green29
JF-Expert Member
- Jul 4, 2007
- 311
- 44
Hizi picha nimeziona kwa Michuzi. Sasa kwa kiwango alichofikia Obama sasa hivi sidhani kama ni sahihi yeye kuonekana akiwa katika Diaper, Hata kama hizi picha zinaonyesha maisha ya kweli ya Obama akiwa kama mtu wa kawaida. Ikumbukwe kuwa yeye sasa hivi anaangaliwa na dunia nzima kama vile mtu anayetaka ku-set a record in the world. Kwa ushauri wangu kama kuna mtu anamfahamu Michuzi au kama Michuzi mwenyewe yupo humu naomba aziondoe basi haswa hizi zenye kuonyesha mapengo na hii aliyovaa diaper. Just giving him some respect.
Hizo Dipers Hazina shida, it is a reality of life, kuwa Obama alikuwa mdogo, akawa mkubwa. Si dhambi kujulikana kuwa sisi ni kina nani na tumetoka wapi. Mgombea urais sio Mungu! NI binadamu kama binadamu wengine. Bush ni binadamu kama wengine, Kikwete ni binadamu kama wewe na mimi. Ndio maana mzee Mwinyi anaenda zake town siku hizi akiwa kajivalia ndala na shati kachomolea utafikiri form one wa Azania enzi hizo!
Unanikumbusha nilipokuwa shule ya msingi rafiki yangu alimpenda msichana, sasa siku moja alikuwa na mawazo sana, nikamuuliza vipi mbona mawazo mengi, akaniambia dah, nawaza hapa kama "Clara" huwa nae anaenda haja kubwa kama sisi!? Nikamuuliza kwa nini, akadai.. msichana mzuri kama huyu ni ngumu kuamini kama akienda kujisaidia anatoka uchafu!!!! NIkimuangalia usoni jamaa hacheki yuko sereous....
nikajua huyu design milembe inamuita!!
We are just natural beings, cheo, pesa, majina hayabadilishi hilo. Tutaheshimika na kuthaminiwa kwa yale yajazayo mioyo yetu, na yale tunayoyatamka, na tunavyoishi mbele za watu, na mchango wetu kwa ujumla kwenye jamii. Kila mtu anafahamu kuwa tumezaliwa kama binadamu wengine na hatujashushwa kutoka kwenye sayari nyingine. Tukipata nafasi yoyote hapa duniani ni muhimu sana kumshinda shetani ili tusitamani kuabudiwa kama miungu ya kolelo.