Updates: Mazishi ya Mama na safari yangu

Updates: Mazishi ya Mama na safari yangu

Umenikumbusha kisa kimoja 😊😊😊.

Miaka kama mitatu hiv na nusu imepita. Ofisi flan , niko kama manager, nasimamia watu 30+ kwenye kitengo changu,

Sasa kuna dogo alikuwa anafanya kaz yangu isiende. Kwanza kuna siku anaamua tu haiingii kazin, na had mm ndio nimpigie ndio atatoa sababu . Most ni excuse za uwongo..

Nikawa nambeba kiaina, ila akirud namwita nakaa nae chini namchamb kidogo then namruhusu aingie mzigon.
akipokea salary anaweza kukaa hata siku 3 hajaingia kazin.
Mlevi flan mbwa.

Kuna siku nikaambiwa hajaingia kama kawaida yake, nampigia simu kapokea ila nasikia yuko kwa gari. Namuuliza vipi sikuoni kituo chako cha kazi. Kasema sorry boss nimepata msiba na hapa ndio niko safarini kwenda kuzika Arusha.

Nikamwambia sawa. Ila nilishakuambiaga mara kadhaa kuwa ukiwa na ishu niage. Nijue naset vip watu wangu. Akajibu sawa nimekuelewa boss.

Nikakata simu nikasema nichat nae kwa sms ili kuweka ushahidi.
Nikamuuliza msiba ni nani amekufa.
Kasema Bibi yake, kafa lini akasema jana asubuh, anaitwa nani akaniambia jina la huyo bibi hadi ukoo. Nikamuuliza anazikwa lini akasema had wafike. Nikamuuliza ni mkristo. Kasema eeeh KKKT.

Basi Nikakausha. Baada ya siku 2 nikamtumia sms kuwa bibi anazikwa lini akasema kesho yake. Nikamuuliza tar flan. Kasema ndio.

😊😊😊😊.
Sasa baada ya kupata hizo info.
Ile siku anazikwa.
Nikampigia tena simu. Nikamrekodi.
nikamwambia nahisi unanidanganya.
Na leo ni siku ya 4 hauko kazin.
Sasa ili nikuamini kuwa unasema kweli.

Naomba fanya uwezalo nitumie kwa
Whatsapp picha ya mazishi.
Picha ya msalaba ili nione details (nikamtajia lile jina aliloniambia, Tar aliyozaliwa na tar anayozikwa.)
Na akishazikwa piga picha kaburi
Kama ukishindwa kufanya hivyo.
Usije ofisini tukutane kwa HR.

Hakutuma hicho nilichomuomba. Kesho yake Nikampigia HR na nikamwambia Ishu nzima na kuwa sio mara ya kwanza dogo anazingua. Na mm simuhitaji. Akirud nakuja nae tufanye kikao na ikibidi mumpeleke Idara nyingne.

HR kampigia kuwa anamuhitaj ofisin siku flan. Tukakaa kikao.
Na dogo tukamtema kazini.
yooooh
 
Pole sana na msiba na wabarikiwe waliokuchangia mpaka umefika huko LAKINI hukutakiwa tena kuweka namba hapo kwaajili ya msaada. Umefika kwenu komaa kwa namna yoyote ile upate nauli ya kurudi ukishindwa uzuri uko nyumbani utabaki mpaka utakapopata. sio kuomba tena ungenyamaza tu kama kuna mtu angewiwa kukusaidia tena basi angekusaidia bila wewe kuomba. HURUMA SIO MALEZI kikubwa wewe ni mzima wa afya na umeshazika tayari,unaweza kupambana. Kila la heri
Changia na wewe ubarikiwe
 
Mtoa mada watu wamejaa kwenye mfumo wakamue kwelikweli ukirudi Dar watoto watahitaji kula omba tena huwezi kukosa humu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom