Urais wa ZZK 2015 Kupitia Chadema: Kwa nini Wanatetemeka!, Kuweweseka! na Kutishika?!.

Status
Not open for further replies.
Mpango huu ni miongoni mwa njama zinazoandaliwa kwa ajili ya Chama Tawala kuangamiza upinzani wa kisiasa nchini.

Mgombea binafsi wa kiti cha urais ama ubunge atakuwepo kwa mujibu wa Katiba Mpya ijayo. Zitto utashawishiwa kugombea nafasi mojawapo kati ya hizo mbili nje na Chama ulichopo sasa. Kisha utaahidiwa uwaziri wa fedha ama madini. Utategwa ujichagulie kati ya nafasi hizo. Lengo litakuwa ni kuhakikisha unajiengua CHADEMA ili kusababisha mgawanyiko katika idadi ya wapiga kura waliowaumini wa vyama vya upinzani, CHADEMA ikilengwa.

Nawe Zitto utashawishika kwenda huko, utagombea urais, utashindwa lkn utakuwa umefanikiwa kuleta mgawanyiko ktk suala zima la wapiga kura. Ila hutaachwa hivi hivi, utapewa ubunge wa kuteuliwa kama ilivyo kwa Mtu Makini Joseph Mbatia, kisha utaingizwa Serikalini kuchukua mojawapo ya hizo nafasi nilizokutajia hapo juu.

Sasa hilo litakuwa ndiyo ANGUKO lako la jumla katika siasa za Tanzania, nawe utafuata nyayo za Waridi Amani Kaborou.

Yawezekana hulijui hilo lkn laandaliwa na laja kwa ajili yako. Tafakari wewe ni kijana mwenye uwezo mkubwa wa kufikiti. FIKIRIA

Mimi tu kukuletea habari.
 
Yaani kama lile Limbulu silipendi mimi na ndo linawajaza wa mbulu wenzake chadema
 
i knew...only ben saanane and mchange would support hili bandiko!!!!huyu mtu pasco kweli mwandishi,manyuzi yake yanakuwaga marefu akiongelea point moja tu,.hawa walikuwaga mabingwa wa essay za history na gs enzi zile za high school..don't worry zitto is reading your posts,atakukumbuka kwenye ufalme wake atakapopewa uwaziri na ccm mwaka 2050
Stay Focused......!

the sustenance of our democracy is important. The can do spirit of intellectual Tanzanians well wishers must be harnessed. Parochial sectional interests must be dislodged. And we must work collectively for peace and stability of the party.Tukubali maoni na ushauri kwa kuwa objective.Alichoandika Pasco kina makosa gani?Ben Saanane anaingiaje tena hapo?
 
Mkuu, ugombea binafsi ni silaha ambayo ikitolewa galani leo basi moja kwa moja ujua hakuna kitu CCM katika ramani ya Tanzania. Chama kitakachoumizwa zaidi na silaha hiyo ni CCM na wala si CHADEMA.

Acha wajaribu hata kesho uone muziki wake kwa Magamba wenyewe kule kule.
 
Kwa upande wangu mimi sipingi kitendo cha huyu kijana kutangaza nia ya kugombea urais.Basi sasa awe na hekima akae kimya angoje vikao halali kumwidhinisha hapo baadaye muda utakapofika.lakini hiki kitendo cha kutangaza tangaza kila mara kinatia dosari ktk umakini wa huyu kijana.Tangu 2010 alipotangaza nia ya kugombea ilikuwa taarifa tosha lkn kitendo cha kila mara kutuangazia na pia kuungwa mkono na watu wengi wa ccm na vyama vingine inaonesha kuna ajenda ya siri ndani yake.Ni sawa na mtu anayeka kuposa anapokwenda kujitambulisha kwa wazazi wa mwanamke kwa mara ya kwanza ili kujulikana na kisha kurudi kila mara kujitambulisha kwa suala lilelile ni wazi kuwa hatimaye atakuchoka na kukudharau kwa kukuona ni mbabaishaji.Baba wa Taifa alituonya kumwogopa kama ukoma mtu anayekimbilia ikulu
 
Watoa mada wa JF yaani wewe unadhani sisi wanachi ni wajinga hatutakuwa na maamuzi yetu lini CCm tangu 1995 walishinda si ni usalama wa taifa umekuwa ukiwaweka maraisi na safari hii tumeapa tutakula sahani moja nao hatutawapa mapanya sisi uraisi kama anaenda naende who is zitto kikaragosi by the way
 
Hakuna habari ya kutetemeka,kuweweseka wala nini. Anayeweweseka ni mwandihsi mwenyewe. Mimi niseme tu inawezekana wengine wa kawa na chuki binafsi na ZZK lakini kiukweli jaamaa kwa sasa ashanunuliwa na magamba.

Hebu tujiulize tangu zoezi la M$C limeanza ni lini ZITTO KABWE amefanya MIKUTANO kamambe ya KUZUNGUKA nchini kama VIONGOZI wengine wa CHADEMA? Je ameshafanya hata mikutano mikubwa ya kutafuta WANACHAMA? Au kutaka kugombea uraisi ndo kunajenga chama!?


Sasa kama hali ndo hiyo ni kwanini tusiamini kuwa sasa ZZK ni mamluki?
Kwa mtazamo wangu nazani ZZK ni mtu MBINAFSI na MPEKEE.
Zaidi sana kwa sasa nia yake si kujenga chama bali ni kukivuruga CHAMA cha CHADEMA!!!

 
Wala isiwatie hofu. Hata hapa Marekani ambako demokrasia imeota mizizi, mgombea binafsi (third party) ni nadra sana kushinda kwenye uchaguzi wa rais, kwa sababu ili kushinda ni lazima uwe na nguvu ya chama nyuma yako. Mgombea binafsi anaweza kushinda katika ubunge lakini ni vigumu kushinda katika urais. Kitakachotokea, kama hivyo ndivyo itakavyokuwa, mgombea binafsi atasaidia tu kugawa kura. Ama kura za CCM au kura za upinzani. It is a two edged sword.
 
Pasco nimepata habari za kuaminika kuwa, mambo yakitulia CCM, Zitto atahamia huko muda si mrefu kuongeza nguvu kambi ya Lowassa na mpango umeandaliwa na Jk na namna ya kumpokea.

Ni Bora gamba ZZK utoke, CHEDEMA tumekuchoka...

Safari aliyoongozana na JK kwenda kuzika waziri Mkuu Ethiopia ndio mipango ilikofanyika au?
 
Mkuu, ugombea binafsi ni silaha ambayo ikitolewa galani leo basi moja kwa moja ujua hakuna kitu CCM katika ramani ya Tanzania. Chama kitakachoumizwa zaidi na silaha hiyo ni CCM na wala si CHADEMA.

Acha wajaribu hata kesho uone muziki wake kwa Magamba wenyewe kule kule.

Uwezo,
Matumizi murua ya kila silaha ni kwanza kuifahamu silaha yenyewe, kuwa na uelewa juu ya matumizi ya silaha, kuwa na uwezo wa kuishika silaha hiyo kwa ajili ya matumizi na kuwa na uzoefu juu ya matumizi ya silaha hiyo.

Kuna taasisi zimejipanga kuitumia silaha hiyo kama nilivyoielezea hapo juu. Muhimu ni adui pia kujipanga.
 
Pasco, vipi maendeleo ya mkono wako? hebu maumivu tu ama ilikuwa ni nini? pole tunakuombea upone mapema kaka, mtafute willy malecela bwana, mambo yake naona yamegoma, mshauri aje chadema ndipo anaweza kutimiza ndoto zake, ndg yangu kwa zitto sina comment, ila ujue hii mitandao itakudharaulisha mbele ya umma, be care full, watu hawa ni wasomi zaidi yako, master, phD za kutosha ziko humu, pasco ile degree yako ya sheria inapwaya humu, ukiwa na makala yako peleka mwananchi , si unajua poor feedback!
 
Sijajua utaratibu huu mpya lkn naona mods mnahamisha michango ya wanajf kutoka kwenye thread hii na kuipeleka kwenye thread nyingine ambayo kwa fani na maudhui havifanani kabisa.mmepeleka michango mingi ya thread hii kwenyee thread ya “zzk 2015 wanaweweseka”.

Ukweli ni kwamba hata kidogo michango ile haifiti kule mlikoipeleka. What is the hidden motive? siyo mata ya kwanza.
 
ZZK ni ndege wa rangi tofauti kwenye kundi la CHADEMA ya leo! Dini, Kanda, kabila vinahusika!

hivi kwanini tukichangia masuala ya msingi mnapenda kuingiza udini na ukabira wakati madhara yake ni makubwa sana kwenye udini tz hatujafikia uko ila kama kawaida yenu na wazee wenu mnazidi kupanda mbegu ya udini
 
Mdini kama mkuu wa kaya,mbinafsi hazungumzi maslah ya chama bali ni yeye kuingia ikulu,na kibaraka.
Akiingia ikulu watanzania tue tayar kuona machafuko ya kidini yakiendelea, na mafisad wakizidi kukumbatiwa. Itakua ni muendelezo tu wa haya tunayoyaona sasa.
 
Pasco
usitupotezee muda kanywe nae chai.
Ukiona mtu anakimbilia ikulu muogopeni kama ukoma (j.k. Nyerere, .....)
Mkuu Wembe Wenge, hakuna anaekimbilia Ikulu!. ZZK ametangaza tuu nia, watu wana weweseka!. kosa la ZZK ni kuwa mkweli!. Wako watu wanaitamani ikulu mpaka wanakosa usingizi, kwa vile hawatangaza nia, basi ndio mnaona its ok!.
Wengine wanasubiri waoteshwe, wengine wanasubiri kuvuka mto wakifika darajani!.
P.
 
pasco,kweli leo nimekushusha!nway,...hakuna wa kutetemeka wala kutishika coz cdm sio zzk,sawaeeh!...halafu kajiunge na habib mchange na wengineo,waambie mjaribu njia nyingine coz kupitia zzk imefeli..period!
 
Pasco, wewe ni mnafiki mkubwa! Chadema na wanachadema wamekukosea nini? Umepitia maoni juu ya Dr Slaa na Zitto hapa Jf nania anastahili kugombea matokeo yake wayaonaje? Wampenda Zitto, nenda kanywe naye chai. Gamba zee wewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom