Updates: Mazishi ya Mama na safari yangu

mimi nakushauri usiwahi kurudi mjini kaa kidogo angalia huko kama kuna fursa
 
Mkuu mm ntakutumia ila mpaka utume picha ulivyokuw unalia msiban
Umenikumbusha kisa kimoja 😊😊😊.

Miaka kama mitatu hiv na nusu imepita. Ofisi flan , niko kama manager, nasimamia watu 30+ kwenye kitengo changu,

Sasa kuna dogo alikuwa anafanya kaz yangu isiende. Kwanza kuna siku anaamua tu haiingii kazin, na had mm ndio nimpigie ndio atatoa sababu . Most ni excuse za uwongo..

Nikawa nambeba kiaina, ila akirud namwita nakaa nae chini namchamb kidogo then namruhusu aingie mzigon.
akipokea salary anaweza kukaa hata siku 3 hajaingia kazin.
Mlevi flan mbwa.

Kuna siku nikaambiwa hajaingia kama kawaida yake, nampigia simu kapokea ila nasikia yuko kwa gari. Namuuliza vipi sikuoni kituo chako cha kazi. Kasema sorry boss nimepata msiba na hapa ndio niko safarini kwenda kuzika Arusha.

Nikamwambia sawa. Ila nilishakuambiaga mara kadhaa kuwa ukiwa na ishu niage. Nijue naset vip watu wangu. Akajibu sawa nimekuelewa boss.

Nikakata simu nikasema nichat nae kwa sms ili kuweka ushahidi.
Nikamuuliza msiba ni nani amekufa.
Kasema Bibi yake, kafa lini akasema jana asubuh, anaitwa nani akaniambia jina la huyo bibi hadi ukoo. Nikamuuliza anazikwa lini akasema had wafike. Nikamuuliza ni mkristo. Kasema eeeh KKKT.

Basi Nikakausha. Baada ya siku 2 nikamtumia sms kuwa bibi anazikwa lini akasema kesho yake. Nikamuuliza tar flan. Kasema ndio.

😊😊😊😊.
Sasa baada ya kupata hizo info.
Ile siku anazikwa.
Nikampigia tena simu. Nikamrekodi.
nikamwambia nahisi unanidanganya.
Na leo ni siku ya 4 hauko kazin.
Sasa ili nikuamini kuwa unasema kweli.

Naomba fanya uwezalo nitumie kwa
Whatsapp picha ya mazishi.
Picha ya msalaba ili nione details (nikamtajia lile jina aliloniambia, Tar aliyozaliwa na tar anayozikwa.)
Na akishazikwa piga picha kaburi.

Kama ukishindwa kufanya hivyo.
Usije ofisini tukutane kwa HR.

Hakutuma hicho nilichomuomba. Kesho yake Nikampigia HR na nikamwambia Ishu nzima na kuwa sio mara ya kwanza dogo anazingua. Na mm simuhitaji. Akirud nakuja nae tufanye kikao na ikibidi mumpeleke Idara nyingne.

HR kampigia kuwa anamuhitaj ofisin siku flan. Tukakaa kikao.
Na dogo tukamtema kazini.
 
Mtu kafiwa na mama anawezaje kupiga mpaka picha kutuma mitandaoni? Hiv kufiwa na mama mnakuchukuliaje wazee?.
 
Ninachoweza kusema Pole sana, Mungu awatunze katika yote, maumivu ya msiba hayaelezekeki.

Katika Umri wangu huu, nimezika Baba, mama, Dada na mdogo wetu wa, mwisho, ni maukivu ambayo nayaebeba moyoni mwangu na sijui kama kuna siku yataisha na kuwa, maisha kuwa kawaida, tena.

Poleni sana
Poleni sana mkuu ase. Mungu akutie nguvu maana maumivu yako hayaelezeki kabisa.
Sijawahi kufiwa na mtu wa karibu zaidi ya msiba wa bibi mzaa baba ambaye alifariki 2012 ,kiukweli nililia sana pale kaburini hata picha ya mwisho ya kumbukumbu macho yana mekundu yana machozi kabisa. Mwingine ni bibi mzaa mama 2017 ambao nilipewa taarifa niliporudi nyumbani kutoka shule kwamba tayari na kuzika walishazikaga miezi 2 nyuma Niliumia sana.
Mwingine ni rafiki yangu niliyesoma naye advanced tumelala kitanda kimoja tumeishi pamoja na chuo pia tulikaa room 1 miezi 4 japo course tofauti ,yeye alipata ajali ya gari na mimi nikapata taarifa nikiwa njiani kwenye basi kuelekea Mbeya safari ilikuwa nzito sana ilibaki kidogo nianze kushusha machozi kwenye gari nikiwa nimekaa. Siblings wote dada na kaka wapo na marafiki wa karibu ,pamoja na baba na mama.
Huwa ninajikaza sana ila nimesoma reply yako ,viatu vyako siwezi kuvivaa mkuu 🙌🏾.
 
Kwanza nianze kwa kutoa shukrani nyingi mno kwa jamii forum na watu wake mmeonesha kuwa ni jamii kweli kwa kuonesha kuguswa na matatizo ya watu wengine hata kama hamfahamiani japo wapo wengi wenye maneno ya karaha lakini wote ni jamii watu kama hawa hawakosagi

katika kitu nimejifunza watu wema bado wapo na wanazidi kutupa funzo ya kuwa wamoja hasa pale mtu anapopata matatizo

Huu si uzi rasmi wa shukrani zangu kwenu bali ni kuwapa updates ya kile kinacho endelea kwasababu niliko internet ni ya shida nitakuja na uzi rasmi siku nyingine.

