watanzania hao kuwa Sheria ya uundwaji wa Idara ya Usalama wa Taifa Na. 15 ya mwaka 1996 imeifanya Idara hiyo kuwa butu na kwa hiyo ipo haja na ulazima wa kuipitia na kuifanyia marekebisho. Kauli ya Mbunge huyo ililenga kuonyesha kwamba ubutu wa Idara ya Usalama wa Taifa ni ule wa kushindwa kukabiliana na vitendo vya kifisadi.

Kauli hiyo ya ZITTO ilinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari likiwemo gazeti la Tanzania Daima la tarehe 8 Mei, 2008. Kimsingi, shutuma za namna hiyo kwa Idara ya Usalama wa Taifa zimekuwa zikitolewa mara nyingi hasa tangu vitendo vya kifisadi kuanza kuitikisa nchi.

Kauli hiyo ya Mhe. ZITTO KABWE pamoja na lawama zinazotolewa kwa Idara ya Usalama wa Taifa zinapaswa kuangaliwa kwa mapana hasa kwa kuzingatia kuwa nchi yetu ya Tanzania inafuata mfumo wa utawala unaoitwa “Parliamentary system of government” ambao chimbuko lake ni Uingereza. Ndani ya mfumo huo kuna mihimili mitatu ya dola yaani Serikali (executive), Bunge na Mahakama. Katika mfumo huo Serikali inakuwa moja kwa moja ni sehemu ya Bunge, lengo likiwa ni kulifanya Bunge na Serikali kuwa ni vyombo vinavyotegemeana na kwa hiyo vinapaswa kufanya kazi zao kwa ushirikiano mzuri ili kuweza kufikia lengo la kuwaletea wananchi maendeleo na ustawi wa jamii.

Ni vyema pia tutambue kuwa wajibu wa Bunge ni kuisimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kama Ibara ya 63(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inavyoeleza. Kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 63(3) ya Katiba hiyo, Bunge linasimamia utekelezaji unaofanywa na Serikali kwa kutumia njia ya kuwauliza Mawaziri maswali Bungeni kuhusu utekelezaji unaofanywa na Wizara, halikadhalika kujadili utekelezaji wa kila wizara uliofanywa katika mwaka uliotangulia pamoja na kutoa ushauri unaofaa kuzingatiwa katika mwaka wa fedha unaofuata.

Aidha, ni wajibu wa Bunge kuiwezesha Serikali kutekeleza wajibu wake kwa wananchi kwa kutunga Sheria na kupitisha bajeti. Hatua hiyo ndiyo inayoiwezesha au kuirahisishia Serikali kutekeleza majukumu yake.

Vivyo hivyo, kwa upande wa Mahakama kama muhimili wa tatu, majukumu yake yemeelezwa bayana katika Ibara ya 107 A na 107 B ya Katiba. Kwa mujibu wa Ibara hiyo, mamlaka ya utoaji wa haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki Mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya Katiba na Sheria za nchi. Kwa maneno mengine Bunge ni chombo cha uwezeshaji kwa Mahakama. Kwamba, Bunge linao wajibu kutunga Sheria zitakazowezesha Mahakama kutekeleza ipasavyo shughuli zake za utoaji haki, kwani bila Bunge kutunga Sheria mbali mbali Mahakama haitaweza kutimiza wajibu wake wa utoaji haki.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa hapo juu ni kwamba, Bunge ni chombo cha uwezeshaji kwa Serikali na kwa Mahakama. Dhana ya utengano wa madaraka baina ya mihimili hiyo mitatu ya Dola, haipo kikamilifu katika mfumo wa utawala unaitwa “Parliamentary System of Government:, badala yake kuna maingiliano na ushirikiano mkubwa wa kimadaraka miongoni mwa mihimili hiyo.

Kwa kuzingatia ukweli huo, je, ni sahihi kuilaumu serikali (executive) peke yake au Idara ya Usalama wa Taifa kwa kushindwa kukabiliana na vitendo vya kifisadi? Kwa nini watu wamekuwa wepesi kuilaumu Serikali (executive) na wamekuwa bubu kwa mihimili mingine ya dola? Je, Bunge pamoja na wabunge wake akiwemo ZITTO KABWE ambao wanailaumu serikali hasa Idara ya Usalama wa Taifa walikuwa wakifanya nini katika kuisimamia serikali vizuri ili kuweza kuondokana na vitendo vya kifisadi? Mbunge ZITTO KABWE anaposema Idara ya Usalama wa Taifa ni butu kutokana na sheria iliyoiunda, anategemea nani atarekebisha sheria hiyo? Sambamba na hilo, sheria hiyo ni ya mwaka 1996, kwa kipindi hicho chote ZITTO KABWE hakutambua kasoro ya sheria hiyo hadi leo mwaka 2008? Je ni kweli anatimiza ipasavyo wajibu wake kama Mbunge?

Kwa maoni yangu, mihimili yote mitatu inapaswa kushutumiwa na kunyoshewa vidole vya lawama kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kifisadi na siyo serikali (executive) au Idara ya Usalama wa Taifa peke yake. Ni ukweli usiopingika kwamba kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa mihimili hiyo mitatu ndiko kulikotufikisha hapa tulipo.

Wanasiasa (Wabunge) akiwemo ZITTO KABWE wasikwepe lawama wanazopaswa kuzibeba kwa uzembe walioufanya. Kama kweli wanathamini dhamana waliyoibeba wanapaswa kwenda kwa wananchi na kuomba radhi (msamaha) kwa uzembe waliofanya ambao umesababisha kukithiri kwa vitendo vya kifisadi ambavyo vimesababisha maisha magumu kwa wananchi waliowachagua. Wabunge hawana haki ya kuilaumu serikali au Idara ya Usalama wa Taifa peke yake, bali wao pia pamoja na Idara ya Mahakama wanapaswa kulaumiwa. Kuilaumu Idara ya Usalama wa Taifa au sheria inayoiunda ni kuitoa kafara kwa makosa ambayo si yake.
 
Mimi wala sisumbuki na Mkapa maana najua hakuna la zaidi litatendeka kwake.

Ila moja tu, kama rais wa nchi mstaafu, madudu yanapoanikwa kwa wananchi ni fedheha na aibu kubwa sana kwako.

Hamfahamu tu lakini adhabu hiyo haina tofauti na wale walioko gereza la Keko!!!

Adhabu zina machungu mbalimbali na tofauti kwa watu!!!!

Mfano adhabu kubwa kwa Mzee Mwanakijiji, ni Kulipua kijiji chake na Kushinda kuaccess JF kwa wiki moja!!!

Adhabu kubwa ya MWK ni CCM inapotekeleza ahadi yake at least moja!

Adhabu kubwa kwa JK, ni neno Mafisadi linapotamkwa!!!

Adhabu kubwa kwa Spika ni anaposikia jina la Mh. Zitto Kabwe.

Kasheshe wa enzi hizo... so daring, patriotic, inspirational and full of wisdom, where is he?!!
 
wanajeshi wetu kazi zao za kulinda nchi zimewashinda hadi wanaingilia kazi za kufanya biashara ya kukodi chopas kwa pesa ya walipa kodi. Nani aliamua iwe hivyo? Je, wamepata faida kiasi gani tangu waanze hii biashara? Hiyo faida nani anachukua Jeshi au kwenye matumbo ya MAFISADI?
very good points!niko pamoja nawe mkuu
 
Ngoja harakati za uchaguzi zianze, hujuma kwa wapinzani zikianza tu basi wamerudi.
 
TUSIWE WAJINGA WATANZANIA HATUHITAJI KUONGOZWA NA SYSTEM BALI TUNAHITAJI NA KUONGOZWA NA VIONGOZI TULIOWACHAGUA SYSTEM IS OLD FASHION ILA VYOMBO HIVYO VINAHITAHI KUPEWA MENO IKIBIDI HATA KUMHOJI MIZENGO PINDA AU KIONGOZI WOWOTE BASI KIWE NA NGUVU SI HIVYO TUTAKUA NA VYOMBO vya kutumaliza wenyewe kam ile Scorpion ya Afrika kusini iliotumika kumuwinda JAcob Zuma.

Hata Tanzania wanaongoza vyombo hivi lazima wawe na akili timamu kwani siku wananchi wakichoka na CCM na kuichagua Chadema au CUF tawala za vyama hivi lazima vitaangalia madhambi ya vyombo hivyi na hapo ndio kina nanihii watakapokosa kibarua.
 
TTUSIWE WAJINGA WATANZANIA HATUHITAJI KUONGOZWA NA SYSTEM BALI TUNAHITAJI NA KUONGOZWA NA VIONGOZI TULIOWACHAGUA SYSTEM IS OLD FASHION ILA VYOMBO HIVYO VINAHITAHI KUPEWA MENO IKIBIDI HATA KUMHOJI MIZENGO PINDA AU KIONGOZI WOWOTE BASI KIWE NA NGUVU SI HIVYO TUTAKUA NA VYOMBO vya kutumaliza wenyewe kam ile Scorpion ya Afrika kusini iliotumika kumuwinda JAcob Zuma.

Hata Tanzania wanaongoza vyombo hivi lazima wawe na akili timamu kwani siku wananchi wakichoka na CCM na kuichagua Chadema au CUF tawala za vyama hivi lazima vitaangalia madhambi ya vyombo hivyi na hapo ndio kina nanihii watakapokosa kibarua.

Mkuu naona umeongea kinyume kabisa na maoni yangu. Kwa nchi kama Tanzania tatizo ni kuwa tuna "rule of man" au kuongozwa na watu, hatuna rule of rules, regulations and laws, ingawa hiyo ndio inaimbwa kila siku.

Kama system ingekuwa functional na effective leo kusingekuwa na matatizo tunayolalamika nayo kila kukicha. Kila kiongozi angejua kuwa baada ya A ni B na baada ya B ni C, nikifanya A basi itakuwa B nikiiba pesa itakuwa C, lakini kutokana na kutofuata, kutotekeleza na kusimamia sheria tulizonazo ndio maana tuko hapa tulipo. Kama tukiendelea namna hii hatutatoka hapa.

Naona tunatakiwa kuwa na idara huru mpya, itakayofanya kazi ya kuwawajibisha viongozi ambao hawakutekeleza majukumu yao kwa makusudi. Labda hiyo itakuwa stick nzuri kwa viongozi ambao wanatamka wazi kuwa mafisadi wametushinda.

Ninachosema ni kuwa, rule of law ni much better kuliko rule of man, rule of law ni ya kisasa na kistaarabu kuliko kama rule of man kama ile ya uchifu ambayo mtu anafanya kazi kutokana na urafiki, au atakavyojisikia akiamka.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom