Uongo wa gazeti la Tanzania Daima

Nilijua watakanusha,
lakini jana katika blog ya michuzi niliona picha ya waziri mkuu akiwa na mawaziri wake wote pamoja na manaibu katika kikao pale magogoni kilichofanyika juzi (Jumanne) Je hicho hakikuwa kikao cha baraza la mawaziri???????????????????????
 
Jana kulikuwa na thread iliyokuwa na kichwa cha habari "Sitta na Mwakyembe wafungwa mdomo kuhusu Dowans" Source ya thread hiyo ilikuwa gazeti la "TZ Daima". Watu wengi tulipoteza MUDA mwingi kuchangia thread hiyo. Katika gazeti hilo kulinukuliwa habari zilizotoka katika kikao cha baraza la Mawaziri ambacho JK alikuwa ni mwenyekiti wake. Nukuu mbalimbali zilitolewa kama ushahidi wa kilichosemwa kikaoni.

Habari zilizothibitishwa na Sitta mwenyewe na Pia Katibu mkuu Ndg. Ph. Luhanjo zinasema HAPAKUWA NA KIKAO CHA MAWAZIRI WALA HAKUNA ALIYEWAZIBA MDOMO SITTA NA MWAKYEMBE. habari hizi zimeandikwa na magazeti yote ya leo kasoro TZ Daima.

Wadau: Katika tasnia ya habari, Je, hamuoni kama gazeti hili ni hatari kwa usalama wa nchi yetu?. Je, gazeti kama hili katika utawala unaojali sheria za vyombo vya habari halipaswi kufungiwa kwa muda? Je, si kweli kwamba waandishi wa gazeti hili ni MAKANJANJA?. naomba tuwe wazalendo katika kujadili hili. Tanzania ni yetu na ni sisi wenye damu mpya tunaoweza kuifikisha nchi tunapopataka kwa AMANI.

Hawa jamaa kukanusha mbona ni jadi kwao, hata rais alipoanguka walikanusha, EPA na mengine mengi wao ni kukanusha tu kwa kwenda mbele.

Mimi wala siwezi kuamini wala kumwamini Luhanjo, Mbona Martin mtoto wa Chikawe alimkemea mtoto wa Sita na yule mtoto wa Mwakyembe. Nae ingekuwa hakuitoa laivu mwenyewe wangekanusha baadae
 
Tumewazoea!!!! Sio mara ya kwanza wala ya pili kwa watu wanaojidai kimbelembele juu ya mafisadi kufungwa midomo katika vikao vyao hawa viongozi wetu!!! Kwa kweli hakuna matumaini ya maendelo TZ chini ya waafrika wenzetu. Labda tuombe waje wazungu watutawale.... Finish!!
 
Jana kulikuwa na thread iliyokuwa na kichwa cha habari "Sitta na Mwakyembe wafungwa mdomo kuhusu Dowans" Source ya thread hiyo ilikuwa gazeti la "TZ Daima". Watu wengi tulipoteza MUDA mwingi kuchangia thread hiyo. Katika gazeti hilo kulinukuliwa habari zilizotoka katika kikao cha baraza la Mawaziri ambacho JK alikuwa ni mwenyekiti wake. Nukuu mbalimbali zilitolewa kama ushahidi wa kilichosemwa kikaoni.

Habari zilizothibitishwa na Sitta mwenyewe na Pia Katibu mkuu Ndg. Ph. Luhanjo zinasema HAPAKUWA NA KIKAO CHA MAWAZIRI WALA HAKUNA ALIYEWAZIBA MDOMO SITTA NA MWAKYEMBE. habari hizi zimeandikwa na magazeti yote ya leo kasoro TZ Daima.

Wadau: Katika tasnia ya habari, Je, hamuoni kama gazeti hili ni hatari kwa usalama wa nchi yetu?. Je, gazeti kama hili katika utawala unaojali sheria za vyombo vya habari halipaswi kufungiwa kwa muda? Je, si kweli kwamba waandishi wa gazeti hili ni MAKANJANJA?. naomba tuwe wazalendo katika kujadili hili. Tanzania ni yetu na ni sisi wenye damu mpya tunaoweza kuifikisha nchi tunapopataka kwa AMANI.

Wewe murongo na murozi....hii itakusuta

Ikulu yaikana Tanzania Daima
 
Wewe murongo na murozi....hii itakusuta

Ikulu yaikana Tanzania Daima

pi.jpg

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Jana amefanya Mkutano na Baraza la Mawaziri la Kazi linalojumuisha Mawaziri na Manaibu Waziri ofisini Kwake Mtaa wa Magogoni Jijini Dar es Salaam Juzi.
 
Jana kulikuwa na thread iliyokuwa na kichwa cha habari "Sitta na Mwakyembe wafungwa mdomo kuhusu Dowans" Source ya thread hiyo ilikuwa gazeti la "TZ Daima". Watu wengi tulipoteza MUDA mwingi kuchangia thread hiyo. Katika gazeti hilo kulinukuliwa habari zilizotoka katika kikao cha baraza la Mawaziri ambacho JK alikuwa ni mwenyekiti wake. Nukuu mbalimbali zilitolewa kama ushahidi wa kilichosemwa kikaoni.

Habari zilizothibitishwa na Sitta mwenyewe na Pia Katibu mkuu Ndg. Ph. Luhanjo zinasema HAPAKUWA NA KIKAO CHA MAWAZIRI WALA HAKUNA ALIYEWAZIBA MDOMO SITTA NA MWAKYEMBE. habari hizi zimeandikwa na magazeti yote ya leo kasoro TZ Daima.

Wadau: Katika tasnia ya habari, Je, hamuoni kama gazeti hili ni hatari kwa usalama wa nchi yetu?. Je, gazeti kama hili katika utawala unaojali sheria za vyombo vya habari halipaswi kufungiwa kwa muda? Je, si kweli kwamba waandishi wa gazeti hili ni MAKANJANJA?. naomba tuwe wazalendo katika kujadili hili. Tanzania ni yetu na ni sisi wenye damu mpya tunaoweza kuifikisha nchi tunapopataka kwa AMANI.
Unauhakika gani kama habari iliyosemwa na Luhanjo ni ya kweli kuwa hakukuwa na kikao, mara ngapi serikali inadanganya kwa mambo ya msingi baadaye inakuja kukubali au wewe ni mara ya kwanza kuona serikali ikidanganya.

Halafu huo usalama uliohatarishwa na Tanzania Daima ni upi kule kusema kulikuwa na kikao au ule wa serikali kulipa kampuni hewa, lipi kati ya hayo linahatarisha usalama zaidi.
 
pi.jpg

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Jana amefanya Mkutano na Baraza la Mawaziri la Kazi linalojumuisha Mawaziri na Manaibu Waziri ofisini Kwake Mtaa wa Magogoni Jijini Dar es Salaam Juzi.

haya sasa. na ww toa picha ikionesha vitina meza viko 2pu. ebo kalakabaho. people power we are well equiped!
 
gazeti hili linamuhariri /makamo muhairiri muislam, au mnalaumu annur tu humu jf?

Mimi nilifikiri moderator wa JF umesha m-delete huyu muhogomchungu kwenye list ya watu wenye ruksa ya kuchangia mada. Maana every day mada zake ni udini.
 
Watanzania wameshapoteza imani kwa zaidia ya asilimia 120 dhidi ya serikali hii.
Tanzania Daima linaaminika kuliko magazeti yote ya serikali na CCM, viongozi wote wa serikali pamoja na makuwadi wao kama Mtanzania, rai, nk.
Hivyo kauli yoyote ya serikali dhidi ya magazeti makini kama Tanzania Daima, MwanaHalisi, Raia mwema, na Mananchi. Hakika, haya ndio magazeti yanayosema kweli kuliko kauli yoyote ya kiongozi wa serikali ya sasa.
tutayaamini na sio porojo za akina Luhanjo. ..finish!
 
pi.jpg

SAKATA LA DOWANS: Sitta afungwa mdomo
• Baraza la Mawaziri chini ya JK lamshambulia yeye na Mwakyembe

na Mwandishi wetu (Tanzania Daima Jana hiyo)

RAIS Jakaya Kikwete amemfunga mdomo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta aliyeingia katika mzozo na waziri mwenzake wa Nishati na Madini, William Ngeleja. Mzozo huo uliibuka baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC), kuamua Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) iilipe Dowans fidia ya sh bilioni 94 kutokana na TANESCO kuvunja mkataba nayo.

Uamuzi wa kumziba mdomo Sitta, ulifikiwa jana katika kikao cha Baraza la Mawaziri, kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, chini ya Rais Kikwete(akiwakilishwa na pinda) mengine, mjadala wa malipo ya Dowans ulitawala kikao hicho. Mwingine aliyepigwa kufuli katika kikao hicho ni Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk. Harrisson Mwakyembe, ambaye naye aliungana na Sitta kumpinga Ngeleja kuilipa Dowans. Vyanzo vyetu vya habari vilisema Sitta na Mwakyembe walikuwa na wakati mgumu kutetea hoja ya kutaka serikali isiilipe Dowans na kwamba hata Rais alisema hafurahishwi na hukumu ya malipo hayo.

"Kikao bado kinaendelea, lakini Sitta na Mwakyembe walibanwa sana na mawaziri na hata Bwana mkubwa (Rais) aliungana na mawaziri wengine kuwalaumu kwa kupeleka mjadala huo hadharani," kilisema chanzo chetu cha habari.

Kwa mujibu wa habari hizo, kuanzia sasa Sitta na Dk. Mwakyembe, wamefungwa mdomo kuzungumzia suala la malipo ya Dowans hadharani na kwamba wanapaswa kuwa kitu kimoja kuhakikisha mipango ya serikali inatekelezwa kama ilivyopangwa.
Kabla ya kibano hicho jana, wiki iliyopita katika kikao cha kamati ndogo ya mawaziri uliibuka msuguano wa hoja kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema na Waziri Sitta.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho ambacho kilifanyika chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda(pichani), zinaeleza kuwa Jaji Werema alieleza kusikitishwa na matamshi ya Sitta katika vyombo vya habari.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zimemkariri Werema akieleza kushangazwa na hatua ya Sitta kuwashambulia yeye na Ngeleja huku akijua kuwa walichokifanya na kuamua kilikuwa kinagusa moja kwa moja mamlaka yao ya kiwajibu na kimamlaka.
Jaji Werema amekaririwa akimweleza Waziri Sitta kwamba iwapo kweli alikuwa ana uchungu na suala la Dowans, basi wakati kesi ikiendelea alipaswa kuisaidia serikali katika kuwasilisha utetezi dhidi ya malalamiko 17 yaliyokuwa yamewasilishwa na kampuni hiyo.

Habari zinaeleza kwamba hatua ya Sitta ambaye alikuwa akitambua fika namna kesi hiyo ilivyokuwa ikiendelea kutochangia jambo lolote wakati shauri hilo likiwa ICC na badala yake kusubiri hadi serikali ishindwe ndipo aanze kutoa matamshi katika vyombo vya habari ilikuwa ni ya kuchochea hasira za wananchi dhidi ya viongozi pasipo sababu zozote.

Wakati Jaji Werema akimshushia lawama Sitta kwa muda usiopungua dakika 15, Waziri Mkuu Pinda alikuwa kimya muda wote.Baada ya kumaliza hoja yake, Waziri Mkuu aliwataka wajumbe wa kamati hiyo ya mawaziri iliyokuwa ikijadili kuhusu Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Manunuzi unaotarajiwa kuwasilishwa katika Bunge lijalo kuendelea na mjadala. Awali kabla ya Werema kuzungumza, Sitta alichangia kuhusu muswada huo na akaeleza haja ya kuwekwa kwa masharti magumu zaidi ili kuzuia uwezekano wa makampuni ya kitapeli kujipenyeza nchini na kuigharimu serikali mamilioni ya fedha kauli ambayo ilionekana kumkera Werema. Awali hofu ilitawala kwamba Sitta na Mwakyembe, wangeweza kupoteza nafasi zao za uwaziri kutokana na hatua yao ya kuibua mjadala dhidi ya mawaziri wenzao nje ya Baraza la Mawaziri kuhusu uamuzi wa serikali kukubali kuilipa Kampuni ya Dowans Holdings SA.
Mkanganyiko wa kauli ya Sitta na Mwakyembe, ulisababisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, kutoa matamshi makali ya karipio kwa mawaziri hao wawili.

Ukali wa matamshi hayo ya Chikawe ambaye anadaiwa kupata baraka za Rais Kikwete, uliongezwa na tamko lake la kuwataka Sitta na Mwakyembe iwapo wanataka kuendeleza malumbano hayo nje ya utaratibu wa kawaida wa mawasiliano wa mawaziri, wajiondoe serikalini. Chikawe amekaririwa akisema kitendo cha Sitta kumtuhumu Ngeleja kwamba alitangaza kulipwa kwa Dowans kabla suala hilo halijafikishwa katika Baraza la Mawaziri kinakwenda kinyume cha miiko ya uwaziri kinachomtaka kutotoa siri za baraza.
Kwa mujibu wa Chikawe, Waziri Ngeleja kwa mamlaka aliyonayo kama waziri mwenye dhamana na masuala ya nishati alikuwa na mamlaka ya kutoa tamko alilotoa baada ya kufanya mashauriano na wataalamu mbalimbali wa masuala ya sheria serikalini.
Chikawe alisema iwapo Sitta na Mwakyembe walikuwa hawajaridhishwa na uamuzi wa Waziri Ngeleja walikuwa na njia za kuwasilisha hoja zao pasipo kutumia vyombo vya habari.

Kwa upande wake, Mwakyembe ameingia matatani kutokana na kunukuliwa na gazeti la Uhuru linalomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) akieleza kushangazwa na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICC) iliyoipa ushindi Dowans dhidi ya serikali na kutakiwa kulipwa fidia ya shilingi bilioni 94. ICC iliamua katika hukumu yake Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) iilipe Dowans fidia ya sh bilioni 94 kutokana na TANESCO kuvunja mkataba nayo.
 
Toa kwanza sababu kwa nini tukuamini wewe na si Tanzania Daima? maana haya makanusho tumeshayazoea, imekuwa kama fasheni fulani hivi

Sina uhakika na tatizo linalokukabili kama ni Elimu mbovu ulopata au ubovu wa kumbukumbu zako, Ina maana wewe na Tanzania Daima hamjui kuwa 'MWAKYEMBE si MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI!!! Manaibu mawziri hawaruhusiwi kabisaaa kwenye kikao cha baraza la mawaziri, kama katiba ngumu huijui hata KWENYE VITABU vya shule ya msingi vipo, Mwakyembe yupi sasa alofungwa mdomo kwenye kikao cha baraza la mawazir???? kama huo wa Tanzania Daima sio uzushi ubatize jina upendalo, but wenye akili wameng'amua

Title inamtaja JK ndo kawafunga mdomo while picha na Maelezo ya ndani yanasema alo chair kikao ni pinda kwa kuwa JK hakuwepo!!!!! Pinda hakaimu u JK anakaimu URAIS, ilipaswa waseme KAIMU RAIS, but habari isingependeza kama asingetajwa wala hapa JF isingekuwa ISSUE, Tujifunze kuwa wakweli japo kwa 0.005%
 
Uongo ni yule anayekanusha bila facts (Luhanjo). Picha huwa ni kielelezo rahisi kuelezea jambo....hapa jamvini tumewekewa. Hivyo kanusha hukuandika gazeti Tanzania Daima ni uongo! Tuweke bandiko lako watu waamue.

Aghalab, hata kama kikao hicho kisingewepo lakini katika uandishi habari kuna malengo lukuki mfano ya kisiasa, utamaduni, elimu & maarifa nk. Unaweza kuandika habari kwa nia ya kuchokonoa upate habari kamili. Hilo hutokea pale vyanzo na upatikanaji habari sahihi kwa wakati huwa sio rahisi. So unamtoa panya shimoni kwa njia kama hizo.
 
Pinda ni mnafiki, na ndio maana hawezi kusimamia madhara wanayopata watanzania dhidi ya mafisadi kama alivyofanya Mrema.
Kwa mtizamo wa hakika Pinda is very weak 2times Mrema na 4times Sokoine.
Kukaa kwake kimya akifumbia macho kilio cha wapigania uhai wa nchi means naye yupo kundi la wanaoangamiza uhai na rasilimali za taifa.ame-fail hatufai kabisa.
 
pi.jpg

SAKATA LA DOWANS: Sitta afungwa mdomo
• Baraza la Mawaziri chini ya JK lamshambulia yeye na Mwakyembe

na Mwandishi wetu (Tanzania Daima Jana hiyo)

RAIS Jakaya Kikwete amemfunga mdomo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta aliyeingia katika mzozo na waziri mwenzake wa Nishati na Madini, William Ngeleja. Mzozo huo uliibuka baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC), kuamua Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) iilipe Dowans fidia ya sh bilioni 94 kutokana na TANESCO kuvunja mkataba nayo.

Uamuzi wa kumziba mdomo Sitta, ulifikiwa jana katika kikao cha Baraza la Mawaziri, kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, chini ya Rais Kikwete(akiwakilishwa na pinda) mengine, mjadala wa malipo ya Dowans ulitawala kikao hicho. Mwingine aliyepigwa kufuli katika kikao hicho ni Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk. Harrisson Mwakyembe, ambaye naye aliungana na Sitta kumpinga Ngeleja kuilipa Dowans. Vyanzo vyetu vya habari vilisema Sitta na Mwakyembe walikuwa na wakati mgumu kutetea hoja ya kutaka serikali isiilipe Dowans na kwamba hata Rais alisema hafurahishwi na hukumu ya malipo hayo.

"Kikao bado kinaendelea, lakini Sitta na Mwakyembe walibanwa sana na mawaziri na hata Bwana mkubwa (Rais) aliungana na mawaziri wengine kuwalaumu kwa kupeleka mjadala huo hadharani," kilisema chanzo chetu cha habari.

Kwa mujibu wa habari hizo, kuanzia sasa Sitta na Dk. Mwakyembe, wamefungwa mdomo kuzungumzia suala la malipo ya Dowans hadharani na kwamba wanapaswa kuwa kitu kimoja kuhakikisha mipango ya serikali inatekelezwa kama ilivyopangwa.
Kabla ya kibano hicho jana, wiki iliyopita katika kikao cha kamati ndogo ya mawaziri uliibuka msuguano wa hoja kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema na Waziri Sitta.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho ambacho kilifanyika chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda(pichani), zinaeleza kuwa Jaji Werema alieleza kusikitishwa na matamshi ya Sitta katika vyombo vya habari.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zimemkariri Werema akieleza kushangazwa na hatua ya Sitta kuwashambulia yeye na Ngeleja huku akijua kuwa walichokifanya na kuamua kilikuwa kinagusa moja kwa moja mamlaka yao ya kiwajibu na kimamlaka.
Jaji Werema amekaririwa akimweleza Waziri Sitta kwamba iwapo kweli alikuwa ana uchungu na suala la Dowans, basi wakati kesi ikiendelea alipaswa kuisaidia serikali katika kuwasilisha utetezi dhidi ya malalamiko 17 yaliyokuwa yamewasilishwa na kampuni hiyo.

Habari zinaeleza kwamba hatua ya Sitta ambaye alikuwa akitambua fika namna kesi hiyo ilivyokuwa ikiendelea kutochangia jambo lolote wakati shauri hilo likiwa ICC na badala yake kusubiri hadi serikali ishindwe ndipo aanze kutoa matamshi katika vyombo vya habari ilikuwa ni ya kuchochea hasira za wananchi dhidi ya viongozi pasipo sababu zozote.

Wakati Jaji Werema akimshushia lawama Sitta kwa muda usiopungua dakika 15, Waziri Mkuu Pinda alikuwa kimya muda wote.Baada ya kumaliza hoja yake, Waziri Mkuu aliwataka wajumbe wa kamati hiyo ya mawaziri iliyokuwa ikijadili kuhusu Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Manunuzi unaotarajiwa kuwasilishwa katika Bunge lijalo kuendelea na mjadala. Awali kabla ya Werema kuzungumza, Sitta alichangia kuhusu muswada huo na akaeleza haja ya kuwekwa kwa masharti magumu zaidi ili kuzuia uwezekano wa makampuni ya kitapeli kujipenyeza nchini na kuigharimu serikali mamilioni ya fedha kauli ambayo ilionekana kumkera Werema. Awali hofu ilitawala kwamba Sitta na Mwakyembe, wangeweza kupoteza nafasi zao za uwaziri kutokana na hatua yao ya kuibua mjadala dhidi ya mawaziri wenzao nje ya Baraza la Mawaziri kuhusu uamuzi wa serikali kukubali kuilipa Kampuni ya Dowans Holdings SA.
Mkanganyiko wa kauli ya Sitta na Mwakyembe, ulisababisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, kutoa matamshi makali ya karipio kwa mawaziri hao wawili.

Ukali wa matamshi hayo ya Chikawe ambaye anadaiwa kupata baraka za Rais Kikwete, uliongezwa na tamko lake la kuwataka Sitta na Mwakyembe iwapo wanataka kuendeleza malumbano hayo nje ya utaratibu wa kawaida wa mawasiliano wa mawaziri, wajiondoe serikalini. Chikawe amekaririwa akisema kitendo cha Sitta kumtuhumu Ngeleja kwamba alitangaza kulipwa kwa Dowans kabla suala hilo halijafikishwa katika Baraza la Mawaziri kinakwenda kinyume cha miiko ya uwaziri kinachomtaka kutotoa siri za baraza.
Kwa mujibu wa Chikawe, Waziri Ngeleja kwa mamlaka aliyonayo kama waziri mwenye dhamana na masuala ya nishati alikuwa na mamlaka ya kutoa tamko alilotoa baada ya kufanya mashauriano na wataalamu mbalimbali wa masuala ya sheria serikalini.
Chikawe alisema iwapo Sitta na Mwakyembe walikuwa hawajaridhishwa na uamuzi wa Waziri Ngeleja walikuwa na njia za kuwasilisha hoja zao pasipo kutumia vyombo vya habari.

Kwa upande wake, Mwakyembe ameingia matatani kutokana na kunukuliwa na gazeti la Uhuru linalomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) akieleza kushangazwa na hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICC) iliyoipa ushindi Dowans dhidi ya serikali na kutakiwa kulipwa fidia ya shilingi bilioni 94. ICC iliamua katika hukumu yake Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) iilipe Dowans fidia ya sh bilioni 94 kutokana na TANESCO kuvunja mkataba nayo.

Jamani: Hivi katika Tasnia ya habari na Ufasaha wa Lugha; Tukio linaloendelea huripotiwa kwa kutumi ME au LI ?.

oh Sorry! Hicho kikao nadhani kimeendele jana! Lugha yangu mbofu!

Jana kulikuwa na thread iliyokuwa na kichwa cha habari "Sitta na Mwakyembe wafungwa mdomo kuhusu Dowans" Source ya thread hiyo ilikuwa gazeti la "TZ Daima". Watu wengi tulipoteza MUDA mwingi kuchangia thread hiyo. Katika gazeti hilo kulinukuliwa habari zilizotoka katika kikao cha baraza la Mawaziri ambacho JK alikuwa ni mwenyekiti wake. Nukuu mbalimbali zilitolewa kama ushahidi wa kilichosemwa kikaoni.

Habari zilizothibitishwa na Sitta mwenyewe na Pia Katibu mkuu Ndg. Ph. Luhanjo zinasema HAPAKUWA NA KIKAO CHA MAWAZIRI WALA HAKUNA ALIYEWAZIBA MDOMO SITTA NA MWAKYEMBE. habari hizi zimeandikwa na magazeti yote ya leo kasoro TZ Daima.

Wadau: Katika tasnia ya habari, Je, hamuoni kama gazeti hili ni hatari kwa usalama wa nchi yetu?. Je, gazeti kama hili katika utawala unaojali sheria za vyombo vya habari halipaswi kufungiwa kwa muda? Je, si kweli kwamba waandishi wa gazeti hili ni MAKANJANJA?. naomba tuwe wazalendo katika kujadili hili. Tanzania ni yetu na ni sisi wenye damu mpya tunaoweza kuifikisha nchi tunapopataka kwa AMANI.

Kwani ulitegemea kuna mtu aseme kuwa tulifanya mkutano? Kwani wameshawahi kusema kuwa huwa siku fulani kuna mikutano? It is still questionable. Hali ya mambo sasa haileweki maana hata gazeti likisema uwongo au ukweli hakuna anayekanusha. Lakini kuna wakati unajiuliza nini kazi ya waziri wa Habari?
 
Back
Top Bottom