Uongozi wa UDOM wajibu madai ya kuwepo kunguni kwenye mabweni ya Wanafunzi

UDOM vyoo ni balaa, hostel unakuta mzigo umerundwa wa kutosha aisee vile vyoo fanyeni jambo vinatia aibu, unaweza kuta katika matundu takribani 10 ya vyoo yote mzigo umeshona pomoni (hawa jamaa wa UDOM sijui wanakula nini😂) maji yawepo ya kutosha vinginevyo itakuwa stori tu
 
Udom kumezidi
Ukikatiza tu korido karibu na choo
Mungu wangu, unaweza utapike.
.mijitu imeshusha mizigo,, wengine wanalengesha tu wadada wa usafi wakimaliza tu, huyo anaenda tua mzigo wake, hataki kujichosha kwenda kisimani kuvuta maji ya kutosha.

Room za wakaka 90%zinanukaa.. 10% ndio pekee Kuna hali nzuri kiasi.

Wanafunzi ni wachafu kwa kweli.
Lakini akiwa nje kachomekea hatari, utafikiri msafi kweli
 
Utakuta wanachuo wengi walizoea kufanyiwa kila kitu na dada wa kazi/mama leo wapo chuo wenyewe wanaona uvivu kuweka mazingira yao safi,mwisho wa siku wanazalisha kunguni na chawa wa kutosha.
Tufundishe watoto wetu kazi za mikono na usafi wao binafsi.
Uvivu ni janga kubwa sana.
 
Baada ya memba wa JamiiForums.com kudai kuwa kuna changamoto ya Wadudu aina ya Kunguni kwenye mabweni ya Wanafunzi wa Chuo Kukuu cha Dodoma (UDOM), ufafanuzi umetolewa kutoka kwenye mamlaka ya chuo hicho.

Taarifa ya awali ya Kunguni hii hapa - Kunguni wanatutesa Wanafunzi tunaolala kwenye mabweni ya UDOM

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Rose Mdami anajibu madai hayo kwa kusema:

“Ukweli ni kwamba suala hilo halina kweli japokuwa sisi kama Chuo tunaelewa kunapokuwa na wingi wa watu kunakuwa na tishio la magongwa mbalimbali ikiwemo uwepo wadudu hao aina ya Kunguni, ndio maana kina Wanafunzi wanapotoka Chuo kinaingia gharama kubwa ya kupuliza dawa ili kuhakikisha kila kitu kipo sawa.

“Ukija chuoni hata sasa utaona tumefanya kazi kubwa na kila kitu kipo sawa lakini changamoto kubwa tunayoipata ni suala la kusisitiza usafi kwa Wanafunzi wetu, wanapokuja wanakuta mazingira masafi, wanapoanza kuweka vyakula kwenye mabweni ndipo wanapoanza kufuga hao wadudu.

“Uchafu unapokithiri ndipo Kunguni nao wanavyopata nafasi, sisi hatufugi Kunguni ila wanatokana na uchafu.

“Chuo tumeweka watu wanafanya usafi kila kukicha kupitia kampuni, suala la kufanya usafi binafsi ni la mtu binafsi kama kwenye chumba chake anacholala atashindwa kuwa msafi itakuwa sio sawa kwa mtu kwenda kumtandikia kitanda.

“Suala la kunguni ni letu sote, ni wajibu wa Wanafunzi kuwajibika anachukia kuwa na hao wadudu, tunatimiza wajibu wetu kwa kupuliza dawa upande wetu kama tulivyofanya, wanapokuja Wanafunzi waendeleza kwa kila mmoja kuchua tahadhari binafsi.

“Tunaomba Wanafunzi wanapokuta mazingira safi wayaendele kama walivyoyakuta.”
Majibu ya kijinga kabisa, siamini kama hayo majibu yametokea chuo kikuu.


Tafadhali tupe chanzo cha taarifa na majibu hayo, aliyeiandika ni nani wa "UDOM?
 
Kwahiyo siku hizi kunguni wanakula viporo?
nadhani mkurugenzi anachotaka kutuambia hapa ni kwamba nje ya kunguni na mende wamo wa kutosha.
majibu mepesi kwa hoja za msingi yanaibua hoja nzito.
 
Katika vyuo nilivyopitia hakuna semehu chafu kama vyooni.Mtu anajisaidia mlangoni kabisa na unakuta hakuna maji ni balaa.
 
Inasikitisha kuona kuona chuo kinachobeba wanafunzi wengi kuliko vyote Afrika mashariki na Kati kukumbwa na Janga la Kunguni ,je ni wanafunzi kushindwa kujisimamia usafi ama uongozi kushindwa kusimamia mazingira?
 
Back
Top Bottom