Unyanyasaji wa kikabila idara ya Uhamiaji

Unyanyasaji wa kikabila idara ya Uhamiaji

Kwa hiyo una declare maeneo ya Mbeya hayana shida ya wahamiaji haramu? Unaifahamu Tunduma? Hebu ona hoja yangu hapa. Kwa mfano, Mmalawi akajiita mnyakyusa na kwa sababu idara yetu ya uhamiaji inawachukulia wanyakyusa kama 1st grade citizens, wasimfanyie verification na wakampatia go ahead ya kwenda kupata kitambulisho cha utaifa NIDA, hapo hauoni tatizo?? Kwamba hakuna Wamalawi ambao wanajichanganya na Watanzania na kutamani Utanzania kwa njia ambazo si halali?
Ninachokiona mkuu, ni ku regard makabila fulani kuwa wao ndio 1st grade citizens, na makabila mengine hayo uliyosema yana "other factors" kuwa treat as if ni 2nd grade. Kwani hiyo verification ingefanyika kwa kila mtu kungekua na hasara gani? Ambacho sikubaliani nacho mimi, ni kum label kila Mnyakyusa (kwa mfano) kama Mtanzania halisia, na "muha" kwamba ni Mtanzania anaehitaji verification (kutumia makabila kama basis ya kwamba verification ifanyike au isifanyike) Roman Israel Esq
Hapana, soma uelewe mkuu. Hilo la kusema haya yanatokea kwasababu ya "first grade and 2nd grade" si kweli. Naifahamu Tunduma vyema sana tu. Watu waache kwenda South Africa wakimbilie Mbeya?tatizo siyo kubwa ndivyo nilivyomaanisha. Kuna maeneo mengine ni korofi zaidi. Tena kuna mipaka ambayo nchi hizo tunazopakana nazo zina amani ya hati hati. Yani hakuna amani ya kutosha. Very likely wakaazi wake watakuwa wanataka kuhamia bongo. Hako ni kamfano kamoja tu. Ni matumaini yangu kuwa mwishowe utaelewa tu.
 
Ndo ujue kwamba Tanzania Muhindi, Mwarabu au Mchotara ana haki kuliko wewe mweusi na hii ni kwa mujibu wa Sheria zetu, Muhindi akienda kuomba hati ya kusafiria anapewa fasta kwani ana makaratasi yaliyonyooka kuliko wewe, kwa kifupi Muhindi aliyezaliwa Tanzania/Tanganyika ni Mtanzania kuliko wewe mweusi hata kama wengi hamtalikubali hili!

Hakuna Muhindi/Mwarabu/Mchotara ataambiwa athibitishe Babu au sijui Bibi alizikwa wapi, hawa kila kitu kiko documented, anahitaji kutoa makaratasi tu, mfumo uliopo unampendelea Muhindi/Mwarabu/Mchotara moja kwa moja zaidi yako wewe uliyezaliwa Biharamuro au sijui Mpwapwa, tumerithi huo mfumo kutoka kwa Muzungu kwamba sisi ni raia daraja la 3 baada ya Muzungu, Muhindi/Mwarabu/Mchotara.

Welcome to the second class citizen of JMTZ!
Naona upo busy mkuu kuchochea chuki kwa waarabu na wahindi toka nyuzi za mo sijajua lengo lako ni nini.

mimi ni mwarabu na nawafahamu waarabu wengi tu wote lazima waulizwe maswali ya babu na bibi hilo ni lazima, sijawahi ona hata mmoja akaenda uhamiaji asiulizwe hilo swali.

Naongea kiswahili vizuri, nina vyeti vyote la 7, form 4, 6, chuo, cha kuzaliwa, vitambulisho vyote official vya serikali kama kura na uraia. Wazazi wana passport etc lakini still wakati wa kuomba passport sikupata urahisi kama unavyosema, lazima upeleke uthibitisho wa bibi na babu kama alivyoleta mtoa mada.
 
Naomba ufafanue zaidi kuhusu 'makabila ya mipakani'?? Mipaka ipi hiyo??
Wanskyusa, Wachagga, Wasukuma yote hayo ni makabila ambayo wanapakana na nchi jirani, ila wao hawapati shida hii, ukishasema tuu wewe ni Mnyakyusa, fasta wanaanguka sahihi na kukupigia mhuri.
Hebu tuelezane vizuri hiyo mipaka inayozungumzwa ni ipi??
Ndumbula Ndema
Zambia kunakabira LA kinyakyusa au Kenya kuna wachaga au wasukuma,Burundi ,kongo,Rwanda wasukuma wapo? Ukifika kigoma au Bukoba ,huwezi kutofautisha mhaya yupi Mganda,yupi wanasikilizana hawa kwa rugha zao zote mbili kigoma ndo usipime,yeyeyeyeeee murundi ndiyo muha muha ndo Mrundi,nashangaa ukianbiwa Ku verify uraia wako unatoa povu ila kwenye WhatsApp huhoji,
 
Hapana, soma uelewe mkuu. Hilo la kusema haya yanatokea kwasababu ya "first grade and 2nd grade" si kweli. Naifahamu Tunduma vyema sana tu. Watu waache kwenda South Africa wakimbilie Mbeya?tatizo siyo kubwa ndivyo nilivyomaanisha. Kuna maeneo mengine ni korofi zaidi. Tena kuna mipaka ambayo nchi hizo tunazopakana nazo zina amani ya hati hati. Yani hakuna amani ya kutosha. Very likely wakaazi wake watakuwa wanataka kuhamia bongo. Hako ni kamfano kamoja tu. Ni matumaini yangu kuwa mwishowe utaelewa tu.
Mkuu, unachofanya, una "cherry pick" mifano michache ya mbali kabisa na kuitumia kujenga hoja ya ku justify ubaguzi unaofanywa na idara yetu ya uhamiaji.
Umetoa mfano wa m South Africa kukimbilia Mbeya... Kuna upande Mbeya inapkana na South Africa? Mfabo wa Tunduma niliokupa; Yenyewe inapakana na South Africa? Tunduma inapakana na Zambia; Je, hakuna Wazambia wengi wanaotamani Utanzania na hata kushawishika kujipa Utanzania kwa njia zisizo halali??
Kyela, mfano mwingine, inapakana na Malawi; hakuna Wamalawi wanaotamani kujipenyeza Tanzania? Hakuna ambao wameshafanya hivyo? Roman Israel Esq
 
Tena wasukuma wana muingiliano mkubwa sana na wanyakyusa sema watu wakigoma kagera ndo wanapaa shida
Kagera siyo wote Kagera watu wanao sumbuliwa ni watu kutoka wilaya ya ngara, hasa Wahangaza, Wahaya hawaguswi wala kusumbuliwa kabisa japo wameingiliana sana na Waganda.
 
Povu limenijaa ndiyo maana umenisoma vibaya au nimeandika vibaya ,nasema hoja yako haina mashiko kama tu una verify account za WhatsApp na Facebook unashindwa nini kuverify uraia wako?
Jifunze kuandika kwanza mkuu.
Nina wasiwasi kama umeweza kusoma na kuelewa nilichoandika, maana hata kuandika tu ni tatizo.
Sina shida na kujaza fomu. Shida yangu ipo kwenye criteria ya kujaza hizo fomu, kwamba kuna watu wa makabila fulani fulani tu ndo wanaambiwa wajaze, ila makabila mengine wao wala hawaambiwi wajaze hizo fomu; na hakuna ambae atakupa jibu la kueleweka kwamba kwa nini makabila fulani tu? nyamatala.
 
Zambia kunakabira LA kinyakyusa au Kenya kuna wachaga au wasukuma,Burundi ,kongo,Rwanda wasukuma wapo? Ukifika kigoma au Bukoba ,huwezi kutofautisha mhaya yupi Mganda,yupi wanasikilizana hawa kwa rugha zao zote mbili kigoma ndo usipime,yeyeyeyeeee murundi ndiyo muha muha ndo Mrundi,nashangaa ukianbiwa Ku verify uraia wako unatoa povu ila kwenye WhatsApp huhoji,
Unaweza kutenganisha Mnyakyusa na Mmalawi?
Zambia kunakabira LA kinyakyusa au Kenya kuna wachaga au wasukuma,Burundi ,kongo,Rwanda wasukuma wapo? Ukifika kigoma au Bukoba ,huwezi kutofautisha mhaya yupi Mganda,yupi wanasikilizana hawa kwa rugha zao zote mbili kigoma ndo usipime,yeyeyeyeeee murundi ndiyo muha muha ndo Mrundi,nashangaa ukianbiwa Ku verify uraia wako unatoa povu ila kwenye WhatsApp huhoji,
Tembea uone. Nenda Kyela ukaone Wamalawi wanaopakana na Kyela jinsi wanavyofanana na kusikilizana na Wanyakyusa wa kule... Hadi majina wanayotumia ni yale yale kiasi kwamba ni ngumu kujua yupi Mnyakyusa, yupi Mmalawi. Hiyo ni feature common kwa makabila YOTE ambayo yako mpakani... Bila kujali kuwa ni waha, au ni wanyakyusa, au ni Wapare;Ila, idara ya uhamiaji imeamua kuchagua makabila ya mipaka ya maeneo fulani tuu,na sio maeneo mengine kwa sababu za kibaguzi, na nyie wengine mnafuata mkumbo tu na kutetea.
Naona tatizo lako kubwa ni kukosa exposure. nyamatala.
 
Povu limenijaa ndiyo maana umenisoma vibaya au nimeandika vibaya ,nasema hoja yako haina mashiko kama tu una verify account za WhatsApp na Facebook unashindwa nini kuverify uraia wako?
Sina tatizo na verification. Tatizo langu ni hiyo verification kuwa "biased", kulingana na kabila lako. Kwamba ukiwa kabila fulani ndo unafanyiwa, ukiwa kabila fulani hufanyiwi verification. nyamatala.
 
Mkuu, unachofanya, una "cherry pick" mifano michache ya mbali kabisa na kuitumia kujenga hoja ya ku justify ubaguzi unaofanywa na idara yetu ya uhamiaji.
Umetoa mfano wa m South Africa kukimbilia Mbeya... Kuna upande Mbeya inapkana na South Africa? Mfabo wa Tunduma niliokupa; Yenyewe inapakana na South Africa? Tunduma inapakana na Zambia; Je, hakuna Wazambia wengi wanaotamani Utanzania na hata kushawishika kujipa Utanzania kwa njia zisizo halali??
Kyela, mfano mwingine, inapakana na Malawi; hakuna Wamalawi wanaotamani kujipenyeza Tanzania? Hakuna ambao wameshafanya hivyo? Roman Israel Esq
Nimekwambia wakazi wengi wa maeneo yale wako more likely kukimbilia SA kuliko Mbeya. Sijui kitu gani huelewi? Kuna watanzania wengi tu wanaopita hizo nchi kuelekea SA. Pia kuna waliokuwa wakitokea Ethiopia, ambao walikamatwa maeneo yale, lakini destination yao ilikuwa SA. Mbona unakuwa mgumu kuelewa? What cherry picking are you referring to?
 
Nimekwambia wakazi wengi wa maeneo yale wako more likely kukimbilia SA kuliko Mbeya. Sijui kitu gani huelewi?
Je, hakuna Wazambia wengi wanaotamani Utanzania na hata kushawishika kujipa Utanzania kwa njia zisizo halali??
Kyela, mfano mwingine, inapakana na Malawi; hakuna Wamalawi wanaotamani kujipenyeza Tanzania? Hakuna ambao wameshafanya hivyo? Roman Israel Esq
 
Je, hakuna Wazambia wengi wanaotamani Utanzania na hata kushawishika kujipa Utanzania kwa njia zisizo halali??
Kyela, mfano mwingine, inapakana na Malawi; hakuna Wamalawi wanaotamani kujipenyeza Tanzania? Hakuna ambao wameshafanya hivyo? Roman Israel Esq
Siyo kwa wingi kama ilivyo kwenye mipaka ambayo hizo nchi tunazopakana nazo hata amani yenyewe ni hatihati mfano warundi na wacongo. Its a matter of common sense.

Bado nina amini kuwa hakuna first wala second class citizen kwenye hoja hii. Ni mitizamo tu.
 
Kwa hiyo itakua ni hasara kubwa sana kama idara ya uhamiaji ikiamua kuwa utaratibu uwe mmoja kwa wote wanaohitaji verification ya uraia kwamba wote wajaze hizo fomu za kuulizia kuhusu walikozaliwa na walikozikwa mabibi na mababu zao bila kujali makabila yao?? Ni hasara zaidi wakifanya utaratibu huo kwa watu wote kuliko utaratibu unaotumika sasa wa kuchagua makabila fulani tuu ambao unaleta ukakasi? Roman Israel Esq
 
Siku chache zilizopita, ilinibidi kujongea katika ofisi za uhamiaji kwa ajili ya kupata sahihi ya afisa ya uhamiaji katika fomu za kitambulisho cha utaifa (kwenye hizi fomu kuna sehemu ambayo inabidi isainiwe na uhamiaji).Kilichonikuta ndio kimenifanya niandike huu uzi.

Baada ya kufika ofisi husika na fomu zangu, swali la kwanza nililoulizwa ni, "wewe ni kabila gani"? Baada ya kumjibu yule mdada alieniuliza, kilichofuata alinikabidhi fomu nyingine ambayo ina page 9, iliyojaa maswali ambayo kiukweli yamejaa ukakasi sana;

Mfano: Mahali walipozaliwa babu na bibi yako mzaa baba (mkoa, wilaya, tarafa, kata, kijiji), Mahali walipozaliwa babu na bibi yako mzaa mama
(mkoa, wilaya, tarafa, kata, kijiji).

Mahali ambapo babu au bibi yako alifariki (mkoa,wilaya,tarafa,kata,kijiji), na maswali mengine mengi ya aina hiyo (imagine kujibu page 9 za maswali ya aina hiyo).

Lakini, kilichoni irritate zaidi, niligundua kwamba si waombaji wote wanajazishwa hii fomu (wengine wanasainiwa kirahisi kabisa bila kujaza chochote); na kinacho determine wakujazishe au wasikujazishe hilo lifomu ni *kabila* lako!! Kuna makabila fulani ukienda pale ukitaja, wanakusainia bila tashwishwi nyingi, ila kuna makabila mengine ndo process inakua ndefu mno (nimetumia muda wa siku mbili ofisi ya uhamiaji kukamilisha hilo,while my other colleagues spent hardly 15 minutes for a similar purpose!!).

Fikiria unamuona mtu mnaefanya nae kazi, yeye anakuja na fomu zake, anaulizwa kabila anataja kabila fulani, anaambiwa lete fomu zako, anasainiwa... Huku wewe umekaa pembeni unahangaika kujaza page 9 za maswali yanayotia ukakasi, hadi wenzako wanakushangaa kwani wewe vipi? Mbona sisi hatujasumbuliwa?
Siku ya kwanza, nimejaza hilo lifomu lao nikaambiwa niliache, nirudi next day saa tatu asubuhi (hapo nilitumia masaa 6 ofisi za uhamiaji).

Nimerudi siku ya pili, nikaambiwa subiri, baada kama ya nusu saa yule mdada akatoka. Nilisubiri kwa zaidi ya masaa sita tena, ambapo ndipo niliweza kukamilisha mchakato huo na wakanisainia fomu yangu hatimaye (namshukuru sana yule kijana alienihudumia siku ya pili, alikua ni mstaarabu na mnyenyekevu sana na hata yeye alionyesha kushangazwa kwa nini nimezungushwa vile).

Nimesikitika sana, kwamba kumbe sisi makabila mengine ni second grade citizens ndani ya nchi yetu!!
Kwa nini kuwe na preferential treatment (huduma tofauti) kwa raia wanaohitaji huduma ya uhamiaji, ambayo iko based kulingana na kabila??
Nadhani wahusika wameliona hili,na hatua stahiki zitachukuliwa haraka.Kama ni kweli,this is extremely serious,sikudhani such nonsense could still exist in Tanzania,very old fashion indeed.
 
Kwa hiyo itakua ni hasara kubwa sana kama idara ya uhamiaji ikiamua kuwa utaratibu uwe mmoja kwa wote wanaohitaji verification ya uraia kwamba wote wajaze hizo fomu za kuulizia kuhusu walikozaliwa na walikozikwa mabibi na mababu zao bila kujali makabila yao?? Ni hasara zaidi wakifanya utaratibu huo kwa watu wote kuliko utaratibu unaotumika sasa wa kuchagua makabila fulani tuu ambao unaleta ukakasi? Roman Israel Esq
Nadhani ume "arrive at conclusion without concrete facts". Ni matukio mangapi ambayo unaweza kuyalist hapa ambayo yamepelekea wewe kufikia ama ku "reach" hiyo "conclusion"? Ni wewe tu ulipoenda mara moja? Unazungumzia "makabila", je ulienda zaidi ya mara moja na ukataja kabila zaidi ya moja kufikia kwenye conclusion kuwa "kuna makabila yanafanywa secondary citizens"? umefanya research gani kufikia hiyo tamati? Hayo makabila unayosema "yanapendelewa", ulisubiri hapo ukaona mwenyewe walipopewa huduma hayo makabila na hawakupewa fomu za ziada kama wewe? Ama je uliwatuma watu wa makabila ya tofauti wakaja na hizo "findings"

It is better not to jump in to conclusions without specific data to prove.

No research, no right to speak so to speak.
 
Nadhani wahusika wameliona hili,na hatua stahiki zitachukuliwa.Kama ni kweli,this is extremely serious.Sikudhani such nonsense could exist in Tanzania.
Pengine utaratibu unaotumika ndiyo unaweza kumfanya mtu akahisi amebaguliwa. Mfano kuulizw kabila lake na huku kwenye fomu hakuna hilo swali.

Lakini pia kwa upande mwingine, suala la uhamiaji haramu siyo la kubeza.
 
Back
Top Bottom