US Election Coverage 2008

Uwezekano wa Obama, kuwa rais wa US huo bado haupo, US ina majimbo 51 so far ni uchaguzi wa jimbo moja tu ambalo hata Bill Clinton mwenyewe hakuweza kushinda, in fact ushindi wa Clinton ulianzia jimbo la Georgia, Iowans ni Conservatives na 93% ni wazungu, weusi ni only 3%, sheria za kura ni kwamba unajiandikisha tu na ukiingia kwenye chumba cha kupiga kura sio lazima ukipigie chama fulani, meaning kwamba unaweza kujiandikisha kama Republican na uakingia kumpigia kura mgombea wa Democrat, that is exactly what happened,

Conservatives Republicans wameenda kumpigia kura Obama, kwa sababu hawamtaki Mama Clinton, thinking kwamba hiyo momentum inaweza ku-catch a fire kwa US nzima, kwa sababu kwa kura alizoshinda Obama, in maana kwamba kama Iowa ingekuwa ni nchi, bsi ukifanyika uchaguzi wa rais leo Obama atakuwa rais wa Iowa, politically, does this make a sense? No way!

Obama, ni a good candidate, tena very clean the black nation huko US limekuwa likihangaika sana kutafuta a hero here they have one, smart, articulative na charismatic, isipokuwa tatizo ni kwamba he is not Black enough kwa weusi wa huko US, so far bado Mama Clinton anaongoza kwenye polls among weusi, na nafahamu for a fact kuwa weusi huko huwa hawatutaki Afrikans,

Binafsi I like Obama, kwa sababu zile zile za kumkosesha tembo usingizi, huwezi kujua time zimefika bila ya kujaribu and that is what Obama is doing now, cha muhimu ni kumpa support as much as we can, kwa sababu the more Obam tries, ni the more anavyo-elevate race yetu weusi na kutupatia heshima zaidi, na kutuweka kwenye ramani ya dunia, it worthy kum-support Obama, kuliko the rest of the candidates!

I hope he wins it all!

Mukulu, kula kumi kabisa! Hicho ulichokisema ndio mimi nimekuwa nakisema. Marekani ina majimbo 50. Na kati ya hayo 50, jiulize ni mangapi yana statewide elected officals? Georgia ambayo asilimia 29 ya wakazi wake ni weusi haijawahi kutoa hata seneta mmoja achilia mbali gavana. Mississipi yenye weusi asilimia zaidi ya 36 haina statewide elected official kwenye congress ya Marekani.Yaani deep south yote kuanzia North Carolina hadi Texas Obama hana fighting chance. I can't imagine a democrat winning the presidency without winning at least 2 or 3 states in the south. Watu wanakuwa wepesi mno kusahahu kuwa hata Jesse Jackson alishinda primary kadhaa ile '84 na nadhani hata '88. Yaani haya ya Obama kushinda hiyo caucus (though it's a good thing anytime you win something) imenikumbusha yale ya Taifa Stars kuishinda sijui timu gani ile ktk mechi za mtoano kwenda kwenye kombe la mataifa huru ya Afrika. Ushindi wa Stars haukuwa na maana yoyote (ktk context ya ku-qualify) lakini watu walivyopagawa utadhani labda tumeshinda kombe la dunia. Zikachangwa hadi shilingi zaidi ya millioni 400 kwa muda wa siku chache tu!! wakati huo huo kuna wanafunzi wanahitaji msaada Ukraine. Jamani mambo ndio yameanza tu. Kuna New Hampshire, kuna South Carolina, kuna Super Tuesday n.k....halafu pamoja na kwamba Iowa overwhelming majority ni wazungu lakini ni very progressive state. Utashangaa Georgia na Alabama ambazo zote zina idadi kubwa ya weusi kuwa na ubaguzi zaidi kuliko Iowa. Kwa hiyo sishangai hata kidogo Obama kushinda Iowa. Kwangu mimi akishinda Georgia, Alabama, Mississipi, Louisiana, South Carolina, Tennessee, hapo ndo ntasema kweli jamaa kiboko. But so far I'm withholding my enthusiasm....
 
