Usafiri enzi zile Mwanza yetu


Sawa ni lucky studio hiyo ingine ilikua mitaa ya bamboo club
 
Kulikuwa na mashine kule sokoni kirumba but tulikuwa hatuendi huko, ilikuwepo mashine hapa karibu na Monarch hotel, hii barabara kama unaenda CCM kirumba

Hizo mashine za kirumba ni zipi? zile za barabara ya kwenda mwaloni au?
 
Kulikuwa na mashine kule sokoni kirumba but tulikuwa hatuendi huko, ilikuwepo mashine hapa karibu na Monarch hotel, hii barabara kama unaenda CCM kirumba

Hapo sawa sawa, na uko sawa kabisa, nimeikumbuka, ila mashine hiyo wakati ule ni kama vile tulikuwa tunasema iko Mbugani au?
 
Reactions: ram
ahahahahahhhh... yaani nimechekaje kwa sauti, duh! kadogori, mie mwenyewe kitambo sana sijazikia hapa town

Hahahaha
Kuna nyimbo moja ilikuwa inaimbwa na lile kundi la kutoka kigoto inaitwa shida haina adabu,Jamaa alikuwa anamalasta, zikianza na zile filimbi hahaha mabinti walikuwa wanakatikaje!!!! LOL.
 
Reactions: ram
kadogori ilikuwa si mchezo, zile filimimbi na zile ngoma automatic tu unajikuta unatikisika, kulikuwa na kundi la kigoto, ibanda na shede. Shede nako ilikuwa balaa, kuanzia kadori, lelemama,vikojozi wanaotembezwa mitaani, ghasi zote zilikuwa zinapatikana shede

Hahahaha
Kuna nyimbo moja ilikuwa inaimbwa na lile kundi la kutoka kigoto inaitwa shida haina adabu,Jamaa alikuwa anamalasta, zikianza na zile filimbi hahaha mabinti walikuwa wanakatikaje!!!! LOL.
 
Kuna magari yao na yule dada wa Kona ya Bwiru, Zainabu Kichaa, Yalikuwa yanaitwaje ram? na mengine yalikuwa pale kwa Bora Kufa, unayakumbuka?
 

Basi Mkuu QSS utakuwa umewafahamu hivi karibuni. Mwanzoni kabisa walikuwa maeneo ya mwanza hotel. Jyoti walihama baada ya jengo lao kuvunjwa ili kupisha ujenzi wa jengo jipya.
 
Basi Mkuu QSS utakuwa umewafahamu hivi karibuni. Mwanzoni kabisa walikuwa maeneo ya mwanza hotel. Jyoti walihama baada ya jengo lao kuvunjwa ili kupisha ujenzi wa jengo jipya.
Mkuu kwa kiasi fulani Mwanza mimi ni mwenyeji. Ngoja nikukumbushe kitu. Waliokuwa jirani na Mwanza Hotel ni Jyoti Art Studio. Hawa QSS mwanzo kabisa 1984 na kurudi nyuma yule mzee na vijana wake wawili walikuwa wakifanya biashara tofauti na walikuwa pale Nyerere road jirani kabisa na zilipo traffic lights. Yaani kama unatokea kule Mwanza Hotel ukifika pale kwenye mataa na kuvuka barabara wao walikuwa jengo la kwanza au la pili kushoto kabla ya kupita kichochoro cha kuelekea Salma cone. Kulia kabla ya kuanza uchochoro kukiwa (hadi leo) na mzee mmoja hivi wa kihindi akiuza juice kwa sana na kadi mbalimbali. Wakiwa pale yule mzee na hao watoto wake walikuwa wakipokea mikanda na negative za picha za rangi kutoka kwa wateja na wao kuwapatia madereva wa magari ya kwenda Kenya kisha kurudi nazo baada ya kusafisha kwa ajili ya watej wao. Kumbuka wakati huo kulikuwa hakujawa na mitambo ya kusafisha picha za rangi kwa Mwanza. Baadae kidogo wakiwa palepale karibu na hizo traffic lights ndipo mwaka 1985 wakaweza kununua na kufunga mitambo ya kusafisha picha za rangi. Hii ilikuwa ni mitambo ya kwanza kabisa ya picha za rangi kuingia mjini Mwanza. Nakumbuka vizuri kijana wake wa pili yule mzee wa QSS (Shakeel?) aliacha masomo kabla hata ya kumaliza form one pale Mwanza Secondary ili aweze kuungana na baba yake katika kusimamia hiyo biashara ya photo printing. Walikaa hapo miezi michache tu kisha wakahamia mtaa wa Uhuru. Hapo Uhuru street ndipo jina la QSS lilipokua kwa kasi na pia mikanda ya Tudor, Konica na Fuji colour kupata umaarufu mkubwa miongoni mwa wapiga picha. Baada ya miaka michache wakahamia walipo sasa hivi Nyerere road kwenye jengo lao jirani na Furniture Centre, Chakula Barafu, mnara wa Nyerere au NBC. Kwa waliokuwepo miaka hiyo na wenye kumbukumbu nzuri palipo hilo jengo la QSS kabla ya jengo la awali kuvunjwa na kujengwa ghorofa la sasa palikuwa na duka la National Pharmaceuticals Company Ltd (NAPCO). NAPCO baadae wakahamia Kenyatta/ Rwegasore. Kuna jamaa alikuwa hapo QSS miaka mingi akiitwa Morgan namkumbuka sana. Sijui kama bado yupo au la. Baadae kidogo kuna studio nyingine ikiitwa Shelui nao waliweka mitambo yao kwenye jengo ilipokuwa Urshers club maeneo ya Liberty kabla ya studio zingine zaidi za picha za rangi kuibuka.
 
Last edited:
Jay ambe na geza ulole
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…