UPDATE: Vifo vya Ajali Ngaramtoni vyafikia 25

UPDATE: Vifo vya Ajali Ngaramtoni vyafikia 25

Na kwa Sheria za Tanzania huyo Dreva kaua watu,lakini kisheria hiyo inaitwa MINOR OFFENCE. Kama kapona atapelekwa tu Mahakamani,atapigwa Faini na Leseni yake kufungiwa basi ataendelea kula Bata mtaani saaafi.
 
Pole kwa wafiwa wote pole kwa wakazi wa jiji la Arusha na pole kwa Tanzania kwa ujumla, Mungu awape faraja katika nyakati hii ngumu yenye majonzi kwa kuwapoteza ndugu zetu.
 
Mitaala yetu (kama ni mTanzania) ya udereva inafundisha hayo? Madereva wenyewe wana regular courses kuwafundisha na kuwaanda kisaikolojia how to minimize casualties during accidents. Dereva aliyeandaliwa vizuri hu-focus kupunguza vifo na majeruhi kwenye ajali. Hawa wenzetu na sisi hujiangalia wao tu!
Namba za usajili ZF
 
watu huwa wanapanick sababu huwa wako kwenye mwendo usio salama.

ni sawa na kuona mtu anakatisha ghafla mbele,kama uko speed sana lazima urukie staring na kuuma meno.
Mimi ilinitokea nikitoka Usevya nilikiwa na tani arobaini pale Sitalike Mtoni lakini nilildhibiti hata Nzi hakujeruhiwa mimi ajali zote huwa naletewa na Walevi.
 
Wacha ujinga wako kuwa binadamu hata kwa muda.Kuna wengi tumepoteza ndugu zetu kwenye hii ajali.Sio kila kitu ni siasa.
Kwenye maisha yako karibu kila kitu ni siasa. Hii ajali ina uhusiano na siasa. Siasa ndiyo inaongoza nchi. Viongozi wasipokuwa makini na kuruhusu magari mabovu na uendeshaji mbovu barabarani watu wakifa huoni hapo kuna siasa? Nimesikia watu wanalalamika kuwa kuna vijana wanakimbilia kupekua maiti na majeruhi mfukoni. Hili kwa mtu mwenye akili siyo jambo la kushangaza na linahusiana moja kwa moja na siasa.
 
Tanzania yenyewe ina malori mabovu mengi sana. Tatizo huwa tunakumbuka wakati wa ajali zikipita siku mbili hali inarudi ile ile. Watu wameshasahu.
Lakini sisi tuliacha kutumia haya Malori aina ya Mack siku nyingi haya yalikuwa yakitembea enzi zile za FIAT lakini siku hizi FIAT zimebakia kwenye Town Trip tu.

Malori mengi mabovu yameachwa yafanye kazi ya kutoa Mizigo Bandarini hadi Store lakini huwezi kulipeleka safari lakini hili la Wakenya limetoka Nairobi.
 
Acha lawama zisizo na maana, hiyo si ajali ya makusudi na mashuhuda wamesema wameliona gari likiwasha hazard likionesha dharura
Wewe ni mpumbavu kama wapumbavu wengine

Gari imefeli breki zaidi ya kilomita 3 nyuma ambapo kulikuwa na advantage kubwa ya kuokoa maisha ya watu, kwanini ni mpumbavu huyu dereva ?!!!

Kwa watu wanaoifahamu Arusha ni kwamba kuanzia Lengi Jave,Kilima Moto ,Radio mpaka shule ya Turkish Maarif Ngaramtoni ni maeneo ambayo yapo wazi sana hakuna msongamano wa nyumba na ni tambarare kwa sehemu kubwa pia eneo hilo kuna mashamba makubwa sana ya serikali yana extend more than 2 kms

Sasa alishindwa nini kulielekeza hilo lori kwenye hayo mashamba?!!

Akili ya kupiga simu kuwa taarifu watu waoliko mbele ya safari wakae pembeni waliipata wapi lkn ya kulitoa gari barabarani hawakuwa nayo!!!

Iweje wapate muda wa kuwaalert watu watoke nje ya barabara kwa zaidi ya km 3 mpk koo zinawakauka sauti haitoki tena

Tatu jeshi la polisi limefanya uzembe sana toka Namanga gari haina escort ya aina yeyote ile yaani inatembea kama gari ya kawaida tu

Matokeo yake imeua watoto wadogo wasiokuwa na hatia ,imeua wakorea wafadhili wa shule ya New Vision,imeua Watanzania wote waliokuwa kwenye hiace ya abiria
 
Back
Top Bottom