wakuu dont underestmate this guy na dont compare him na kina Jesse jackson ni watu tofauti sana na historia/background zao ni tofauti sana,kwanza mjue Jesse alipoingia kwenye race tayari alikuwa na enemies kutokana na kujihusisha na zile civil rights movements,wasiwasi wangu ni rangi tuu maana siwaamini hawa wazungu ingawaje nilikuwa wrong kwenye American idol maana niliamini hakuna mweusi anaweza kushinda lakini i was wrong ingawaje walioshinda walikuja kuwa big dissapointment.
Mkuu Ngabu kuhusu South hiyo Democrats wanaijua na siyo siri hata wazungu wa Democrats huwa wanashindwa sana huko south na sometimes hata kampeni hawaendi kupiga maana ni kujisumbua na ujue wana uwezo wa kushinda WH bila hata state moja ya South na imetokea mara nyingi tuu,anyway big up to Obama hata akishindwa amesaidia kuonyesha mtu mweusi can do it na hope atampelekesha mama mpaka mwisho.....basi hata VP jamani asipokuwa nominated itakuwa nzuri tuu.
 
..inaelekea Obama atashinda ticket ya Democrats.

..nimesikiliza CNN na nikashangaa jinsi wanavyomsagia Hillary. Inaelekea hawamtaki kabisa.

..sidhani kama Obama anaweza kusimama na mweupe toka Republican na akashinda.

..sidhani kama Obama anaweza kustahimili mashambulizi ya GOP,Conservatives, na Avenjelical Christians, wakati wa uchaguzi mkuu.

..mmeona jinsi John Edwards anavyojitahidi kumuondoa Hillary? He knows White America. Anajua wakibaki yeye na Obama, WEUPE wenzake watamheshimu na kumpa ticket ya Democrats.
 
wakuu dont underestmate this guy na dont compare him na kina Jesse jackson ni watu tofauti sana na historia/background zao ni tofauti sana,kwanza mjue Jesse alipoingia kwenye race tayari alikuwa na enemies kutokana na kujihusisha na zile civil rights movements,wasiwasi wangu ni rangi tuu maana siwaamini hawa wazungu ingawaje nilikuwa wrong kwenye American idol maana niliamini hakuna mweusi anaweza kushinda lakini i was wrong ingawaje walioshinda walikuja kuwa big dissapointment.
Mkuu Ngabu kuhusu South hiyo Democrats wanaijua na siyo siri hata wazungu wa Democrats huwa wanashindwa sana huko south na sometimes hata kampeni hawaendi kupiga maana ni kujisumbua na ujue wana uwezo wa kushinda WH bila hata state moja ya South na imetokea mara nyingi tuu,anyway big up to Obama hata akishindwa amesaidia kuonyesha mtu mweusi can do it na hope atampelekesha mama mpaka mwisho.....basi hata VP jamani asipokuwa nominated itakuwa nzuri tuu.

Ktk miaka 40 iliyopita nitajie mgombea uraisi mmoja wa Democratic aliyeshinda uraisi wa Marekani bila kushinda hata jimbo moja kusini. Nitajie mmoja tu.
 
..inaelekea Obama atashinda ticket ya Democrats...nimesikiliza CNN na nikashangaa jinsi wanavyomsagia Hillary. Inaelekea hawamtaki kabisa.

Mkuu Joka,

Heshima mbele, US ni Capitalist State, kwanza biashara halafu the rest of the story, katika huu uchaguzi mzima kuna one factor kuweza kuuza biashara za media, nayo ni kuwapiganisha Hillary na Obama,

Mwanzoni, ilikuwa ni bisahara nzuri kuwapiganisha Hillary na Giuliani, baadaye ikawa a Mormon Romney Vs Huckabee, sasa imekuwa Hillary Vs Obama, kumbuka ni hao hao CNN walio onyesha kipindi cha Obama for at least 2 Hours, wakimuita Osama, walipoambiwa baadaye what they did wakasema walikuwa wakikosea kwenye typing, kweli una amini hiyo?

CNN hawachagui rais wa US, na wala hawawakilishi mwananchi yoyote maana wangekuwa basi Kerry na Gore wangekuwa marais, polls za New Hampshire zinaonyesha ikiwa imebakia siku mbili tu, Hillary 37%, na Obama 25%, lakini CNN wanasema Obama is closing the gap! Huoni kuwa hii ni hadithi ya biashara?

When Iowa, talks, sio kweli kwamba the US listens, mara ya mwisho Democrat aliyeshinda Iowa, alikuwa Kerry 2004 lakini hakuweza kuwa rais, kabla yake alikuwa Jimmy Carter peke yake ndiye aliyeshinda urais mwaka 1976, my point ni kwamba tuwe objective katika hope kwamba huenda Obama atashinda, tungependa ashinde lakini sio on a false hope kutoka CNN ambao hawana any influence katika kuchagua rais wa US!
 
Field Marshal,

..kama nimekuelewa ujumbe wako ni kwamba it is not over yet.

..mimi kilichonishangaza ni jinsi kila mmoja[anchors,commentators,consultants..] ktk CNN anavyomtabiria "mauti" Mama Clinton.

..siyo kwamba hawampi nafasi tu, bali inaelekea pia HAWAMTAKI.

..hata Mzee Clinton ameliona hilo, na amelalamika.

..hisia zangu ni kwamba kuna kitu Mama Clinton amewatenda. si bure.

..ningependa Obama ashinde. sijui kama itatusaidia WAAFRIKA. nimemsikia mke wake akisema "Obama's father was not there, or he didnt have his father around."

..my reading ni kwamba ile safari ya Obama Kenya/Africa was to seek CLOSURE, and not to re-connect with his partenal heritage.

..Uraisi wa Marekani ni TAASISI. Waafrika tunajipa matumaini kwamba huenda Obama atakuwa kama Papa John Paul alivyokuwa kwa Poland.

..Hivi Obama akiwa Raisi ataweza kufanya yafuatayo:-

1.kusitisha mauaji ya Darfur.

2.Kumuondoa Mugabe na kusitisha vikwazo vya uchumi dhidi ya Zimbabwe.

3.Kuanzisha Marshal Plan for Africa.

..How will US policies towards Africa change with Obama's presidency?
 
Field Marshal,

..kama nimekuelewa ujumbe wako ni kwamba it is not over yet.

..mimi kilichonishangaza ni jinsi kila mmoja[anchors,commentators,consultants..] ktk CNN anavyomtabiria "mauti" Mama Clinton.

..siyo kwamba hawampi nafasi tu, bali inaelekea pia HAWAMTAKI.

..hisia zangu ni kwamba kuna kitu Mama Clinton amewatenda. si bure.

..ningependa Obama ashinde. sijui kama itatusaidia WAAFRIKA. nimemsikia mke wake akisema "Obama's father was not there, or he didnt have his father around."

..Uraisi wa Marekani ni TAASISI. Waafrika tunajipa matumaini kwamba huenda Obama atakuwa kama Papa John Paul alivyokuwa kwa Poland.

..Hivi Obama akiwa Raisi ataweza kufanya yafuatayo:-

1.kusitisha mauaji ya Darfur.

2.Kumuondoa Mugabe na kusitisha vikwazo vya uchumi dhidi ya Zimbabwe.

3.Kuanzisha Marshal Plan for Africa.

..How will US policies towards Africa change with Obama's presidency
?

Hapana. Obama akishinda uraisi atakuwa na wajibu wa kuitumikia Marekani ambayo na yenyewe ina matatizo kibao. Sidhani hata kwenye kampeni zake anaahidi kuifanyia hivi ama vile Afrika. Ahadi anazotoa ni kurudisha majeshi yake kutoka Iraq, Social security, medicare, na mengineyo. Sisi tuangalie ni jinsi gani tutavyojisaidia wenyewe badala ya ku-worry Obama atatusaidiaje.

Kuhusu Mugabe, ni Wazimbabwe wenyewe watakaomuondoa. Mugabe ni binadamu kama wengine na inawezekana kabisa kumuondoa kama nia ya kweli wanayo.

Hii mentality ya "if Obama wins" will he do this or that for us ni mbofu sana. Halafu tukisema Waafrika Ndivyo Tulivyo watu wanakuja juu.
 
TRUTH muda unao?

Are you planning on explaining how someone with mediocre grades as Obama has admitted to had can get into Harvard Law School? To me it seems like affirmative action played a part in his admission. Let's remember affirmative action is a direct consequence of the 1964 Civil Rights bill that Ron Paul correctly voted against its renewal. We can probably make a connection that if Obama had not gone to Harvard Law School he would not have got to where he is today. So he is an affirmative action presidential candidate not necessarily the best qualified.
 
Sidhani kama smartest ya candidate kama Ron Paul ina positive impact yeyote. Its not a matter of smartness, kama ingekuwa hivyo George W. Bush asingechaguliwa kuwa nominee wa GOP. I don't know how this guy made it through Yale and Harvard...labda kulikuwa na influence ya George Walker. Kwa GOP wengi wanataka candidate atakayekuwa mnoko..atakae restore conservative values..atakae kuwa mkali kuhusu mambo ya border..atakae lower taxes especially kwa makampuni. Mwenye ushawishi wa udini Christianiaty. Na ndio maana unaona Mike Huckabee amekuwa popular sana siku za karibuni.
Kwa upande wa Dems..they want a candidate who is a true liberal, who is going to clean up the mess in Washington from the War in Iraq to big corruptions kwa mfano...kwa makampuni ya mafuta (e.g., Halliburton), defense e.g., Black Water,.
Ron Paul hata awe smart namna gani pamoja na kuwa daktari lakini he is a LIBERTARIAN REPUBLICAN not a true conservative and for that he will never get anywhere near GOP nomination. However, ninampenda kwa sababu si mnafiki kama Mitt Romney ambae yupo kwenye kila issue. Romney will be a version of John Kerry kwa GOP kwa sababu ya ku FLIP FLOP
 
Are you planning on explaining how someone with mediocre grades as Obama has admitted to had can get into Harvard Law School? To me it seems like affirmative action played a part in his admission. Let's remember affirmative action is a direct consequence of the 1964 Civil Rights bill that Ron Paul correctly voted against its renewal. We can probably make a connection that if Obama had not gone to Harvard Law School he would not have got to where he is today. So he is an affirmative action presidential candidate not necessarily the best qualified.

...nasmell hate hapo..hata Bush was not smart he got into Yale because he was a legacy( His father and grandfather were Yale men)....you can call rich affirmative action.
 
...nasmell hate hapo..hata Bush was not smart he got into Yale because he was a legacy( His father and grandfather were Yale men)....you can call rich affirmative action.

Ktk miaka 40 iliyopita nitajie mgombea uraisi mmoja wa Democratic aliyeshinda uraisi wa Marekani bila kushinda hata jimbo moja kusini. Nitajie mmoja tu.
 
Nyani Ngabu said:
Hapana. Obama akishinda uraisi atakuwa na wajibu wa kuitumikia Marekani ambayo na yenyewe ina matatizo kibao. Sidhani hata kwenye kampeni zake anaahidi kuifanyia hivi ama vile Afrika.

Nyani Ngabu,

..haya bwana.

..hapa nilipo mke wangu aliposikia huu ushindi wa Iowa basi akaniambia tuongeze watoto.

..mimi mwenyewe nilishaanza hesabu za kuongeza mke mdogo.

..sasa wataalamu[Field Marshal,Koba,The truth] wangu hapa jambo forums mnaniambia ngoma bado mbichi.
 
Ktk miaka 40 iliyopita nitajie mgombea uraisi mmoja wa Democratic aliyeshinda uraisi wa Marekani bila kushinda hata jimbo moja kusini. Nitajie mmoja tu.

...imebidi nicheke tuu na jibu utapata lakini sio unalotaka,sasa ni hivi kumbuka Al Gore & Kelly hakuna hata mmojawao alishinda state kutoka south lakini wote walikuwa wanahitaji just one state of Ohio(ambako now is getting more liberal) to beat GW Bush and win the presidency,hapo inakuonyesha Democrats can afford to lose every southern states and still win the WH
 
Sijui kichekesho kiko wapi lakini ujweli wa mambo ni kwamba marais wa kutoka chama cha Democratic wa miaka ya hivi karibuni (Jimmy Carter na Bill Clinton) wote walishinda Arkansas, Georgia, Alabama, na majimbo mengine ya kusini. Ni stratergy mbaya kusema wanaweza ku-afford kushindwa kusini nzima na ndio maana wamekuwa wakishindwa. Al Gore hakuhitaji Florida kushinda uraisi. Kama hata angechukua Arkansas au Tennessee, it was a wrap for G.W. Yaani kama wakikusikiliza wewe wataendelea ku-lost tu.
 
Ngabu...who cares about racist south,kuweka pesa kule ni kupoteza muda tuu na resource,na ukizingatia this time woman/black ndio wanaweza kuwa nominee wa Democrats,hapo ndio balaa zaidi....siasa za south ni za kibaguzi sana ujue,bora Dem wamwage pesa zao na muda states kama Nevada,Arizona & Colorado labda huko wanaweza kutoboa maana spanish na immigrant from north wameanza kubadilisha mambo huko lakini Mississippi,Alabama,Wyoming,Lousiana etc sahau kabisa na usijaribu kama wewe ni Dem or kinda of Obama or Hillary
 
Hiyo ni recipe ya kushindwa kila chaguzi.
 
...nasmell hate hapo..hata Bush was not smart he got into Yale because he was a legacy( His father and grandfather were Yale men)....you can call rich affirmative action.

And look how bad Bush's presidency was. Do you want Americans to elect another under qualified affirmative action candidate such as Obama? God help us all!
 
And look how bad Bush's presidency was. Do you want Americans to elect another under qualified affirmative action candidate such as Obama? God help us all!

LOl bush pamoja na kuwa prez for 8 years bado haqualify kuwa president, Ron paul anajaribu tangu 88 sijui, huoni atumie busara zake na kukaa pembeni?
 
Hapana. Obama akishinda uraisi atakuwa na wajibu wa kuitumikia Marekani ambayo na yenyewe ina matatizo kibao. Sidhani hata kwenye kampeni zake anaahidi kuifanyia hivi ama vile Afrika. Ahadi anazotoa ni kurudisha majeshi yake kutoka Iraq, Social security, medicare, na mengineyo. Sisi tuangalie ni jinsi gani tutavyojisaidia wenyewe badala ya ku-worry Obama atatusaidiaje.....

Nakubaliana nawe kwa hayo, na kwa kuongezea tu nina uhakika kwa afrika itapata ile negative effect zaidi, kwani itabidi awe mwangalifu na ajilinde ili asionekana anasaidia au tetea huko kwao yaani Afrika. Halafu tena atakuwa ana kazi kubwa ya kujaribu ku convince umma wa marekani kuwa yeye (mtu mweusi) siyo mkabila au mrangi rangi! na anaiweza hiyo kazi.

Si mnaona hata hapa JF, JK akiteua mtu tu na akawa na jina la kiislamu, basi mayowe yanaanza JK mdini!, Akiteua mtu na akawa na ni wa Pwani au Mzaramo au Mkwere basi moja kwa moja anaitwa mkabila! Na kwa Obama itakuwa hivyo hivyo na kwa sababu yeye ni smart atajitahidi sana kuji distance na huko Afrika.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom