Mkuu China Isikutishe sana kijeshi hasa katika hayo makombora ya nyuklia, wakati Urusi (USSR wakati huo) inaeneza teknolojia ya nyuklia kwa mataifa machache ya Kikomunisti baada ya kuiwezesha Korea Kaskazini, sasa ikawa zamu ya Cuba ili kuinyamazisha US mwaka 1962 lile tikisiko la amani ya dunia lililoitwa Missile Crisis, baada ya Urusi kukubali kusitisha kupeleka yale makombora na mpango wa kujenga vinu vya kinyuklia Cuba, kuliibuka mgogoro mkubwa sana kati ya China na Urusi, hivyo China hakuwa mfaidika wa teknolojia hii, na hakukuwepo taifa lingine la kuipatia china teknolojia hii kwa sababu China ilikuwa nchi ya kijamaa na hivyo ni Urusi tu ndo wangeweza kuwapatia. China sasa hivi silaha yake KUBWA ni watu, yaani idadi, ndo imekuwa tishio kwa uchumi wa mataifa makubwa hasa unapoingia naye uhasama. kwa sababu ya soko CHINA IKIGEUKIA KUNUNUA BIDHAA TOKA TAIFA FULANI INAWEZA KULIFANYA KUWA TAJIRI NDO MAANA MAREKANI AKAONDOA UHASAMA NA KUANZA KUWEKEZA CHINA. Hivo China imekuwa ni taifa linalogombaniwa kuwa rafiki wa kila taifa kubwa kwa sababu za kiuchumi.
Kama unakumbuka vizuri mwaka 1999 wakati majeshi ya NATO yakiishambulia Yugoslavia kumtoa Slobodani Milosovic yalipiga ubalozi wa China yalivodai kwa bahati mbaya, lakini nafikiri pia ilikuwa kutingisha kiberiti, China iliwaka na kudai iombwe radhi, nakumbuka Marekani ilijibu kihuni kwamba tumetoa maelezo kwamba shambulizi lilikuwa la bahati mbaya na hamna haja ya kurudia kutoa maelezo, hii ni kwa sababu ile nguvu ya China kijeshi ambayo wengi tumeipachikia haina ni PSEUDOPOWER ipatayo kutoka kwa tusio makini na historia ya Dunia.
The same ikatokea 2005 marekani ilishambulia masafara wa barozi wa Italia na kumwua afisa upelelezi wa Italia, wakidai walidhani msafara wa kumtorosha Saadam Hussein, Italia ikakasirishwa na jambo hilo, ikataka maelezo ya msingi, pia askari waliohusika katika tukio hilo wapelekwe italia mashtaka. Marekani chini ya Bushi ilijibu kwa ustaarabu na umakin mkubwa na kuomba radhi juu ya hayo yaliyotokea kisha kuandika maelezo ya kutosha juu ya shambulizi lenyewe na kosa lilitokea.
Nakukumbusha kuwa kuna mataifa yenye nguvu yanayoogopwa si China kama tunavowapamba, China ina nguvu ila Magiants hawahofu mno kama tunavopenda kusema. Mataifa yasiyotabilika na yanaogopwa ni, Urusi, German, Italy, N. korean na Cuba. Sijataja US, UK na France maana husimama upande mmoja kuchokoza wengine. France anjificha kwa US na UK, mataiofa hayamuhofu sana siku zote. Kumbuka sakata la Edward Snowden, ndio maana yeye pia kakimbilia Urusi, nchi nyingine ingepigwa mkwara, ingevamiwa au CIA wangemfuata na kumwulia humohumo, lakini sasa Snowden amepewa kibali cha kuishi na ameajariwa.