Undumilakuwili wa Zitto Kabwe

MWANDAMBO

Member
Feb 2, 2011
19
17
Wakati Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar kikijipambanua kupitia sakata la Bandari kumtetea Rais Samia kwa misingi ya Uzanzibari, Kiongozi wa chama hicho Ndugu Zitto ametumia mwanya huo wa kimsimamo kutetea Mradi wa DP World wa Bandari za Tanganyika chini ya kivuli cha Faida za bandari na mtazamo ya wengine.

Viongozi wa ACT Wazalendo Zanzibar wamechagua kutumia mjadala wa DP World katika umiliki Bandari za Tanganyika milele kuibua hoja ya Muungano na kuhalalisha hoja zao za KUVUNJA Muungano kwa madai kwamba Rais Samia anaonewa kwasababu ni Mzanzibari. Wakati Zitto na Rostam Azizi wakidai anashutumiwa kwasababu za Udini, lkn Kwao mkataba huo hauna shida ila shida ni kwasababu ni Rais Mzanzibari na Muislamu.

Katika Sakata hili la uuzwaji wa bandari za Tanganyika, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto alianza kwa kujificha na mafumbo mitandaoni na Sasa amejiweka hadharani kutetea Mradi wa DP World na umuhimu wake huku akirusha vijembe dhidi ya wale wote wanaohoji maslahi sahihi ya Tanzania na mgogoro wa kisheria wa Mkataba huo mbali ya harufu kali ya Rushwa na Ufisadi wa Mradi huo pamoja na vifungu vibovu ktk mkataba huo.

Tunafahamu pia mahusiano ya muda mrefu ya Zitto Kabwe na baadhi ya wanasiasa na wafanya biashara nguli nchini kama Rostam Azizi ambao wamekuwa wakihangaika kuidhibiti na kudhibiti rasilimali za nchi hii kwa maslahi yao wenyewe na wafaidika wao chini ya mwavuli wa siasa kupitia Vyama vya Siasa.

Katika mbinu hizo, wamekuwpo wanasiasa nje ya mfumo wa chama Tawala (Upinzani) kama sauti mbadala ya kupunguza makali ya sauti za umma na wapinzani ambao wamekuwa wakidai na kuibua mjadala mkali wa maslahi ya umma na Zitto Kabwe ni ushahidi tosha. Kazi kubwa ya Zitto ni kuhakikisha Upinzani unagawanyika kwenye masuala mazito ambayo yanagusa maslahi mapana ya umma lkn yakiathiri kundi la watu ambao Zitto anafanya kazi nao au kwa niaba yao nje ya mfumo wa chama tawala.

Nimewai kuandika huko nyuma kwamba chama cha ACT Wazalendo si chama cha kisiasa kimsingi katika malengo ya kimsingi ya chama cha siasa tangu uanzishwaji wake na hata ktk uendeshaji wake hadi sasa. Msingi mmoja wa chama hicho ni kwamba, kilianzishwa kama Daraja na Jukwaa la kupunguza nguvu ya ushawishi wa UKAWA kuelekea 2015 na baada ya 2015 (Uchaguzi Mkuu) chama hicho chini ya mwavuli wa Zitto kabwe kiligeuka kama jukwaa la kuwagawa wapinzani na wanaharakati dhidi ya hoja na madai yao dhidi ya chama na serikali iliyoko madarakani.

Baada ya Rais Magufuli kuharibu miundombinu ya mshikamano na Uimara wa Upinzani halisi na kuwageukia wale wapinzani wa ndani mwake (Team Kikwete) ndipo Zitto kabwe tena akageuka na kuanza vita dhidi ya Chama Tawala na serikali ya Magufuli tu kwasababu jamaa zake ndani ya dola na ccm wameguswa na akitumia nguvu kubwa kutaka uungwaji mkono kutoka kwa upinzani halisi.

Baada ya mabadiliko ya kisiasa ambayo yamemuingiza Rais Samia Madarakani - chini ya ushawishi na udhibiti wa watu wa Kikwete ndipo Zitto amegeuka tena na kuendelea na Mradi wake wa kulinda maslahi yake na kuendelea na kazi yake ya msingi ya kuhakikisha upinzani unakuwa mdogo dhidi ya serikali ya sasa hata kama kuna dosari kubwa sana. Hatari kubwa ni kwamba anatumia jukwaa ambalo ni chama cha siasa ambacho wengine ndani yake wanaamini wanapigania maslahi ya umma lkn pia jukwaa hilo ambalo ni rahisi kuwahadaa watanzania kwenye maslahi yao. Kiongozi wa chama huyu amefanikiwa kukifanya chama kizima na Viongozi wake hata wale wa Zanzibar ambao wamekuwa na rekodi ya kuwa watu wenye msimamo kuwa watu wenye sura mbili mbili.

Chama hakina msimamo wa kisera, Itikadi, mwelekeo. Leo wekundu, kesho weusi, na keshokutwa wabluu. Asubui weupe, usiku weusi. Ni hatari kwa demokrasia, usalama na ustawi wa nchi kama kuna chama cha siasa ambacho hakieleweki mwenendo wake, msimamo wake wa kisera na itikadi. Maslahi yao ni maslahi ya makundi yenye nguvu ndani ya Nchi. Kimsingi chama hichi ni jukwaa la kisiasa ambalo maafisa wa waandamizi wa chama Tawala na serikali wanakitumia kama Jukwaa la kudhibiti upinzani na sauti mbadala za Utetezi wa Haki na umma na ni fursa kwa baadhi ya waandamizi wa chama hicho kwenye miradi huo kwa kujua au kutokujua kujipatia fursa mbalimbali na maslahi binafsi wakati kwenye masuala ya Maslahi ya Umma hiki sio mdau wa kupigania hayo.

Historia inatuonyesha kwamba, Zitto kabwe amekuwa akitumia njia ya kuanzisha hoja kinzani dhidi ya hoja inayokubalika na makundi halisi ya upinzani kwenye maslahi ya nchi au huanzisha hoja mbadala ya kuwagawa wapinzani au kuwavuruga wananchi kushindwa kujua wasimame na nani, Aidha huendesha kampeni wakati mmoja dhidi ya makundi mengine ya Upinzani kwenye masuala ya Maslahi ya nchi. Mathalani, 2015, Zitto kupitia chama chake cha ACT alipinga vikali Madai ya kuheshimiwa matokeo ya uchaguzi Zanzibar yaliompa ushindi Maalim Seif chini ya UKAWA kiasi kwamba aliwai kumuita Maalim Seif kuwa Msaliti wa nchi alipokuwa akizishawishi nchi wadau wa maendeleo ya Tanzania kushinikiza Serikali ya Tanzania kuheshimu matokeo ya octoba 25 2015. Pia wakati wa vuguvugu la katika Mpya chini ya UKAWA, Zitto aliupingana vikali na msimamo wa UKAWA wa kuunga mkono Rasimu ya Warioba ambapo UKAWA waliiunga mkono kwa Asilimia 80.

Mwaka mmoja baada ya Rais Samia kuingia madarakani, ikaibuka tena Hoja mpya ya Katiba Mpya - zitto akaja na hoja mbadala dhidi ya Katiba Mpya ambayo ni Tume huru ya uchaguzi kwanza kama mbadala wa katiba Mpya na baada ya kubanwa na migawanyiko ilioanza kujitokeza ndani ya ACT, Wakabadilisha mwelekeo na kusema Tume huru kuelekea Katiba mpya (confusion). Msingi wa madai ya tume huru ya uchaguzi dhidi ya katiba mpya ilikuwa ni kupunguza nguvu ya Umma ilivyokuwa ikishika kasi kwenye madai ya Katiba Mpya ambapo tunajua wazi kwamba, yanahatarisha uwepo wa chama Tawala kuendelea kubakia madarakani na ambapo kwa sasa, chama hicho kiko chini ya udhibiti wa ushawishi wa Kikwete watu ambao Zitto anawatumikia.

FB_IMG_1667367768516.jpg
FB_IMG_1667367768516.jpg

Watu kama January Makamba (mgombea wa Urais mbadala wa ccm), Rostam Azizi, ni sehemu ya Mradi huu chini ya ushawishi wa Kikwete na watu wake ijapokuwa ni ukweli kwamba Rostam Azizi na Kikwete mwenyewe hawako sawa kutokana na historia ya uhusika wake kwenye kashfa kadhaa kama Kagoda na baadae kutelekezwa na Kikwete kwenye ushiriki wake kwneye siasa za Kitaifa mpaka ambapo Rais Samia alipoamua kumpa fursa ya kuendelea kuifilisi nchi chini ya mwavuli wa uwekezaji, na kwasababu ya Rostam kutumika dhidi ya Maslahi ya Umma pamoja na tofauti binafsi walizoea nazo (Mjadala wa siku nyingine).

Anderson Ndambo
andambo@yahoo.com
 
Kwani wote lazima tuwe na mtazamo mmoja? Yeye Katoa maoni yake, nawe toa yako. Usimpangie mwenzio cha kusema.

Kwani Kuna utawala wa rais muislamu wakristo hamjapiga makelele? Mbona tumewagundua ujinga wenu Sasa?

Kaeni mtulie, mbona sisi huwa hatupigi kelele Kama nyie? Bandari inabinafsishwa kibiashara. Wewe unataka Nini Sasa?

Kama una wivu lamba limao au ita wanaume wakuletee ukwaju ulambe
 
Zito anajua kujenga hoja katika kila uwanja ambao haki inakiukwa.

La bandari amekengeuka na amejiunga na samia na Rostam ambaye ni mshirika wake wa kifedha miaka mingi.
Kwa samia /Zanzibar inaweza kuwa sababu ya kikundi chake cha ACT kiko Zanzibar na hivyo kwenda kinyume ni kuhatarisha uhai wa kikundi chake. Simuweki sana kwenye dini, ingawa ana elements za kuegemea dini.

Kweli Zito huoni kuwa mkataba wa bandari una walakii mkubwa? na ujuzi wako na power of analysis yako huoni ubaya wowote ndani ya mkataba wa bandari?

Huyu ndiye Zito, ni msaliti.
Once a Traitor Always a Traitor is a quote that means that once you betray someone, you're always going to be seen as untrustworthy.
 
Wewe ndo Una matatizo..
Lazima Zitto atazame Jambo Sawa na Chadema?.
Zitto mbona alishauri ianzishwe kampuni ya Dpworld na TPA...ndo wafanye biashara 50/50...

Nyinyi mnataka kila mnaemchukia achukiwe na kila mtu??

Kuunga kwake mkono Kwa kushauri nini kifanyike kwako wewe ni tatizo??
 
Wanasiasa na siasa zao hawawezi kuwa wakweli daima.
Wana angalia shibe yao ipo wapi.
 
Wewe ndo Una matatizo..
Lazima Zitto atazame Jambo Sawa na Chadema?.
Zitto mbona alishauri ianzishwe kampuni ya Dpworld na TPA...ndo wafanye biashara 50/50...

Nyinyi mnataka kila mnaemchukia achukiwe na kila mtu??

Kuunga kwake mkono Kwa kushauri nini kifanyike kwako wewe ni tatizo??
Kuna sehemu hapo jamaa kataja CDM? kwa hio wanaopinga DP Bandari wote nchi hii wako CDM?
 
Wewe ndo Una matatizo..
Lazima Zitto atazame Jambo Sawa na Chadema?.
Zitto mbona alishauri ianzishwe kampuni ya Dpworld na TPA...ndo wafanye biashara 50/50...

Nyinyi mnataka kila mnaemchukia achukiwe na kila mtu??

Kuunga kwake mkono Kwa kushauri nini kifanyike kwako wewe ni tatizo??
Hakuna aliyekukataza kumpenda Zitto, kwasababu afterall wote wawili tabia zenu zinafanana, wanafiki.
 
Zito anajua kujenga hoja katika kila uwanja ambao haki inakiukwa.
La bandari amekengeuka na amejiunga na samia na Rostam ambaye ni mshirika wake wa kifedha miaka mingi.
Kwa samia /Zanzibar inaweza kuwa sababu ya kikundi chake cha ACT kiko Zanzibar na hivyo kwenda kinyume ni kuhatarisha uhai wa kikundi chake. Simuweki sana kwenye dini, ingawa ana elements za kuegemea dini.
Kweli Zito huoni kuwa mkataba wa bandari una walakii mkubwa? na ujuzi wako na power of analysis yako huoni ubaya wowote ndani ya mkataba wa bandari?

Huyu ndiye Zito, ni msaliti.
Once a Traitor Always a Traitor is a quote that means that once you betray someone, you're always going to be seen as untrustworthy.
Msingida TL alipomiminiwa malisasi kisa usaliti wa kuwatetea Accasia kwenye issue za makinikia uliisahau hii quotation?
 
Wewe ndo Una matatizo..
Lazima Zitto atazame Jambo Sawa na Chadema?.
Zitto mbona alishauri ianzishwe kampuni ya Dpworld na TPA...ndo wafanye biashara 50/50...

Nyinyi mnataka kila mnaemchukia achukiwe na kila mtu??

Kuunga kwake mkono Kwa kushauri nini kifanyike kwako wewe ni tatizo??
Nyie madalali ya bandari ni mapumbavu sana sasa hao warabu wenu wauza watumwa wajaribu kuja waone kama hapatachimbika mpaka wakimbie.
 
Back
Top Bottom