Makampuni ya gas toeni elimu ya usalama kwa wateja

Makampuni ya gas toeni elimu ya usalama kwa wateja

Nevergive up

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2024
Posts
600
Reaction score
944
wakuu ningependa kutoa ushauri juu ya makampuni ya gas hapa nchini. Msikimbilie kuuza na kupata faida tu pasipo kumfikilia yule mtumiaji kama ana elimu ya kutosha ya kiusalama.

Muwe mna kawaida ya kutembea mtaani kutoa elimu namna ya kuzuia majanga yatokanayo na gas ya kupikia.

Mfano unakuta mtumiaji wa gas ameona gas yake inavuja na haitaki kufunga na gas inatoka na hajui nini chakufanya zaidi ya kuiangalia tu huku inavuja hii ni hatari sana.

Hivyo muwe na kawaida kwa mwezi angalau mnaingia mtaani kutoa elimu juu ya gas na namna ya kuzuia majanga endapo gas inavuja .
 
Back
Top Bottom