A
Anonymous
Guest
Sina haja ya kutaja jina langu wala kuandika maelezo mengi, lakini kwa ufupi mimi ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Kwakweli suala la kunguni UDOM limekuwa linasumbuwa na lina kera kwa muda mrefu.
Ajabu ni kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa sasa wadudu hao wamekuwa wengi sana yaani nahisi hata Ufaransa tunaposikia wamefunga vyuo hawajafikia huku, ni kero sana.
Kunguni hao wanapatikana kwenye mabweni tunapolala, mfano kwenye college ya Education ndio balaa.
Siku za nyuma uongozi wa chuo ulikuwa na kawaida ya kupuliza dawa kwenye mabweni, lakini ndani ya miaka hii miwili hali imekuwa tofauti.
Tulipofunga Chuo Juni na Julai 2023 tulitegemea tukirudi tutakuta wamepuliza dawa lakini hali imekuwa tofauti, matokeo yake watu tumeanza kulazimika kutandika na kulala chini kwani vitandani hakulaliki.
Changamoto hii sio kwenye college yetu pekee bali karibia zote Wanafunzi tumekuwa tukilalamika kunguni.
Majibu ya UDOM yako hapa: Uongozi wa UDOM wajibu madai ya kuwepo kunguni kwenye mabweni ya Wanafunzi