Update: Mashtaka dhidi ya makampuni manne ya simu

Nakutakia kila LA heri mkuu ila usisahau watu wasiojulikana kama wapo na wataanza kukufuatilia hivyo kumbuka kusali au dua kwa wingi huku na sisi tunaendelea kukuombea kwa Mungu awe nawe daima.Ubebari ni unyama wahenga walisema miaka iliyopita.
 
Huyu mwanasheria Yuko vizuri kusimama na public kuitetetea mi chadema na ACT imekenua meno tu kazi kuongelea vitu hewa tu visivyosaidia wananchi walio wengi afadhali wakili umesimama kutetea wananchi

nimefurahi michadema na mi ACT mingi imekatwa ugombea serikali za mitaa they are hopeless hawana agenda nzuri Kama za huyu wakili za kutetea wananchi
Ukiwa unajinasibu kua mtu wa dini halafu unachukia ndugu yako huna tofauti na mchawi...kweli huko mbinguni tutakuta wateule wachche sana
 
Wasiwasi wangu Ni kwamba watakupa mpunga usiopungua billion moja na dalali atakuwa TCRA..na wewe utachukua mpunga na kutekeleza wanyonge
 
Kushinda hiyo kesi ni ngumu maana huo wizi unaofanywa na hayo makampuni ya simu kwa kiasi kikubwa unamfaidisha pia Zakayo kwenye kukusanya kodi. Kwa hiyo Kaisari na tamaa yake ya kutunisha mfuko hawezi kuwa tayari kupoteza hayo mapato.
 
UPDATE MASHTAKA DHIDI YA MAKAMPUNI MANNE YA SIMU.

Bashir Yakub, WAKILI
0714047241
.

Niliwaahidi kwamba nitakuwa nikiwaeleza kila tukio kuhusu mchakato wa kuyashitaki makampuni ya simu kwa unyonyaji.

Mnakumbuka kuhusu yale mambo yetu matano, vifurushi kutokuwa na muda wa kuexpire,ruhusa ya kuhamishiana vifurushi, kutochanganya vifurushi na muda wa kawaida wa maongezi bila ruhusa ya mtumiaji, vifurushi vya watu kuisha wakati mtu hajatumia au ametumia kidogo, na utaratibu wa kutoa taarifa kifurushi kinapokaribia kuisha na si kinapoisha.

Muda wa siku thelathini niliowapa haujaisha ukiisha nitawaambia.

Aidha, niliitwa na ndugu wa TCRA kitengo cha walaji. Nilifanya nao majadiliano kuhusu mambo haya na kuwaeleza nia yangu ya kuhakikisha Mtanzania analindwa. Nimeelewana nao vizuri.

Zaidi, wanaandaa kikao ambacho kitakuwa kati yangu, TCRA kitengo cha walaji, na makampuni yote ya simu. Mimi nilikusudia kuyashitaki makampuni manne(the big 4) lakini wao wamependekeza kikao kijumuishe wote. Ni jambo zuri na nimelipokea.

Na nimewaeleza kuwa hatua yoyote ambayo inalenga kuondoa unyonyaji wa aina hii na usumbufu mwingine wowote wanaoupata Watanzania wakati wakitumia simu, ninaupokea kwa mikono miwili. So far, kikao kinaweza kuandaliwa wiki ijayo ili kuona tunafikia wapi.

Zaidi, leo nimepata taarifa ambazo sijathibitisha kuwa Airtel wamefanya mabadiliko kwenye utumiaji wa data ambapo muda wa kifurushi cha data ukiisha hawaunganishi tena moja kwa moja na salio, bali sasa wameweka chaguo(option) ambapo wana kuuliza ikiwa unataka kuendelea kutumia muda wa kawaida au ungetaka kujiunga upya. Mnaotumia Airtel angalieni hili likoje.

Hata hivyo, Airtel kama wamefanya hivyo nawaambia haitoshi. Ni LAZIMA watekeleze na hayo mengine. Lakini pia ni LAZIMA watoe taarifa ya masaa 72 kabla ya mabadiliko yoyote kama Kanuni ya 5(5) ya Kanuni za Kielektroniki na Mawasiliano ya Posta GN No.61/2018 kuhusu kumlinda mlaji inavyotaka.

Wasifanye mabadiliko kwa kujifichaficha hii nchi sio yao, mtumiaji ana haki ya kujulishwa mabadiliko.

Pia, kwa wale mnaonipigia simu kunitisha nitumie jukwaa hili kuwaambia kwamba nitafurahi sana, tena sana, kufia kwenye vita hii kuliko kufia sehemu nyingine yoyote. Mwanaume kamili hafi kwa malaria bali hufia mambo kama haya.

Mwisho, niwashukuru nyinyi Watanzania kwa namna mlivyopokea jambo hili. Sijawahi kuona jambo ambalo Watanzania wote wanaunga mkono kama ilivyo kwa hili. Hii inadihihirisha ni kwa namna gani mlikuwa mmechoka.

Niishie hapa, nitawapa taarifa za kikao cha wiki ijayo.

Pia Soma
Hongera kwa ku copy Kenya.

Coz Kenya judgement ilikuwa Mwezi uliopita. Na jamaa alishinda. But in reality nothing has changed. Coz wameweka vifurushi vya aina2. With No expire date and With Expire date.
 
Sasa mbona wanaweza kubadilisha kifurushi wamavyotaka kama Halotel 10, 000 ilikuwa gb10 walipoona ngoma inogile elfu 10 hiyo sasa ni Gb 6. Na wanaweza shusha hata gb 5.

Ebu fafania hapo taf. Mi nadhani tuna hoja ya kulalamika
Hakuna sheria inayokataza bei ya bidhaa kupanda au kushuka ata sukari walipojaribu imewatokea puani.

Pili bei kupanda au kushuka inategemea na gharama zao za uzalishaji au kutokana na ushindani sokoni kwenye kuvutia wateja this is why developed economies don’t like monopolies or too large companies merging together kwa sababu zinauwa nguvu ya soko kwenye ushindani wa bei,

Tatu makampuni mapya yanapoingia sokoni as an entry strategy yanaweza kubali faida ndogo au hata hasara kiasi kwa kuuza huduma zao bei rahisi hili kuvutia wateja kwanza (penetration pricing). Mkishakuwa wengi inabidi warudi katika competition prices au bei ambazo zinafaida kwao baada ya gharama za kuzalisha; whichever suits them best.

Kwa ivyo kampuni mpya ukiona wapo rahisi chances are that is just a marketing ploy hila hizo bei zitapanda tu eventually.
 
Bundles ni bidhaa kama chips mayai ambapo unaponunua tu kanuni za mkataba zina apply.

Uwezi kwenda kununua zege usipomaliza ukamfuata muhudumu akurudishie chenji kisa umeshiba kati kati it doesn’t work that way.

Hivi vyuo vyetu avifundishi masuala ya contract law
Kwani nikiamua kuichuka na kuila tens baadae kuna MTU wa kunifuatilia?
Wewe uza chipsi habari za nimekulaje niachie mnunuzi
 
UPDATE MASHTAKA DHIDI YA MAKAMPUNI MANNE YA SIMU.

Bashir Yakub, WAKILI
0714047241
.

Niliwaahidi kwamba nitakuwa nikiwaeleza kila tukio kuhusu mchakato wa kuyashitaki makampuni ya simu kwa unyonyaji.

Mnakumbuka kuhusu yale mambo yetu matano, vifurushi kutokuwa na muda wa kuexpire,ruhusa ya kuhamishiana vifurushi, kutochanganya vifurushi na muda wa kawaida wa maongezi bila ruhusa ya mtumiaji, vifurushi vya watu kuisha wakati mtu hajatumia au ametumia kidogo, na utaratibu wa kutoa taarifa kifurushi kinapokaribia kuisha na si kinapoisha.

Muda wa siku thelathini niliowapa haujaisha ukiisha nitawaambia.

Aidha, niliitwa na ndugu wa TCRA kitengo cha walaji. Nilifanya nao majadiliano kuhusu mambo haya na kuwaeleza nia yangu ya kuhakikisha Mtanzania analindwa. Nimeelewana nao vizuri.

Zaidi, wanaandaa kikao ambacho kitakuwa kati yangu, TCRA kitengo cha walaji, na makampuni yote ya simu. Mimi nilikusudia kuyashitaki makampuni manne(the big 4) lakini wao wamependekeza kikao kijumuishe wote. Ni jambo zuri na nimelipokea.

Na nimewaeleza kuwa hatua yoyote ambayo inalenga kuondoa unyonyaji wa aina hii na usumbufu mwingine wowote wanaoupata Watanzania wakati wakitumia simu, ninaupokea kwa mikono miwili. So far, kikao kinaweza kuandaliwa wiki ijayo ili kuona tunafikia wapi.

Zaidi, leo nimepata taarifa ambazo sijathibitisha kuwa Airtel wamefanya mabadiliko kwenye utumiaji wa data ambapo muda wa kifurushi cha data ukiisha hawaunganishi tena moja kwa moja na salio, bali sasa wameweka chaguo(option) ambapo wana kuuliza ikiwa unataka kuendelea kutumia muda wa kawaida au ungetaka kujiunga upya. Mnaotumia Airtel angalieni hili likoje.

Hata hivyo, Airtel kama wamefanya hivyo nawaambia haitoshi. Ni LAZIMA watekeleze na hayo mengine. Lakini pia ni LAZIMA watoe taarifa ya masaa 72 kabla ya mabadiliko yoyote kama Kanuni ya 5(5) ya Kanuni za Kielektroniki na Mawasiliano ya Posta GN No.61/2018 kuhusu kumlinda mlaji inavyotaka.

Wasifanye mabadiliko kwa kujifichaficha hii nchi sio yao, mtumiaji ana haki ya kujulishwa mabadiliko.

Pia, kwa wale mnaonipigia simu kunitisha nitumie jukwaa hili kuwaambia kwamba nitafurahi sana, tena sana, kufia kwenye vita hii kuliko kufia sehemu nyingine yoyote. Mwanaume kamili hafi kwa malaria bali hufia mambo kama haya.

Mwisho, niwashukuru nyinyi Watanzania kwa namna mlivyopokea jambo hili. Sijawahi kuona jambo ambalo Watanzania wote wanaunga mkono kama ilivyo kwa hili. Hii inadihihirisha ni kwa namna gani mlikuwa mmechoka.

Niishie hapa, nitawapa taarifa za kikao cha wiki ijayo.

Pia Soma
Umeshalipoti kwahao wanaokutisha polisi?na nivizuri uwaanike nanamba zao
 
Nakubaliana na wewe asilimia zote.MUNGU akulinde katika mpambano huu.
 
Hiyo neno walaji, nadhani limetumika kumaanisha consumers, lakini nahisi neno consumer lipewe maana nyingine kwa context yako
Maana ni ile ile Consumer ni Mlaji na Mlaji ni yule Mtumiaji wa Mwisho hivyo hakuna haja ya neno hilo kupewa maana nyingine.
 
Sawa mtalaam lakini nikizingatia maelezo yako sukari sisi tunanunua kokote hapa kwenye simcard haziingiliani una banwa na mtoa buduma mmoja unalazimika kufuata chochote anachotaka kwa mkataba aliotunga yeye na anachokwambia ni kwamba uzingatie masharti na vigezo alivyo seti yeye mwenyewe. Bado hoja ya msingi ipo.
Hakuna sheria inayokataza bei ya bidhaa kupanda au kushuka ata sukari walipojaribu imewatokea puani.

Pili bei kupanda au kushuka inategemea na gharama zao za uzalishaji au kutokana na ushindani sokoni kwenye kuvutia wateja this is why developed economies don’t like monopolies or too large companies merging together kwa sababu zinauwa nguvu ya soko kwenye ushindani wa bei,

Tatu makampuni mapya yanapoingia sokoni as an entry strategy yanaweza kubali faida ndogo au hata hasara kiasi kwa kuuza huduma zao bei rahisi hili kuvutia wateja kwanza (penetration pricing). Mkishakuwa wengi inabidi warudi katika competition prices au bei ambazo zinafaida kwao baada ya gharama za kuzalisha; whichever suits them best.

Kwa ivyo kampuni mpya ukiona wapo rahisi chances are that is just a marketing ploy hila hizo bei zitapanda tu eventually.
 
Muktadha wa habari ndiyo unatoa mwelekeo wa maana ya maneno yenye maana zaidi ya moja. Mathalan, mtu akiwa kwenye mazingira ya jikoni pakiendelea kufanyika maandalizi ya mapishi, akimwagiza mwanae akaletee Mbuzi, moja kwa moja fikra zitajielekeza kwenye Mbuzi chombo cha kukunia Nazi na si Mbuzi mnyama
Hiyo neno walaji, nadhani limetumika kumaanisha consumers, lakini nahisi neno consumer lipewe maana nyingine kwa context yako
 
Usifananishe mpambano wako na kampuni za simu na magonjwa, ugonjwa wowote ni hatari kwa afya yako ndo maana unauwa, we umeleta hoja punguza mbwembwe
We ndo jinga kweli bado tu unauguaga malaria ????,vipi kati yahuyu mwanasheria akafa mfano kisahayo makampuni nakukupigania wewe usiejielewa...halafu wewe ukafa kwa ukimwi nani ataeziwa vizuri
 
Hongera sana ..naona airtel wameanza
Screenshot_20191113-001721.jpeg
 
Back
Top Bottom