Update: Mashtaka dhidi ya makampuni manne ya simu

Nishasikia kikao basi mchezo kushney....

Hao TCRA wenyewe wanajua hili na walaji wameshalalamika sana lkn wanajifanya hawalioni, hivi hapo umeitwa itaoenyezwa rupia hapo huku TCRA wakiwa ndio wapatanishi na baada ya kupewa kipande chako utakua kimya hatutakusikia tena,na Jf utapotea kabisa
 
Bravooo Arawa usiangalie nyuma songa mbele sisi tupo nyuma yako wanao kutisha ni waoga wa fikra mbadala na ni wahujumu haki za wananchi Mungu atakulinda Haki huinua Taifa
UPDATE MASHTAKA DHIDI YA MAKAMPUNI MANNE YA SIMU.

Bashir Yakub, WAKILI
0714047241
.

Niliwaahidi kwamba nitakuwa nikiwaeleza kila tukio kuhusu mchakato wa kuyashitaki makampuni ya simu kwa unyonyaji.

Mnakumbuka kuhusu yale mambo yetu matano, vifurushi kutokuwa na muda wa kuexpire,ruhusa ya kuhamishiana vifurushi, kutochanganya vifurushi na muda wa kawaida wa maongezi bila ruhusa ya mtumiaji, vifurushi vya watu kuisha wakati mtu hajatumia au ametumia kidogo, na utaratibu wa kutoa taarifa kifurushi kinapokaribia kuisha na si kinapoisha.

Muda wa siku thelathini niliowapa haujaisha ukiisha nitawaambia.

Aidha, niliitwa na ndugu wa TCRA kitengo cha walaji. Nilifanya nao majadiliano kuhusu mambo haya na kuwaeleza nia yangu ya kuhakikisha Mtanzania analindwa. Nimeelewana nao vizuri.

Zaidi, wanaandaa kikao ambacho kitakuwa kati yangu, TCRA kitengo cha walaji, na makampuni yote ya simu. Mimi nilikusudia kuyashitaki makampuni manne(the big 4) lakini wao wamependekeza kikao kijumuishe wote. Ni jambo zuri na nimelipokea.

Na nimewaeleza kuwa hatua yoyote ambayo inalenga kuondoa unyonyaji wa aina hii na usumbufu mwingine wowote wanaoupata Watanzania wakati wakitumia simu, ninaupokea kwa mikono miwili. So far, kikao kinaweza kuandaliwa wiki ijayo ili kuona tunafikia wapi.

Zaidi, leo nimepata taarifa ambazo sijathibitisha kuwa Airtel wamefanya mabadiliko kwenye utumiaji wa data ambapo muda wa kifurushi cha data ukiisha hawaunganishi tena moja kwa moja na salio, bali sasa wameweka chaguo(option) ambapo wana kuuliza ikiwa unataka kuendelea kutumia muda wa kawaida au ungetaka kujiunga upya. Mnaotumia Airtel angalieni hili likoje.

Hata hivyo, Airtel kama wamefanya hivyo nawaambia haitoshi. Ni LAZIMA watekeleze na hayo mengine. Lakini pia ni LAZIMA watoe taarifa ya masaa 72 kabla ya mabadiliko yoyote kama Kanuni ya 5(5) ya Kanuni za Kielektroniki na Mawasiliano ya Posta GN No.61/2018 kuhusu kumlinda mlaji inavyotaka.

Wasifanye mabadiliko kwa kujifichaficha hii nchi sio yao, mtumiaji ana haki ya kujulishwa mabadiliko.

Pia, kwa wale mnaonipigia simu kunitisha nitumie jukwaa hili kuwaambia kwamba nitafurahi sana, tena sana, kufia kwenye vita hii kuliko kufia sehemu nyingine yoyote. Mwanaume kamili hafi kwa malaria bali hufia mambo kama haya.

Mwisho, niwashukuru nyinyi Watanzania kwa namna mlivyopokea jambo hili. Sijawahi kuona jambo ambalo Watanzania wote wanaunga mkono kama ilivyo kwa hili. Hii inadihihirisha ni kwa namna gani mlikuwa mmechoka.

Niishie hapa, nitawapa taarifa za kikao cha wiki ijayo.

Pia Soma
 
Komaa mzee, maana kuna malalamiko mengi ya watu kukatwa pesa zao bila kutumia na hata vifurushi kuisha bila kutarajia. Kama TCRA wameshindwa kazi ya kuthibiti haya makampuni ya simu kuwaibia wateja, ni bora sasa watu kama nyie mpewe hiyo kazi
 
Kumbe inawezekana aisee, endelea kukomaa naona mahakama ya Kenya tayari imeweka precedent nzuri
#MITANDAONI Baada ya
@SafaricomPLC
ya Kenya kuondoa "ukomo wa vifurushi" vya muda wa maongezi na intaneti kwa wateja wake, naibu waziri wa Mawasiliano, Atashasta Nditiye ameelezea msimamo wa Serikali kuhusu vifurushi. Bashir Yakub
 
Bundles ni bidhaa kama chips mayai ambapo unaponunua tu kanuni za mkataba zina apply.

Uwezi kwenda kununua zege usipomaliza ukamfuata muhudumu akurudishie chenji kisa umeshiba kati kati it doesn’t work that way.

Hivi vyuo vyetu avifundishi masuala ya contract law
Hapo umejiona umeongea point kabisa.
 
Narudia tena kusema, kugusa makampuni ya simu ni kugusa maslahi ya moja ya chanzo kikuu cha mapato cha serikali...

Terms zozote zitazofikiwa kama muafaka bado zitaegemea kwa makampuni ya simu
Na haohao wakubwa wataguswa moja kwa moja.

Hawatakubali.

Hii vita ni kubwa sana. Inatakiwa wanasheria nguli wahusishwe moja kwa moja.
 
Hivi mnalazimishwa kujiunga vifurushi? Mbona haya ni masuala yaliyo wazi sana kibiashara? Vifurushi ni mkataba wa hiari wenye vigezo na masharti yake unayoyakubali kuyazingatia!!!B
Hivyo vimekuwa ni mahitaji muhimu/ msingi (basic needs) katika dunia ya sasa. Hivyo huwezi amua kuweka bei kadiri unavyojisikia. Ndio maana zinawekewa hadi mamlaka ili kulinda na maslahi ya walaji.
 
Hivi mnalazimishwa kujiunga vifurushi? Mbona haya ni masuala yaliyo wazi sana kibiashara? Vifurushi ni mkataba wa hiari wenye vigezo na masharti yake unayoyakubali kuyazingatia!!!B
Tatizo hujaelewa maada inahusu nini,narukia tu ili mradi wewe ni mtumiaji wa simu,nenda mwanzo kasome mtoa maada anakusudia nini?
 
Biashara ya telco kwa vifurushi ni ya muda.. kwa jinsi gharama zinavyo shuka tutarudi kwenye Pay As You Go . Kwa hiyo kesi yako haina mashiko kabisa utapoteza muda wako.

Kwa kasi ya technolgy na urahisi wa mambo kutakua na baishara za aina mbili.

1. Wavivu kununua vocha wataenda kwenye post paid

2. Wakwangua vocha watapiga on demand ( Pay as you go).

Vifurushi tutawachia supermarket.
Zero
 
Bundles ni bidhaa kama chips mayai ambapo unaponunua tu kanuni za mkataba zina apply.

Uwezi kwenda kununua zege usipomaliza ukamfuata muhudumu akurudishie chenji kisa umeshiba kati kati it doesn’t work that way.

Hivi vyuo vyetu avifundishi masuala ya contract law
Umesoma contract law umemaliza, hukutaka kujua kuna sheria zingine za mawasiliano...

Mfano. Ukiwapigia wana kupa alert kuwa simu yako ita rekodiwa, kwa maana kumrekod mtu bila hidhini yake ni kosa...
 
We jamaa ni kiazi. Huwezi kuniuzia chipsi unipangie muda wa kula. Kwamba nisipokula mpaka saa fulani unaninyang'anya sahani.
Bundles ni bidhaa kama chips mayai ambapo unaponunua tu kanuni za mkataba zina apply.

Uwezi kwenda kununua zege usipomaliza ukamfuata muhudumu akurudishie chenji kisa umeshiba kati kati it doesn’t work that way.

Hivi vyuo vyetu avifundishi masuala ya contract law
 
Pambana mkuu na Mungu akuajaalie maana haya makampuni ya mitandao ni janga mfano Tigo ile saizi yako huwezi angalia hata salio la kifurushi chako ni mwendo wa kukalili muda uliojiunga na siku
 
Angalizo mkuu, pesa haijawahi kushindwa jambo kwa binadamu anaepumua, angalia usije ukatusaliti kwa kupokea mlungula wa maana na kuyoyoma kusikojulikana.
Kupitia hili jambo naamini utakutana na vitisho kama vilivyoanza theni ukikomaa utakutana na mlungula wa haja kitu ambacho naamini kukikwepa inahitaji moyo wa pekee maana hata yuda eskarioti ilimshinda.
Sisi Watanzania tupo nyuma yako na tutakukumbuka daima kama utalifanikisha jambo hili muhimu linalotunyonya uchumi wetu mifukoni na kuhamishia kwa wezi/wahuni wachache.
 
Umesoma contract law umemaliza, hukutaka kujua kuna sheria zingine za mawasiliano...

Mfano. Ukiwapigia wana kupa alert kuwa simu yako ita rekodiwa, kwa maana kumrekod mtu bila hidhini yake ni kosa...
Rejea post #82 utaona nimeeleza kanuni za terms za mkataba zina apply kama offer ilivyokuja isipokuwa pale ambapo kuna sheria inasema matakwa fulani lazima yazingatiwe.

Halafu humu hoja ni mkataba wa vifurushi sio kuingiliwa kwa mawasiliano hilo sasa ni swala la katiba na mambo ya faragha za mtu.
 
Back
Top Bottom