Mbeya: Madereva wa mabasi ya New Force, Zanuni, Rungwe Express, Super Rojas, Abood Bus Service na Kyela Express wafungiwa leseni kwa muda

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kuzuia na kudhibiti ajali za barabarani kwa kushirikiana na mamlaka na wadau mbalimbali wa usafirishaji katika Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamini Kuzaga amesema Jeshi hilo linaendelea kuimarisha na kufanya misako na doria katika maeneo ya barabara kuu ili kuzuia uhalifu na ajali zinazotokana na uzembe na sababu nyingine za kibinadamu.
Kuzaga.JPG
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya katika kuzuia na kudhibiti makosa ya barabarani pamoja na ajali za barabarani kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari 2023 hadi Juni 2023 limefanikiwa kuchukua hatua mbalimbali kwa madereva wa vyombo vya moto hususani mabasi ya abiria.

Kwa kipindi hicho, jumla ya madereva saba (07) wa mabasi ya abiria wa Kampuni ya New Force, Zanuni, Rungwe Express, Super Rojas, Abood Bus Service na Kyela Express walikamatwa na kuchukulia hatua za kufungiwa leseni zao za udereva kwa kipindi cha miezi miwili, mitatu na wengine kufikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha, miongoni mwa makosa ya usalama barabarani yaliyoripotiwa kufanywa na madereva hao ni pamoja na kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi, kusababisha ajali ya kifo, kusababisha ajali ya majeruhi na uharibifu wa magari na miundombinu ya barabara.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa madereva kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya litaendelea kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo madereva kwa kushirikiana na vyuo vya udereva pamoja na kuwakumbusha madereva sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.
 
Madereva wenye kesi ya kuendesha mwendo kasi bila kusababisha ajali wafutiwe kesi na warudishiwe leseni zao

Spidi zilizoko kwenye basi hazikuwekwa kama mapambo zinatakiwa kufikiwa cha msingi umakini tu

Dereva ana kosa gani kukimbia spidi ya kufa mtu kama yuko makini?

Binafsi kama abiria napenda kupanda basi linalokimbia hasa

Kama mwendo.kasi kesi basi polisi waruhusu matrekta yaanze kusafirisha abiria mikoani

Waanze kutoa leseni za safari zs.mbeya Dar na Dar Mbeya. Matrekta yaanze kusafirisha abiria ili roho za polisi wa usalama barabarani mioyo yao isiuzike wasisumbue mabasi yanayotimua mbio hasa na hayasababishi ajali
 
Exactly mkuu,tatizo barabara zetu bado sana, tukijua ukweli huu itatusaidia sana,hii T1 ni barabara ya miaka ya 60s, inabidi tuijenge upya, Zambia wameshaanza kuijenga upya upande wao, kwa sasa wapo Nakonde, ila kutoka isoka hadi chinsali mkeka umetulia, power Tools from Lusaka hadi nakonde anatoboa within 12hrs(1000km),Dar to Mbeya ni 800km huu ni mwendo wa saa 9 kwa bus
 
Back
Top Bottom