UPDATE: Vifo vya Ajali Ngaramtoni vyafikia 25

Semahengere

JF-Expert Member
Nov 29, 2020
1,186
1,955
Habari wadau

Nipeni muda kidogo nitawajuza uharibifu ni wa kiwango gani lakini ukweli ni kwamba hali ni mbaya sana, watu wengi wamefariki.

Kwa wasiojua Ngaramtoni ni Arusha, Nairobi Road.

Kwa kifupi ni kwamba imeua wazungu wengi sana. Walikuwa kwenye Coaster pamoja na Raia na waendeshaji wa hiyo Truck pia.

=============

Watu 15 wameripotiwa kufariki dunia katika ajali iliyohusisha Lori la Mizigo (Semi Trailer) na magari madogo matatu iliyotokea katika eneo la By Pass Ngaramtoni, Wilayani Arumeru ambapo chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

Kwa mujibu wa taarifa za mashuhuda, Lori hilo aina ya Scania lenye namba za Usajili ZF 6778 lilikuwa likionesha ishara Taa za Hatari likiwa katika mwendo mkali na baadaye kuyagonga magari matatu ambayo ni Basi dogo la Abiria (Hiace), Basi la Shule ya New Vision lililokuwa na Watumishi wa Shule na Gari lingine dogo.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP, Justine Masejo, amethibitisha taarifa hiyo na kuwataka Wananchi kufika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru kutambua Miili ya waliofariki katika ajali hiyo.

...............

UPDATE:

ARUSHA: Idadi ya Vifo kutokana na ajali iliyotokea Februari 24 eneo la Ngaramtoni na kuhusisha Lori na magari mengine madogo Matatu imefikia 25 huku wengine 21 wakijeruhiwa

photo_2024-02-24_21-00-06.jpg

photo_2024-02-24_20-58-02.jpg

photo_2024-02-24_21-00-17.jpg
 
Back
Top Bottom