Nilifanikiwa kusafiri na nilifika salama na kila kitu kilienda vizuri japo changamoto hazikosi msiba tushamaliza ila tumebaki ndugu kuangalia maisha yatakuwaje hasa kwa wadogo zetu na mambo mengine pia na mimi jinsi ya kurudi dar kutafuta japo tunachotafuta hakitoshi hata kutufuta jasho tunapopata matatizo kama mnavo jua msiba huenda na kila kitu kama kuna yeyote mwenye kutaka kutoa chochote no ni 0703644801 tigopesa
Mwisho niseme asanteni kwa kila kitu hapa nimeweka picha japo nilikuwa sitaki kuziweka ila ni kwa wale wenye mashaka wanao hisi labda kila mtu hupenda matatizo nimeweka picha tiketi niliyotumia kwenda pia na picha ya mazingira ya msiba

Nb: Mods naomba muunganishe.uzi huu na ule ili watu wapate updates 🙏🏻
Poleni sana mkuu ,mitihani ya maisha hii ase Mungu awatie nguvu mkuu
 
Pole sana kwa msiba ila hii ni man to man talk acha tabia ya kuomba omba mtoto wa kiume ulipata nauli ya kufika huko inatosha pambana na ww sasa huko si home ... Mwanaume inatakiwa ujue kukaza na kupambana
Huyu hatakiwi hata kurudi Dar.

Kama ni lazima atoke huko home bora aishie Mwanza au hata Kahama kuna Wahangaza na Wanyambo wenzie mamia wanaendesha boda.

Mpaka asafirishwe Kama parcel anarudi Dar kufanyaje?
 
Mtu kafiwa na mama anawezaje kupiga mpaka picha kutuma mitandaoni? Hiv kufiwa na mama mnakuchukuliaje wazee?.

sijasema yeye atume picha. Nimetoa kisa tu cha kazini.
Na nilikuwa boss wake na hajaniaga wakat anaenda msiban. Kwahiyo nilikuwa na haki kuomba uthibitisho.

Ila tulikuja gundua dogo hakwenda Arusha wala nini😊😊😊 alikuwa mjin hapa hapa. Alikuwa na mwana wake mmoja kapiga mshindo . Kwahiyo walikuwa wanazunguka tu na gar na kula kadamsee ya kutosha.

Ila ilimgharimu na kaz yake.
 
Wala sio utabiri, ni kitu kilikua wazi akienda ni lazima arudi, kikubwa wameumbuka wote waliomtilia mashaka na kumdhihaki, atachangiwa tena na kurudi kwenye mapambano yake this time atapata na ajira ya kudumu
Amen aisee
 
Ishi humu Dogo , niko vibaya
1755.jpg
 
Huyu hatakiwi hata kurudi Dar.

Kama ni lazima atoke huko home bora aishie Mwanza au hata Kahama kuna Wahangaza na Wanyambo wenzie mamia wanaendesha boda.

Mpaka asafirishwe Kama parcel anarudi Dar kufanyaje?
Kwanza huko sasa hivi watu wanalima akalime kibarua .. Kuna kina sisi aisee kuomba omba hatuwezi aisee ni bora nikabebe zege au kulima kibarua nipate changu hata kma nimefiwa ama naputia ugumu wowte
 
Kwanza nianze kwa kutoa shukrani nyingi mno kwa jamii forum na watu wake mmeonesha kuwa ni jamii kweli kwa kuonesha kuguswa na matatizo ya watu wengine hata kama hamfahamiani japo wapo wengi wenye maneno ya karaha lakini wote ni jamii watu kama hawa hawakosagi

katika kitu nimejifunza watu wema bado wapo na wanazidi kutupa funzo ya kuwa wamoja hasa pale mtu anapopata matatizo

Huu si uzi rasmi wa shukrani zangu kwenu bali ni kuwapa updates ya kile kinacho endelea kwasababu niliko internet ni ya shida nitakuja na uzi rasmi siku nyingine.

Nilifanikiwa kusafiri na nilifika salama na kila kitu kilienda vizuri japo changamoto hazikosi msiba tushamaliza ila tumebaki ndugu kuangalia maisha yatakuwaje hasa kwa wadogo zetu na mambo mengine pia na mimi jinsi ya kurudi dar kutafuta japo tunachotafuta hakitoshi hata kutufuta jasho tunapopata matatizo kama mnavo jua msiba huenda na kila kitu kama kuna yeyote mwenye kutaka kutoa chochote no ni 0703644801 tigopesa
Mwisho niseme asanteni kwa kila kitu hapa nimeweka picha japo nilikuwa sitaki kuziweka ila ni kwa wale wenye mashaka wanao hisi labda kila mtu hupenda matatizo nimeweka picha tiketi niliyotumia kwenda pia na picha ya mazingira ya msiba

Nb: Mods naomba muunganishe.uzi huu na ule ili watu wapate updates 🙏🏻
Pole sana na msiba na wabarikiwe waliokuchangia mpaka umefika huko LAKINI hukutakiwa tena kuweka namba hapo kwaajili ya msaada. Umefika kwenu komaa kwa namna yoyote ile upate nauli ya kurudi ukishindwa uzuri uko nyumbani utabaki mpaka utakapopata. sio kuomba tena ungenyamaza tu kama kuna mtu angewiwa kukusaidia tena basi angekusaidia bila wewe kuomba. HURUMA SIO MALEZI kikubwa wewe ni mzima wa afya na umeshazika tayari,unaweza kupambana. Kila la heri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom