Mkuu kuna baadhi ya biashara ukiangalia flow yake unaona zinakosa uhalisia , Sauli anajulikana ni mfanya biashara wa dhahabu, kwake yeye kununua basi zile ilikuwa sahihi kabisa na hata struggle ya kuongeza gari nyingine unaona kabisa kuna connection ya hustling. Esther hana hata miaka 10 kwenye game yet ana magari ya kumwaga , sidhani kama ana gari chini ya namba' D'. Kampuni mpya zinazokuwa kwa kasi ya ajabi mara nyingi zinakuwa na connections za wanasiasa .
Esther ana
Basi nane rombo dar
Basi nne arusha dar
Huko singida dar sijui idadi yake
 
Unamjua mumiliki wa Esther? Hakuna biashara pake.. ni utakatishaji wa ngawira
Ni nani huyo? Kuna siku korogwe Tanga asubuh nikadamkia mombo, mtu niliekua nakutana nae kwa bahati mbaya akachelewa nikaa kwenye kiosk nikawa namsubiri, zilipita bus 13 za Esther hadi mda naondoka, za kwenda na kurud

Hapo hapo bado zipo za kiomboi huku

Muda uliotumika vs Success n mfupi mno

I think aliwakuta Marangu, Extra Luxury , hata Tilisho pia. Ila kakua kwa speed ya umeme
 
Abood ana mabasi zaidi ya 300 unashangaaje hayo20
Abood alinunua mabasi mawili ya kwanza miaka ya themanini mara to baada ya kumaliza Forest hill kwa kutumiea pesa za mishen town. Hata hivyo inaonekana alikuwa na discipline kubwa sana kwenye hela kwani takriban miaka 40 sasa bado hajateteteleka. Kwa hiyo kutafuta hela ni jambo moja, ila plani nzuri ya kutumia hela hizo ni jambo kubwa sana
 
Ameishika njia ya morogoro -dar hana mpinzani,biashara anaijua
 
Hapa kwenye mishen town uongo!!..Miaka ya 80 Hadi 90 Abood hakua na basi Nyingi!!..Miaka hiyo Kwa biashara za usafirishaji Morogoro/Dar na Tanzania Kwa ujumla Abood hakua Moto wala hakuna ailyewaza angekua kama sasa!!..Kuna Historia nyingi za Mji wa Morogoro na wafanyabiashara wengi wameondoka mji huo na wanafanya biashara zingine ndio Abood alipochukua uongozi!!
mabasi ya kwanza ya Aboud yalinunuliwa nadhani kati ya mwaka 81 na 82 au 83 hivi. Mtaji wa kwanza wa Aboud kwenye mabasi ulitokana na "misheni town" mzee. Ila jamaa ana akili, baada ya kutake off akaachana na hizo misheni town.
 
Wakati huo superfeo kaingiza scania GX sab.G7 angalau scania wamejitahidi finishing japo mchina bado yupo moto kwenye finishing na comfortability
Mchina hana confotability, siti ndogo mno na ukiegemea hupati raha yoyote, basi lina siti nyingi mno kwahiyo zipo karibu karibu zinaumiza miguu, sasa usiombe uwe mnene hizo siti ni changamoto,
 
Ameishika njia ya morogoro -dar hana mpinzani,biashara anaijua
Dar moro hata wewe ukipewa nafasi lazima utoke, ila kuna fitna za chini chini sana hapo ,
Hii ndo ruti fupi sana iliyo busy muda wote , ni kama vile sirari to mwanza ilivyo busy.na basi za kichina zinapenda sana aina hiyo ya route.
 
Aboud anaposikia SGR roho inamuuma sana, huenda aao ndio watakaohujumu SGR kusudi biashara zao zisiathirike.
Mkuu Sgr ipo mombasa to nairobi huu mwaka karibu wa tatu kama sikosei , na basi hazijaathirika, Train ina limitations kadhaa hasa katika ulimwengu wa tatu ! Cha kwanza ni connection zake , Mfano masoko ya mbao yapo buguruni hapo na Tazara ipo hapo hapo , , kule makambako soko la mbao halipo mbali na station ya Tazara na katika njia zake reli ya Tazara inapita uwani kabisa kwenye msitu wa mbao wa serikali ,Sao hill, Ulishawahi juiuliza kwa nini mbao bado inakuja na malori mjini hapo?
Abood hata Sgr wajenge kituo msamvu , bado ataongeza mabasi
 
Ni kama mwendokasi vs daladala. Daladala ilibidi ziwekewe vikwazo katika ruti zake wakati tulitegemea daladala ziachiwe ili zishindwe zenyewe(kifo asilia).
Picha inaanza nauli 400tsh vs 650tsh .
Kwa hiyo SGR labda ITASHINDWA kwenye nauli. Tofauti ya sh 3000 tu itafanya watu wapande mabasi.
 
Back
Top Bottom