UPDATE: Vifo vya Ajali Ngaramtoni vyafikia 25

UPDATE: Vifo vya Ajali Ngaramtoni vyafikia 25

Japokuwa sijaliona vizuri kwa mbele lakini nadhani hilo Lori ni Mack Bulldog old model kama hili na sio Scania

old-american-mack-truck-MYMAYR.jpg

Picha:Kwa Hisani ya Google/alamy
 
1. Nchi haitakiwi kuwa na udereva na madereva wa kuunga-unga
2. Kama ulipata mafunzo vizuri na ukafuzu, wakati wa ajali hutakuwa umesahau yale uliyofundishwa hivyo hutakuwa na sababu ya kukumbuka
#1. Nakubaliana na wewe 100%
#2. Hapo kuna mashaka kwani Ajali sio huwa inapangwa. Hutokea ghafla. Ni katika hali hiyo utashangaa dereva au hata mwenda kwa miguu anafanya kitu ambacho katika hali ya kawaida asingefanya.
NB: Ukizingatia pia kwamba sio madereva wote wapo sawa kiafya e.g. msongo wa mawazo, sukari n.k. au dereva anaweza akapuuzia hali ya kutokujisikia vizuri au uchovu akapitiwa na usingizi akaendelea na safari n.k. vitu ambavyo unaweza kusema kuna ka-uzembe fulani umetokea.
 
Mitaala yetu (kama ni mTanzania) ya udereva inafundisha hayo? Madereva wenyewe wana regular courses kuwafundisha na kuwaanda kisaikolojia how to minimize casualties during accidents. Dereva aliyeandaliwa vizuri hu-focus kupunguza vifo na majeruhi kwenye ajali. Hawa wenzetu na sisi hujiangalia wao tu!
Kwa hiyo wewe ungejiua kwa kwenda mtaroni?
 
Sijawahi kuona dereva ku****a kama huyo

Lori limekata breki toka kilima moto more than 3 kms to kibaoni ( bypass) kuanzia hiyo kilima moto mpaka habari maalum radio kuna uwazi mkubwa mno angeweza kabisa kuepusha haya tunayoyaongea sasa .Kakomaza fuvu kwamba atalihimili mpaka anafika kwenye population kubwa ya watu
Wewe usijitoe fahamu, lishatokea tayari
 
Habari wadau

Nipeni muda kidogo nitawajuza uharibifu ni wa kiwango gani lakini ukweli ni kwamba hali ni mbaya sana, watu wengi wamefariki.

Kwa wasiojua Ngaramtoni ni Arusha, Nairobi Road.

Kwa kifupi ni kwamba imeua wazungu wengi sana. Walikuwa kwenye Coaster pamoja na Raia na waendeshaji wa hiyo Truck pia.

=============

Watu 15 wameripotiwa kufariki dunia katika ajali iliyohusisha Lori la Mizigo (Semi Trailer) na magari madogo matatu iliyotokea katika eneo la By Pass Ngaramtoni, Wilayani Arumeru ambapo chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

Kwa mujibu wa taarifa za mashuhuda, Lori hilo aina ya Scania lenye namba za Usajili ZF 6778 lilikuwa likionesha ishara Taa za Hatari likiwa katika mwendo mkali na baadaye kuyagonga magari matatu ambayo ni Basi dogo la Abiria (Hiace), Basi la Shule ya New Vision lililokuwa na Watumishi wa Shule na Gari lingine dogo.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP, Justine Masejo, amethibitisha taarifa hiyo na kuwataka Wananchi kufika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru kutambua Miili ya waliofariki katika ajali hiyo.
Mbna mmechelewa kuileta tumekutana nayo leo njiani wakati narud dar
 
Back
Top Bottom