Unyanyasaji wa kikabila idara ya Uhamiaji

Unyanyasaji wa kikabila idara ya Uhamiaji

mkuu mtoa post ni watu wa Kabila la mkoa Gan hawakupata kashkashi ktk vérification ?
 
Kama kuna fomu namba 10 ulitakiwa kupewa kwa sababu kiswahili kina kupa tabu "irritate" umeshindwa kutafsiri. Pale uhamiaji ukianza na lugha isiyo ya taifa ni balaa
 
Siku chache zilizopita, ilinibidi kujongea katika ofisi za uhamiaji kwa ajili ya kupata sahihi ya afisa ya uhamiaji katika fomu za kitambulisho cha utaifa (kwenye hizi fomu kuna sehemu ambayo inabidi isainiwe na uhamiaji).Kilichonikuta ndio kimenifanya niandike huu uzi.

Baada ya kufika ofisi husika na fomu zangu, swali la kwanza nililoulizwa ni, "wewe ni kabila gani"? Baada ya kumjibu yule mdada alieniuliza, kilichofuata alinikabidhi fomu nyingine ambayo ina page 9, iliyojaa maswali ambayo kiukweli yamejaa ukakasi sana;

Mfano: Mahali walipozaliwa babu na bibi yako mzaa baba (mkoa, wilaya, tarafa, kata, kijiji), Mahali walipozaliwa babu na bibi yako mzaa mama
(mkoa, wilaya, tarafa, kata, kijiji).

Mahali ambapo babu au bibi yako alifariki (mkoa,wilaya,tarafa,kata,kijiji), na maswali mengine mengi ya aina hiyo (imagine kujibu page 9 za maswali ya aina hiyo).

Lakini, kilichoni irritate zaidi, niligundua kwamba si waombaji wote wanajazishwa hii fomu (wengine wanasainiwa kirahisi kabisa bila kujaza chochote); na kinacho determine wakujazishe au wasikujazishe hilo lifomu ni *kabila* lako!! Kuna makabila fulani ukienda pale ukitaja, wanakusainia bila tashwishwi nyingi, ila kuna makabila mengine ndo process inakua ndefu mno (nimetumia muda wa siku mbili ofisi ya uhamiaji kukamilisha hilo,while my other colleagues spent hardly 15 minutes for a similar purpose!!).

Fikiria unamuona mtu mnaefanya nae kazi, yeye anakuja na fomu zake, anaulizwa kabila anataja kabila fulani, anaambiwa lete fomu zako, anasainiwa... Huku wewe umekaa pembeni unahangaika kujaza page 9 za maswali yanayotia ukakasi, hadi wenzako wanakushangaa kwani wewe vipi? Mbona sisi hatujasumbuliwa?
Siku ya kwanza, nimejaza hilo lifomu lao nikaambiwa niliache, nirudi next day saa tatu asubuhi (hapo nilitumia masaa 6 ofisi za uhamiaji).

Nimerudi siku ya pili, nikaambiwa subiri, baada kama ya nusu saa yule mdada akatoka. Nilisubiri kwa zaidi ya masaa sita tena, ambapo ndipo niliweza kukamilisha mchakato huo na wakanisainia fomu yangu hatimaye (namshukuru sana yule kijana alienihudumia siku ya pili, alikua ni mstaarabu na mnyenyekevu sana na hata yeye alionyesha kushangazwa kwa nini nimezungushwa vile).

Nimesikitika sana, kwamba kumbe sisi makabila mengine ni second grade citizens ndani ya nchi yetu!!
Kwa nini kuwe na preferential treatment (huduma tofauti) kwa raia wanaohitaji huduma ya uhamiaji, ambayo iko based kulingana na kabila??



Mkuu,pole sana kwa madhila yaliyokukuta.

Naomba kuuliza kama hautajali, wewe ni kabila gani??,

Nauliza hivyo kwa sababu ni watu wa kutoka Mkoa wa Kigoma tu ndiyo hasa huwa tunanyanyaswa tunapofika uhamiaji.

Mimi mwenyewe nilipata kunyanyasika vibaya uhamiaji Mkoa wa Morogoro.
 
Pole sana.
Mimi mwenyewe kitambulisho cha taifa nilikwama pale uhamiaji.Kisa natoke Kagera wilaya inayopakana na Rwanda.Kuna makabila akitaja wanamgongea mhuri mara moja.
Mpaka sasa sijafaulu kwenda NIDA.
hata sijui nifanyeje?
 
Rafiki yangu wa Kigoma aliwahi kwenda pale RITA naye akaletewa upuuzi wa aina hiyo, alinitumia sms akaniambia plz naomba uje unitolee dhamana police station kuna watu wananivuruga hapa. Baada ya hapo alianza kutukana mule RITA kuanzia mfanya usafi mpaka mkurugenzi, na kweli nilimkuta police jamaa.

Nakumbuka aliniambia kuwa kuna unynyasaji mkubwa sana kwa maadhi ya mikoa akanimbia Kigoma ilikuwepo kabla ya vita ya Burundi na watu waliishi huko.
 
Makabila ya mipakani ni yapi??
Wasukuma hawapo mpakani?
Wanyakyusa hawapo mpakani?
Wachagga hawapo mpakani?
Makabila yote hayo matatu hapo juu, nimeshuhudia wanasainiwa bila kujazishwa hilo lifomu lenye maswali ya kipumbavu.
Kwa hoja hiyo, sidhani kwamba hoja ni makabila ya mipakani. Jini Kisiranii
Wasukuma wapo mpakani ? Unaweza kufafanua ni mpaka gani wasukuma wapo ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaona sasa! Kwa nini utaje muha na si mhaya, mkurya, mmasai, mnyakyusa, makonde, mfipa, mndali, msambaa, mjaluo na wengine ili hali nao wapo mipakani?

Kwa nini burundi na rwanda inaogopwa na tanzania, na kwa nini mha na mhangazwa tunapachikwa uraia wa rwanda na burundi?
Hofu iliyopo kutokana na matendo yao tu wakiwa nchini mwao ndio inahisiwa hata majiani wanaweza ambukizwa u genocide


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sisi waha pekee na wahangaza tunaobaguliwa na uhamiaji. Hata usipotaja, wewe ni muha tu.

Watuoneshe nchi yetu twende
Hatubaguliwi Bali ni hofu iliyopo kutokana na majirani Wa hizo nchi tunaofanana nao
Inaaminika kuwa warundi,wakongo na wanyarwanda ni makatili sana, tofauti na mipka ya nchi zingine kama Ujaluoni au unyanja...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole kwa process hiyo ndefu.

Sandawe people - Wikipedia.

Umesema wewe ni msandawe.

Unaweza uwe msandawe kweli.

Au unaweza uwe mtu wa kabila lingine la kitanzania.

Your good level of reasoning and intellect, your boldness, na pia the way you slightly underestimate other people's intellect, na kwa jinsi ulivyoitaja na kuielezea hiyo list ya 'first class tribes', inaelekea wewe ni mtanzania wa Kigoma au Kagera.

NB: Ni vigumu kwa baadhi ya hao 'first class tribes' kupata nafasi ya urais kwenye mfumo wa sasa.
 
Back
Top Bottom