fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 6,108
- 8,128
Leo ni Mothers Day.Nakushukuru sana mama yangu,japo haupo duniani,sitakusahau kwa mema yako.Japo hukusoma japo darasa moja,kila nilipotoka shule ulikuwa ukichukua madaftari yangu kukagua tiki na kosa,na ulikuwa anahesabu tiki ni ngapi na kosa ngapi,na baba aliporudi jioni ulimwambia kama nimekosa nyingi au nimepata nyingi.Yote niliyofanikiwa ni kwa ajili yako.Mungu akupe mapumziko ya milele