Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 799
Looks like it sasa kabla hamjaanza kumshambulia R.O tuanze kwa kuangalia hao wazungu walikuwa ni akina nani na je walipewa security clearance na nani? Na kwa nini walikuwa wanaopiga picha wakati wananchi wa kawaida hata kulima maboga jirani na kambi za jeshi hawaruhusiwi
Je hii failure ni ya watu wa ARMY INTELLIGENCE au watu wa USLAMA WA TAIFA? Je uslama wa Taifa wako likizo? na kwa nini SALVA AJIBU maswali yasiyo mhusu? MBONA KUMEKUWA NA MEDIA BLACKOUT kwenye hili?
Kazi kwenu
HELIKOPTA YA JESHI NA UTALII
SITAKI Rais Jakaya Kikwete aende likizo wakati kuna "suala kubwa linaloshusu usalama wa nchi."
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyememu aliviambia vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Ijumaa kuwa rais yuko likizo, lakini aweza kufanya kazi iwapo kuna suala kubwa linalohusu usalama wa nchi.
Ukweli ni kwamba rais asingekwenda likizo, kwani suala linalohusu usalama wa nchi lipo mezani kwake. Ni lile linalohusu usalama wa mipaka ya nchi na wananchi wake.
Ni suala la kuingia katika ghala la silaha za Jeshi la Wananchi (JWTZ), kuchukua helikopta ya jeshi na kuruka hadi Arusha, huku waliokuwemo, tena watu kutoka nchi za nje – Uingereza, Canada, Marekani na Australia, wakipiga picha.
Tutake tusitake, hili ni suala la usalama wa nchi. Linahusu usalama wa wananchi na mali zao. Linahusu maisha ya nchi na viumbe wake.
Katika safu hii wiki iliyopita, nililalamikia ukimya wa serikali kuhusu tukio hilo. Niliuliza maswali 42. Nilidhani wahusika wataelewa. Watakuwa wepesi wa kujibu. Wataona wanawajibika kutoa majibu. Wataonyesha uadilifu.
Leo hii, wiki tatu tangu kupatikana kwa taarifa za helikopta ya jeshi kutumiwa na watalii kupiga picha, hakuna taarifa yoyote ya serikali – kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Juma Kapuya au Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya Mrisho Kikwete.
Katika hali hii, sharti watu wenye uchungu na nchi hii; wale wanaojali usalama wa nchi na watu wake, waendelee kuuliza. Hii ni kutokana na uzito wa suala lenyewe; ni kubwa na "linahusu usalama wa nchi."
Ingawa wanaoiuzia silaha Tanzania wanajua kuna aina gani, kiasi gani, kutoka wapi, kwa bei ipi, zinaweza kutumiwa vipi na zina uwezo gani; kuna mambo kadhaa hawajui. Kwa mfano, hawajui lini silaha hizo zinahitajika kufanyiwa kazi.
Lakini hatua ya watu kutoka nchi za nje, kukodi, au kupewa, au kuiba helikopta ya jeshi na kuitumia kwa kazi binafsi, inaonyesha kuwa: Jeshi limeingiliwa. Kuna wanaojua taratibu za kila siku jeshini, matumizi ya zana; zipi zinahitajika sasa, zipi zikodishwe na zipi zikae "stendibai."
Hao ndio wanakwenda ama kuchukua, kukodi au kupewa helikopta za jeshi. Au kuna "Idara ya Masoko" jeshini inayotangaza na kufuatilia wateja wa kutumia hekikopta zake.
Aidha, hatua ya kupata helikopta ya jeshi kwa matumizi binafsi, inaonyesha ama ulinzi ndani ya jeshi umepungua au umelegezwa. Nani kapunguza au kalegeza ulinzi na kwa nini; ndilo swali kubwa hivi leo.
Nani amekataa kuweka suala hili mezani kwa Rais Kikwete, mpaka rais anakwenda likizo bila kulishughulikia? Au, nani amemshauri rais kuwa ni "jambo dogo" kwa hiyo alale na kusahau?
Au tafsiri ya "usalama wa nchi" ndiyo inagomba? Na hili linawezekana. Kuna wanaodhani usalama wa nchi ni usalama wa rais kutopinduliwa, kutopingwa au kutoseng'enywa. Huo ni ufinyu na upofu.
Nani anaweza kumuaga rais, na kumtakia likizo njema, wakati katika jeshi lake kuna biashara inayoweza kuzaa mtafaruku mkubwa wa kuweza kumeza amani nchini au kurudisha nyuma maendeleo madogo ya kidemokrasi yaliyopatikana?
Labda rais awe anajua kuwa kinachoendelea "ni kidogo kisicho na athari mbaya na kubwa;" au anaridhika kuwa kinachofanyika ni sahihi; au hana taarifa kamili juu ya kinachotendeka.
Vyovyote itakavyokuwa, hapo ndipo rais anapaswa kujenga mashaka juu ya chochote kinachotendeka; hasa chochote ambacho wananchi wametilia mashaka; na hasa kile ambacho wachambuzi wameonyesha kinaweza kuleta madhara kiulinzi, kisiasa na kiuchumi.
Ukimya wa serikali unaleta tafsiri nyingi. Kwamba wanaokataa kutoa kauli, wanajua kinachoendelea lakini wanashindwa kutoa majibu ambayo wanajua vema kwamba hayatazima kiu ya wananchi na wapenda nchi.
Kwamba wanaokataa kutoa kauli wanajua nani aliidhinisha matumizi ya helikopta nje ya utaratibu; wanajua kama ndio utaratibu na wanajua nani anachuma kutoka mradi huu ambao bila shaka unaingiza fedhi nyingi.
Na katika hili, tukizungumzia viongozi serikalini ambao wanapaswa kutoa kauli, tuna maana ya kwanza na moja kwa moja, Rais Kikwete, Waziri Mkuu Edward Lowassa, Waziri Kapuya, mteule wa rais, Jenerali Mwamunyange na Waziri wa Habari Mohamed Seif Khatib.
Kama wasemaji wanaona suala hili la kuvunja na kuingia kwenye ngome ya jeshi na kuchukua, kuiba au kupewa helikopta ni suala dogo, kwa nini hawatoi majibu yanayolingana na "udogo" huo?
Kama wanaona ni suala kubwa, tena la ulinzi na usalama wa nchi, kwa nini wanakaa kimya na kumwacha rais aende likizo wakati kuna suala kubwa la kumzuia kwenda kulala?
Mkuu wa Mawasiliano ikulu, Salva Rweyemamu, anasema likitokea jambo kubwa la usalama wa nchi, rais anaweza kufanya kazi akiwa likizoni.
Salva, mpelekee rais suala hili. Mfafanulie kwamba, kama ngome ya jeshi imepenywa, na watu kutoka nje wakachukua helikopta ya jeshi kwa raha binafsi, basi yeye na wananchi wake wote, wako uchi!
Mwambie avae na avalishe nchi yake. Lakini muhimu zaidi, mwambie ajibu maswali ya wananchi yaliyowasilishwa kupitia safu hii – wiki iliyopita na leo – ili wajue nafasi yake katika hili na hatua anazochukua.
(Makala hii imeandikwa kwa kuchapishwa katika safu ya SITAKI ya gazeti la Tanzania Daima, Jumapili, 23 Desemba 2007. Mwandishi anapatikana kwa simu: 0713 614872; imeili: ndimara@yahoo.com)
Huyu mzee alianza na article hii:
JWTZ NA BIASHARA YA KITALII
Na Ndimara Tegambwage
SITAKI serikali ikae kimya kuhusu matumizi ya helikopta ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) iliyoanguka mkoani Arusha siku 11 zilizopita. Sitaki!
Maelezo ya awali ni kwamba helikopta ya jeshi ilikuwa imebeba "watalii" kutoka Canada, Marekani, Uingereza na Australia na kwamba ilianguka na kuwaka moto.
Watalii na helikopta ya jeshi? Watalii kutoka nchi za nje, na siyo watalii wa ndani ya nchi, na helikopta ya jeshi? Watalii wasiokuwa na uwezo kifedha wa kukodisha ndege yao mpaka watumie helikopta ya jeshi?
Watalii kutoka nchi tajiri, Canada, Marekani na Uingereza, nchi washirika wakubwa katika maendeleo ya Tanzania kwa kutoa mikopo na misaada, hawana uwezo wa kukodi ndege kutoka kampuni binafsi? Mpaka watumie helikopta ya jeshi?
Eti watalii walikuwa wanapiga picha za Ziwa Natron na mlima Oldonyo wenye volcano hai! Kwamba ziwa na mlima haviwezi kuonekana vizuri kutoka ndege ya kiraia mpaka mpigapicha awe katika ndege ya jeshi?
Katika hili kwa nini serikali inakaa kimya? Inataka habari hii ife? Inataka wananchi waendelee kujiuliza maswali mengi bila kupata majibu sahihi? Au inataka baadaye, itoke na kauli kwamba mambo ya jeshi hayajadiliwi katika vyombo vya habari?
Hakika, hapa serikali isisubiri kuumbuliwa. Ni jana, Jumamosi, baadhi ya waandishi wa habari walikabidhiwa tuzo za uandishi wa uchunguzi nchini. Ukweli ni kwamba bado wanatambaa, lakini tuzo hizo ni motisha kubwa katika kuandika habari za uchokonozi.
Leo hii, hakuna habari nono kama hii. Rubani wa helikopta ni nani? Helikopta ilianzia wapi safari ya kwenda Natron na Oldonyo. Ilipita wapi na "watalii" walikuwa wakifanya nini kabla ya kukaribia maeneo waliyokuwa wakitaka kupiga picha?
