Uongo na uzushi wa Jambo Leo
Vichwa hivi vya habari vinaweza kuandikwa na gazeti la namna gani ?
(Slaa ana Wazimu)
Tarehe 20.01.2011 gazeti la Jambo Leo lilinadi habari yake muhimu kama ifuatavyo: 'Slaa ana wazimu: Adaiwa Sasa anebakiza Kuvua Nguo.'
Kwa heshima na taadhima zote, Dk. Wilbroad Slaa (dokta kwa kusoma na sio kupewa) ni kiongozi wa nchi sawasawa na Mheshimiwa Mrisho Jakaya Kikwete. Kumuandika kwa namna ambayo Jambo leo imemuandika kunazua maswali mengi na hususan, nani hasa ni waandishi na wahariri wa gazeti hilo na wamiliki wake ni kina nani na wana ajenda gani dhidi ya Slaa na CHADEMA.
Ingawa gazeti hilo lina waandishi na wahariri wachache wanaostahili kuitwa waandishi kutokana na rekodi zao za huko nyuma, kazi kubwa inafanywa na watu walisohdindwa maisha na kazi nyingine na kuokolewa na watu waliojikuta wanapata fedha kirahisi sana katika nchi hii kiujanja ujanja na kwa kuwa watwana na vijakazi wa ofisi moja kubwa nchini.
Wanaomiliki gazeti hilo ni watu ambao hawana hata elimu ya sekondari na walikuwa makanjanja kwenye vyombo vya habari wakati wa enzi ya mheshimiwa Mkapa.
Mmojawao ni mpiga picha ambaye amewahi kulifanyia kazi gazeti la majira bila kuwa na elimu na ujuzi wowote unaoendana na photographer katika dunia hii ya leo, ikiwemo ugwiji katika matumizi ya digital camera.
Yeye ni kama kaokolewa na mmiliki wa kwanza, kwa kumfanyia kazi zake mbalimbali za nyumbani, ikiwemo pia kumtafutia wanawake wazuri wa jijini Dar es salaam na kokote mwenzake huyo anakokwenda duniani isipokuwa tu Uingereza (tutaeleza baadaye kwanini haendi uk.)
Kuwadi huyo pia anasimamia biashara nyingine mbalimbali na ujenzi wa nyumba za Kifahari ufukweni mwa bahari ya Hindi katika maeneo mbalimbali hapa jijini ikiwemo Masaki na Kigamboni. Pamoja na kukodi magari ya kifahari kwa sherehe za harusi na kadhalika.
Tajiri mwenyewe wa jambo leo ni bwana mmoja mfupi, mnene (kibushuti) ambaye aliishia darasa la sita huko Morogoro mji kasoro bahari nchi hizo.
Bwana huyo amepigwa marufuku uingereza kutokana na kughushi vyeti mbalimbali, kutumia majina ya uongo, wizi katika supamaketi na ulaghai wa aina mbalimbali. Lakini bwana huyu ndiye aliyesaidia sana jamaa wa wakubwa wa nchi hii walipokuwa na matatizo huko Ulaya. Hvi leo aruhusiwi kutia mguu wake ulaya ingawa inadaiwa bado mke wake wa pili au wa tatu anaishi huko Uingereza.
Neema ilimwangukia pale rais alipotembelea Uingereza na kuagiza wasaidizi wake wampe kitita cha fedha na baadaye kontrakti mbalimbali ambazo hakustahili kuzipata kwa sababu hana elimu wala ujuzi wa kuvipata. Lakini amri ya wakubwa nchi hii na waoto zao ndio inayofanya kazi na sio vinginevyo.
Jamaa hawa ni watu wanaokula vizuri sana kwa kutumia uhusiano wao na ofisi kuu nchini-ambayo si zamani sana baba taifa alitahadharisha isije iakgeuzwa makao ya makahaba. Lakini kwa bahati mbaya wameingia humo aina mpya ya makahaba wa kisiasa na wahuni wa ukweli, haki na ufuataji sheria. Wakiongoza na mmojawapo wa wamiliki wa zamani wa magazeti ya Mtanzania na nduguze.
Kihistoria, watu hawa ni kombamwiko kwa maana watu wanaopenda kulamba wakubwa, wanapenda sana wanawake wadogo na wanaendesha hata mashindano ya urembo nchini na ni watu wanaotumia fedha kwa fujo na wanaoishi kifahari mno ukilinganisha na umasikini unaowazunguka.
Pamoja na kupewa tenda mbalimbali hapa nchini kaitka biashara mbalimbali, si watu wanaoweza kutengeneza chochote cha kudumu maana hawana uwezo wala akili ya kufanza kitu kama hicho.
Wote wanaowafanyia kazi wanawafanyia tu basi kwa kuwa hawajapata ajira nyingne iliyo bora. Lakini si watu kabisa wa kuwaamini kwa lolote lile. Wapo tu kwa ajili ya matumbo yao na jamaa zao na warembo wao wanaowabadilisha kama nguo kila siku. Au sawasawa na utitiri wa magari ya kifahari wanayoyamiliki bila tija yoyote ya maana duniani.
Utajiri walionao katu usingelikuja kama isingelikuwa koneksheni yao na Ikulu na wakazi wake wa leo. Utaona kifadhila, wana deni kubwa sana kwa ikulu na ndio maana wanaweza wakachukua uharo na matapishi toka ikulu na kuyabandika bila aibu wala haya kwenye magazeti yao na yale ya watwana na wajakazi wao yakiwemo Habari Leo, Mtanzania, Daily News na vijarida visivyona sura wala jina vya kusafisha uoza uliopo leo hapa nchini.
Msomaji ukisoma vichwa kama hicho cha Jambo Leo hapo juu, na ukabahatika kujua kwa ufupi historia ya wamiliki na waendeshaji wake inakuwa ni rahisi kujua hilo ni gazeti la namna gani, liko kwa ajili ya nani, linalipwa na nani hata kama linaendeshwa kihasara na vilevile kiwango chake cha ukweli na kuaminika ambacho ni chini ya sifuri kwa hivi sasa.
Huwezi kamwe kwa akili yangu ndogo, ukaisafisha nguo chafu kwa kuchafua nguo safi.
Sihitaji kumwambia Slaa na chama chake kwamba uandikaji wa kichwa kama hicho una dhamira na umekusudia kufanya yeye aonekane si mkweli na mwenda wazimu na hilo gazeti na hao linaowafanyia kazi eti ndio wenye akili timamu na wanaosema ukweli. Bado waandishi, wahariri na wamiliki wa gazeti hilo wanaishi katika enzi ambazo Watanzania walikuwa wajinga na wasioweza kupambanua kati ya nafaka safi na pumba, kati ya uongo na kweli, kati ya kilicho safi na bora na kilichooza na kimeshaanza kunuka kwa hivi sasa!!!!