New Force 2015
Member
- Oct 25, 2013
- 63
- 262
Fedha ,Vitisho na Propaganda zatawala Tuhuma za ubakaji mtoto wa miaka 14 zinazomhusu Prof. Kapuya.
Ndugu Watanzania, tumezoea kusikia mambo makubwa ya udhalilishaji, Unyanyasaji, Uteswaji na Ukandamizaji unaofanywa na watu walioshikilia madaraka, mambo haya hutia hasira sana Jamii na wakati mwingine jamii kujaribu kuchukua hatua mbalimbali za kisheria, mara nyingi matukio haya huvamiwa na wataalamu wa kupotosha wanaotumia Nguvu na fedha nyingi pamoja na vitisho kuhakikisha wanafanya watu wasahau tukio hilo na lisizungumziwe tena na hata lisifanyiwe kazi tena.
Ndugu zangu Watanzania, huu ni ugonjwa ambao tumeulea wenyewe na sasa umetufanya tuamini kwamba ukiwa na mamlaka au na Pesa nyingi hapa nchini kila utakalofanya wewe ni sahihi hata kama ni kosa la jinai.
wote tunafahamu kwamba hata makundi kama MAFIA yalianza baada ya wale wanaokuwa wamekabidhiwa madaraka kushindwa kuyaheshimu mamlaka hayo na kuwafanya wananchi wenye hasira kuanzisha makundi mbalimbali kupingana na mamlaka hizo ili angalau nao wapate haki zao za msingi.
Suala la Ubakaji lililoripotiwa wiki hii kumhusu Prof. Kapuya ni kati ya mambo mabaya kabisa ambayo hayapaswi kuishia juujuu na badala yake sheria inatakiwa kuchukua mkondo wake hatimaye haki itendeke.......
Maswali ya kujiuliza; ni kwanini kuwe na vitisho vingi kama kweli tuhuma hizi si za kweli? kwanini Kapuya asifungue Kesi kama kweli anasingiziwa?, kwanini Kapuya aseme kwamba Simu iliyotumika aliigawa miezi 6 iliyopita bila kumtaja aliyemgawia na ili huyo ndo akamatwe kwa sms za VITISHO?
kwanini maelezo ya Kapuya yameshindwa kuthibitisha kwamba hamjui huyo msichana? kwanini Jeshi la Polisi limeshindwa kukana kwamba huyo msichan na Kapuya walishafanya Maridhiano Oysterbay mwaka 2012 baada ya kumbaka mara ya 2?
kwanini viongozi waandamizi wa CCM waliotajwa kwenye tuhuma hiyo (Mwigullu,Makinda,Kinana, Katibu wa Bunge nk) wameshindwa kukana uhusika wao?
Kuna Mtu anajiita W.J. Malecela, anadai kuomba radhi kwa Kapuya na kueleza kwamba amegundua tuhuma hizo ni za uongo.. Swali, yeye anaomba radhi kupitia Jamii forums kama nani? Mbona kwenye post zake kabla ya kuomba radhi hakuna hata moja iliyokuwa inamhukumu Kapuya sasa anaomba radhi kwa niaba ya nani...
kama yeye hakuwahi kumhukumu kapuya kwenye mtandao, na tangu jana hadi sasa kashaandika post 89 kumtetea Kapuya ,kazi hiyo anaifanya kwa maslahi gani?
wapo wengine wengi wa aina ya malecela wanaojaribu kurudisha nyuma utafutaji haki wa mtoto aliyebakwa, ninachosema mimi ni kwamba suala hili ni la kisheria, sheria ichukue mkondo wake na sio propaganda..kama kweli kapuya hahusiki basi sheria hiyohiyo ndiyo itakayompa haki na sio vitisho anavyovitoa kwa wanaharakati wanaotaka haki itendeke kwenye tuhuma hizi.
mimi binafsi niko tayari kuhakikisha suala hili halizimiki bila kufuata mkondo wa kisheria..leo ni kwa huyu mtoto yatima kesho ni kwa mtoto wako....TAFAKARI...CHUKUA HATUA...