Je, kuna kitengo cha utalii katika JW? Kama kipo, kina ndege na helikopta ngapi? Vifaa vyake vingine kwa shughuli hii ni vipi? Je, utalii ni moja ya miradi ya jeshi ya kuzalisha fedha za matumizi ya nyongeza? Je, jeshi linapungukiwa fedha kiasi cha kuanzisha miradi ya "kubangaiza?"
Je, helikopta iliyobeba watalii iliidhinishwa na nani kufanya kazi hiyo? Ilitoka ngome ipi ya jeshi? Kwa nini iliamuliwa kuwa hiyo ndiyo ilikuwa inafaa? Rubani wa helikopta ya jeshi alijuaje maeneo ya kupita ili watalii wapate picha nzuri waliozotaka?
Kuna maswali mengi. Wanaoitwa watalii walitoka wapi kabla ya kuingia Tanzania? Nani anaweza kuthibitisha kweli kwamba ni watalii? Viwanja vya ndege na, au mipaka ya nchi ina rekodi gani juu ya kuingia nchini kwa watalii hao?
Tayari helikopta imeanguka na kuungua. Watalii wamepona! Nani amethibitisha uraia wa watalii? Balozi za nchi watokako watalii hao, zilizoko Dar es Salaam, zinasemaje juu ya raia wake, kama kweli wanatoka huko?
Balozi ambazo nchi zao huning'iniza serikali za nchi nyingi zikizitaka kuwa adilifu, zinasema nini juu ya raia wake kutumia helikopta ya jeshi la ulinzi kwa raha na mafao ya binafsi?
Kuna uhusiano gani kati ya watalii wa Canada, Marekani, Australia na Uingereza kwa upande mmoja, na balozi na nchi watokako, kwa upande mwingine? Je, inawezekana "watalii" wametumwa kutoa mtihani wa uimara au ulegevu wa jeshi?
Nani alichora mpango wa watalii kutumia helikopta ya jeshi? Huyo lazima awe mtu muhimu katika mahusiano ya jeshi. Kwamba ndege ndogo za kibiashara zinagombea maegesho kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, ni motisha gani watalii walipata kutumia ndege ya jeshi?
Hapa ni muhimu kujua iwapo rubani alikuwa askari wa JW au raia anayejua kuvurumisha kikata hewa hicho Je, rubani wa helikopta alikodishwa kwa kiasi gani au alikuwa wa kujitolea?
Je, helikopta ya jeshi ilichukuliwa kwa mkataba upi? Kuna malipo yoyote yaliyotolewa au ahadi ya kulipa? Kiasi gani cha malipo – fedha taslimu au asante kwa njia mbalimbali? Lini malipo hayo yatatolewa au yalitolewa?
Lakini muhimu pia ni kujua nani hasa anafaidika na malipo hayo – aliyeidhinisha matumizi ya helikopta, rubani na aliyemtuma, baadhi ya maofisa wakuu jeshini, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa au ikulu? Nani anapokea "mshiko?"
Muhimu pia ni kwamba Amiri Jeshi ni rais. Mara hii ni Jakaya Mrisho Kikwete ambaye wakati anaondoka wiki hii kwa ziara ya Marekani aliacha helikopta yake imetumiwa na "watalii" na imeanguka na kuungua.
Amiri Jeshi anasemaje juu ya matumizi ya helikopta "yake?" Helikopta za jeshi, kama zilivyo ndege na magari ya jeshi, ni sehemu ya zana za kazi; waweza kusema, zana za ulinzi wa taifa. Vimeundwa na vinapaswa kutumika na kusimamiwa kwa misingi ya ulizi.
Nafasi ya Amiri Jeshi ni ya kulinda maisha na mali za wananchi ndani ya mipaka ya nchi yao na dhidi ya uchokozi au uvamizi kutoka nje. Kwa maana pana, helikopta ni mali ya wananchi, waliyonunua kwa kodi wanazotozwa na inayopaswa kutumiwa kwa ulinzi wao.
Katika mazingira ambamo serikali imekataa kutoa taarifa juu ya helikopta ya jeshi kutumiwa na watalii kutoka nje kufanya shughuli binafsi, ni uandishi wa wa uchokonozi ambao pekee unaweza kusaidia kuleta nuru juu ya kilichotendeka.
Hadi hapo taarifa zitakapowekwa wazi, acha kila mwananchi awe na mawazo yake: Kwamba sasa jeshi linabangaiza kama machinga; au halina ulinzi kwani kila mmoja aweza kuingia na kujichukulia ndege anavyotaka; au ulinzi wa wananchi sasa mashakani; au wakubwa wameamua kutumia jeshi kufanya biashara ya anga; au amiri jeshi kaenda likizo.
(Makala hii imeandikwa kwa ajli ya safu ya SITAKI, gazeti la Tanzania Daima Jumapili, 16 Desemba 2007. Mwandishi anapatikana kwa simu: 0713 614872; imeili: ndimara@yahoo.com)

========================
HELIKOPTA YA JESHI NA UTALII
- Likizo ya rais na usalama wa taifa