Update: Mashtaka dhidi ya makampuni manne ya simu

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
88
1,613
UPDATE MASHTAKA DHIDI YA MAKAMPUNI MANNE YA SIMU.

Bashir Yakub, WAKILI
0714047241
.

Niliwaahidi kwamba nitakuwa nikiwaeleza kila tukio kuhusu mchakato wa kuyashitaki makampuni ya simu kwa unyonyaji.

Mnakumbuka kuhusu yale mambo yetu matano, vifurushi kutokuwa na muda wa kuexpire,ruhusa ya kuhamishiana vifurushi, kutochanganya vifurushi na muda wa kawaida wa maongezi bila ruhusa ya mtumiaji, vifurushi vya watu kuisha wakati mtu hajatumia au ametumia kidogo, na utaratibu wa kutoa taarifa kifurushi kinapokaribia kuisha na si kinapoisha.

Muda wa siku thelathini niliowapa haujaisha ukiisha nitawaambia.

Aidha, niliitwa na ndugu wa TCRA kitengo cha walaji. Nilifanya nao majadiliano kuhusu mambo haya na kuwaeleza nia yangu ya kuhakikisha Mtanzania analindwa. Nimeelewana nao vizuri.

Zaidi, wanaandaa kikao ambacho kitakuwa kati yangu, TCRA kitengo cha walaji, na makampuni yote ya simu. Mimi nilikusudia kuyashitaki makampuni manne(the big 4) lakini wao wamependekeza kikao kijumuishe wote. Ni jambo zuri na nimelipokea.

Na nimewaeleza kuwa hatua yoyote ambayo inalenga kuondoa unyonyaji wa aina hii na usumbufu mwingine wowote wanaoupata Watanzania wakati wakitumia simu, ninaupokea kwa mikono miwili. So far, kikao kinaweza kuandaliwa wiki ijayo ili kuona tunafikia wapi.

Zaidi, leo nimepata taarifa ambazo sijathibitisha kuwa Airtel wamefanya mabadiliko kwenye utumiaji wa data ambapo muda wa kifurushi cha data ukiisha hawaunganishi tena moja kwa moja na salio, bali sasa wameweka chaguo(option) ambapo wana kuuliza ikiwa unataka kuendelea kutumia muda wa kawaida au ungetaka kujiunga upya. Mnaotumia Airtel angalieni hili likoje.

Hata hivyo, Airtel kama wamefanya hivyo nawaambia haitoshi. Ni LAZIMA watekeleze na hayo mengine. Lakini pia ni LAZIMA watoe taarifa ya masaa 72 kabla ya mabadiliko yoyote kama Kanuni ya 5(5) ya Kanuni za Kielektroniki na Mawasiliano ya Posta GN No.61/2018 kuhusu kumlinda mlaji inavyotaka.

Wasifanye mabadiliko kwa kujifichaficha hii nchi sio yao, mtumiaji ana haki ya kujulishwa mabadiliko.

Pia, kwa wale mnaonipigia simu kunitisha nitumie jukwaa hili kuwaambia kwamba nitafurahi sana, tena sana, kufia kwenye vita hii kuliko kufia sehemu nyingine yoyote. Mwanaume kamili hafi kwa malaria bali hufia mambo kama haya.

Mwisho, niwashukuru nyinyi Watanzania kwa namna mlivyopokea jambo hili. Sijawahi kuona jambo ambalo Watanzania wote wanaunga mkono kama ilivyo kwa hili. Hii inadihihirisha ni kwa namna gani mlikuwa mmechoka.

Niishie hapa, nitawapa taarifa za kikao cha wiki ijayo.

Pia Soma - Bashir Yakub: Nitayashitaki makampuni manne ya simu
 
Hongera mzee kwa kutumia uelewa vizuri wa taaluma yako kwa jamii yako kwa ujumla nafkiria wale jamaa wananguvu Sana hii kwa waziri wa mawasiliano umemsaidia pakubwa mno nafkiri angeanza kukupa ulinzi huku hayo mengine yakiendelea kutatuliwa hongera Sana ukimaliza hili tunaihitaji tuwafuate na wa ving'amuzi
 
Biashara ya telco kwa vifurushi ni ya muda.. kwa jinsi gharama zinavyo shuka tutarudi kwenye Pay As You Go . Kwa hiyo kesi yako haina mashiko kabisa utapoteza muda wako.

Kwa kasi ya technolgy na urahisi wa mambo kutakua na baishara za aina mbili.

1. Wavivu kununua vocha wataenda kwenye post paid

2. Wakwangua vocha watapiga on demand ( Pay as you go).

Vifurushi tutawachia supermarket.
 
MKUU NAKUTAKIA MAPAMBANO MEMA KWA MAANA HOJA ZAKO ZIMESHIBA PIA UNA USHAHIDI KISHERIA
WASIWASI WANGU NAOMBA MTAKAPO KUWA MAKINI MAANA HAYA MAKAMPUNI HAYAFURAHII UKWELI HUU AMBAO TUMEKUA TUKINYONYWA MUDA MREFU
 
Bundles ni bidhaa kama chips mayai ambapo unaponunua tu kanuni za mkataba zina apply.

Uwezi kwenda kununua zege usipomaliza ukamfuata muhudumu akurudishie chenji kisa umeshiba kati kati it doesn’t work that way.

Hivi vyuo vyetu avifundishi masuala ya contract law
 
Bundles ni bidhaa kama chips mayai ambapo inaponunua tu kanuni za mkataba zina apply.

Uwezi kwenda kununua zege usipomaliza ukamfuata muhudumu akurudishie chenji kisa umeshiba kati kati it doesn’t work that way.

Hivi vyuo vyetu avifundishi maswala ya contract law
Huwezi mnyanganya sahani kisa muda wa lunch umeisha, halafu sio contract Law Ni "Law of Contract"
 
Back
Top Bottom