Uongo wa Zitto Kabwe

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
2,866
2,000
Fack check

Supreme leader and Chief Advisor wa ACT Wazalendo Bw. Zitto Kabwe ameandika kwenye mtandao wa Twitter kua Tanzania haijawahi kutokea mkuu wa mkoa, RC ama mkuu wa wilaya DC kushtakiwa akiwa ofisini katika historia ya Tanzania.

Zitto hua sio mwanasiasa wa kumuamini, wanasiasa wote ni waongo ila Zitto yeye ni muongo zaidi.

Sasa wanasiasa waongo aina ya Zitto wakienda unchecked wataendelea kuwaaminisha wafuasi wao uongo na kupelekea kua na jamii iliyojazwa Uongo.

Zitto anasema Sabaya ndie mkuu wa wilaya wa kwanza kushtakiwa akiwa madarakani kwa makosa ya jinai.

Naomba kumbukusha Zitto kua November 6, 2006 aliewahi ama aliekua mkuu wa mkoa wa Tabora Bw. Zitopile Mzuzuri alifikishwa mahakamani kwa kosa la jinai la mauaji na jambo hilo lilijadiliwa humu.

Zitto acha uongo.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,902
2,000
Uteuzi unatafutwa!

Wanasahau kina Mramba na Yona waliokuwa mawaziri waliwahi shitakiwa na kuhukumiwa hata kama walishaondoka ofisini?

Kumshitaki Waziri hata kama ni wa zamani ni sawa na kumshitaki RC au DC iliyopo ofisini?

Na huyo Sabaya kashitakiwa akiwa ofisini au baada ya kuondolewa?

Kama angekuwa ofisini, angeshitakiwa kama Sabaya au DC?

Zitto aache vihoja.
 
Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
517
1,000
Halafu kuifananisha kesi ya jinai na kesi ya ajali ya barabarani ni kuchanganya mambo.
Labda umepitiwa. Ditopile aliuwa au lugha ya kisheria alisababisha kifo cha conductor. Wala haikuwa kosa la barabarani, kulitokea mzozo baina yake na conductor wa daladala. Baada ya hapo Ditopile alitoa bastora na kufyatua risasi kwa konda iliyoleteleza mauti. Ndipo baadae alivuliwa ukuu wa mkoa na kushitakiwa. Na alishitakiwa na Jamhuri. Lilikuwa kosa la jinai. Na hii kesi ilijaa utata kwa madai kuwa aliuwa bila kukusudia.
Hata kesi za usalama barabarani zote uwa ni za jinai.
Waliokuwa mawaziri, Mramba na Yona nao pia walishawahi kushitakiwa wakiwa viongozi waandamizi wa Serikali, hivyo Zito kakurupuka bila kutazama historia. Si hivyo tu Zombe na wenzake alivuliwa wadhifa wake na kushitakiwa. Alikuwa mtumishi mwandamizi tena wa polisi.
 
The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,503
2,000
Sasa Mkubwa ndiyo umechoropoka huko ndani na kupiga kelele kubwa hivyo...??

Kwanini kumwita mwenzio "muongo" kana kwamba wewe ni "mkweli...??"

Ungetofatautiana naye tu kwa wewe kuleta hoja pingamizi dhidi ya hoja yake...!

Hivyo ndivyo waungwana tunavyojadilianaga na kamwe si kwa namna ulivyokuja wewe....!!!
 
Ryaro ryaro

JF-Expert Member
Feb 10, 2021
326
1,000
Lakini mkosa ya Sabaya ni unique yaani Ujambazi wa kutumia silaha, tuhuma Ambazo hazijawa rasmi kama Kubaka..Hii kweli sijawahi kutokea Tanzania..
 
Muuza viatu

JF-Expert Member
May 14, 2020
1,809
2,000
Labda umepitiwa. Ditopile aliuwa au lugha ya kisheria alisababisha kifo cha conductor. Wala haikuwa kosa la barabarani, kulitokea mzozo baina yake na conductor wa daladala. Baada ya hapo Ditopile alitoa bastora na kufyatua risasi kwa konda iliyoleteleza mauti. Ndipo baadae alivuliwa ukuu wa mkoa na kushitakiwa. Na alishitakiwa na Jamhuri. Lilikuwa kosa la jinai. Na hii kesi ilijaa utata kwa madai kuwa aliuwa bila kukusudia.
Hata kesi za usalama barabarani zote uwa ni za jinai.
Waliokuwa mawaziri, Mramba na Yona nao pia walishawahi kushitakiwa wakiwa viongozi waandamizi wa Serikali, hivyo Zito kakurupuka bila kutazama historia. Si hivyo tu Zombe na wenzake alivuliwa wadhifa wake na kushitakiwa. Alikuwa mtumishi mwandamizi tena wa polisi.
Hakuwa kondakta alikua dereva
 
Ng'wale

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
3,710
2,000
Ditopile alishtakiwa kwa kosa la kuuwa bila kukusudia.

Kuna tofauti kubwa hapo.
Suala la kwamba ni "kuua bila kukusudia" ni baada ya hukumu kuendeshwa. Hakuna case inayofunguliwa kwa jina la "kuua bila kukusudia" Hayo ya kutokusudia yalikuja baada ya hukumu kuendeshwa.
 
Ng'wale

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
3,710
2,000
Labda umepitiwa. Ditopile aliuwa au lugha ya kisheria alisababisha kifo cha conductor. Wala haikuwa kosa la barabarani, kulitokea mzozo baina yake na conductor wa daladala. Baada ya hapo Ditopile alitoa bastora na kufyatua risasi kwa konda iliyoleteleza mauti. Ndipo baadae alivuliwa ukuu wa mkoa na kushitakiwa. Na alishitakiwa na Jamhuri. Lilikuwa kosa la jinai. Na hii kesi ilijaa utata kwa madai kuwa aliuwa bila kukusudia.
Hata kesi za usalama barabarani zote uwa ni za jinai.
Waliokuwa mawaziri, Mramba na Yona nao pia walishawahi kushitakiwa wakiwa viongozi waandamizi wa Serikali, hivyo Zito kakurupuka bila kutazama historia. Si hivyo tu Zombe na wenzake alivuliwa wadhifa wake na kushitakiwa. Alikuwa mtumishi mwandamizi tena wa polisi.
Point of correction. Ni daladala driver siyo daladala conductor.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
120,965
2,000
Huyu ni mnafiki mkubwa ni mtu wa kumuogopa kama ukoma.
Fack check

Supreme leader and Chief Advisor wa ACT Wazalendo Bw. Zitto Kabwe ameandika kwenye mtandao wa Twitter kua Tanzania haijawahi kutokea mkuu wa mkoa, RC ama mkuu wa wilaya DC kushtakiwa akiwa ofisini katika historia ya Tanzania.

Zitto hua sio mwanasiasa wa kumuamini, wanasiasa wote ni waongo ila Zitto yeye ni muongo zaidi.

Sasa wanasiasa waongo aina ya Zitto wakienda unchecked wataendelea kuwaaminisha wafuasi wao uongo na kupelekea kua na jamii iliyojazwa Uongo.

Zitto anasema Sabaya ndie mkuu wa wilaya wa kwanza kushtakiwa akiwa madarakani kwa makosa ya jinai.

Naomba kumbukusha Zitto kua November 6, 2006 aliewahi ama aliekua mkuu wa mkoa wa Tabora Bw. Zitopile Mzuzuri alifikishwa mahakamani kwa kosa la jinai la mauaji na jambo hilo lilijadiliwa humu.

Zitto acha uongo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom